Chombezo : Utamu Wa Zege
Sehemu Ya Pili
(2)
JANETH alipatwa na
aibu. Alimwangalia Amosi kwa macho ya kuibia. Ile hali ya kujibu kwa ukali
haikuja na wala hakuifikiria. Upole ulemvaa na kusahau kuhusu
maji.
“Saa nne na robo usiku, simu ya Amos ilianza kuita. Hakuwa na
haraka nayo kwani alijua ni Janeth anabipu. Alimalizia kumimina chai yake tayari
kwa kuinywa. Alipiga funda mbili na kuichukua simu yake. Alikuta ni Janeth
aliyebipu. Alitabasamu kidigo na kujiweka sawa.
“Halow, “ Amos alianza
kumwita Janeth.
“Ehh, mambo,” Janeth aliitikia na kumsalimia
Amos.
“Poa, nimefurahi ulivyonibipu.”
“Ndio, ulikuwa
unasemaje kwani.” Sauti ya Janeth ilikuwa ya woga. Ilitetema kama mtu
aliyehojiwa kwa mara ya kwanza na polisi kwa kosa la
kusingiziwa.
“Janeth, ni kama bahati leo nimekutana na wewe. Haikuwa
mara ya kwanza kukuona.Ila kwa uzuri wako na jinsi ulivyo umenivutia sana. kwa
kifupi tu. Napenda tuwe wote.”
“Haloow,” Amos aliita.Janeth alikuwa
amenyamaza kimya akimsikiliza Amos. Aliona kama bahati ikija
mbele.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
******
Akiwa
ni mtoto wa kwanza na wa mwisho katika familia ya mzee Joshua. Janeth alilelewa
katika maisha ya tabu. Wazazi wake walifariki na kumwacha akiwa hana hili wala
lile. Alihangaika na maisha peke yake maada ya wazazi wake kumwacha akiwa na
miaka kumi na tatu. Hakubahatika kusoma hata darasa moja.
Baada ya
wazazi wake kufariki aliishia kuzurura mitaani. Aliokota chupa za maji na
kuziuza. Alikumbana na mambo mengi ya hatari ikiwemo kubakwa. Hata hivyo mbakaji
hakufika mbali kwani alifanikiwa kumchoma na kitu chenye ncha kali
kilichosababisha kifo chake.
Janeth alilia sana baada ya kufanyiwa
unyama huo. Alijikongoja hadi katika nyumba ya bibi mmoja na kujilaz nje karibu
n mlango wake hadi asubuhi alivyokutwa na bibi huyo.
Yule bibi
alimchukua na kumwingiza ndani. Hakuwa na redio na hivyo hakusikia lolote juu ya
taarifa kuhusu yule mtu aliyembaka. Hakujali. Alikubali kuishi na yule bibi ilia
pate pa kulala na kumsaidia.
Yule bibi alifurahi kwani ni miaka mingi
alikuwa akiishi peke yake. Alimhudumia uji baada ya kumfanyia usafi mwili wake
ambao ulikuwa umechoka sana.
“Asante sana bibi,” Janeth alimshukuru
yule bibi.”
“Karibu mjukuu wangu.”
Janeth alipata pa kuishi.
Alianza maisha mapya na bibi. Bibi alikuwa na shilingi elfu tano. Alimkabidhi
Janeth. Alifanya hivyo kwa kuwa hakuweza kufanya lolote katika biashara. Aliishi
kwa kuokoteza na kuomba chakula.Janeth alifikiria cha kufanya. Alikuwa na
shilingi elfu tano alizopewa na yule bibi.
Alianza kazi ya kuuza maji
mjini. Aliondoka nyumbani kwa yule bibi Kikuyu asubuhi sana na kuzunguka mjini
hadi jioni. Alinunua chakula na kurudi nyumbani baada ya kumaliza kuuza
maji.
Aliendelea na biashara hiyo kwa muda mrefu mpaka alipokutana na
Amosi. Alikuwa tayari ameshafikisha miaka kumi na tisa.
Alikuwa na
umbo lililovutia. Mweupe kiasi na mfupi kiasi. Hali duni ilifanya wanaume wengi
wamwone havutii. Nguo zake zilikuwa ni chakavu na kana zilizoraruka hadi pale
alipoweka hela na kununua kanga moja na kugawana na yule
bibi.
*****
Amos
alikutana na Janeth siku iliyofuata. Alidhamiria kuwa na Janeth. Uzoefu wake wa
kuangalia wanawake katika nchi alzosafiri ilikuwa ni moja ya sababu za kuona
Janeth angemfaa. Alikumbuka jana yake alivyokitazama kifua cha Janeth wakati
akishusha ndoo yenye maji. Alihisi msisimuko usiomithilika.Akili yake yote
ilihama.
Sasa alimtafta Janeth. Alimpigia simu na kukutana naye.
Waliongea mengi pasipo kufichana jambo lolote. Janeth alikubali kuolewa na
Amos.
Taarifa hizo zilifika kwa yule bibi. Janeth alienda na Amosi
hadi kwa yule bibi na kuongea naye. Janeth alishamfanya kama mzazi wake na hivyo
asingeweza kufanya jambo lolote kubwa pasipo kumweleza yule bibi. Yule bibi
hakukataa pendekezo lao. Baada ya ujua Amosi ni mtu mzuri. Alikubali kuishi
mwenyewe na kumwacha Janeth aede kwa Amosi.
Japokuwa Amos alikuwa na
wazazi na ndugu zake. Alichelewa kuwaambia kuhusu mipango yake juu ya kukmuoa
Janeth. Aliamua kwanza kuishi na Janeth ili kujua vizuri alivyo.
Ni
mara ya kwanza ambapo Amos alikuwa na Janeth kitandani kwake. Amos alijua Janeth
hakufahamu chocote kutokana na ugeni wake katika mapenzi. Alimwona ni mwanamke
mwenye aibu sana. Alitaka kujaribu ili amjue.
“Usizime taa,
hatutafaidi hivyo,” Janeth alimsihi Amos asizime taa. Hakuwahi kumsikia Janeth
akiongelea mapenzi wala kuhusu ngono. Janeth hakuwa na mpenzi wala hakuwahi
kufanya mapenzi. Aliyembaka alimuumiza kiasi cha kumfanya asitamani kufanya
mapenzi tena. Huo ukawa msimamo wake. Aliyasikia tu na wakati mwingine alijionea
katika video nyumbani kwa rafiki yake Agness ambaye yeye alikuwa akifanya hivyo
ili kumshawishi Janeth ajiingize katika mapenzi baada ya kumwona kama asiyejua
lolote. Hilo halikumshawishi Janeth zaidi ya kupuuzia.
Amos alizidi
kumshangaa Janeth. Janeth alimvaa Amos katika kochi lake na kukaa juu yake.
Alikuwa amevalia kanga moja tu baada ya kutoka kuoga. Alimkumbatia kwa nguvu
Amos na kupitisha ulimi wake sikioni. Amos alijiondoa haraka. Hakuamini
kinachotokea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Amos!” Janeth
alimshangaa Amos.“Unaenda wapi, tafadhali rudi hapa. Nimeishia tu kuona
wenzangu, naomba leo na mimi niwajibike,” Janeth alilalamika huku akimfuata
Amos. Amos alirudi, hakuamini macho yake. Aliiondoa kanga aliyokuwa amejifunga
ili Amos aone umbo lake. Amos alichanganyikiwa.
Amos alimshika Janeth
na kumbeba. Alimwaga kitandani huku wakiendelea na mfululizo wa mabusu
yaliyomchanganya Amos. Amos alifanya kazi yake sawa sawa. Kilio cha Janeth
kilimfanya Amos azidishe kasi huku Janeth akizidisha utundu.
“Huyu
atakuwa ananidanganya, kashafanya sana huu mchezo.” Aliwaza Amos huku akiendelea
na zoezi lake.
Asubuhi Amos hakuona sababu ya kuongelea juu ya
lililotokea jana usiku. Furaha aliyokuwa nayo hakutaka kuchelewesha mpango wake.
Amosi alifanya mipango ya ndoa na kumpeleka Janeth kwa wazazi wake. Haikuwa na
pingamizi kwao. Walifunga ndoa na kuanza maisha ya ndoa. Amos alimfungulia
Janeth kibanda cha kuuzia chakula na matunda. Alijua kitamsaidia kwa matumizi ya
nyumbani wakati yeye akiwa
safarini.
*****
Baada
ya mienzi miwili ya ndoa yao. Janeth alipata mimba. Hali hiyo ilimfanya Amos
afute baadhi ya safari zake ili kumsaidia mke wake hadi atakapojifungua.
Alishinda naye nyumbani wakati mwingine ili kumfariji na hali aliyokuwa nayo.
Amos alimpenda sana Janeth.
Miezi mbele walibahatika kumpata mtoto
Jane. Ilikuwa ni kama ndoto kwa Janeth. Amos alisimamisha safari kwa mwezi mmoja
akikaa nyumbani na kucheza na kichanga chake.
Ndugu wa Amos na rafiki
wa Janeth walifika kwa Amos na kumsalimia Janeth pamoja na kumbeba mtoto.
Ilikuwa ni faraja kwa baba na mama yake Amos kupata mjukuu. Kwa uzur aliokuwa
nao Jane, kila mtu alipenda kumbeba na hata kupiga naye picha.
Janeth
alikuwa akibaki tu kitandani akiendelea kuuguza maumivu ya kichwa chake.
Alisaidiwa na baadhi ya ndugu wa Amos. Maumivu yalikuwa makali hali iliyopelekea
kukimbizwa hospitali kupatiwa matibabu. Huko aligundulika kwamba alikuwa ana
malaria kali sana. Kwa hali aliyokuwa nayo Janeth, Amos alikata tamaa juu ya mke
wake kupona. Haikuwa rahisi kuzuia kwani jitihada alizozifanya daktari pamoja na
Amos hazikuzuia uwezo wa Mungu kumchukua kiumbe chake. Hatimaye Janeth alifariki
dunia akimwacha Jane akiwa na miezi miwili. Hilo lilikuwa pigo kali sana kwa
Amos. Hakuamini kilichotokea. Alikuwa kama amechanganyikiwa na kukosa raha.
Alimlilia sana mke wake
Janeth.
****
Amos
alikuwa amesimama mlangoni kwake. Alikuwa amemkumbatia Jane huku amembeba. Jane
alikuwa akilia sana kuliko ilivyokuwa akiwa na mama yake aliyekuwa akimbeba huku
Jane akiwa anasikilizia joto la mikono ya mama yake akiwa katulia. Amos
alibembeleza sana Jane. Alizunguka naye kila kona. Chupa ya maziwa haikuwa
mbali. Alimpa kila wakati. Hakujua ameshiba au la. Yeye alimpa kila tu
aliposikia Jane akilia.Wazo la kuoa mke mwingine lilimjia. Haraka Amos alifunga
safari hadi kwa wazazi wake.
Alitaka kumwoa Debora Mwilego. Mwanamke
aliyekutana naye baa na baada ya kuongea naye kwa kirefu na kuelewana hatimaye
Debora aliamua kuolewa na Amos.
Debora, mwanamke aliyeonekana nadhifu
wakati wote. Uso wa mviringo wenye mashavu manene. Umbo la mwanamke wa Kichaga
mfupi kiasi na mweusi kiasi aliyejilazimisha kuwa mweupe huku akijipa matumaini
ili kumvutia zaidi Amos.
Vipodozi vyote viliijaribu ngozi yake
iliyokuwa ikipambana na ngozi ya walimbwende waliokutana nayo barabarani. Muda
mwingi aliishia kwenye kioo akitafakari mwonekano mpya wa ngozi yake. Weusi
aliokuwa nao ulikuwa ukibadilishwa taratibu kwa mchanganyiko wa
vipodozi.
Kitandani ndio hasa alipopajali hasa alipokuwa na Amos.
Alijua kikubwa kilichomshawishi Amos hadi kumtamkia maneno ambayo aliona ni
ndoto kwake ni kwa sababu alimpagawisha mara ya kwanz walipokutana katika nyumba
ya wageni ya Royal Inn.
Hakukata pumzi hadi alipohakikisha anamshinda
Amos ambaye nay eye alionyesha kwamba ni mwanaume aliyekamilika. Takriban saa
zima Amos na Debora walilitumia kugaragara na kubinuka kitandani. Hakuna
aliyekuwa mchoyo katika kuonyesha ufundi wake. Mihemko ilitawala chumba
chao.
Baada ya kilichowapeleka, Amos alimtamkia tena na tena Debora
kama amekubali kumlea Jane.
“Siwezi nikakataa kwa hilo. Naona pia ni
bahati kwangu kupendwa na wewe. Nakuahidi nitamlea vizuri kama alivyotarajia
kumlea marehemu mama yake. Nitampa mapenzi ya mama kwa mtoto.”
Amos
alifurahi kusikia aliyoyasema na hapo hapo alimrukia tena Debora na kurudia
tendo lile lile lililowaleta pale. Ilikuwa ndo kama wameingia. Amos hakuonyesha
kuchoka wala Debora. Alimmpokea vizuri Amos na kumpa kile alichokitaka.
Alimzungusha hivi na kumgeuza vile. Sasa kila mmoja aliridhika na kumshukuru
mwenzake.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****
Ndoa
ilifungwa na Jane alipata mama wa kumlea. Alimlea kwa mapenzi yote. Kila Jane
alilotaka Debora alimpa. Alitaka kumridhisha Amos. Hadi pale Jane alipoanza
kucheza mwenyewe na akaambiwa kitu akaelewa Debora alimshawishi Amos wamtaftie
Jane mwenzake wa kucheza naye. Haikuwa pingamizi kwa Amos.
Baada ya
miezi tisa ya ujauzito. Debora alijifungua mapacha wa kike, Marry na Neema. Jane
aliwapenda wadogo zake. Hadi walipoanza kujitambua Jane alikuwa amekua.
Walimpenda sana Jane. Walimheshimu sana Jane kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa
mkubwa kwao kiumri. Walimsikiliza sana japo kuwa Jane hakupata malezi mazuri
kutoka kwa Debora. Neema na Marry waliona utofauti kati yao na Jane lakini
hawakuwa na la kufanya.
Jane alipigwa sana na mama kwa kosa dogo huku
Neema na Marry walipendwa sana. Mashtaka ya Jane kwa baba ilikuwa ni kawaida.
Jane alivumilia sana. Kipigo kutoka kwa mama wa kambo kilimfanya abadilike na
kuwa mjeuri kupita kiasi. Alijua anaonewa sana, akili yake ilimfanya ajiulize
kama kweli huyu ni mama yake au la. Aliwaza sana. Akakosa raha na hata kupungua
mwili wake uliokuwa na nyama mwanzo.
Alionekana mnyonge muda wote hali
iliyomfanya aanze hata kumchukia mama ambaye hakujua kama si mzazi wake. Kwa
nini aliwapenda sana Marry na Neema, kwa nini hapewi malezi kama ya Marry na
Neema? Jane aliwaza sana.
Alisoma hadi kidato cha nne. Hakuweza
kuendelea kwa sababu ya mama yake wa kambo kumsema vibaya. Mazungumzo kati ya
baba yake na mama yake wa kambo aliyasikia. Katika mabishano hayo baba ake
alikubali Jane asisome. Alifanya hivyo ili mke wake asiondoke. Alichosema Debora
baba yake Jane hakudiriki kukataa.
“Mke wako baada ya kufariki
ulinifuata mimi. Nilikuwa na ndoa yangu nikaitoroka kwa ajili yako kwa taarifa
yako. Najua hadi leo yule mwanamume ananitafuta lakini siwezi kurudi kwake. Mi
nasema sasa ni zanu ya Neema na Marry kusoma. Jane asubiri kwanza. Mtu mwenyewe
unasema huna hela,” Debora alifoka chumbani huku Jane akisikiliza mabishano yao
kupitia katika upenyo wa mlango.
Baba yake alisafiri tena.Hakumwambia
lolote kuhusu shule. Hapo sasa Jane alipata jibu kwa nini mama yake hakumpenda.
Baba yake Jane alikuwa ni dereva wa lori ambalo lilikuwa linapeleka mizigo nje
ya nchi. Leo lingekuwa Zambia, kesho Kenya, Malawi, Msumbiji na
Congo.
Ni wakati baba yake akiwa safarini ndiyo Jane alionja joto ya
jiwe kutoka kwa mama yake huyo. Pindi baba akirudi hakudiriki hata siku moja
kunyanyua mdomo wake na kusema lolote bali mama ndiye aliyekuwa akimsema kwa
baba'ake na kuambulia kipigo kikali.
“Pole dada Jane,” Marry na Neema
walikuwa wakimpa pole mara apatapo kipigo kutoka kwa mama au pindi baba'ake
arudipo.
“Mwacheni huyo amezidi,” mama wa kambo alizidi kumshambulia
Jane. Alimpa kazi zote na kuwakataza Neema na Marry kumsaidia.
“Yeye
ndo mkubwa anatakiwa afanye kazi, nyie bado hamjaweza.Subirini
mkue.”
“Lakini mama si tunamsaidia dada Jane?” Marry ambaye ndiye
mdogo alisema.
“Nimesema nyamaza, siyo kazi zenu hizo.” Jane aliona
tabu sana. Shule hapelekwi tena na mama anamshambulia. Uhuru hakuna na hakujua
hatima yake. Baba alionekana kwa nadra sana. Alijiona kama yuko ndani ya mto
wenye mamba wengi. Aliamua asubiri hadi baba'ake atakaporudi ili amweleze,
lakini ataanzaje wakati hata baba hakumwamini. Aliamua ni bora atoroke
nyumbani.
*****
Alikuwa na miaka 20,
Jane alikuwa na akili ya kutambua zuri na baya. Alijua wazi kwamba yule hakuwa
mama yake aliyemzaa. Aliona utofauti kati yake na wadogo zake Marry na Neema,
watoto wa mama'ake wa kambo. Hawakufanana naye. Yeye alifanana na baba'ke na
watoto wale hawakufanana na baba yao, walifanana na mama yao. Hata hivyo
hakutaka kujua juu ya hilo. Yeye alikuwa ni mzuri zaidi yao. Hata neema na Marry
walimsifia sana kwa uzuri wake. Alikuwa ni mweupe mwenye mvuto sana. Ni kovu
dogo sana ambalo aliachiwa na mama'ake wa kambo karibu na sikio lake la kushoto
lakini uzuri wake haukujificha. Umbo lake lilikuwa nadhifu.
Ni siri
ambayo hakuijua. Mama yake wa kambo alimwonea wivu sana kwa sababu aliwazidi
watoto wake kwa kila jambo. Hata darasani alifanya vizuri lakini ni hila tu za
mama wa kambo ndizo zilizomkwamisha asiendelee na shule. Jane hakujali kwani
hakuelewa, kutokuendelea na shule kulimuumiza sana lakini hakuwa na la kufanya.
Mama wa kambo alisisitiza kwa mumewe kwamba ni zamu ya wadogo zake kusoma kwanza
na hivyo Jane asubiri kwanza kisha baadaye na ye ataendelea. Ni kauli hiyo
ambayo ilimfanya Jane kuamua kutoroka.
Aliondoka nyumbani jioni sana
ili awahi magari yaliyokuwa yakiondoka asubuhi sana. Jioni hiyo alipoondoka
nyumbani alienda na kulala guest moja iliyoko karibu na kituo cha mabasi ya
mikoani cha Dodoma. Neema na Marry walimtafuta sana bila mafanikio. Baba yake
alikuwa bado yu safarini nchini Zambia. Mama yake wa kambo
hakujali.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Inatosha, hakuna
kumtafuta tena, kwani ye mtoto? Anajua afanyalo. Mwacheni aende atarudi,” hiyo
ni kauli ya mama yake wa kambo akiwarudisha nyumbani Marry na Neema wasiendelee
kumtafuta dada yao Jane. Jane alifanikiwa kuondoka. Kiasi cha pesa
alichokichukua nyumbani, kilimtosha kumfikisha Dar es Salaam. Hakujua atafikia
wapi lakini hakujali. Aliona ni bora akafie huko kuliko kuendelea kuishi na mama
yake wa kambo.
Taarifa za Jane kuondoka nyumbani zilimfikia Amos.
Alirudi haraka kuhoji wapi alipokwenda. Debora alionyesha kutokujali wala
kuogopa.
“Hakuna anayejua alikoenda. Na ye ni mkubwa anajua kutafuta
acha akatafute. Angekuwa anajali nyumbani asingeondoka.” Kauli hiyo Amos
haikuifurahia. Aliingia ndani na kupumzika. Jane alikuwa
ameshaondoka.
AMOS ANAMTAFUTIA JANE MAMA. DEBORA
ANAOLEWA NA AMOS. ANAMLEA JANE KWA MAPENZI YOTE LAKINI BAADAYE ANABADILIKA NA
KUWA MBOGO KWA JANE. JANE ANATOROKA AKITAKA KWENDA DAR ES SALAAM KUTAFUTA
MAISHA.
JE ATAFANIKIWA KUFIKA NA KUPATA MAISHA
ANAYOYATAKA……
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment