Search This Blog

Monday, October 24, 2022

JAMANI DADA MARTHA... LOOO! - 1

 





    IMEANDIKWA NA : 2JIACHIE



    *********************************************************************************



    Chombezo : Jamani Dada Martha... Looo!

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    “Wewe una hoja Martha, kumbe unajua chakula kizuri...nikuambie kitu mke wangu.”

    Martha alipoisoma meseji hiyo, akaguna kwanza, akamjibu”

    “Mh! Nimekuwa mkea mara hii jamani?”

    “Kwani umeboreka kukuita hivyo?”

    JIACHIE MWENYEWE SASA…

    Martha hakujibu haraka, Roi akawa na presha kubwa ya kutaka kuiona meseji iliyofuatia msichana huyo angejibu nini...

    “Si vibaya ila....”

    “Ila nini tena?”

    “Basi tuyaache kwanza.”

    “Sawa, nahitaji nikuone leo jamani,” aliandika Roi.

    “Leo?”

    “Ndiyo! Mbona umeshtuka hivyo mke wangu?”

    “Kwa leo hapana.”

    “Mpaka lini?”

    “Labda siku nyingine.”

    “Ndiyo nataka kuijua hiyo siku nyingine.

    “Ila si nimekwambia nitakwambia jamani!”

    “Basi sawa, hakuna tatizo.”

    Katika kila hatua aliyokuwa akipiga, Roi alijiona kuwa mshindi, uzuri wa Martha ulikichanganya kichwa chake mpaka kufikia hatua ya kumuona mjinga mwanaume aliyezaa naye na kisha kuuacha mzigo mzuri kama ule ukiondoka zake...

    Siku hiyo alifanya kazi harakaharaka, kitu pekee alichokuwa akikihitaji ni kutaka kuzungumza na msichana huyo tu. Alipomaliza kazi zake, akaondoka. Ilipofika usiku kama kawaida yake akachukua simu yake na kumtumia meseji.

    “Jamaniiiiiii....” alianza kumchokoza...

    “Nini tena kababaaaa?”

    “Hata kunikumbuka!”

    “Nilikuwa bize kidogo.”

    “Naomba nikupigie basi niisikie sauti yako.”

    “Nipo kwenye kelele, nitakushtua.”

    “Sawa.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roi akabaki akiwa na presha kubwa, kila wakati alipokuwa akimkumbuka Martha, mwili wake ulikuwa unamsisimka kupita kawaida. Hakujua kama alikuwa amempenda mwanamke huyo au alimtamani, lakini kila wakati alihisi kuwa na hamu ya kutaka kuwasiliana naye....

    Alisubiri meseji ya Martha mpaka zilipopita dakika thelathini, akasikia mlio wa meseji, kwa haraka sana huku akiwa na presha tena akikenua meno yake akaiwahi simu, akaichukua na kufungua meseji. Hakuwa Martha, alikuwa rafiki yake Sudi ambaye alimshtua kwenda kuchukua hela yake aliyokuwa akimdai....

    “Mjinga kweli huyu mtu, watu tupo kwenye presha, yeye anatushtua tu, na hiyo hela abaki nayo,” alisema Roi kwa hasira na kumalizia na msonyo mkubwa. Baada ya hapo, wala hazikupita dakika nyingi, Martha huyo simuni....

    “Nipigie sasa,” ilisema meseji aliyotuma Martha.

    Roi hakutaka kupoteza muda, alijiona kama angechelewa vile, kwa haraka sana akaanza kumpigia Martha simu, ikapokelewa, Roi akashusha pumzi ndefu na nzito.

    “Mambo,” ilisikika sauti nyororo ya Martha....

    “Poa, mzima mke wangu...”

    “Mi mzima sijui wewe kababaa.”

    “Nipo poa. Nimekumisi sana wangu, unanibania kweli kukuona,” alisema Roi.

    “Unasema kweli?”

    “Ndiyo. Nimekukumbuka mno. Nataka nikuone, lini utakuwa tayari?”

    “Sijajua, nina kazi zinanibana sana kwa sasa.”

    “Kwa hiyo hatutaweza kuonana?”

    “Nitaangalia.”

    “Ushaanza.”

    “Nimeanza nini tena?”

    “Tangu siku ile umesema utaangalia, huko kuangalia hakuishi tu?”

    “Hahaha! Sawa, nitakujibu kesho, usijali.”

    “Sawa. Ila nikwambie kitu?”

    “Niambie tu.”

    Una sauti nzuri sana, nampa pongezi mama aliyekuzaa, hata Mungu kakupendelea sana,” alisema Roi, sauti yake ilisikika kimahaba....

    “Hahaha! Nashukuru jamaniiii...”

    “Upo wapi sasa hivi?”

    “Nipo kitandani, nimejiachia tu.”

    “Upo na nani?”

    “Peke yangu, halafu kuna kibaridi, si unajua mvua zinazoendelea, natamani ningekuwa na mtu hapa,” alisema Martha maneno yaliyompagawisha Roi...

    “Nielekeze nije.”

    “Mmh! Hapana. Usiku sana sasa hivi!”

    “Si nachukua bodaboda tu...”

    “Hapana bwanaaaa, usiku ushaingia,” alisema Martha, wakati akiongea na Roi kipindi hicho, tayari mwanaume huyo alishainuka kitandani, alikuwa akivitafuta viatu vyake kwa kuona kwamba angekubaliwa kwenda...

    “Sawa. Basi tutazidi kuwasiliana.”

    “Hakuna tatizo kababaa...”

    Roi akakata simu, alikuwa hoi bin taabani, alipojiangalia, hakujiona kama alikuwa vizuri, akainuka pale alipokuwa na kwenda bafuni kuoga. Sauti ya Martha iliutetemesha moyo wake, mwili wake ulisisimka sana...

    Kila alipokuwa akizungumza naye alichanganyikiwa zaidi mpaka kufikia kipindi akawa halali vizuri kwa kumkumbuka msichana huyo...

    “Yaani simuelewielewi, anaingia bandani, anatoka, anaingia, anatoka, ila poa tu, akiingia tena, nafunga banda,” alijisemea Roi huku akijiandaa kulala na kichwa chake kikiwa kimechanganyikiwa kwa mwanamke huyo.



    “Yaani simuelewielewi, anaingia bandani, anatoka, anaingia, anatoka, ila poa tu, akiingia tena nafunga banda...”



    “Martha...Martha...anaonekana ni mwanamke mwenye kujitambua. Inaonekana ameshaumizwa sana sasa machale yanamcheza namna ya kumkubali mtu,” alisema moyoni Roi akiwa amelala anaangalia juu...

    “Da! Iko siku lakini...naweza kusema atakuwa wangu lakini kumbe ana mwingine ndiyo maana anaingia na kutoka.”

    ***

    Kwa upande wake, Martha kule kwake alikokuwa alikuwa amelala huku akiwaza...

    “Mh! Roi bwana. Anaonekana ananitaka, lakini mimi siwezi kwa kweli. Nimeshalizwa sana tu. Wanaume wa siku hizi ndivyo walivyo,” alisema moyoni Martha, akajikuta akishika simu na kumtumia meseji Roi...

    “Baba!”

    Roi alikuwa anaangalia muziki kupitia runinga, meseji ya Martha ikaingia, akaisoma...

    “Nikwambie kitu baba?”

    Roi aliachia tabasamu, akaamini kwamba anachotaka kukisema Martha ni kwamba amekubali wawe na uhusiano, akamjibu...

    “Niambie baby wangu...”

    “Unanipenda?”

    “Sana!”

    “Kweli?”

    “Kweli kabisa.”

    “Mimi naomba...tena naomba sana baba, tuwe kaka na dada.”

    Roi alikuwa peke yake lakini aliguna kwanza, akaangalia kulia na kushoto kama aliyeamini kwamba, kuna mtu anamwona alivyong’onyea...

    “Sawa,” alijibu Roi meseji kwa ufupi sana...

    “Loo! Asante God...sasa naweza kuwa huru na wewe kama kaka yangu...nakupenda sana kaka, nitakuheshimu na kukuthamini. Nimetokea kukupenda sana Roi, amini hivyo.

    “Kifupi mimi sina kampani yoyote ile, wewe ndiyo utakuwa kampani yangu kama kaka.”

    “Usijali sista...hata mimi nakupenda sana kama dada yangu, nitakuheshimu na kukuthamini,” alijibu Roi.

    Baada ya hapo, waliagana kwa ajili ya kulala...

    “Bro, usiku mwema, Mungu akulinde...”

    “Na wewe sista. Mungu akutangulie, ulale salama chini ya ulinzi wake.”

    “Asante kaka...”

    ***

    Kulikucha, Martha ndiye alikuwa wa kwanza kumtumia meseji Roi...

    “My love bro.”

    Mlio wa meseji ndiyo uliomwamsha Roi kutoka usingizini, akaisoma meseji hiyo na kuijibu...

    “Yes darling sista.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Umeamkaje my sweethaert kaka?”

    “Niko vizuri my baby sister. Wewe je?”

    “Mimi pia...niko njiani bro nakwenda job. Leo tunaweza kuonana?”

    “Hakuna tabu sista.”

    “Oke...basi kazi njema na wewe bro wangu, nakupenda sana.”

    “Nakupenda sana pia sista.”

    ***

    Jioni walipomaliza kazi, walikwenda kukaa baa ya Ground Pub! Waliipenda pub hiyo kwa sababu ilikuwa inauza pweza na supu yake ‘mchuzi wa pweza’ na wakazi wengi wa Jiji la Dar walipenda kwenda kukaa hapo jioni.

    Wakiwa hapo, Martha alimtumia meseji Roi...

    “Sweetheart bro!”

    Roi baada ya kuisoma meseji hiyo alianza kuweweseka akitingisha kichwa na kuachia tabasamu. Kuitwa sweetheart bro alihisi mwili kusisimka kimahaba..!

    “Duu! Huyu Martha huyu...sijui! Huu ni usista kweli au kuna lingine?” alijiuliza mwenyewe, akamjibu...

    “Darling sista!”

    “Wapi?”

    “Nipo hapa Ground Pub Sinza...wewe je?”

    “Mimi ndiyo natoka. Je, tunakutana?”

    “Yes! Njoo hapa, si unapajua?”

    “Yes! Nikifika hapo?”

    “Ukifika nipigie.”

    Roi alipomaliza kuzungumza na Martha aliwaambia wenzake...

    “Jamani...jamani...sikieni...”

    “Vipi?” walimuuliza...

    “Kuna mgeni wangu anakuja hapa, anatokea Kariakoo.”

    “Ni shemeji yetu au?” aliuliza Julio...

    “Acha maswali mengi wewe, mtamuona hapahapa akifika.

    Lakini Roi akatumia nafasi ile kuwasimulia kisa chake na msichana huyo. Aliwasimulia ishu yote kuhusu Martha walivyokutana, walikofikia na wanakoelekea...

    “Aaah! Mtu kama huyo bwana ngumu sana kumwelewa. Hapo unatakiwa kujiongeza katika kila neno lake. Pengine yeye yupo siriasi kwamba anataka wewe uwe kaka yake halafu wewe unawaza mapenzi, utamboa” alisema Julio...

    “Hakuna, huyo ameshaingia laini, hapo Roi ni wewe tu,” alisema Pauli wakiwa tayari wapo kwenye moja baridi, moja moto.

    Walibadilishana mawazo kuhusu Martha mpaka wakafikia hatua ya kuachana na mazungumzo hayo, wakahamia kwenye mambo mengine.

    Baada ya nusu saa, simu ya Roi iliita...

    “Jamani huyo, ameshafika...halooo sista...”

    “Ee... nimefika hapa barabarani.”

    “Ngoja nimtume mhudumu akufuate.”

    “Poa.”

    Roi alimpa simu yake mhudumu mmoja wa baa hiyo aende nayo barabarani...

    “Ukifika pale piga namba hii, utakutana na dada mgeni wangu mmoja mlete hapa,” alisema Roi, mhudumu akaondoka na simu.

    Baada ya dakika mbili, mhudumu aliongozana na Martha mpaka alipokaa Roi na marafiki zake. Kazi ikawa, Martha akae wapi sasa? Akae kwenye kiti cha jirani na kaka yake, Roi au?



    “Karibu hapo,” alisema Roi akimtengea kiti Martha ili akae jirani na yeye.

    Martha siku hiyo alivaa suruali ya jinzi iliyomkaa sawasawa kwa kumbana, alionekana ni mwanamke mwenye kujiamini sana. Ongea yake, tazama yake ilimfanya kila mmoja kati ya Roi mwenyewe, Pauli na Julio kujua kuwa, Martha ni mwanamke...

    “Bro,” Martha alituma meseji palepale kwenda kwa Roi...

    “Sema sweet sista.”

    “Mimi nina majina mawili. La kwanza, Martha. La pili ni Liz. Lakini jina ambalo limezoeleka sana ni Liz. Kwa hiyo kuanzia leo nitapenda uniite Liz na achana na jina la Martha.”

    Roi alipoisoma meseji hiyo aliona sawasawa tu. Atumie jina la Martha, atumie la Liz sawa, kwake majina yote yalikuwa ni mazuri...

    “Poa sista, love u sana...”

    “Love u too.”

    Mazungumzo kati ya Roi na marafi zake yaliendelea huku Liz akiwa ametulia kimya pembeni kwenye kiti akiwasikiliza. Ilifika mahali, Roi akawaomba watulie ili atoe utambulisho...

    “Jamani...jamani...” Roi alisema kwa maana ya kuomba utulivu...

    “Sema kaka...”

    “Huyu anaitwa Liz, ni dada yangu kipenzi,” alisema Roi huku akimshikashika begani dada yake huyo...

    “Kumbe hapa Dar upo na dada yako? Sisi tulikuwa hatujui,” alisema Julio...

    “Hata mimi nimeshangaa sana,” alidakia Pauli huku wote wakimkaribisha Liz tena na tena...

    “Asanteni jamani, nashukuru sana.”

    Baada ya utambulisho huo, mazungumzo ya wote yalikata, sasa ikawa wote wako na simu zao. Kila mmoja alituma meseji alikokujua yeye...

    “Bro!” alituma Liz kwa Roi...

    “Yes, niambie...”

    “Upo oke?”

    “Nipo sawa mama, wewe?”

    “Hata mimi my bro. Nipo happy kuwa na wewe.”

    “Wewe kama mimi.”

    “Kumbe tuko sare!”

    “Umeona ee?”

    “Yes! Sijakuboa lakini?”

    “Wala! Hujaniboa! Hivi sista wewe ni mwenyeji wa wapi?”

    “Natokea Iringa bro.”

    “Oke...oke...kamwene,” alitania Roi...

    “Kamwene...”

    “Mnogage?”

    “Ndi mnofu...Teh! Teh! Teh! Sijakaa sana Iringa lakini nakijuajua bro...teh!”

    Roi naye alimrudishia meseji kwa kicheko huku akimchombezea kwa maneno kama...

    “Umependeza sana my darling sista...”

    “Hata wewe sweetheart bro.”

    Walikunywa, walikula, ikafika mahali Liz akaamua kuaga kwa Roi kwa njia ya meseji...

    “Baby bro, mimi naondoka zangu.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mh! Mara hii sista?”

    “Usijali, siku nyingine tutakaa wote kwa muda mrefu sana.”

    “Basi poa.”

    Roi alisimama, Liz naye akasimama, akawaaga Pauli na Julio, Roi akamsindikiza hadi barabarani kwa ajili ya kupanda daladala.

    Walisimama kando ya barabara, Roi akapeleka mdomo wake pembeni mwa shavu la Liz, akambusu...

    “Mmmwaaa....”

    “Thanx my bro, usiku mwema, tutachati,” alisema Liz...

    “Poapoa.”

    Roi alirudi kuungana na marafiki zake, Julio na Pauli...

    “Ee bwana naona sista kama hajayazoea mazingira haya,” alisema Pauli...

    “Ni kweli, amesema pana kelele sana.”

    “Lakini jamani ni kweli. Mnajua kukaa hapa panataka moyo maana hakuna utulivu. Kama umetoka kazini na unataka kupumzika, si mahali pazuri sana.”

    “Ni kweli kabisa,” alidakia Julio...

    “Ni kweli,” alidakia Roi mwenyewe sasa.

    ***

    Liz alipofika nyumbani kwake, alimtumia meseji Roi kwamba amefika...

    “Bro, nimefika. Leo nimefurahi sana kukutana tena na wewe.”

    “Hata mimi...”

    “Oke, nataka kuoga kwanza halafu baadaye tutaendelea kaka yangu.”

    “Usijali dada yangu Martha.”

    “Bro! Nilikwambia tumia Liz na siyo Martha.”

    “Ha! Nilisahau sista jamani! Oke dada Liz...”

    Roi na wenzake waliendelea kunywa, wakanywa wee! Wakanywa mpaka kila mmoja akaanza kuonesha dalili kwamba amelewa...

    “Jamani vipi? Suni tunatimua?” Julio aliwasilisha hoja binafsi...

    “Ni kweli,” alishadadia Pauli...

    “Sawasawa,” alimalizia Roi.

    ***

    Usiku wa saa tano, Roi alikuwa kitandani, alilala chali akiwa ndani ya bukta tu. Alikuwa ameingia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuangalia nini kinaendelea. Mara meseji kwenye WhatsApp ikaingia...

    “Baby...” ilitoka kwa Liz, Roi akashangaa kuona meseji ya Baby imeingia bila nyongeza. Alizoea baby bro, sweetheart bro na mengineyo...

    “Darling,” na yeye alitingisha kiberiti, akatuma meseji hiyo bila kuongezea neno sista...

    “Umeshatoka hapo?”

    “Zamani sana sista, niko home.”

    “Unafanyaje muda huu?”

    “Nimejilaza kitandani tayari kwa kusinzia. Wewe je?”

    “Hata mimi nimelala my bro...”

    “Umelalaje hapo kitandani my sweetheart sista? Please niambie..



    “Nimelala chali au niseme nimelala naangalia juu.”

    “Umejifunika shuka?”

    “Hapana my bro! Na joto lote hili? Wewe je?”

    “Mimi nimelala naangalia chini, yaani tumbo limegusa godoro, tofauti na wewe mgongo ndiyo umegusa godoro.”

    “Duu! Tumebadilishana, mimi naangalia juu wewe unaangalia chini...teh! teh!”

    “Kumbe tumelala vizuri sana. ndiyo inavyotakiwa, mwanaume analala hivyo na mwanamke analala hivyo kama wewe.”

    “Teh! Teh! Mi nalala bwana kaka, kesho.” “Kabla hujalala nataka nikuombe kitu kimoja sista...”

    “Kipi hicho braza?”

    “Kesho tukutane lakini iwe sehemu ya siri sana.”

    “Sehemu ya siri kama ipi bro? Unanitisha.” “Kama hotelini.”

    “Mh! Jamani kaka! Hotelini tena? Yaani chumbani au?”

    “Yes!”

    “Ah! Sasa itakuaje mtu na kaka yake chumbani? Inawezekana kweli?”

    “Mimi naweza sana.”

    “Mimi siwezi kaka.”

    “Kwa nini huwezi dada?”

    “We unajua ni vigumu. Unaweza kuzidiwa ukanibaka bure, sitaki.”

    “Yaani sikia sista...tukiwa mle hatutakaa pamoja, wewe kona nyingine na mimi kona nyingine. Halafu kila mmoja atakuwa ndani ya mavazi...”

    “Lakini kisa cha yote hayo ni nini?” aliuliza Liz...

    “Sikia Martha...”

    “Nilisema usiniite Martha, niite Liz.”

    “Oke. Sikia Liz...hakuna kisa ila nimependa tu. Isitoshe mimi na wewe ni mtu na dada yake, siwezi kuwaka tamaa kama ambavyo najua na wewe hutaweza kuwaka tamaa.”

    “Mh! Una maneno matamu sana bro! Haya sawa, lakini asitokee mtu akakiuka.”

    “Hatutaweza sista bwana.”

    “Sawa. Usiku mwema basi, kesho my kaka.”

    “Lala salama my sista.”

    Liz alipanda kitandani huku akiwa na maswali kibao kuhusu ombi la Roi kwamba kesho yake wakutanie chumbani hotelini...

    “Hivi amekusudia nini? Au anataka kuonesha kwamba, hata tukiwa chumbani wawili hatuwezi kuzini kwa vile tumeshakuwa kaka na dada? Anyway, tutaona hiyo kesho,” aliwaza Liz na kupitiwa na usingizi.

    Kwa Roi hali ilikuwa hiyohiyo, naye aliwaza...

    “Lakini si naweza kabisa...naingia naye hotelini, chumbani lakini sifanyi naye chochote...mwenyewe atashangaa sana.”

    ***

    Kulikucha, Liz ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtumia meseji Roi...

    “Morning my bro...”

    Roi alifurahi sana kuamshwa na Liz, akamjibu...

    “Morning my sista...umeamkaje?”

    “Nimemka salama bro...wewe?”

    “Hata mimi pia.”

    “Oke, kumekucha.”

    “Ni kweli sista...sasa vipi ile safari yetu?”

    “Saa ngapi?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nataka iwe mchana wa leo.”

    “Utaniambia ni wapi!”

    “Poa sista.”

    “Lakini bro, ni kweli hutafanya lolote kwangu?”

    “Ni kweli kabisa sista, wala usiwe na shaka.”

    “Basi sawa.”

    ***

    Ilikuwa saa saba mchana, Roi alimtumia meseji Liz ya kumshtua kwa ajili ya kumfuata alipo...

    “My sweetheart sista...”

    “Honey bro!”

    “Sasa?” “Nakusikiliza wewe kaka’angu mpenzi.”

    “Mimi nipo hapa Kisasa Hotel, Kinondoni. Njoo basi.”

    “Duu! Bro uko shap sana! umeshatafuta na hoteli kumbe? Poa nakuja sasa hivi.”

    Roi alikuwa ndani ya chumba cha hoteli hiyo. Mwili ulimtetemeka kila mara. Alianza kuhisi kwamba, kiapo chake kwa Liz si cha kweli...

    “Hivi nitaweza kweli kukaa naye mpaka mwisho bila chokochoko?” alijiuliza.

    Dakika kumi na tano mbele, Liz alimpigia simu kwamba amefika yuko nje...

    “Njoo mpaka ndani sista, utaoneshwa chumba nilichopo. Ni namba hamsini.”

    “Poa bro.” Mara mlango uligongwa, Roi akaruhusu mtu kuingia, Liz akazama ndani...

    “Oohooo! Huyu mchokozi sasa,” alisema moyoni Roi baada ya kumwona Liz amevaa suruali ya matirio kama t-shirt, mbaya zaidi imembana vilivyo na juu kiblauzi chepesi mpaka unaona ramani ya kifua chote.

    “Karibu sana sista,” alikaribisha Roi.

    Liz aliweka kipochi chake kwenye meza kisha akakaa upande wa miguuni mwa kitanda na kuangalia ukutani wakati Roi alikaa eneo la kichwani naye akiangalia ukutani...

    “Za hapa?” alisalimia Liz...

    “Poa sista, za safari?”

    “Njema tu. Ndiyo umeamua kweli kabisa kuchukua chumba kaka jamani?”

    “Usijali sista, hili ni eneo salama sana kwetu.”

    “Mh! Mfano akija mtu akauliza sisi ni akina nani tukasema ni mtu na kaka yake itakuaje? Ataamini kweli bro?”

    “Nani kwanza atakuja sista?”

    “Mfano yaani bro...”

    “Hamna cha mfano sista, hakuna atakayekuja humu ndani.”

    Walianza maongezi ya mbali kwa mbali, kila mmoja akiangalia ukutani. Mwishowe Liz alilala chali, nusu ya mwili kuanzia kiunoni kwenda juu kitandani, nusu iliyobaki ikining’inia chini...

    “Umechoka nini sista?” aliuliza Roi...

    “Nahisi kusinzia bro...”

    “Hata mimi pia,” alisema Roi na kulala kama alivyolala Liz, wakakutana vichwa!



    “Basi tulale ili tupunguze usingizi japo kidogo tu!”

    “Sawa sista.”

    “Lakini tulale hivihivi,” alisema Liz kwa sauti iliyokuwa ikienda kwenye kukatika.

    Ulipita ukimya kidogo, ni lazima wote, kila mmoja alikuwa kwenye mawazo yake anayoyajua yeye...

    “Huu mtihani...tena mtihani mkubwa sana,” alisema moyoni Roi...

    “Halafu alivyovaa sasa...yaani mtu anajua wazi kwamba anakuja kukutana na mwanaume ambaye si ndugu yake, tena chumbani halafu anavaa nguo za kuonesha mwili namna hii? Kwa kweli hajanitendea haki,” Roi aliendelea kusema moyoni mwake...

    “Lakini inataka moyo kweli! Na hivi sijaduu siku nyingi halafu nakutana na mwanaume, tena gesti lazima niwe na roho ngumu sana,” aliwaza Liz.

    Wakati wakiendelea kuwaza hayo, Roi alipitiwa na usingizi mzito kwani alisikika akikoroma moja kwa moja...

    “Kroooo...kroooo...”

    “Mh! Kweli alikuwa na usingizi,” alisema Liz baada ya kumsikia Roi akikoroma.

    Katika kulala huko, Roi alifika mahali akakunja miguu, akapanda juu kidogo na kurusha mkono pembeni, ukaangukia kwenye paja moja la Liz...

    “Mh! Huyu naye...ameanza sasa...” alisema Liz. Akautoa mkono huo na kuuweka pembeni kwa taratibu kabisa.

    Roi hakuona sababu ya kuendelea kulala huku akining’inia, alipanda moja kwa moja mzimamzima na kulala sanjari na Liz sasa...

    “Mh! Kaka...bro...” aliita Liz akimtingisha, Roi akaamka...

    “Mh! Mh!”

    “Mbona unakiuka sasa?”

    “Nakiuka nini sista?” aliuliza Roi huku akijifuta usoni...

    “Unapanda kulala juu...”

    “Ah! Usingizi, jana nilichelewa kulala ndiyo maana. Panda basi na wewe ulale.”

    “Aaah! Bro, si utavuka mipaka jamani?”

    “Wala! Nilishakwambia kwamba siwezi kwenda kinyume na makubaliano.”

    “Oke,” alisema Liz akipanda kitandani kulala sawasawa. Alimwamini Roi kwamba hawezi kufanya kitu chochote.

    Sasa walilala sambamba, Liz aliangalia ukutani, Roi aliangalia mlangoni. Wakaanza kuzungumza kwa staili hiyohiyo, Liz ukutani, Roi mlangoni...

    “Ina maana sista wewe bado una wasiwasi na mimi siyo?”

    “Hapana, ila natoa tahadhari tu.”

    “Ooo! Sawa, niamini mimi sista.”

    “Nakuamini sana bro.”

    Walilala, wakapitiwa na usingizi mzito. Kwa hiyo hakuna aliyekuwa akiukontroo mwili wake. Kuna wakati Liz alirusha mikono na kumfikia Roi na kuna wakati Roi alijikuta amegeuka upande wa Liz wakalala wakiangalia kumoja.

    Kuna wakati, Roi akageuka, Liz naye akageuka, wakaangalia kumoja, mlangoni, Liz akapitiliza, mkono wake mmoja ukaenda ubavuni kwa Roi, Roi naye akaushika na kung’ang’ania.

    Liz akautoa, akamshika kifuani, akamsogelea, wakawa beneti zaidi, Liz akatoa mkono ubavuni, akaupeleka kwenye kiuno, Roi akashtuka kwamba mbali na kubaini kuwa, yuko kitandani na Liz..

    “Daa! Kumbe sista! Lakini mbona na yeye ananifanyia hivi, anakiuka makubaliano?” alijiuliza Roi.

    Akaamua na yeye kukiuka makubaliano...

    “Kama ni hivyo na mimi nakiuka.”

    Roi alimgeukia Liz, wakawa wamelala kwa kuangaliana, Liz bado alikuwa katika usingizi lakini siyo mzito kama awali. Roi alimsogelea Liz mpaka mdomoni, akatoa ulimi kuelekea kwenye kinywa cha mrembo huyo.

    Liz akiwa hajui lolote, alijikuta akipanua kinywa, ulimi wa Roi ukapenya ndani, Liz akaanza kuburudika nao huku akiguna.

    Liz alijikuta akishtuka kutoka usingizini, akatumbua macho na kumwona Roi mbele yake...

    “Haa! Broo,” alisema kwa tabu huku ulimi wa Roi ukiwa bado kinywani mwake, lakini hakuutoa!

    Walikaa kimya, kilichosikika wakati huo ni dalili na mihemko tu, kila mmoja alishapanda joto la mahaba...

    “B...ro...”

    “M...mm...”

    “Ah!”

    “Mh!”

    “Oo!”

    “Ha!”

    Liz alimvutia Roi kifuani kwake, akamweka karibu kabisa na kuanza kufaidi denda kwa uwazi. Ndani ya dakika kumi nzima walizama huko, Liz alipokuja kumtoa Roi kwenye kifua chake, akalala chali na kuchojoa.

    Roi hakutaka kusubiri na yeye alichukua hatua hiyo, akajichojoa mwenyewe, wakawa saresare.

    Walijikuta wapo uwanjani, kila mmoja alikuwa moto wa kuotea kwa mbali. Walijitamani sana, wakaamua kuingia uwanjani bila kuulizana wala kulaumiana.

    Mchezo ulianza vizuri kabisa, kila upande ulisukuma mashambulizi kwa mwingine mpaka mchezo kuwa wa vuta nikuvute!

    “Bro...ooo.”

    “Si...staaa...”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tume...tumekiuka?”

    “Daa...aaa!”

    “Mwisho leo...”

    “Kufanyaje?”

    “Tusirudie tena, sawa?”

    “Kweli kabisa sista...tusirudie tena,” alisema Roi huku akikazana. Alikazana sana mpaka Liz akabadili mawazo...

    “Bro...oooo...”

    “Sist...aaa...”

    “Una..unaonaje tukiachana na undugu? Mbona kama huku ni kuzuri zaidi...”

    “Broooo...oooo...”



    “Noo...tuendelee sista...lakini tusirudie tena baada ya leo, tena tujikanye kabisa na tukome kama tulivyokoma kwenye nido za mama zetu, si ndiyo... eee?” alijibu Roi kwa sauti ya kubabaika...

    “Bwana...aaa! Mimi sitaki undugu tena kuanzia leo na ufe, kwanza una faida gani kwetu?” alihoji Liz lakini kikubwa kilichoonekana ni tamaa ya mwili iliyombamba kwa wakati huo pale kwenye kitanda...

    “Mimi nataka mbona,” aliendelea kusisitiza Roi.

    “Ba...aaa...si tumalize kwanza...tu...tajadili.”

    Wawili hao, waliendelea kuchekecha mpaka wakacheketuka!

    Kwa Liz, moyoni aliamua kuwa, baada ya mechi hiyo, yeye na Roi waendelee kuwa kaka na dada kama walivyokubaliana...

    “Si mbaya kama tumeanguka dhambini leo tu, lakini nakuhitaji tuendelee kuwa kaka na dada,” alisema Liz akiwa kwenye kasi ya kupiga mpira kwenye kona karibu na goli!

    “Hata mimi ndivyo nitavyotaka. Leo tukimaliza hapa tutubu dhambi zetu, tuanze upya kama kaka na dada, sawa dada angu?” alisema Roi...

    “Si sawa...kwa...kwa muda huu tuendelee kuwa wapenzi si mpaka tumalize.”

    “Haya.”

    Liz alichekecha, akafika mwisho, akatangaza nia na kunyoosha miguu, akatulia tuli huku Roi akijitegemea mwenyewe mpaka naye alipotangaza nia yake.

    ***

    Wote walilala wakiangalia juu huku mazungumzo yao yakiwa ya machalechale. Yalikuwa mazungumzo ya kama ni wapenzi, wakati mwingine kama kaka na dada.

    Katika kuonesha kwamba, Liz alijutia kitendo cha kuivunja amri ya sita ya Mungu, aliamua kukaa kitandani badala ya kulala...

    “Kaka...”

    “Dada...”

    “Tutubu dhambi yetu sasa ili tuendelee kuwa kaka na dada kama mwanzoni.”

    “Kweli bwana, hebu tubu wewe kwa niaba yangu,” alisema Roi baada ya kuhisi hakuna maneno rasmi ya kutubu...

    “Tumwombe Mungu tusirudie tena kufanya dhambi hii, mimi na wewe kuanzia sasa ni kaka na dada tena. Kwa kulitambua hilo naomba tukaoge, tuvae tuondoke,” alisema Liz huku akitoka kitandani. Alikwenda bafuni, akaoga na kurejea, akavaa, akasimama akimsubiri Roi ili waondoke wote...

    “Sasa dada wewe umeshavaa, kwa hiyo na mimi nivae mbele yako kama dada yangu?”

    “Oo! Ngoja nitoke kaka, nisamehe sana.”

    Liz alitoka, akasimama nje ya mlango. Roi alikwenda kuoga, akarudi na kuvaa chapchap, akatoka, akaungana na Liz...

    “Dada wewe unaondokea kwa njia gani?”

    “Nitapanda Bajaj hapo nje kaka.”

    “Oke, basi itabidi tuachane kwa nje au vipi sista?”

    “Sawa kaka‘angu.”

    Nje ya hoteli hiyo, Roi na Liz waligawana njia, kila mmoja akachukua usafiri wake, wakatawanyika kwa ahadi ya kuwasiliana kwa simu...

    “Basi baadaye bro,” alisema Liz...

    “Sawa, baadaye dada’angu,” alisema Roi.

    Baadhi ya watu walipowaona wanatokea kwenye hoteli hiyo na kuitana dada, kaka walishangaa kwani dalili zote ziliashiria kwamba, wawili hao ni wapenzi.

    ***

    “Ila anajitahidi sana kitandani, hivi kweli tunaweza kuwa kaka na dada maisha yetu yote?” alihoji moyoni Roi...

    “Mh! Kaka...kaka kweli! Kaka mzima uwanjani kama Pele...kakaaa...” alisema moyoni Liz akisifia.

    ***

    Ilikuwa usiku wa siku hiyohiyo tu, Roi ndiye aliyeanza kumchokoza Liz...

    “Dada Martha mambo?”

    Martha aliachia tabasamu kwanza maana alishamwambia mara kadhaa Roi kwamba, asimwite Martha, amwite Liz...

    “Kaka Roi,” aliitika kwa kulitaja jina Liz...

    “Naam sista...”

    “Unalipenda jina la Martha ee?”

    Roi ndiyo akashtuka kwamba kumbe alitumia jina hilo...

    “Da! Nisamehe sista, kusema ule ukweli nililizoea sana kuliko Lizie...”

    “Ona sasa! Siyo Lizie kaka ni Liz...sasa sikia bro, nakuruhusu utumie jina la Martha kuanza leo. Hilo la Liz lifute kabisa kwenye akili yako.”

    “Daa! Sista nakushukuru sana mama. Hakuna jina nalipenda kama la Martha kuliko Liz, nashukuru kwa kuniruhusu...”

    “Oke usijali baby bro...uko wapi sweetheart kaka?”

    “Nipo nyumbani darling sista...”

    “Oke! Mtoto mzuri kumbe, wewe ndiye kaka wa kweli.”

    “Hata wewe ni dada wa kweli. Good sista...hujalala?”

    “Ndiyo nataka kulala sasa. nimechokaaaa!”

    “Umechokeshwa na nini sista jamani?”



    “Kwani hujui bro?”

    “Sijui chochote.”

    “Aaah! Si kule tulikokuwa,” alisema Martha lakini akilini mwa Roi alijua kilichomchokesha sista wake ni nini!

    “Kule gesti?” aliuliza Roi...

    “Ndiyo kulekule bro...daa!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Daa! Ila sista uko vizuri unajua?”

    “Teh! Teh! Mh! Wewe je kaka? Mbona uko vizuri zaidi...”

    “Mh! Kweli...?”

    “Kweli bro...”

    “Uliipenda chenga ipi pale uwanjani?”

    “Mmh! Kaka bwana...chenga zote zilikuwa nzuri sana kaka, wewe ni kiboko.”

    “Hamna! Lazima kuna chenga moja uliipenda sana...iseme tu sista jamani...”

    “Ha! Ha! Ha! Niliipenda ile ulipokaribia golini ukawa unapiga chenga za zigzaga. Halafu hata ile ya mimi kuchunga ng’ombe ilikuwa nzuri...”

    “Nyingine, lazima kuna nyingine...”

    “Nyingine ni ile uliponiambia una hamu ya kula mboga ya matembele, si ikabidi nikachume.”

    “Mh! Sista...”

    “Nini tena braza..?”

    “Mwenzio hoi hapa...”

    “Mimi je? We acha tu! Hivi hapa nataka kwenda kuoga.”

    “Umechafuka na vumbi?”

    “Kumbe je?”

    “Kwa hiyo? Nije nini?”

    “Ha! Ha! Mbali...halafu ukaka si unaendelea kama kawa au?”

    “Laa! Aisee...huu ukaka na udada halafu tunapeana njaa si mzuri...nataka kuruka nije...”

    “Njoo...”

    “Kweli?”

    “Kweli njoo.”

    “Nikija?”

    “Si utakula chakula kama mgeni.”

    “Chakula gani?”

    “Utakacho...kuna ndizi za kuiva na maandazi ya donati.”

    “Mh! Unanitamanisha sista...mimi nitakula donati...”

    “Haya mimi nitakula ndizi za kuiva,” alisema Martha.

    “Lakini sista...”

    “Nini tena jamani kaka..?”

    “Kwani umelala sista?”

    “Nipo kitandani bro...”

    “Umelalaje hapo kitandani?”

    “Nahesabu paa...wewe bro?”

    “Mimi nasoma kitabu.”

    “Kumbe tupo sawa basi!”

    “Basi acha kuhesabu paa.”

    “Na wewe utaacha kusoma kitabu?”

    “Nimeshakiweka pembeni.”

    “Oke, mimi nimeshaacha kuhesabu paa.”

    “Miguu ikoje?”

    “Mashariki na Magharibi mwa nchi.”

    “Basi mimi niko kanda ya kati nakuja kwako.”

    “Njoo broo.”

    “Ndiyo nakuja sasa...”

    “Njoo tu. Na mimi nimeanza kukuona unavyokuja.”

    “Kwa hiyo utanipokea..?”

    “Ukifika nakupokea bro tena kwa mikono miwili kaka...njoo!”

    “Nakaribia, nimeanza kukuona umesimama mlangoni unanisubiri...”

    “Karibu broo...njoo...”

    Roi alitumia meseji nyingine lakini hakujibiwa, akatuma nyingine, hakujibiwa, akapiga, Martha hakupokea...

    “Jamani dada...nini tena?”

    Baada ya dakika kumi na tano, meseji ikaingia, Roi akaisoma kwa haraka sana...

    “Brooooo...”

    “Sistaaa...”

    “Nipo vibaya, please kama unaweza njoo kweli sasa hivi...chukua usafiri wowote ule nitakuelekeza kwangu please bro njoo tucheze...”

    “Sista Martha...”

    “Yes brooo...ooo!”

    “Ukaka na udada je? Ufe?”

    “Aaaah! Potelea mbali bwana...kwani lazima wakati mi nateseka?”

    “Hapana dada...undugu ni bora kuliko mapenzi...tutag

    ombana kila siku tukiwa wapenzi dada...”

    “Hapana kaka...basi leo tu...”

    “Baada ya leo?”

    “Tusirudie tena bro...”

    “Haya nakuja...kaa tayari...”

    “Njoo kaka mpaka Kimara Mwisho, kuna barabara inaingia kulia, fuata hiyohiyo mpaka sehemu kuna pub, kuna muziki nje...nipigie...”

    “Kwani saa hizi unafanyaje dada?”

    “Natandika kitanda kaka, si unakuja kweli?”

    “Nakuja dada...”

    “Njoo kaka...”

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya dakika kumi, Roi alimpigia simu Martha akiwa kwenye pub aliyomwelekeza...

    “Nakuja kaka...”

    “Poa dada.”

    Usiku huo, Martha alivaa gauni la kulalia kwa hiyo lilimwonesha umbo lake kwa usahihi wote kiasi cha kumfanya Roi kuanza kufikiria upya kuhusu kuendelea na ukaka na udada baada ya tukio la muda huo...

    Martha alikuwa akiishi na wapangaji wengine, wanawake wenzake ambapo kwa usiku huo walikuwa wamekaa nje jirani na dirisha la chumba cha Martha wakiongea...

    “Karibu sana kaka...! Jamani huyu kaka ‘angu, anaitwa Roi...”





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog