Search This Blog

Monday, October 24, 2022

SHEMEJI MONICA - 5

 





    Chombezo : Shemeji Monica

    Sehemu Ya Tano (5)



    James alibaki pale akiwa na wasiwasi mwingi maana hakujua nini kitafuata baada ya Julieth kufika nyumbani kwao. Tayari mama yake alikuwa amemtafuta na alionekana kuwa na wasiwasi kwa kutomkuta pale kituoni ilhali alijua fika kuwa mwanae alikuwa na James, bila shaka hofu ya mama yake Julieth juu ya uhusiano wao itakuwa imeongezeka. "Mama yake akimuona katika hali hii lazima atajua mimi ndo nimehusika, sijui nini kitafuata", aliwaza James na akili yake ikamwambia pale hapakuwa mahali salama tena kuendelea kuwepo maana Julieth angeweza kumleta mama yake kama angebanwa vizuri. Akaondoka haraka kuelekea kule nyumbani kwa kaka yake ambapo hawakuwa wakipajua.

    ********************

    Kwa namna moja au nyingine James alikuwa akijutia maamuzi yake, matamanio yake yalimuweka katika mazingira mabaya sana wakati ndio kwanza alikuwa anajaribu kuonja maisha mazuri baada ya muda mwingi wa maisha yake kuutumia shule na shamba kule kijijini.

    " James naomba leo usiende kazini, lazima mama atakuja kukutafuta maana jana alinitaka kumleta kwako nikadanganya sipajui", ulikuwa ni ujumbe ambao James alikutana nao kwenye simu yake asubuhi alipoamka, ujumbe huu ukitoka kwa Julieth.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ujumbe ule ulimshitua saa James, moja kwa moja akajua kuwa mambo yalikuwa yamekwisha haribika tayari. Ujumbe ulijieleza vizuri tu kuwa hakutakiwa kufika katika eneo lake la kazi maana mama yake Julieth angeweza kumpata mara moja kama angemtaka. Hivyo akaamua kubaki pale kwa kaka yake ambapo alikuwa na uhakika kuwa hata Julieth tu hakupajua, sembuse huyo mama yake??...

    Mida ya saa tatu asubuhi kaka yake James akatoka na mtoto wake ambaye alikuwa anampeleka hospitali kutokana na maumivu ya jino, pia walipanga kupitia mjini kwaajili ya kufanya shopping maana muda wa Peter kurudi shule ulikuwa umekaribia. James akabaki nyumbani na shemeji yake tu ambaye alikuwa wakiendelea na shughuli za usafi wa asubuhi na James akajifungia chumbani mbapo alijaribu kulala lakini usingizi haukuwa karibu, akatoka mpaka sebuleni ambapo alikaa akiangalia luninga, huku akiwa na mawazo tele kichwani mwake. "Shem leo huendi kazini?" Aliuliza Monica baada ya kuwa amepita maraka kadhaa pale sebuleni na akawa anamuona James akiwa katika mkao ambao ulionesha kuwa hakuwa na dalili ya kutoka hivi karibuni ingawa muda wake wa kwenda kazini ulikuwa umetimia. "Hapana leo siendi" alijibu kifupi James, kisha akajifanya kama alikuwa makini sana kufuatilia kilichokuwa kinaendelea kwenye luninga ilhali ukweli ni kuwa alikuwa haoni chochote.

    "Kuna nini kwani?" Aliendelea kuhoji Monica ambaye alionekata kutaka maongezi yasiishe kwa sababu zake mwenyewe. "Najisikia uchovu tu leo" alijibu James huku akihitahidi kuyaepuka macho ya Monica ambayo yalikuwa yametua usoni kwake kwa muda mrefu sasa. "Mficha maradhi kifo humuumbua, hebu nambie nini kinakusibu mpenzi" alisema Monica huku akikaa karibu kabisa na James. James akajikuta anashindwa kudanganya zaidi, alitamani kupata mtu wa kuzungumza naye juu ya mkasa wake, hivyo akamuelezea Monica kwa kifupi. "Huyo msichana ana umri gani?" Alihoji Monica baada ya kupewa mkasa ule. "Ana miaka 17" alijibu James. "Mmmmh bado ni mdogo sana, kama wakiamua kwenda mbali itakuwa balaa" alisema Monica. Maneno yale yalikuwa yamoto sana masikioni mwa James, sio kama hakuwa akilijua hilo ila alitamani kupata maneno ya faraja. Monica aligundua kuwa alikuwa ameharibu, hali ya James ilibadilika na kuwa mbaya zaidi toka atamke maneno yale, uoga ulijidhihirisha machoni kwake bila kificho. "Ila hakuna jambo gumu mjini, niachie mimi nitalimaliza hili" alisema Monica, maneno haya angalau yalileta faraja kwa James ingawa hakuona ni kwa namna gani shemeji yake yule angeweza kulimaliza janga lile.

    Monica akajitahidi kumchangamsha shemeji yake kwa matani ya hapa na pale ili aweze kurudi kwenye hali yake, na kwakiasi fulani akawa amefanikiwa. Lakini Monica hakuishia hapo, akaendelea na utundu mwingine ambao haukukawia kumteka James kwenye hisia za kimahaba, kila James alivyojaribu kuepuka kuelekea alikokuwa akipelekwa ndivyo Monica alivyozidisha ushawishi, na alijua fika James hakuwa na ujanja mbele yake. Ndani ya dakika chache Monica akawa ndiye bosi, James alikuwa akifuata maelekezo yake yote. Tayari Monica alikuwa amemvua fulana akaitupa mbali, kisha akaanza kutalii kwenye mwili wake kwa kutumia ncha ya ulimi wake. James alikuwa akipaparika kama vile alikuwa anachinjwa, ghafla akasikia kitu cha baridi kikigusa sikoni kwake, hapa James alijitahidi sana kujizuia asipige kelele, akajitahidi kumzuia Monica asiendelee na kile alichokuwa akikifanya lakini hakuwa hata na nguvu ya kunyanyua kijiko cha chakula, akakwama na kumuacha Monica aendelee kumsulubu atakavyo, hata hakujua saa ngapi Monica alimvua pensi aliyokuwa amevaa, alijikuta tu akivuliwa boxer na mshiranga wake ukikamatwa vizuri, kisha kupotelea kinywani mwa Monica.

    Mara mlango ulafunguliwa na Paul, kaka yake James akaingia akiwa ameambatana na mwanae. Monica akaacha haraka kile alichokuwa anafanya lakini alikuwa amechelewa, kila kitu kilikuwa kimeonekana. James alikuwa katika hali mbaya zaidi maana alikuwa uchi wa mnyama, akachukua mto wa kochi na kuziba kiungo chake muhimu, kisha akabaki akiwa ametahayari, uoga ulijidhihiri machoni mwake. "James wewe ni wakunifanyia hivi?" Alihoji Paul huku akitetemeka kwa hasira, macho yake yalikuwa yanaangaza huku na huku kama ambaye alikuwa anatafuta kitu cha kumpiganacho. "Nisubiri nje Peter" alisema Paul kumwambia mwanaye ambaye alitii, kisha akavamia kistuli cha kioo ambacho kilikuwa pale sebuleni na kukirusha kwa James ambaye alikiona akakikwepa na kutoka haraka pale kwenye kochi. Paul akarudi mpaka ulipokuwa mlango, akaufunga kwa funguo na kuziweka mfukoni mwake, kisha akamrudia James. "Sasa leo tutagawana majengo ya serikali, kenge usiye na shukuruani wewe" alisema Paul akimsogelea James tayari kwa mapambano.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Paul usifanye hivyo please, mwenye makosa ni mimi" alisema Monica huku akimvuta Paul ili asiende kumshambulia James. "Pumbavu!! Wewe ndo usiongee kitu kabisa" alisema kwa ukali Paul,huku akimnasa Monica kofi zito lililompeleka chini. "WEWE UNAFANYA MANGAPI? MBONA MIMI SISEMI?" Alihoji Monica kwa sauti ya ukali huku akilia, lakini Paul hakumsikiliza, shida yake ilikuwa James ambaye tayari alikuwa ameokota pensi yake lakini hakupata wasaa wa kuivaa, akawa anakimbianayo kuzunguka meza iliyokiwepo pale sebuleni ili kumkwepa Paul ambaye alidhamiria kumdhuru.



    Wakati kukuru kakara ile ikiendelea ikasikika sauti ya mlango kugongwa, sauti ile ilizidi kupanda kadri dakika zilivyozidi kwenda. Paul akasitisha zoezi lake na kusimama akisikilizia kujaribu kujua nani alikuwa anagonga kwa kasi ile.

    Monica akasogea na kuchungulia kupitia dirishani, “ni polisi” alisema kuwajuza wenzake ambao bado hawakuwa wakijua juu ya mgongaji wa mlango ule. Kimya cha ghafla kikatawala, wote walikuwa kwenye mshituko mkubwa. “MNAFUNGUA MLANGO AU TUVUNJE?” sauti kali kutoka nje ikahoji na kumgutusha Paul ambaye alitoa ufunguo mfukoni mwake na kuelekea kufungua mlango akimuachia James wasaa wa kuvaa nguo zake harakaharaka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nini kinaendelea hapa?” Alihoji mmoja wa askari polisi wawili ambao waliingia ndani, mmoja wao alikuwa na silaha ya moto. Swali lile halikujibiwa hivyo askari wale wakaamua kuendelea na jambo ambalo liliwapeleka pale, “tuna shida na James” alisema askari ambaye hakuwa amebeba silaha, James akajitambulisha kwamba alikuwa ni yeye, askari yule akatoa pingu na kuanza kumfunga huku akimwambia kuwa alikuwa chini ya ulinzi. James aliishiwa nguvu, akakosa hata swali la kuhoji, akatii maelekezo ya askari wale ambao walimtaka kuelekea kituoni. Monica alikuwa tayari amejua kilichopelekea James kukamatwa lakini Paul bado alikuwa gizani, japo hakuweza kuhoji chochote, alibaki akiwa amepigwa na bumbuwazi wakati James akiondoka na polisi wale.

    “Nilikuonya kistaarabu kabisa lakini hukutaka kusikia, sasa tusilaumiane kwa maamuzi ambayo nitachukua” alisema mama Julieth ambaye walimkuta kule kituoni. James akaingizwa mahabusu akimuacha mama Julieth akiwa anaongea na askari wale. “Kwahiyo mama tunamfungulia kesi?” Aliuliza askari ambaye alionekana kupokea maelekezo ya nini afanye ama nini asifanye kutoka kwa mama Julieth. “Ngoja kwanza, mzee amesema tumaubirie. Ataingia usiku” alisema mama yake Julieth akimtaka askari yule kungojea baba yake Julieth afike kutoka ughaibuni ambako alikuwa akifanya kazi.

    Mara simu ya mama Julieth ikaita, ilikuwa ni namba ngeni kwenye simu yake. Akaipokea na kupata habari ambazo zilimchanganya na kumfanya aondoke pale kituo cha polisi mbio mbio.

    *******************************************

    Baba yake Julieth alipotua tu akakutana na habari ambazo hazikuwa nzuri hata kidogo, Julieth alikuwa mhututi hospitali baada ya jaribio la kujiua. Moja kwa moja akaenda hospitali ambapo alimkuta mkewe akiwa amechanganyikiwa akisubiri kuona kama jitihada za madaktari zingetosha kuokoa maisha ya mwanae, wakaungana kusubiri pamoja huku wakiendelea kumuomba Mungu anusuru maisha ya mtoto wao wa pekee.

    ******************************************

    “Hali ya mgonjwa inazidi kuimarika, tumemtundikia drip ya maji ili kuweza kupunguza kiasi cha sumu ambacho tayari kipo kwenye mzunguko wa damu, itachukua muda kidogo hivyo mngeenda kupumzika tu” yalikuwa maneno ya daktari ambaye alikuwa akimshughulikia Julieth. “Tafadhali docta, fanya kila uwezalo mwanangu apone” alisema baba yake Julieth ambaye alionekana kuchanganyikiwa. “Hali yake inazidi kuboreka, tumuombe Mungu tu” alisema daktari yule kwa kifupi kisha akawaacha na kwenda kuendelea na majukumu yake.

    ********************************************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kule kituoni majira ya saa kumi za jioni James akatembelewa na shemeji yake, Monica, ambaye alijaribu kumdhamini lakini ikashindikana. “Tuhuma alizonazo mtuhumiwa ni miongoni mwa tuhuma mbazo hazina dhamana, hii ni kesi ya ubakaji” alielezea mkuu wa kituo ambaye Monica aliomba kuonananaye baada ya askari aliyekuwa zamu kimnyima dhamana. “Jambo unaloweza kumsaidia ni kumtafutia wakili mzuri tu, maana kama atashindwa kesi hii mtuhumiwa atahukumiwa miaka mingi sana”. Maneno yale yalimkata maini Monica, akakaa kimya kwa muda, kisha akapata cha kusema. “Naweza kumuona?”, hili halikuwa gumu kwa mkuu yule wa kituo, akaagiza Monica apelekwe ambapo angeweza kumuona James. James alipigwa na butwaa kuona Monica alidiriki kumfuata tena mpaka kule baada ya kuwa wamefumaniwa muda mfupi uliopita. ” kaka anajua kama umekuja huku?” Alihoji James. “Sina mpango tena na kaka yako, wala sina ndoa naye tena, sasa nafanya ambacho najisikia” aijibu Monica na kumfanya James azidi kuchanganyikiwa, Paul alikuwa amechangia kwa kiasi kikubwa kumfikisha ambapo alikuwepo kielimu, alijiona mkosaji sana kumvunjia ndoa yake. “Shem nakuomba ufanye kila uwezalo kuhakikisha hamuachani, hivi nani atanielewa hata huko nyumbani wakisikia mimi ndo chanzo cha kuachana kwenu?” Aliongea kwa uchungu mkubwa James ambaye aliona kama maisha yake yalikuwa yameharibika tayari.

    “Sina mpango wa kurudi kwa Paul, mimi nakupenda wewe James. Mpango wangu ni kuhakikisha unatoka kisha tukaishi mbali, ambako hatutopata usumbufu wa mtu yeyote” alisema Monica..



    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog