Search This Blog

Monday, October 24, 2022

NAMPENDA ADUI YANGU - 4

 







    Chombezo : Nampenda Adui Yangu

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilipoishia…..



    Mtu yeyote ambaye angemuona angegundua Kenny alikuwa mtu wa mazoezi, kutokana na muonekano wake wa kuvutia ndiyo uliosababisha atafutwe na wasichana wa shule tofauti mkoani Kilimanjaro, lakini alipuzia hisia zao na siku zote hakufikiria kitu kingine zaidi ya malipo ya kisasi. Kenny alifahamika vizuri shule tofauti mkoani Kilimanjaro kutokana na kipaji chake cha kuigiza kilichowavutia wanafunzi wa kike.Katika matamasha mengi ya mashule,watu walifurahishwa na jinsi alivyokuwa mcheshi katika kuigiza akiwa na kila sababu ya kuwa muigizaji.



    Endelea….



    Hatimaye alimaliza kidato cha nne na kuchaguliwa kujiunga shule ya sekondari Azana ya jijini Dar es salaam. Hiyo ilifuata baada ya kufaulu vizuri mtihani wake wa kidato cha nne kwa kupata daraja la kwanza.Alichaguliwa kujiunga shule hiyo kupitia masomo ya biashara aliyokuwa anayaweza vizuri.Watu kadhaa wa karibu wa familia hiyo ya Kibosho, Moshi vijijini walichanga fedha na kuziwasilisha kwa mama Mushi amabaye alikuwa akiishi naye.Kenny anafurahishwa na upendo wa watu ambao waliuonesha moyoni aliwaza kusoma kwa bidii na mwishoe kutimiza ndoto zake.

    Baada ya maandalizi yake kukamilika alijiunga na shule hiyo ya Azana kidato cha tano akiwa na mipango mingi kichwani mwake.Masomo yalianza na yeye hakuchelewa kufuatilia kwa umakini kilichokuwa kinafundishwa.Alijitahidi kusoma kwa bidii ili elimu yake ije kumsaidia malipizi ya kisasi kwa Mr.Carlos.Siri ya mauaji aliyoyafanya Mr.Carlos kwenye familia yake hakuna aliyeijua.Ilikuwa ni siri ambayo hakuwahi kumueleza mtu katika maisha yake.Hakupenda siri hiyo ijulikane kwa vile aliamini ingemfikia Mr.Carlos na kuwa tatizo.

    Baada ya miezi mitatu akiwa anaendelea na masomo yake kama kawaida tayari alishaifahamu nyumba ya Mr.Carlos iliyokua maeneo ya Mbezi Beach.Hizo zilikua jitihada zake ambazo zilimpa taabu sana na kumumiza kichwa kwa vile aligundua Mr.Carlos alikuwa na uwezo mkubwa wa kifedha tofauti na alivyofikiria.Siku moja ya Jumapili alikuwa katika matembezi kama ilivyokuwa kawaida yake kufanya hivyo siku hiyo kila wiki.Baada ya muda mrefu wa kutembea aliamua kuanza kurudi shule kwa mguu akitokea maeneo ya Magomeni.

    Alikuwa akitembea taratibu na kichwani alikuwa na mawazo kadhaa.Aliendelea kutembea na kuzidi kukisogelea kituo cha daladala cha Jangwani ambacho kwa umbali aliliona gari likiwa limeegeshwa, alipofika kituoni hapo aliwaona wasichana wawili waliokuwa na sifa zote za kuitwa warembo wakiwa nje ya gari hilo.Walivaa nguo za rangi nyekundu na kuendana kila kitu, mmoja wao alimuita na alitimiza wito huo na kuanza kusogea karibu na eneo walilokuwa.Mara baada ya kuwasogelea aligundua mrembo mmoja alikuwa ni mtu mzima tayari ingawaje sura yake ilimuonesha kama alikuwa na umri mdogo lakini mrembo mwingine kati ya hao aliyemuona alibaini alikuuwa na umri mdogo kama yeye au alimzidi kabisa.

    “samahani kaka tunaomba ukatununulie mafuta ya gari”Alisikika yule mkubwa akiongea wakati huo yule msichana mwingine alibaki kimya akimtazama vizuri Kenny

    “Hakuna shida nipeni fedha”Alijibu Kenny, alipewa fedha na kuambiwa kidumu cha kuchukulia akinunue pia kwa vile hawakuwa nacho.Alianza kuondoka kuelekea kituo cha kuuza mafuta kutimiza ombi hilo.Aliwaacha wakibishana kutokana na kuisha mafuta kwa gari hilo.Wakati akiendelea kuelekea kituo cha kuuza mafuta,kuna jambo lilimtatiza kichwani,alihisi kumfahamu mrembo aliyembaini ni mtu mzima lakini hakukumbuka ni wapi alionana naye.Baada ya kukumbuka kwa muda mrefu bila mafanikio aliamua kupuuzia.Mara baada ya kununua mafuta alirejea haraka na kuanza kuwasaidia kuweka mafuta kwenye gari lao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Warembo ambao Kenny aliwaona waliua ni watoto wa Mr.Carlos mkubwa akiwa ni Jane ambaye awali alisoma na dada yake marehemu Juliana.Na mwingine aliitwa Mary ambaye alikuwa mtoto wa mwisho wa Mr.Carlos.Mary alikuwa amepata mshtuko wa moyo pale Kenny alipowasogelea baada ya dada yake Jane kumuita awasaidie kuwanunulia mafuta.Alikuwa amevutiwa na muonekano na sura ya Kenny ikiwa pamoja na mwili wake ulionekana kujengeka kimazoezi.Hata punde alipowasogelea bado alimchunguza Kenny na kugunua mambo mengi yaliyomvutia.Aliamini hakuwahi kukutana na mwanaume aliyemvutia kama Kenny lakini kitu kilichomuumiza kichwa ni jinsi gani angeweza kupata nafasi ya kuwa naye karibu.Mara baada ya Kenny kuondoka kuelekea kununua mafuta ndipo mawazo yalimzidia akiamini alikuwa na muda mfupi wa kumuona Kenny kwa mara ya mwisho.

    Baada ya kufikiria kwa muda kidogo aliamua kumuliza dada yake ni kiasi gani cha fedha watampa Kenny kwa msaada wake alioutoa. “Tumpe elfu ishirini,siumeona mtu mwenyewe anatembea kwa mguu….”alijibu dada yake Jane akiongeza kuwa kama kijana huyo alikuwa na matatizo kifedha wangekuwa wamemsaidia kidogo. Mary aliona huo ndiyo upenyo wa kumpata Kenny,aliingia kwenye gari na kufungua pochi yake akatoa elfu ishirini.Mara baada ya kutoa fedha hizo alichukua kadi yake ya mawasiliano ya namba ya simu na barua pepe kisha akaiviringisha na zile fedha kwa pamoja.Alitoka nje ya gari na tayari Kenny alikuwa amerudi, alianza kuweka mafuta hayo kwenye tenki la gari hilo.Muda wote huo Mary aliutumia kumchunguza vizuri Kenny, alibaki kimya ingawaje dada yake Jane aliongea na Kenny mara kadhaa. Mapigo yake ya moyo yalimwenda mbio na hisia juu ya mahusiano na Kenny zilizidi kila sekunde iliyojiri, alitamani wabaki eneo hilo akimtazama Kenny. Mara baada ya zoezi hilo Jane alizunguka upande wa uskani na kuwasha gari ambalo liliwaka bila shida yeyote. “mpe fedha hizo tuondoke”alisikika Jane akiwa ndani ya gari.

    Mary alimsogelea Kenny na kushika mkono wake wa kulia akamuwekea ile kadi aliyoviringisha na zile fedha.Mapigo yake ya moyo yaliendelea kwenda mbio hususani alipoushika mkono wa Kenny.Mara baada ya kuweka zile fedha na kadi kwenye mkono aliufunga mkono huo kwa vidole vya Kenny.”Tafadhali usisahau kunitafuta….”Alisikika Mary kwa sauti ya chini huku akiuachia mkono wa Kenny,aligeuka na kuelekea kwenye gari.Punde alipanda gari hilo liliondolewa eneo hilo na kumuacha Kenny akiwa amuduwaa.

    Kenny alifungua mkono wake wa kulia na kuona aliwekewa fedha zilizo viringishwa na kitu.Akaamua kuzitoa fedha hizo punde alipotoa aliona kadi ya mawasiliano ikiwa na jina moja la Mary.Kilichomfurahisha zaidi ni fedha alizoziona kwani hakuwa na fedha hata kidogo.Lakini hakutambua ni kwa nini Mary, kama kadi yake ivyoandikwa alitaka amtafute.Hakuelewa kitu cha ziada ambacho mrembo huyo alikitaka kutoka kwake,alianza kutembea kuelekea shule kwao akiwa na furaha.Siku hiyo ilisha pasipo kumpigia Mary kila wakati alipoazima simu akitaka kumpigia hakufanya hivyo.Siku mbili baadaye aliamua kumpigia,baada ya kuona yeye aliombwa kumpigia Mary na hakuwa na tatizo lolote.Simu iliita kwa muda mfupi na ikapokelewa,Kenny alijitambulisha kwa jina kabla ya kumweleza kuwa yeye ndiye aliyewasaidia gari lao lilipoisha mafuta. Mary alimweleza Kenny akate simu na muda mfupi baadaye alimpigia na kuanza kumpeleleza Kenny kiundani na kugundua alisoma Azana.Maongezi yao yaliendelea kwa muda mrefu na Kenny alibaini Mary alisoma Nchini Ufaransa.Alikuwepo nchini Tanzania katika likizo yake ndefu, Mary alimwomba Kenny akihitaji wawe marafiki jambo ambalo Kenny alikubali.

    Baada ya mazungumzo yao marefu Kenny alikuwa amegundua vitu vingi kutoka kwa Mary aliyegundua alikuwa na huruma.Mary alikuwa amejitambulisha kwa jina la Mary Benson alifanya hivyo ili Kenny amchukulie alitoka katika familia ya kawaida.Aliamini angesema alitwa Mary Carlos Mato, Kenny angemuogopa kutokana na utajiri mkubwa wa baba yake.Walinza urafiki wao huku Mary akimtembelea Kenny mara kwa mara akimpa zawadi tofauti ikiwa ni pamoja na simu. Kudhihirisha umuhimu wa Kenny kwake alimlipia ada ya shule ya miaka yote miwili.

    Mambo ambayo anatendewa Kenny kama fadhila ndiyo yanayomuibua hisia moyoni mwake,anagundua anampenda Mary, lakini alijawa na hofu ya kumweleza akiamini huenda msichana huyo alitaka wawe marafiki tu.Wiki moja ikiwa imebaki Mary aanze safari ya kurudi shule aliamua kumpigia simu na kumweleza ukweli wake.Alishangazwa na furaha ambayo Mary aliionesha kupitia simu ya kuelezwa anapendwa na Kenny.Siku iliyofuata alimpelekea zawadi ya kadi na maua shuleni kwao.Mary akiwa na furaha alimweleza alikuwa anajiandaa kumwambia anampenda baada ya kuona hambiwi,walianza uhusiano wao wote wakiwa na furaha.

    * * * * *CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mary Carlos Mato alikuwepo nchini Tanzania katika likizo yake na alisoma shule ilokuwa jijini Paris,Ufaransa.Alifurahishwa na mwanzo wa urafiki wa kimapenzi na Kenny John mtu aliyemuwaza toka siku ya kwanza kumuona.Kichwani aliwaza kusoma kwa bidii na kuweka mazingira ya Kenny kusoma nchini Ufaransa kama yeye.Ingawaje aligundua Kenny hakuwa na maisha mazuri katika familia yake lakini aliamini hakuna lililoshindikana kwa wao kuandaa maisha yao ya baadaye yenye furaha.Dada yake Jane alikuwa tayari ameshaolewa nchini Uingereza na alikuwa akirudi nchini Tanzania kuwasalimia wazazi wake na baada ya siku chache alikuwa akirudi tena London,Uingeraza.

    Hatimaye muda wa likizo wa Mary ulisha na safari ilianza akisindikizwa na baba yake mpaka uwanja wa ndege.Alikua amemuaga Kenny na waliahidiana kuwa wangewasiliana kwa barua pepe na simu.Mary ambaye muda mwingi walikuwa pamoja au kupigiana simu akiwa katika likizo yake,hatimaye alipofika shuleni alianza masomo pasipo kusahau kuwasiliana na Kenny kila mara hususani kwa kutumia barua pepe.Mara nyingi siku za mwisho wa wiki Mary alimpigia simu Kenny kumjulia hali.

    Baada ya miezi kadhaa Mary alirudi tena Tanzania katika likizo yake nyingine alipokelewa na familia yake na walielekea mpaka nyumbani kwao Mbezi Beach.Siku iliyofuata mapema aliondoka kwao na kwenda kukutana na Kenny kama walivyokuwa wameahidiana.Kila mmoja alimfurahia mwenzie na kumuona kama alikuwa mzuri wa kuvutia zaidi ya awali.Baada ya siku kadhaa Mary anaamua kumueleza ukweli wa jina lake baada ya kutoona umuhimu wa kumficha Kenny.Hilo lilifuata baada ya kuona tayari walishakuwa kwenye uhusiano na aliamini ni vema Kenny akamtambua vizuri.Wakiwa katika maongezi yao Mary aliamua kumueleza “Eeh wewe siyo Mary Benson! kwa hiyo wewe ni Mary nani?”Alimiliza Kenny wakati huo walikuwa kwenye fukwe ya bahari ya hindi wakipulizwa na upepo.

    “Mimi naitwa Mary Carlos Mato”Alimjibu Mary akiwa amemgeukia Kenny. “Aaah Mary Car.lo.s Maato…” Aliuliza Kenny akiwa na kigugumizi,alipata mshtuko na kudondosha hata kopo la juisi alilokuwa nalo mkononi.Mary alimueleza tena jina lake hilo,Kenny aliondoka kwa kukimbia eneo hilo la fukwe hata alipoitwa hakugeuka.Hakuamini kitu alichokuwa ameelezwa na Mary alipanda daladala na kuelekea shuleni kwao.Kichwani alijawa na mawazo akiwa haamini alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na adui yake.

    Punde alipofika shuleni kwao aliongoza moja kwa moja katika bweni na kulala katika kitanda chake akiwa na mawazo na kutoelewa vizuri kilichoendelea, akiwa na mawazo hayo anakumbuka siku ya kwanza alipokutana na Mary akiwa na dada yake ambaye alijaribu kumkumbuka bila mafanikio.Aliamka na kwenda kuchukua begi lake na kufunua kasha alitoa bahasha ambayo alikuwa akiwekea picha, katika moja ya picha zilizokuwa katika bahasha hiyo alimuona dada yake Mary yaani Jane akiwa na dada yake marehemu Juliana.Sura ya Jane ilikuwa ni ileile ambayo alikutana nayo akiwa na Mary ingawaje alikuwa mtu mzima tayari.Hapo aliamini kile alichoambiwa na Mary kuwa aliitwa Mary Carlos Mato.

    Hasira zilimpanda na kutoona umuhimu wa uhusiano wake na Mary kilichomshtua ni hisia zake za kuwa huenda Mary alitumwa na baba yake.Mawazo ya kulipiza kisasi yanaanza kumjia akiwaza kuanza na Mary,aliamini angeweza kumuua Mary kirahisi ili iwe taarifa kwa Mr Carlos kuwa kazi ilianza.Siku zote alikuwa akimchukia Mr.Carlos na famila yake na wakati huo alimchukulia Mary akimuona kama Mr.Carlos.



    * * * * *

    Mary akiwa anashangaa jinsi ambavyo Kenny alishtuka kuelezwa yeye alikuwa mtoto wa Mr.Carlos Mato.Jambo alilolifikiria ni uwezo wa baba yake kifedha, alihisi jambo hilo huenda lilimuogopesha Kenny.Alijaribu kumuandikia ujumbe mfupi wa maneno kumuelezea kilichomfanya asimwambie jina lake hilo awali lakini haukujibiwa.Mara kadhaa alimpigia simu Kenny lakini hakupokea zaidi ya kukata.Alijaribu kumfuata shuleni kwao lakini Kenny hakuwa tayari kuonana naye.Mambo hayo yalimuumiza kichwa Mary nakuona alifanya makosa kumueleza Kenny awali juu ya jina lake.

    Kenny alikuwa haingii darasani muda mwingi akiwa bwenini kwake akiwaza ni jinsi gani ataweza kumbaka na hatimaye kumuua Mary.Alitaka kufanya hivyo kama alivyofanyiwa dada yake Juliana.Kuna wakati alihofia maamuzi yake hayo lakini alijipa moyo kuwa angeweza.Kutimiza hilo alimpigia simu Mary akimweleza siku ya jumapili alitaka waende maeneo ya Bagamoyo.Alimweleza alitaka kumjulisha Mary jambo lililomfanya akate mawasiliano naye. Hatua hiyo Mary aliipokea kwa furaha na siku hiyo ilipofika aliwahi kwenda kumchukua Kenny na wakaanza safari kuelekea Bagamoyo.Njiani Kenny alibaki kimya tu, hakuongea hata kidogo na hakuonyesha ucheshi wake alioufanya siku nyingine.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mary alijitahidi kumchekesha na kumsimulia mambo tofauti lakini Kenny alikuwa mbali akiwa na mawazo mengi kichwani.Hatimaye walifika Bagamoyo na Mary alimpeleka Kenny katika hoteli moja ya kitalii.Mara baada ya kutulia na kuagiza vinywaji Kenny alianza kumueleza Mary sababu iliyomfanya ashtushwe baada ya kuelezwa kuwa Mary alikuwa mtoto wa Mr Carlos Mato.Kenny alimweleza kuwa aliogopa kuwa na uhusiano na mtoto wa mtu mwenye fedha kama Mr.Carlos Mato.Sababu ambayo Mary aliielewa kwani ndivyo hivyo ambavyo hata yeye alihisi.Muda wote wakiwa katika hoteli hiyo Kenny alikuwa akitumia pombe kali jambo ambalo lilimshtua Mary. Hakuwahi kumuona akinywa pombe hizo,hakutaka kumueleza lolote akihofia kumtibua tena.Baada ya muda mrefu wa kuwepo Bagamoyo walianza kurudi Dar es salaam,kilometa kadhaa kutoka Bagamoyo Kenny alimwambia Mary asimamishe gari.Baada ya kusimamisha gari Kenny alishuka kwenye gari akimtaka Mary pia ashuke.Mary alikubali akidhani Kenny alitaka kumwambia kitu, mara baada ya kushuka Kenny alimsogelea kama alitaka kumweleza jambo.Baada ya muda mfupi wa kutazamana pasipo Kenny kusema kitu,Mary alishtuka kuona Kenny alikurupuka na kumpiga ngumi ya uso, iliyompasua mdomo wake na damu zilianza kumtoka.

    Mary alikuwa ameanguuka chali baada ya kupata dhoruba hiyo,Kenny ambaye alikuwa amelewa aliikamata miguu ya Mary na kuanza kumvuta akimbuluza kuelekea katika vichaka vilivyo kuwa pembeni kidogo na barabara hiyo.Mary alikuwa akilia kwa sauti kubwa akiwa haelewi kilichoendelea.Baada ya kumbuluza umbali wa mita kadhaa toka barabarani alimwachia Mary na kuanza kumtazama akiwa anatetemeka na mishipa ikiwa imemtoka usoni mwake.Wakati huo Mary alitetemeka na tayari alikuwa amelowa damu nguo zake alizozivaa.

    Baada ya muda mfupi wa kumtazama akivua shati lake na kuanza kumshushia kipigo Mary kila sehemu ya mwili wake. Baada ya dakika kumi Mary alikuwa anavuja damu nyingi na tayari alipoteza fahamu.Kenny alikuwa anatokwa jasho kama maji akiwa anatafakari nini cha kufanya alisikia sauti za watu wakija mbio wakielekea kwenye kichaka alichokuwa.walikuwa wakipiga kelele za kila aina ,akagundua tayari zoezi lake liliuwa limeingia dosari.Alitoka mbio na kuanza kukimbia akielekea vichaka vya mbele zaidi akimucha Mary pale pale.

    Watu wanne wapita njia walishtushwa na kelele za mwanamke akilia kama vile alitendewa unyama.Waliliona gari likiwa limesimama barabarani,waliamua kuanza kukimbia kuelekea katika kichaka ambacho kelele hizo zilitoka.Wakiwa wanaendelea kukimbia kuelekea kwenye kichaka hicho walimshuhudia mtu mmoja akikimbia kutokomea vichaka vya mbele zaidi.Lakini walimuona msichana mmoja akiwa amevuja damu nyingi kunzunguka eneo alilokuwa na hakuwa na fahamu.Waliamua kuachana na mtu aliyekimbia kutokomea vichakani na kuanza kumsaidia msichana huyo aliyeumizwa vibaya.Walimtathimini mtu aliyefanya kitendo kile alikuwa na lengo la kumuua kutokana na vile msichana huyo alivyokuwa ameumia.Wakiwa barabarani wanabahatika kupata gari lililompeleka Mary hospitali ya wilaya ya Bagamoyo. Baada ya taarifa hizo kuwafikia Polisi walifanya uchunguzi wao na kubahatika kuipata namba ya simu ya Mr.Carlos Mato, baba wa msichana aliyopigwa waligundua aliitwa Mary.Walimpigia simu Mr.Carlos Mato na kumweleza kila kitu kilichokuwa kimetokea.Masaa machache baadaye aliwasili katika hospitali hiyo.Mr.Carlos Mato alipandwa na hasira baada ya kumuona mwanaye akiwa na majeraha mengi baada ya kupata kipigo.

    Hakuelewa kilitokea nini mpaka mwanae aliumizwa vile,alikuwa akisubiri azinduke ili aweze kuujua ukweli.Saa tatu na nusu usiku Mary alipata fahamu na kuanza kumueleza Mr.Carlos yale yaliyojiri mpaka wakati huo.Mary alikuwa na hasira na Kenny kutokana na vile alivyompigwa, alimueleza baba yake Mr.Carlos Mato kuwa mtu aliyempiga alimuomba msaada wa kusafiri naye toka Bagamoyo.Mary alieleza kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kenny John alimweleza alikuwa akisoma shule ya Azana.Alitoa maelezo yaliyodhihirisha hakuwa na uhusiano wowote na Kenny John.

    Mr.Carlos Mato alipandwa na hasira hata machozi yalimtoka bila mawasiliano.Alimtaka kamanda wa polisi wa wilaya hiyo kuhakikisha Kenny anakamatwa.Usiku mzima askari wa jeshi la polisi walimtafuta Kenny John pasipo mafanikio ,mpaka siku iliyofuata msako bado uliendelea.Vijana wa Mr.Carlos waliungana na polisi wa Bagamoyo kimyakimya kumsaka Kenny John.Lakini siku hiyo pia ilisha pasipo mafanikio yeyote jambo lililomuongeza hasira Mr.Carlos.Akiwa anamtathimini kijana mdogo Kenny John, jina hilo linampa hisia za kutaka kuujua ukweli zaidi wa mtu huyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kumbukumbu zake zilimkumbusha huenda mtu huyo alikuwa ni mtoto wa John Mushi.Baada ya kukumbuka kwa muda kidogo aligundua hakuwahi kumuua mtoto wa mwisho wa John Mushi.Alichukua simu yake na kuanza kumpigia mwanae Jane aliyekuwa Uingereza kutaka kujua mtoto wa mwisho wa John Mushi aliitwa nani.Alifanya hivyo kwa vile mwanae Jane ndiye alikuwa karibu sana na familia hiyo.Jane alimjibu kwa kumweleza mtoto wa mwisho wa John Mushi aliitwa Kenny.Jambo hilo ndilo lilianza kumumiza kichwa Mr.Carlos akiamini kama Kenny ni mtoto wa John Mushi basi alitaka kulipa kisasi.Hasira zilimpanda akijilaumu kwa nini hakumuua Kenny, kilichomuumiza zaidi ni kwamba siri ya mauaji aliyoyafanya ilikuwa na dalili zote za kuwa imevuja.Aliwasha gari lake na kuondoka kwa kasi kuelekea shule ya sekondari ya Azana mara baada ya kufika katika shule hiyo alitaka kujua maelezo yaliyohusiana na Kenny. Hakupata taabu kupata maelezo yote kutokana na uwezo wake kifedha na hapo ndipo alipogundua aliyempiga mwanae alikuwa ni Kenny John Mushi.Hasira zilimpanda na alitokwa na jasho ndani ya dakika chache tu, aliondoka shuleni hapo bila kuaga jambo lililowashangaza walimu wa shule hiyo.Aliongoza mpaka kwenye nyumba yake ya Mikocheni aliyoitumia katika vikao vya ujambazi na biashara ya dawa za kulevya.

    Aliitisha kikao na vijana kadhaa akitaka kukamatwa kwa Kenny.Tayari aligundua kuwa siri yake ya mauaji ilikuwa imevuja,alitaka Kenny auawe haraka iwezekanavyo ili siri hiyo isimfikie mtu mwingine.Aliwataka vijana saba kufanya doria maeneo ya shule ya Kenny John akiamini angerudi baada ya siku kadhaa.Vijana wake hao walikuwa na picha za Kenny wakifanya doria hiyo ili kuhakikisha wanamkamata.Mr.Carlos hakuwa na amani kabisa kwa vile hakuna taarifa zozote zilizopatikana za kukamatwa kwa Kenny jambo lililomfanya asipate usingizi.

    * * * * *

    Baada ya kutoroka toka eneo alilokuwa anampiga Mary alikimbia kwa kasi kwa masaa kadhaa mpaka katika kijiji cha Fukayosi.Alifika katika nyumba ya babu mmoja na kumuomba msaada wa kukaa kwa siku kadhaa.Kenny moyoni aliumia kwa kipigo alichokua amempiga Mary lakini alijitahidi kupuuzia jambo hilo.Hisia zake za kumpenda alizozijenga kwa muda mrefu ndizo zilizomuibulia mawazo kuwa hakufanya vyema.Alimuonea huruma Mary lakini aliona kipigo kilikua haki yake kutokana na matendo ya mauaji aliyofanya Mr.Carlos ilikuwa haki yake kwani hata familia yake ilifanyiwa hivyo.

    Hakutaka kumkumbuka tena Mary na alijaribu kuziweka hisia zake katika mambo mengine, lakini babu huyo aliyempa elfu kumi aligundua kupigwa kwa Mary kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na kulewa sambamba na hasira alizokuwa nazo Kenny.Tayari alielewa mambo yalishaharibika na shule haikuwa na maana tena.Alichowaza ni kukaa kwa babu aliyemhifadhi kwa siku kadhaa ili arudi shule kuchukua begi lake na kuikimbia Dar es salaam hakujua angeenda wapi,lakini kilichokuwa kichwani mwake alielewa tayari kazi ya kulipa kisasi ilikuwa imeanza.Siku sita alikuwa anashinda ndani ya nyumba ya babu aliyofikia na alikuwa akipanga mipango tofauti.Muda huo pia aliutumia kukumbuka mazoezi ya ngumi aliyokuwa amejifunza kwa miaka kadhaa.Aliamini hakuna jambo ambalo lingemshinda katika kulipa kisasi kwa Mr.Carlos.Siku ya saba alimuaga babu ambaye alikuwa akiishi naye na alianza safari kuelekea jijini Dar es salaam akiwa na kofia na miwani.Vyote hivyo alivitafuta kijijini hapo Fukayoni na vilipoteza muonekano wake wa awali.

    Majira ya saa mbili usiku aliingia shuleni kwao kwa ukimya mkubwa na kuongoza mpaka kwenye bweni lake.Taarifa za haraka alizipata toka kwa rafiki zake zilidai tajiri maarufu Mr.Carlos Mato alifika shuleni hapo kumulizia.Hakupoteza muda zaidi ya kuchukua begi na kuanza kutoka eneo la shule hiyo.Mita kadhaa akiwa ameliacha geti la shule hiyo aliwaona watu watatu wakiwa mbele yake.Walikuwa wamevaa suti nyeusi na miwani rangi nyeusi iliyopoteza muonekano wa sura zao.Alisita kidogo kutokana na muonekano wao,aligeuka nyuma na kuona watu wawili waliovaa vilevile wakiwa nyuma yake.Aligundua tayari palikuwa na shari,akiwaza nini cha kufanya akiwa anatembea taratibu.Alisikia mmoja wa watu hao waliokuwa mbele akisema “simama hapohapo kwa usalama wako”Alitii amri na kusimama akatupa begi lake pembeni kidogo,tayari alielewa kazi ilkuwa imeanza.Alianza kukunja shati lake mkono wa kushoto na mara baada ya kumaliza alikunja na mkono wa kulia.Wakati akifanya hayo watu hao walitabasamu wengine walicheka “kijana unataka kutupiga?”Aliuliza mmoja wao huku akinyosha mikono yake, aliwakonyeza wenzake na kuwataka watulie alimsogelea Kenny na walianza kupigana kwa kasi ya ajabu.Baada ya dakika kadhaa yule aliyeanzaa kupigana na Kenny tayari alikuwa amepasuliwa paji lake la uso na damu nyingi zilimtoka.Kenny alikuwa salama kabisa na hakuumizwa hata kidogo.Alifanikiwa kumpiga mtu huyo baada ya kumpiga ngumi kadhaa zilimpata vizuri usoni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati mtu huyo damu zikiendelea kumtoka alingia mwingijne na kuendeleza kupigana.Kenny aliendelea kujipanga sawasawa na kukwepa mateke na ngumi vilivyo rushwa na adui yake huyo.Dakika tano baadaye mtu huyo wa pili naye alianza kuumizwa jambo hilo liliwapa hofu wenzie ambao waliamua kutumia njia nyingine.Wakati Kenny akiendelea kupigana na mtu huyo aliyetambua alikuwa ni kijana wa Mr.Carlos Mato alishtushwa akipigwa kichwani na kitu kizito.Alianguka chini na baada ya muda mfupi alipoteza fahamu.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog