Chombezo : Utamu Wa Zege
Sehemu Ya Tatu
(3)
KIASI cha pesa
alichokichukua nyumbani, kilimtosha kumfikisha Dar es Salaam. Hakujua atafikia
wapi lakini hakujali. Aliona ni bora akafie huko kuliko kuendelea kuishi na mama
yake wa kambo.
Taarifa za Jane kuondoka nyumbani zilimfikia Amos.
Alirudi haraka kuhoji wapi alipokwenda. Debora alionyesha kutokujali wala
kuogopa.
“Hakuna anayejua alikoenda. Na ye ni
mkubwa anajua kutafuta acha akatafute. Angekuwa anajali nyumbani asingeondoka.”
Kauli hiyo Amos haikuifurahia. Aliingia ndani na kupumzika. Jane alikuwa
ameshaondoka.
*****
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alifika Dar es
Salaam mchana wa saa saba. Ni saa sita tu au saba kutoka Dodoma mjini hadi Dar
es Salaam. Jane alishuka kituo cha mabasi cha Ubungo. Watu walikuwa ni wengi
sana kituoni muda huo. Alisimama akiangaza huku na huko pasipo kuelewa mahali
alipo kutokana n wingi wa watu. Alianza kuwa fuata watu walikokwenda pasipo
kujua anakwenda wapi. Kila mmoja alikuwa anajali la kwake. Hakujua aanze
kumuuliza nani.
“Samahani, naomba ni ya kwangu
nimeangusha,” mmoja wa wateja aliyekuwa amesimama dukani Ubungo, aliangusha kadi
ya benki wakati akitoa pesa kwa ajili ya kulipia vitu alivyochukua. Jane alimpa
ile kadi. Hapo hapo Jane aliamua kuuliza kwa yule dada aliyekuwa
dukani.
“Asante kwa
kuniokotea.”
“Usijali
dada.”
“Unaonekana kama unamtafuta mtu humu
ndani.” Yule dada alimuuliza Jane baada ya kumwona akiangaza huko na huko
akiangalia pa kuelekea.
“Hapana simwangalii mtu
dada, mi ni mgeni hapa. Nimepata matatizo ndo maana nimeamua kuja huku
kuhangaika na maisha. Sina pa kuishi nimeondoka leo nyumbani, nimekuja huku ili
niweze tu kutafuta maisha nipate japo chakula, naomba nisaidie dada sina pa
kwenda,” yule dada alimwangalia sana Jane na kumwonea huruma kisha
akamuuliza.
“Unaitwa
nani?”
“Naitwa Jane Amos.”
“Kwani we
unatokea wapi Jane?”
“Natokea Dodoma
Mjini.”
"Ahaa, unaonekana umechoka sana. yule dada
alifikiria kidogo. Aliona Jane atamfaa kwa kazi za nyumbani. ilikuwa ni vigumu
sana kupata mfanyakazi wa ndani. Alitokea kumpenda jane na kuamua
kumchukua.
“Twende nyumbani kwangu nitakusaidia.
Si unajua kufanya kazi za ndani?"
“Ndiyo dada,”
Jane alijibu kwa upole hadi kumfanya yule dada apate huruma zaidi. Alizidi
kuvutiwa alivyomwangalia Jane alivyo mzuri.alimwangalia juu hadi chini.
Hakuamini kama Jane alikuwa mgeni pale Dar es
Salaam.
“Haya subiri nimalize kuchukua vitu alafu
twende.”
“Sawa dada,” Jane aliitikia na kusimama
pembeni akisubiri. Alikuwa akishangaa sana huku ameukumbatia mfuko wake ulokuwa
na nguo zake chache. Gauni lake alilovaa na malapa, nywele zilizochoka kwa
kukosa matunzo na ushamba aliokuwa nao. Vilitosha kumdhihirishia yule dada
kwamba Jane alikuwa ni mgeni.
Baada ya kuchukua
vitu alivyoagiza dukani yule dada aliongozana na Jane hadi kwenye gari lake.
Alimfungulia mlango Jane na kuingia ndani kisha akazunguka na kuingia upande wa
dereva na kupiga gari moto. Walitoka nje ya geti la kuingilia kituo cha basi
Ubungo na kuelekea maeneo ya Kimara Baruti. Wakiwa njiani yule dada
alijitambulisha kwa Jane.
“Mi naitwa dada
Sara.”
“Nashukuru kukufahamu dada....umependeza
dada Sara,” Jane alimsifia Sara juu ya mwonekano wake uliomvutia. Alikuwa mweupe
kama alivyo Jane na mwenye umbo kubwa lakini lililokaa
maridadi.
“Nashukuru Jane mdogo wangu, mwanamke ni
kujithamini na kujiremba, n'na uhakika hata wewe ukijiremba utapendeza kama
mimi. We ni mzuri sana Jane.” Sara alitokea kumpenda Jane japo ilikuwa ni mara
ya kwanza kuonana naye.
“Asante dada Sara,” Jane
alishukuru.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwangu siyo mbali
tumeshafika.” Nyumbani kwa Sara hapakuwa mbali na barabarani. Walitumia dakika
15 kufika nyumbani kwake. Sara alikuwa akiishi peke yake, aliolewa na mzungu
ambaye baadaye waliachana na kurudi kwao Canada.
Sara maisha
yalibadilika baada ya kuoana na mzungu wake 'Graham'. Alimwachia Sara utajiri na
pesa nyingi zilizomsaidia kufungua biashara mbalimbali za maduka makubwa ya nguo
ambazo aliagiza kutoka nje ya nchi. Hawakubahatika kupata mtoto na hivyo mzungu
hakuona sababu ya kuendelea kuishi na Sara ambaye aliona ni
mgumba.
Hivyo aliamua kurudi kwao. Sara aliumia sana lakini hakuwa na
la kufanya zaidi ya kuendeleza maisha yake mwenyewe. Alijiuliza kwa nini Graham
hakutaka kupima ili wajue tatizo na kuamua kukimbia. Sara
hakujali.
“Karibu Jane, hapa ndiyo nyumbani
kwangu. N’takuonyesha kila kitu kilipo, jisikie poa sana,” Sara alimkaribisha
Jane nyumbani kwake, Jane alionekana kushangaa kila alionalo ndani kwa
Sara.
“Ukaoge kwanza kisha ule afu upumzike
mengine tutaongea kesho asubuhi.”
“Sawa dada
Sara.” Sara alimwonyesha Jane mahala pa kuogea na Jane aliingia na kuoga.
Alimtayarishia chakula na wote wakala na kisha akamwonyesha chumba ambacho
angepumzika hadi
asubuhi.
*****
Asubuhi
Jane aliamka akionekana mchangamfu sana. Sara alifurahi sana kumwona katika hali
ile. Jane ndiye alikuwa wa kwanza kuamka na kwenda kuketi katika sofa akimsubiri
Sara aamke. Sara alimwonyesha sehemu ya kunawia uso. Sara alitayarisha chai na
wote wakaanza kunywa.
“Jane, ulisema kwenu
Dodoma?”
“Ndiyo dada
Sara.”
“Ulikuwa unaishi na nani
huko?”
“Baba na mama wa kambo, mama angu
alishafariki dunia nkiwa mdogo.”
“Ooh, pole sana
Jane. Ikawaje ukaondoka huko nyumbani?”
“Ni kwa
sababu ya mama angu ninayeishi naye sasa hivi. Mambo yake yamenishinda n'kaamua
niondoke.”
“Baba naye akasemaje au alikuwa haoni
maana najua hayo ni mateso tu ya huyo
mama.”
“Nimetoroka bila kumwambia yeyote, baba
anasafiri na kutuacha nyumbani hata mwezi,” Jane aliendelea kumwelezea Sara
matatizo yaliyomfanya apachukie nyumbani na kukimbilia Dar es
Salaam.
“Sasa ulijua huku unakuja kukaa kwa
nani?”
“Hapana sikujua dada Sara, hivyohivyo tu,
bora nife huku kuliko kubaki nyumbani na mateso ya yule
mama.”
“Pole sana Jane, matatizo yako hayapo
tufauti na yangu kwani hata mimi nimelelewa na mama wa kambo ambaye alisababisha
hadi nkatoroka na kuanza maisha yangu binafsi hadi maisha yangu yalivyokuwa
mazuri. Sara alimwelezea Jane maisha aliyoyapitia hadi akafikia hapo
alipo.
“Wanaume ni watu washenzi sana Jane, hawana
mapenzi ya kweli kama jinsi wanawake wengi wanavyojali. Mwanamume akikupenda
utamjua na ambaye anakuchezea tu utamjua kama utakuwa mwangalifu. Usitegemee
mwanamume akuambie tu nakupenda alafu awe ni wa kuhitaji tu kila wakati uwe naye
kitandani au kwenye starehe. Mwanamume anayekupenda siku zote atakujali na
kukuthamini kwa kuona kwamba huyu naye ni mwenzangu na anastahili heshima kama
mimi ninavyojiheshimu.”
“Dada Sara, sasa utamjuaje
mwanamume wakati ndiyo anakufuata?”
“Ukiwa huna
tamaa na mali wala fedha na starehe, utampata tu mwanamume anayekupenda kwa
dhati na atakayekuheshimu na kukulinda. Pia atakuwa na faida kwako katika malezi
ya familia mtakayoianzisha.”
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ina maana wanaume
wengi ni waongo sana?”
“Jane mdogo wangu, mimi
niliolewa na mzungu, lakini sikuonja penzi lake zaidi ya kuniona mimi ni mgumba
bila ya yeye kwenda kujichunguza pia. Alinioa tukakaa miaka miwili lakini
hatupati mtoto. Ni mwaka jana ndiyo aliondoka na kuniachia hizi mali na ye
kurudi kwao Canada. Sitamani tena wanaume kwa jinsi alivyonifanyia yule mtu.
Hakuthamini mawazo yangu. Nilitaka na yeye akachunguzwe tujue tatizo lakini
hakukubali na kuniona mimi ni mgumba. Sikujali kabisa, kwa sababu aliniachia
mali, niliamua tu nijiendeleze mwenyewe nikajimilikisha kila kitu na ndiyo mpaka
sasa naishi peke yangu hapa.”
“Nimekuelewa sana
dada Sara. Sitaweza kuharibu mwili wangu kwa kutembea na wanaume. Nitajitahidi
kujitunza hadi nitakapompata mwanamume atakayekuwa tayari kunijali na
atakayenipenda kwa dhati,” Jane alikuwa akisema hayo huku akiondoa vyombo mezani
na kuvipeleka
jikoni.
*****
Baada
ya kujitayarisha kwa muda, Sara na Jane walitoka na kuelekea mjini. Jane
alipendeza sana. nguo alizopewa na Sara zilimpendeza na kuonekana mrembo zaidi.
Walikuwa kwenye gari aina ya Toyota Rav4. Njiani Jane aliangalia huku na huko
akiliangaza jiji kwa mara ya kwanza. Wakiwa maeneo ya Magomeni, Sara alikuwa
akimwonyesha Jane na kumwelekeza taa za barabarani zilivyokuwa zikifanya kazi.
Ghafla alishindwa kuumudu usukani na almanusura amgonge kijana aliyekuwa akivuka
barabara.
“Dada Saraa! Jane aliita kwa nguvu baada ya kumwona Sara
akielekea kumgonga yule kaka. Haraka alifunga breki na kumgusa kidogo. Yule
kijana hakuumia. Sara alipaki gari lake pembeni na kushuka na kumfuata. Jane
naye alishuka na kumfuata Sara ili ajue kitakachoendelea.
“Samahani
kaka yangu. Sijakuona. Umeumia?” Sara alitoa noti ya shilingi elfu kumi na
kuishika mkononi na kumuuliza yule kijana kama ameumia.
“Hapana dada
angu, sijaumia. Ila uwe makini sana.” yule kijana alisema huku akivuka barabara
kuelekea kibandani kwake.
“Pole sana kaka,” Jane alimpa pole yule
kijana.
“Nashukuru bibie,” Sara alimkabidhi yule kijana ile noti ya
elfu kumi.
“Hapana dada, usijali. Kikubwa ni uzima nashukuru Mungu
sijaumia kwani ningeshindwa hata kuipata hiyo noti kwenye biashara zangu,
nashukuru, asante sana,” yule kijana aliikataa ile noti na kushukuru kwa kuwa
hakupata majeraha.
“Hapana, naomba tu uichukue. Mi nakupa
tu.”
“Haya, asante sana dada angu. Nawatakia safari
njema.”
“Tunashukuru.” Jane alisema huku akimwangalia sana yule
kijana. Alidhani kutokana na kugongwa angeleta fujo kana baadhi ya vijana
wanavyofanya ikiwemo na kuiba kwenye magari na kumshambulia dereva
aliyesababisha ajali. Haikuwa hivyo kwa yule kijana. Alichukua ile noti
aliyopewa na Sara na kuiweka mfukoni kisha kuwaaga na kuondoka. Watu nao
walitawanyika.
Sara na Jane waliingia ndani ya gari na kuondoka.
Walikuwa wakiogopa sana baada ya watu kujaa pale. Walikuwa wakielekea Kariakoo
ambako maduka ya Sara yalipatikana. Sara alimpitisha katika duka moja baada ya
lingine na kumtambulisha kwa wafanyakazi wake kwamba ni mdogo wake. Wengi
walimsifia kwa uzuri wake. Walimpenda sana Jane.
Sara alimzungusha
maduka ya nguo na kumnunulia nguo nzuri za kutumia. Jane alifurahi sana.
Alijihisi mpya katika dunia. Alitamani angewahi zaidi kuja Dar es Salaam ili
ajue mengi.
Jane alikuwa akiwaangalia wapitanjia na watu waliokuwa
wakiingia dukani kuulizia bidhaa na kuchagua. Yeye alibaki kimya kusikiliza
wateja wakizungumza na wauzaji wa duka hilo. Alikuwa akitazama nguo zilivyojaa
ndani ya duka. Alitamani sana kuwa na duka kama hilo.
Sara alimaliza
mazungumzo yake na wafanyakazi na kuondoka na Jane. Waliendelea kuzunguka mjini
na kumwonyesha Jane sehemu mbalimbali za jiji kama Posta, baharini na maeneo
mengi ya kuvutia. Jane alifurahia sana safari
yao.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****
Ilikuwa
imepita mwaka mmoja tangu Jane alipoondoka kwao. Maisha ya yake yalianza
kubadilika. Alipendeza. Alizidi kuvutia na kuonekana mrembo zaidi ya alivyotua
Dar es Salaam kwa mara ya kwanza. Sara alimchukulia kama mdogo wake na siku zote
Jane alimpenda Sara kama dada yake wa kuzaliwa pamoja. Kila mmoja alijivunia kwa
mwenzake. Hakika walishibana. Alilosema Sara Jane hakukaidi kufanya. Alimheshimu
sana Sara kwa kila kitu. Alijua bila yeye asingefika hapo alipo. Alimshukuru
kila siku pasipo kujaribu kufanya kile ambacho kingemfanya Sara
achukie.
Sara alichoka kukaa bila ya kuwa na mume. Alishawahi kuongea
na Jane kuhusu mipango yake ya mbele lakini hakuwahi kumtajia mpango wa kuolewa.
Sasa alihitaji mtu wa kuishi naye ili amfariji na apate ladha ya
mapenzi.
Sebastian Ndauli alikuwa ni mwanamume pekee aliyemvutia Sara.
Alikuwa ni mfanyabiashara pia ambapo mara nyingi walisafiri pamoja. Sara aliweza
kumjua na kufahamu mengi kuhusu Sebastian. Hakika aliona huyo ndiye angekuwa
mwanamume pekee ambaye angeweza kuishi naye.
Aliamua kumwelezea Jane
juu ya uhusiano wake na Sebastian toka wafahamiane miaka miwili iliyopita.
Alimwita Jane akiwa jikoni na kumwambia.
“Mdogo wangu Jane, ni mwaka
sasa umeisha tangu tuwe wote.”
“Ndiyo dada,” Jane
aliitikia.
“Hivi karibuni nitamleta mtu wa tatu.”
“Nani huyo
dada Sara,” Jane aliuliza huku akinawa mikono baada ya kumaliza kuosha vyombo.
Alifunga maji na kuketi katika sofa ili kumsikiliza Sara.
“Ni mchumba
wangu nataka umjue, atakuja hapa siku moja.”
“Dada Sara unataka
kuolewa?” alihoji Jane kwa huzuni.
“Ndiyo Jane, kukaa peke yangu
inatosha sasa nataka niolewe na mwanamume ambaye nimempenda na ni mwaminifu. Ni
mfanyabiashara mwenzangu ambaye kwa kweli ninaweza nikasema ndiyo chagua
langu.”
“Dada Sara mi nakuaminia sana. Natamani sana niwe kama wewe
dada Sara.”
“Usijali mdogo wangu, tupo pamoja. Nitahakikisha unakuwa
kama mimi, umeshamaliza kuosha vyombo?”
“Ndiyo dada,” Jane alimjibu
kwa tabasamu. Umlete nnyumbani dada nimwone.”
“Usijali mdogo wangu.
Atakuja siku yeyote na utamjua.”
“Sawa dada.”
“Ahaa, sawa,
leo tunatoka, sema nikupeleke wapi tukatembee?”
“Aaah, dada Sara, kila
wikiendi tunatoka, leo tukae nyumbani tu.”
“Hapana Jane, mi sitaweza
kukaa hapa hadi jioni, n’takuacha wewe mi n’tatoka.”
“Mmmh! Sitabaki
mwenyewe, na mi n’tatoka na wewe, n’takuwa mpweke sana.”
“Haya sema
unataka twende wapi leo?”
“Napenda twende ufukweni kama siku ile
tukale urojo,” Jane alifurahia sana siku ambayo ilikuwa ni mara ya kwanza
kutembea katika fukwe za Bahari ya Hindi. Alitamani kurudi tena na tena. Sara
alimpeleka sehemu alipojisikia kwenda kila wikiendi. Jane aliuzoea sana mji na
kuwa karibu sana na Sara wakati wote.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****
Siku
hiyo Jane alikuwa mwenyewe nyumbani. Sara alikuwa akijivinjari na Sebastiani.
Aliitamani hiyo raha kwa muda mrefu pasipo kuipata baada ya mzungu kurudi kwao.
Ni Sebastiani pekee aliyeweza kumfanya ajisikie mpya katika dunia ya mapenzi.
Sara alionekana kuzidiwa na hali aliyokuwa nayo.
Hakuupa muda nafasi
upite usiku huo kutokana na mihemko yao. Ni usiku uliojikoleza na penzi zito la
wawili hao. Hakuwahi kuskia hali hiyo tofauti kwa muda mrefu. Sasa haki yake
anaipata. Tena kwa mwanamume aliyediriki kumvulia nguo na kumkabidhi kila
kilicho chake akifanye anachokitaka. Mwanamume aliyempenda na
kumjali.
Sebastian alifanya kile alichokijua. Alimshika kila mahali
Sara ambaye na yeye alirudisha mapigo kwa ufundi wake. Aliutumia vizuri ulimi
wake na kinywa katika kuiburudisha nafsi ya Sebastian na kumlegeza kwa maneno
matamu. Wote walifurahia siku hiyo. Ya kwanza kukutana miili yao kama
wapenzi.
Sara alifurahia zaidi. Upole wa Sebastian alihisi haupo
tena. Hakuwa Sebastian yule aliyemzoea. Si mwongeaji sana bali wa vitendo. Kweli
alitenda. Akatenda vile alivyokaribishwa atende. Sara alifurahi
sana.
JANE ANAONYESHWA JIJI. ANAFURAHIA KUANZA
MAISHA MAPYA AKIWA PEKE YAKE KUWAPISHA SARA NA SEBASTIAN.
JE NINI
KITAMTOKEA AKIWA
MWENY
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment