Search This Blog

Monday, October 24, 2022

RIGWARIDE LA AFANDE - 5

 





    Chombezo : Rigwaride La Afande

    Sehemu Ya Tano (5)



    “Bwana mimi naogopa peke yangu.”



    “Hivi husikii wewe. Unadhani nani atakuja kujibanza hapa kwa maafande, hajipendi?”



    Nikatoka hadi chooni. Ile nageuza kurudi ndani, yule afande mbaba naye anatoka kwake, akanishika mkono…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    TAMBAA NAYO MWENYEWE…



    “Wewe binti utakula jeuri yako. Nimesikia habari zako zote…kwa nini umefanya hivi lakini? Kama si mimi ungemjua afande Mwita wewe?”



    “Bwana niache,” nilimwambia kwa sauti ya chini lakini yenye hasira…



    “Sikuachi, wewe ni wangu, nikuachie nini sasa? twende kwangu…”



    “Ha! Sitaki bwana.”



    Alinishika kwa mabavu na kuniingiza chumbani kwake, akanikalisha kitandani…



    “Kaa hapa!” aliniambia kwa ukali kidogo, nikakaa!



    “Lakini sasa kule kwa afande Mwita kuna nguo zangu,” nilimwambia…



    “Kachukue urudi hapa. Tena angalia asiamke. Wewe unaacha kuja kwetu wenye pesa unahangaika na afande mwenye mkopo kazini, atapata wapi pesa?” alisema yule afande mbaba.



    Nilijikuta nasimama, nikatoka…



    “Basi usifunge mlango,” nilimwambia. Moyoni niliamini niko sahihi kwa vile, afande huyo ndiye wa kwanza kuniona mimi, wengine ndiyo wakanitamani.



    Yeye ndiye niliyekutana naye maeneo ya hospitali akiwa amekaa kwa msafisha viatu.



    Basi, niliingia chumbani kwa afande Mwita, nikaweka shuka kitandani, nikavaa nguo zangu na kutoka polepole nikifunga mlango kwa machale sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliingia chumbani kwa afande yule mbaba. Chumba kilikuwa kimepoa. Afande alikaa kitandani akinisubiria kwa hamu kweli. Nilipoingia tu, akasimama na kwenda kufunga mlango na funguo, kachakacha, akanirudia na kunipandisha kitandani…



    “Hapo sawa…hapo sawa,” alisema afande huyo kwa sauti iliyojaa uchu wa hali ya juu.



    Tulikuwa wote kitandani sasa, joto la Dar usipime. Mlio wa feni ulitikisa chumba kizima…ziii…ziii!



    Mara kwa mbali tukasikia mlango wa chumba kimoja wapo mle ndani ukifunguliwa…



    “Afande Mwita huyo. Huo ndiyo mlango wake unavyolia,” alisema afande huyu mbaba.



    “Haa! Atakuwa ananitafuta. Si ataingia kila chumba?” nilimuuliza…



    “Hapana, ulipotoka kwenda kuchukua nguo zake na mimi nilitoka kwenda kufungua mlango wa uani nikauacha wazi…”



    “Ili..?” nilimuuliza kwa kushangaa…



    “Ili akitoka na kuukuta uko wazi ajue umeondoka zako.”



    Niliachia tabasamu la kitandani. Niliamini kweli ni mbinu ya hali ya juu. Moyoni nikamsifu kwa ujanja huo.



    Afande alitoka kitandani na kwenda kuzima feni haraka kisha akarudi…



    “Huyu binti mjinga sana…inaonekana ni malaya tu… sasa anavyotoroka saa hizi akiuawa je? Mama yake si atanila nyama. Nikimkamata atanijua mimi ni nani?” tulimsikia afande Mwita akisema kwa kulalamika.



    Tukacheka ndani kwa ndani, afande akanikumbatia na kunipa busu moja tu, zito!



    Mara tukasikia mlango wa uani ukifungwa, mara tukasikia mlango wa chumbani kwa afande ukifungwa. Tukajua ameingia ndani kulala. Amesalimu amri…



    “Lakini asubuhi nitatokaje mimi?” niliuliza.



    “Nitajua mimi, wewe tulia.”



    Kweli nilitulia. Afande akanishika na kunivutia kwake. Tukawa beneti, ziro distensi. Nikajua anataka nini. Mwee! Nilichoka lakini basi tu…



    “Si tungelala kwanza baby,” nilimwomba…



    “Wee! Utakula jeuri yako. Hapa hakuna kulala.”



    “Plizi mpenzi wangu, kama hautajali naomba nilale kidogo ndipo nitakuwa huru kwa chchote utakachohitaji kutoka kwangu,” nilizidi kumwomba.



    “Nasema hivi, utakula jeuri yako hapa hakuna kulala,” alisisitiza huku akiniangalia kwa macho ya uchu wa mapenzi.



    Nilijua hata nikibisha vipi, hata nikiomba msamaha vipi, afande asingekubali. Lazima angetaka mpira uchezwe.



    Na hii yote ilichangiwa na umbo langu kwani kwa mwanaume yeyote rijali, akiniona tu nilivyo hawezi kulala hata kama angetoka muda huohuo kucheza soka.



    “Haya baba nakusikiliza,” nilimwambia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wewe utakula jeuri yako, mimi siyo baba yako,” aliniambia na kunivutia mwilini mwake.



    Sikuwa na la kufanya zaidi ya kujiachia kwa mbaba huyo mjeshi huku nafsi yangu ikiwa mbali kabisa na jambo alilotaka tulifanye kwani muda mfupi nilitoka kuchezeshwa ligwaride na afande Mwita tena kwa staili ya kusimama.



    Basi, kwa tabutabu hivyo tuliingia uwanjani. Ushirikiano haukuwa wa kutosha kwangu, ila afande yeye alijitutumua mwenyewe mpaka mwishomwisho wakati anatangaza nia ndiyo na mimi nikapata nguvu ya kumsaidia kufika safari yake!!



    Baada ya hapo tulilala zetu. Usingizi wenyewe kwangu ulikuwa wa maruweruwe.



    Hali hiyo ilitokana na hofu niliyokuwanayo kufuatia kuwachanganya maafande wale kwa nyakati tofauti na kwenye jengo moja.



    Niliwaza itakuwa vipi kama atafika saa kumi na mbili na kuambiwa na afande Mwita kwamba mimi nilitoroka usiku.



    ***



    Nilikuja kushtuka kwenye saa kumi baada ya kuangalia saa ya kwenye simu yangu. Nikajisikia kwenda haja ndogo, nikamwamsha afande huyu mbaba…



    “Nataka kwenda chooni.”



    “Si unakujua?” aliniuliza.



    “Ndiyo…”



    “Nenda tu, mimi nakulinda.”



    “Unanilinda wakati uko ndani?” nilimwuliza.



    “Wewe nenda tu, usiwe na wasiwasi.



    Nilitoka kitandani. Huyu bwana hakuwa na shuka, alikuwa akitumia blanketi. Na kwa joto la Dar blanketi hilo lilikuwa tu pembeni kwa kitanda limetulia.



    Kwa hiyo ili kwenda chooni ikabidi nivae nguo zangu ndiyo nitoke. Nilivaa zote bwana!



    Nikaenda chooni. Wakati natoka, afande alikuwa macho,  tena aliwasha taa kwa kutumia swichi ya kitandani, wenyewe mnaiita bed nini sijui..! nadhani ni bedi swichi!



    Nikiwa chooni, nikasikia miguu ikitembea kuja usawa huo nikajua ni afande mbaba ameamua kunifuatulia.



    Mara nikasikia ikiingia bafuni, nikasikia kukohoa. Mkohowo huo ulitaka kufanana na wa afande Mwira. Nikatulia kimya na kufuatilia ili nijue ni nani!



    “Ee nivumiliee…nakupenda sana wewe…hata moyo wangu eee…” aliimba na ndipo nikajua ni nani sasa…



    “Mh!” niliguna. Moyo ukaanza kwenda mbio. Nilijua nimeumbuka…



    Ilipita kama sekunde kadhaa, nikasikia maji yakimwagika, mtu akiwa anaoga.

    Nikajua mtu huyo hawezi kutoka muda huo, nikatoka mbio hadi chumbani kwa yule afande mbaba, nikamkuta amesimama eti alitaka kunifuatilia chooni maana nilichukua muda mrefu.



    Kulipokucha, baadhi ya maafande walishaondoka kwenda kazini, lakini afande Mwita alibaki. Afande yule mbaba pia alibaki.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa moja juu ya alama, afande Mwita akaja kumgongea afande wangu mbaba…

    “Mura,” aliita afande Mwita. Sijui mura maana yake nini!!

    Jamaa naye huku chumbani akaitika kwa kusema neno hilohilo.

    “Upo?” aliuliza afande Mwita…



    “Nipo mura…vipi, hujuenda kazini leo?”

    “Bwana nina msala…”

    “Msala gani tena?”



    Afande Mwita akamsimulia mwenzake kuhusu kisanga chake chote…

    “Mura…hivi ninavyokwambia sasa hivi hapa nawaza. Je, mama yake akija sasa hivi itakuaje? Nitamwambia binti yake yuko wapi?”



    “Daa! Mura hapo kweli umeshikwa pabaya. Ni kuomba Mungu, maana isijekuwa alipotoroka amekumbana na majambazi ameuawa, itakula kwako mura.”

    Walipitisha ukimya kila mmoja akitafakari, mimi nikashikwa na hali ya kutaka kupiga chafya! Ilibidi nijizuie kwa nguvu zangu zote mpaka nikachukua shuka na kulitumbukiza kinywani ili tu nisipige chafya. Nikafanikiwa.



    Baadaye afande Mwita alirudi chumbani kwake, afande wangu mbaba naye alirudi kitandani akiwa anafunga mlango…

    “Da! Jamaaa anasumbuka sana. Angejua upo ndani kwangu sijui ingekuwaje? Angenifyatua na risasi,” alisema afande wangu.



    Mimi niliachia tabasamu tu kwani dhamira ilinisumbua kuona mtu hakulala kisa mimi na kumbe nipo sehemu ya usalama kabisa…

    “Sasa mimi nitatokaje?” nilimuuliza afande wangu kutaka kujua…



    “Ala! Sasa uondoke kwenda wapi mpenzi wangu? Hapa umefika! Mimi nikienda kazini nakufungia ndani mpaka nitakaporudi. Yaani wewe na mimi ndiyo tumeshakuwa mke na mume tayari.”



    Niliogopa kusikia hivyo kwani nilijua mazingira yatakuwa magumu sana. yaani nikae chumbani mchana kutwa au usiku mwingine nikimsubiri yeye, ngumu sana!

    ***

    Nyumba ilikuwa kimya sana, afande Mwita aliondoka na afande wangu pia aliondoka. Yeye afande wangu aliondoka baada ya kupika ubwabwa na nyama akaniachia, eti nikijisikia njaa nile.



    Nilikuwa nimepitiwa na usingizi wa asubuhi baada ya ule wa usiku kuamkia asubuhi. Nadhani mnaujua. Yaani watu wakiamka asubuhi, baadaye kama watakuwa bado kitandani lazima wapitiwe na kausingizi kengine ka mwishomwisho!

    Nilishtuliwa na mlango mkubwa kugongwa…



    “Ngo ngo ngo…hodi!” Ilikuwa sauti ya kiume, nikajua siyo mama. Awali nilijua ni mama amenijihimia.



    Sikuamka, niliendelea kumsikiliza lakini ikafika mahali hodi hiyo ikawa ni kero sasa. nikatoka kitandani, nikafungua mlango na kwenda hadi mlango mkubwa lakini nilikwenda kwa kunyata ili kuchunguza kwanza…



    “Ngo ngo wenyewe hodi humu ndani,” ile sauti iliendelea kuita baada ya kugonga.

    Nilipata upenyo na kuangalia nje kupitia nafasi ya mlango, kipande cha mbao na kipande kingine. Niliwaona wanaume wawili wamesimama.



    Nilisonya, nikarudi zangu ndani, chumbani, nikapanda kitandani kulala. Sikumbuki waliondoka muda gani, lakini nilishtuka mimi saa sita na nusu baada ya simu yangu kuita sana. Nilitoka kitandani na kuifuata ilipo. Alikuwa afande wangu, mbaba maana si nilimsevu siku ya kwanza kabisa…



    “Haloo…”

    “Dear hujambo?” alinisalimia…

    “Sijambo, mzima wewe?”

    “Mimi mzima, umeshaamka wewe?”

    “Khaa! Sasa ningekuwa sijaamka, ningepokea simu? Si ningekuwa bado usingizini,” nilimuuliza…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kumbe wewe jeuri ee? Basi kuna siku utakula jeuri yako, mimi nipo kazini, take care hapo nyumbani, nimegundua umebaki peke yako,” aliniambia kwa sauti yenye amri…

    Wakati tunaongea, nikasikia mlango wa uani ukifunguliwa, nikakata simu haraka sana bila kumwambia kwa nini nakata simu.



    Nikatoka kitandani, nikatembea hadi mlango wa chumbani, nikatulia hapo kimya kabisa! Aliyefungua mlango nikasikia anaufunga, kwarakachakwarakacha.

    Nikaogopa, sikujua ni jambazi au mtu wa aina gani! Mara nikasikia mlio wa viatu kutembea…ko…ko…ko! Nilitetemeka.



    Nilipata tabu sana kumwambia inatosha maana kila nilipojaribu kusema, hakuwa ametoa ulimi wake kinywani mwangu, nikabaki namsukuma lakini wapi! Alining’ang’ania mpaka nikajikuta naishiwa nguvu na kulegea…

    SASA ENDELEA…



    “Twende chumbani basi,” akaniambia…”

    Aliponieleza hivyo nikabaki nikimwangalia kwa kumlegezea macho, kwa kuhofia kufumwa na afande Marwa na Mwita nilishindwa kumkubalia au kukataa.



    “Mbona unaniangalia ina maana hujanisikia?” aliniuliza.

    “Mimi kwenda ndani na wewe sitaweza kufanya hivyo…”

    “Kwa nini?” aliniuliza.



    Nilimweleza kwamba ikitokea wenzake wamerudi ghafla itakuwa balaa kwani wanaweza kunijeruhi kwa kipigo kama siyo kuniua kabisa.

    Nilipotoa kauli hiyo, alicheka na kuniambia kumbe nilikuwa muoga, sasa kama sikutaka kuingia ndani atatoa siri yangu.



    Aliponiambia hivyo, moyo ulipiga paa kwani nilielewa hatari iliyokuwa mbele yangu kama angemwambia afande Mwita kwamba niliingia chumbani kwa afande Marwa lingekuwa bonge la msala.



    “Bado unaendelea na msimamo wa kutotaka kuingia ndani, kwanza hatuendi kukaa muda mrefu sijui unaogoa nini binti mzuri,” aliniambia.

    Aliponisifia kwamba nilikuwa binti mzuri, japo moyoni sikuwa tayari kufanya naye mapenzi nilifurahi na kuachia tabasamu.



    Moja kwa moja alipoona nimetabasamu akajua nilikubaliana naye akanishika mkono na kuniongoza chumbani kwake kama vile nilikuwa mkewe.

    Tulipofika hakunipa nafasi, akakivamia kifua changu na kuanza kukishika na kuhamia maeneo mengi aliyopendezwa nayo.



    Licha ya pale mlangoni kula denda lililonifanya niishiwe nguvu na kulegea, jamaa huyo ambaye kwa muda mfupi niliokuwa naye nilibaini alikuwa akipenda sana kula denda, akanivutia maungoni mwake, akatoa ulimi na kuuelekeza kinywani mwangu.

    Alipofanya hivyo, niliudaka na kinywa changu, akaanza kuuchezesha huku akiuvuta na kuung’ata kimtindo ulimi wangu mwili ukanisisimka.



    Pamoja na utundu alionifanyia, moyo wangu haukuwa radhi kubilingika na jamaa huyo ambaye hakunivutia kama ilivyokuwa kwa maafande wenzake akina Mwita.

    Aliporidhika kwa denda, alinivutia kitandani ambapo aliniomba nivue nguo ili tuingie katika awamu ya mwisho lakini nilimkatalia kwamba sikujisikia vizuri.



    “Wewe binti unajua sikuelewi hata kidogo,” aliniambia.

    Nilimweleza kwamba ni kweli sikujisikia vizuri na kumpa ahadi kwa kuwa bado nitakuwepo pale asijali nikiwa vizuri nitampa penzi ambalo hakuwahi kulipata tangu alipoanza mapenzi.



    Kauli yangu ilimchekesha na kunieleza niache kumtania kwani kwa umri wake alikuwa amekutana na wanawake mbalimbali waliojua mapenzi.



    “Sijakataa lakini siku hiyo ndiyo utaamini maneno yangu wewe kuwa mvumilivu, si unaelewa kwamba siku zote mvumilivu hula mbivu?”

    “Huo msemo umeshapitwa na wakati, tafadhali naomba japo mara moja, hivi huwezi kujua kama hapa nilipo nipo katika wakati mgumu sana binti mzuri?”



    “Si wewe pekee uko katika hali hiyo, mimi mwenyewe nipo kwenye mateso lakini hali yangu hainiruhusu kwa leo,” nilimwambia.

    “Unaumwa nini kwani?” aliniuliza.



    “Jamani wewe, hivi kwa nini huniamini ninapokwambia siko vizuri, matatizo mengine ni ya sisi wanawake,” nilimwambia.



    Nilipomweleza maneno hayo, nilimuona akiwa mpole kisha akaniuliza nilitarajia kuwepo pale kwa muda gani, nikamwambia pale yangekuwa makazi yangu ya kudumu.

    “Kwa hiyo Mwita ndiyo kaamua kukuchukua jumla uwe mke wake?” akaniuliza.

    “Yeye ndiyo kasema hivyo, sijui sasa kama atabadilika lakini kwa upande wangu naelewa nitakuwa hapa kwa muda mrefu,” nilimwambia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Haya lakini umenikatili sana wewe mtoto, leo nilitaka kufurahi na wewe na wewe ufurahi na mimi,” aliniambia.



    Kwa kuhofia kukutwa na afande Mwita, nilimuomba aniruhusu niondoke ombi ambalo hakulipinga zaidi ya kusisitiza kwamba nitakupojisikia vizuri nimfahamishe kumpa asante yake ya kunifichia siri.



    “Usijali kwa hilo,” nilimjibu kisha nilitoka mle chumbani kwake na kwenda chumbani kwa Mwita.



    “Mh! Hawa maafande sasa wataka kunigeuza chombo chao cha starehe maana kila kunapokucha anaibuka mwingine na kunitaka, huyu ningemlegezea naye angenitafuna,” Rhoda alijisemea moyoni akiwa ameketi katika kitanda cha afande Mwita.



    Wakati Rhoda akiwaza hivyo, yule afande aliyemkosa alilaani sana kitendo cha Rhoda kutojisikia vizuri na kujipa imani kwamba zisingepita siku mbili lazima angempata.



    Rhoda akiwa anatafakari vitendo vichafu alivyokuwa akifanya na maafande wale, akasikia sauti ya mwanamke aliyekuwa akizungumza kama mama yake akisalimiana na mtu nje.



    “Mh! Huyu mbona ana sauti kama ya mama, au atakuwa yeye!” aliwaza.

    “Humo ndani hakuna mtu wenyewe wamekwenda kazini na leo watachelewa kurudi,” yule afande aliyetaka kutoka kimapenzi na Rhoda alimfahamisha mwanamke huyo.



    Mimi nilibaini ni mama haraka sana, nikashtuka!

    “Nimekuja kumfuata mwanangu, yupo humu ndani?” mama alimuuliza yule afande.

    “Yule binti mzuri, mfupi hajasuka nywele?” yule afande ambaye hakumfahamu mama alimuuliza. Mimi moyoni nikawa nasema we afande, mbona unajiweka kimbelembele sana, una nini lakini?



    “Ndiyo huyohuyo!” mama alijibu.

    “Yupo ndani na dakika chache nilikuwa nazungumza naye, wewe ingia hapo ndani kisha bisha hodi kwenye mlango wa kulia kwako,” yule afande alimwambia mama.

    Kila kitu kikawa wazi sasa.



    Wakati mama Rhoda anatembea kuelekea alikoelekezwa, yule afande akamwomba samahani, aliposimama akamwuliza kama ni kweli mimi nilikuwa mwanaye wa damu.

    “Ni binti yangu kabisa, leo nimemfuata nataka arudi nyumbani. Binti ni malaya sana huyu, ananitia aibu kubwa. Mimi mama yake sikuwahi kuwa hivi,” mama alifoka.

    “Kwa hiyo mama unataka kuondoka naye au?” aliuliza afande.



    “Si mwanangu,” alisema mama kwa sauti ya kuwaka akimaanisha swali la afande lilikuwa la hovyo.“Da! Mimi nilizungumza naye kitu fulani mama. Sasa kama unaondoka naye, basi ungeniacha nimalize naye mazungumzo,” alisema yule afande mpaka mimi nikahisi hana akili nzuri kichwani…



    “Yanahusu nini?” mama alimuuliza akiwa anagonga mlango wa chumba nilichokuwemo…

    “We malaya,” mama aliniita kwa jina hilo.



    Niliumia sana moyoni. Mama yangu mzazi kuniita mimi malaya.

    “Abee,” niliitika kwa nidhamu ya hali ya juu.

    Nilikwenda kufungua mlango huku moyoni nikiwa namlaani sana yule afande kwa kumwambia mama kwamba nilikuwemo ndani.



    Nilipofungua tu mlango, nilikutana na uso wa mama. Alinishika mkono na kunitoa kwa nguvu kwenye chumba hicho…

    “Leo ndiyo utajua mimi ni nani?” alisema.



    Nilimsihi mama aniache nizirudie sendozi zangu lakini alikataa, nikawa natembea pekupeku.

    Yule afande alitoa kichwa chumbani kwake kutuangalia. Akatingisha kichwa…

    “Mama ungemwacha afunge basi japo mlango wa watu,” alisema yule afande…

    “Kwani na nyie mnaibiwaga!?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sasa kazi ilikuwa ni kuikata mitaa, kutoka upande wa Hospitali ya Temeke, kuvuka barabara na kuingia upande wa pili kuelekea Mtaa wa Wailes ambako ndiko nyumbani.

    Mama kama kawaida yake, wakati akinikokota, mimi nilikuwa kwa nyuma, yeye mbele ila mkono wangu wa kulia ndiyo ulikuwa mkononi mwake. Vuta picha hapo nilikuaje?!

    Watu njiani walikuwa wakinicheka, wengine walinijua wakasema…



    “Rhoda leo vipi! Polisi nini? Pole wa kwetu.”

    Sikuwa na muda wa kuwajibu si kwa kupuuza bali kwa kasi ya kupelekeshwa.

    Sikujua ni kwa nini kama mama alishindwa kujua kwamba aibu ninayoipata hata yeye inamhusu. Maana kama mimi ni malaya, yeye anahusika kwa sababu si ndiyo mlezi wangu!



    Kufika mtaani sasa, ndiyo usiseme. Wasichana wenzangu walitoka majumbani kwa kuitana kiumbeya…

    “Jamani Rhoda kakamatwa na mama yake, alilala kwa mwanaume,” alisema binti mmoja anaitwa Pashuu.



    Mama aliniingiza ndani, chumbani kwangu, akaniweka kitandani…

    “Vua nguo nakwambia,” alisema kwa ukali mama.

    Moyoni nilishangaa sana mama kuniambia nivue nguo kwani nilijua anajua mimi nilikuwa kwa mwanaume maana aliniacha mwenyewe, japo ni kwa wanaume, sasa alitaka nivue nguo ili iweje?



    “Sasa mama nikivua nguo halafu…”

    “Weee! Paka shume we,” mama alikuja juu.

    Ilibidi nivue ili nisubiri hatua nyingine kutoka kwake. Nilipomaliza nikabaki nimemtumbulia macho kumwangalia tu…

    “Enhe! Ulilala naye?”



    “Nani mama?”

    “Pumba** kwani nilikuacha kwa nani?” mama aliniuliza huku akinipiga…

    “Ndiyo mama.”

    “Yupi?”



    “Mhh!” Swali hilo la mama lilinifanya nigune kwanza. Yupi kivipi wakati anajua aliniacha kwa nani!

    “Sijakuelewa mama.”

    “Hujanielewa nini? Wewe si ulikuwa chumba cha kushoto? Mbona leo umetokea chumba cha kulia?”



    Moyo ulifanya paa! Nikaamini kwamba, kweli mzazi ni mzazi tu, huwezi kumdanganya! Kumbe mama alijua niliingia chumba cha kushoto na amenikuta chumba cha kulia…

    “Alihamia kule.”



    “Wewe, siyo kwamba umewachanganya? Nakujua mwanangu Rhoda.”

    “Hapana mama alihamia kule. Lakini ni yuleyule.”

    Mama aliniacha, akaniambia ni marufuku kuanzia siku hiyo kutoka hata kufika kibaraza cha nyumbani. Akasema nikija kuvunja amri yake hiyo nitakiona cha moto!

    ***

    Saa tisa usiku siku hiyo, nikiwa chumbani kwangu nimelala, simu yangu iliita, kuangalia hivi ni afande Mwita anapiga, sikupokea.



    Alipiga kama mara saba, alipoacha ikaingia simu ya afande Chacha, nayo iliita weee, sikupokea. Ikaja simu ya afande Mwira, nayo ikaitaa weee sikupokea! Nikaanza kuogopa sasa.



    “We Rhoda, hiyo simu inatoka wapi usiku huu?” mama aliniuliza kutokea chumbani kwake…

    “Siijui namba mama, labda amekosea.”



    Nilichofanya, niliamua kuizima simu. Lakini kabla sijafanya hivyo, meseji iliingia. Ilitoka kwa afande Chacha, yaani yule wa kwanza kabisa mbaba, aliandika…

    “Utakula jeuri yako.”

    “Poa,” nilimjibu, ndiyo nikazima simu.



    Nilipata tabu kuupata usingizi maana muda mwingi nilikuwa najifikiria ni kwa nini walinipigia simu wote? Ina maana wako pamoja? Kivipi?



    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwezi mmoja ulikatika bila kupata mawasiliano kutoka kwa yeyote kati yao. Lakini siku hiyo niliamka ninaumwa. Afya haikuwa njema. Nilipokuwa najisaidia, nilisikia maumivu makali sana, halafu sehemu ya chini ya tumbo ikawa inauma pia…

    “Mama,” nilimwita…



    “Nini?” mama aliniitikia kindava. Eti nini!

    “Naumwa mama…tumbo linaniuma, hapa chini linauma sana,” nilimwambia mama baada ya kuja.

    “Ni kwa sababu gani?”

    “Sijui mama,” nilisema nikijishika tumbo kwa maumivu…

    “Lakini wakati nimekwenda chooni nilihisi haja ndogo yangu ina rangi ya maziwa,” nilimwambia mama…

    “Hee! Twende hospitali haraka sana. Jiandae,” alisema mama na kunipa hofu kwani niliamini mshtuko wake una jambo alilolijua.

    Nilijiandaa harakaharaka, nikamwambia mama, tukaondoka hadi Hospitali ya Temeke. Mimi wasiwasi wangu mkubwa nimenasa ujauzito. Nikawa najiuliza kama ni kweli ni wa nani sasa..?

    “Itakuwa Afande Mwira? Mh! Sidhani, labda afande Mwita…lakini yule siyo, ila itakuwa afande Chacha yule mbaba.”

    Niliwaza mengi mpaka ikafika mahali nikawa nasubiria niingie kwa dokta na kuambiwa maelekezo.

    Daktari alikuwa amekaa kwenye kiti chake miwani usoni wakati mama akimsimuliza matatizo yangu, ninavyojisikia.

    Vipimo vilichukuliwa kwa kuambiwa nikajisaidie haja ndogo. Nilipomaliza, nikawapa kikopo kisha tukaambiwa tukae nje. Mama hakuonekana mwenye raha sana. Kila mara aliniangalia kwa kuibia.

    “Rhoda…” aliita daktari kabla hata hajamalizia jina la baba, nikawa nimeitika, tukaenda na mama…

    “Karibuni sana,” alisema daktari…

    “Eee…kipimo tayari…eee! Kipimo chetu kinaonesha Rhoda umeambukizwa ugonjwa wa zinaa.”

    Palepale mama aliangua kilio, mimi nikafuatia…

    “Sasa hapa…sasa hapa si mahali pa kumalizia vilio vyetu. Tunaruhusu kulia kwa mtu aliyefiwa tu. Haya ni matatizo ya kujitakia, msinipigie kelele,” alisema yule daktari huku akiniandikia dawa…

    “Itabidi uchome sindano za PPF tatu kwa siku tatu na utumie dawa inayoitwa Azithromycin. Fuata maelekezo tafadhali,” alisema dokta huku akiniangalia kwa macho makavu.

    Tulitoka na mama tukiwa tumeinamisha vichwa chini. Nilijiuliza kisa cha mama kulia ni nini! Nilitarajia baada ya maelezo ya daktari palepale angenishika masikio yangu na kuyang’ata lakini sivyo…

    “Mwanangu Rhoda nisamehe mimi…nisamehe sana mwanangu. Mimi ndiyo sababu ya wewe kuupata huo ugonjwa, nisingekuacha naamini yasingekukuta,” alisema mama mpaka nikamshangaa…

    “Usijali mama…Mungu atanisaidia mama. Nitapona tu,” nilimwambia mama…

    “Sawa mwanangu, lakini lazima twende kwa yule askari tukamwambie, lazima atoe pesa za kukutibu. Leo atanitambua mimi ni nani!” mama alikuja juu.

    Nilimkubalia mama kwenda kwa wale maafande lakini yeye akijua ni afande mmoja tu. Moyoni nilisema hata kama nitakwenda kuumbuka lakini yote aliyataka mama na ameshakiri mwenyewe.

    Tulikata mitaa, tukachanja uchochoro mpaka tukatokea kwenye ile nyumba na kuwakuta wanawake wawili nje, mmoja akichagua mchele. Kwanza nilishtuka sana, nikajua wale wanawake ni wake wa wale maafande. Nilitaka kumwambia mama lakini hakuonesha dalili ya kunisikiliza…

    “Hodi hapa,” alisema mama akiwa amenishika mkono…

    “Karibuni,” tulipokelewa…CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tunamuulizia askari mmoja anaitwa…eti wewe anaitwa nani yule askari wako?” mama alisema, akaniuliza mimi.

    Kutaja jina nilishindwa, nilijua kama ana mke kati ya wale, itakuaje sasa! Si nitakula kichapo?! Nikakaa kimya!

    “Wewe si nakuuliza?” mama alinijia juu…

    “Anaitwa afande Mwira,” niliamua kumtaja yule wa kwanza kabisa.

    Wale wanawake waliangaliana, kisha mmoja akasema…

    “Hapa wamekuja askari wapya! Wale wa zamani wote wamehamishwa! Si mnajua polisi hawakai sehemu moja kwa muda mrefu!”

    Nilimwangalia mama, naye akaniangalia mimi…

    “Kwa hiyo na nyinyi ni maaskari?” aliuliza mama…

    “Hapana, sisi ni wake zao.”

    Mama alinishika mkono tukageuza kuondoka…

    “Kwani kuna nini mama?”

    “Ah! Basi! Mungu atatulipia,” alisema mama tukiwa tunakata kona kuingia kwenye uchochoro.

    Tulifika nyumbani na kukaa kwenye mkeka, mama alilia na mimi nililia. Mimi nililia kwa sababu niliamini niko kwenye starehe kwa sababu ya ujana wangu na uzuri lakini kumbe nachuma janga sasa nakula na wa nyumbani.

    Nilijuta kuutumia mwili wangu vibaya. Nilijuta kutotumia akili yangu kujiongeza kwamba, natakiwa kutulia. Kama ni boifrendi nilikuwa naye, sasa kwa nini nilizama kwenye mapenzi ya mchanyato!

    “Rhoda,” aliniita mama…

    “Abee mama.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tulia mwanangu, utapona na Mungu atakusaidia.”

    “Natulia mama. Nakuahidi kuanzia leo, tena kuanzia sasa, mimi nimetulia mama.”

    Mama alinifuata, akanikumbatia, tukakumbatiana!



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog