Search This Blog

Monday, October 24, 2022

PLAY GAL (TINA ZOA ZOA ) - 5


Chombezo : Play Gal ( Tina Zoa Zoa )Sehemu Ya Tano (5)“...Hivi jamani nikupe nini ili uridhike mwanaume wewe..? eti Baba Jose..? Kwanini unanifanyia mimi hivi..? kitu gani hujaridhika kutoka kwangu..? kitu gani sikupi mie..?” Nilishusha pumzi chini huku macho yangu nikiyatoa kwa tahamaki nikiendelea kumshuhudia yule Mama akilalama. Kumbe yule mzee niliokuwa nafanya nae mapenzi alikuwa ni mume wake wa ndoa. Na kwa sasa alikuwa kama kishamfumania akiwa na mimi. Aliendelea kumlalamikia sana mume wake huku akimshika shingoni vilivyo. “..Lakini mama Jose..?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “..lakini nini..? hivi kweli baba Jose ndio mchezo wako huo unaofanyaga..? lini utakuwa mume wangu..? kama ni watoto tunao wanne, badala tupange ni jinsi gani tutawatunza na kuwasomesha we ndio kwanza unahangaika nakutangatanga na visichana vidogo.. embu inuka twende nyumbani huko..?” Bado yule Mama alionekana kuwa na hasira iliyoambatana na kwikwi kali kwani kila muda alikuwa akihema kwa shida huku akiishiwa pumzi kwa hasira ambayo alikuwa nayo ya kumfumania mume wake. Akiwa bado anagombana na mume wake mara mwanangu Adrian akaanza kulia pale chini yao. “..tobaa..!!!, na tena kumbe binti mwenyewe ana mtoto mchanga..? wewe baba Jose nini unafanya jamani..? twende..!!, twende..!!, twende nyumbani nimesema..? Nilisogea mpaka karibu yao kiuwoga woga huku nanyata mithili ya simba anaponyemelea kitoweo nakumchukuwa mwananagu Adrian nakuanza kumbembeleza huku nikiwaacha yule Mama na mumewe wakiendelea kuvutana. Waliendelea kuzozana tena kwa sauti ya juu nakusababisha watu waanze kuchungulia madirishanai huku wakipiga kelele za uchochezi. Baada ya muda kama wa dakika tano nzima za ugomvi na kuvutana huku na kule ndipo wakaondoka zao wakiniacha nikiendelea kumbembeleza mwanangu Adrian ambaye kwa muda huu ni kama alikuwa akizidisha kulia. Baada ya muda kama wa dakika kumi ndipo mwanangu Adrian akaanza kunyamaza nakunifanya nijisikie faraja tele moyoni. Tabasamu aliokuwa akiendelea kulitoa ni wazi kuwa alikuwa mtoto msikivu anapobembelezwa. Niliinua mkono wangu wa kulia nakuanza kumpapasa maeneo ya shingoni, mpaka usoni mwake. Alinishtua sana kwani mwili wake ulionekana wamoto sana. Kamasi za majimaji zilizokuwa zinamtiririka kupitia puani mwake ni wazi zilionesha kuwa anaumwa. Nilimvua nguo zake haraka haraka nakuanza kumuogesha. Nikiwa bado namuogesha mara tena nikasikia kama mtu anabisha hodi. Mwanzo nilionesha kusita lakini kadri nilivyokuwa naendelea kumuogesha mwanangu Adrian ndivyo na yule mtu alizidi kupiga hodi. Nilimtoa kwenye beseni lake la kuogea nakumuweka kitandani nakuelekea mlangoni kujua ni nani alikuwa anapiga hodi. “Mama Adrian..? Mambo..? Samahani unahitajika na meneja yupo mapokezi..?” “..sawa Salma.., mwambie nakuja sasa hivi..?” Alikuwa ni rafiki yangu wa humu ndani ambaye nayeye ni mfanyakazi na yupo mapokezi na kwa muda huu alikuwa amekuja kuniiita kuwa nahitajika na meneja. Ile hali yangu ya uwoga ilianza kunitawala tena, mwili wangu wote uliishiwa nguvu nakujihisi kama ile hali ya kutetemeka imenianza tena kwani safari hii nilikuwa natetemeka sana maeneo ya mdomoni na nywele kunisisimka. Nilichokifanya nilivaa nguo zangu haraka haraka na kisha kumchukuwa mwanangu Adrian nakuelekea mpaka mapokezi ambapo ndipo alipokuwa meneja akiniita. “..naam bosi wangu nasikia unaniita..?” “..ndio nakuita, hivi mama Adrian kwanini unataka kutuchafulia jina hapa mtaani..?” “..kwani vipi meneja..?” “ina maana hujui kitu ulichofanya muda si mrefu..?” “..anhh..!!, unajua meneja ni kwamba..” Kabla sijaanza kumsimulia meneja. Alinikatiza kuendelea kuongea neno lolote. Sura yake ilikuwa imembadilika na hakuwa kama meneja yule wa awali niliomzoea kwani alionekana dhahiri kuchukizwa na kile kitendo cha mimi kufumaniwa na yule Mzee. “..sitaweza kuvumilia ujinga unaoendelea kufanya kila siku humu ndani. Katafute gesti nyingine za kufanya huo ujinga hapa kuanzia sasa hatukuitaji na mambo yako ibilisi we..?” “..Jaribu kunisikiliza na mimi basi meneja..?” “..hapana..?, hapana nimesema siwezi kukusikiliza tena wala kukuelewa kwa namna yeyote zaidi ya kukuona umeenda huko chumbani nakutoa kila kilicho chako na ufunguo wangu nauhitaji ndani ya dakika kumi, umenisikia na kunielewa..??” Nilikuwa sina tena ujanja Tina mimi kwani pamoja nakumpigia magoti meneja huku nikitoa machozi ya hapa na pale lakini haikusaidia chochote wala kunielewa. Inaonekana kile kitendo cha mimi kufumaniwa kilimuuma sana nakuona kuwa amechafuliwa jina na atakosa wateja. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuelekea tena chumbani nakukusanya kila kilichokuwa changu. Sikuwa na begi lakuwekea nguo hivyo nilichukuwa nguo zangu na za mwanangu Adrian kisha nikaziweka kwenye fuko kubwa la lambo, na vitu vidogo vidogo kama chupa ya maziwa na vijipodozi niliviweka kwenye ule mkoba wa kipindi kile nilioondoka nao kutoka kwa mama yake na huyu mtoto. Nilirudi mpaka pale eneo la mapokezi nilipomuacha Meneja. “..funguo wenu huu hapa..?” “…Nenda huko hatukuhitaji tena hapa Malaya uliokubuhu wee..?” Niliumia sana moyoni kwa maneno aliokuwa akinitolea yule meneja nakujiona kuwa sifai na sina hata haja ya kuishi hapa duniani. “..Adrian..? najua wewe huna hatia lakini sina jinsi inabidi nikuhifadhi nakukulea mpaka utakapokuwa kwa hali yeyote ile. Kubali vitu vyote utakavyokutana navyo ukiwa na mimi mpaka utakapokuwa mkubwa..?” “Nilijikuta naongea na mwanangu Adrian japo alikuwa haelewi ninachokiongea kwakuwa bado mchanga sana lakini alitoa tabasamu nakunifanya nimbusu paji la usoni mwake nakuelekea kituo cha dala dala huku nisielewe ninapoelekea. “..nitaishi tu, Mungu ndio ajuaye..!” Nilijikuta naongea peke yangu huku mwanangu Adrian nikimuweka vizuri kwani alikuwa ameshalala. Ilinichukuwa zaidi ya dakika karibu kumi nzima nikiwa nimezubaa peke yangu kituo cha daladala huku nikifikiria nitaelekea wapi na huyu mtoto. Akili yangu ikawa si ya Tina yule wa zamani bali ni ya Tina mlezi tena yule wa mlezi wa katoto kachanga ‘Adrian. Hatimaye nikaingia kwenye daladala iendayo mwananyamala na bado nilikuwa sijielewielewi. “…Sitakuacha na wala sintokuwa msaliti kwako mwanangu Adrian..!!” Bado niliongea peke yangu nilipoingia kwenye daladala. Baadhi ya abiria karibu wote ndani ya daladala walikuwa wakinishangaa sana na nadhani nikutokana na kuonesha sura ya huzuni na kuchanganyikiwa kwa mawazo juu ya mwanangu Adrian. Safari ya kutokea Temeke na kuelekea Mwananyamala ilianza. Njia nzima nilikuwa mtu wa mawazo tu haswa ni jinsi gani nitaishi huko niendako. Kuna wakati nilifikiria hata kwenda pale chuo kwa rafiki yangu Aisha japo anipe ushauri wa huyu mtoto na maisha yangu kwa ujumla lakini nikaogopa kwanza kuchekwa na pili mara ya mwisho nilipata uchizi nikiwa pale chuo hivyo kama wataniona na mtoto mdogo watanishangaaa sana na kunicheka kwa dharau. “ahh..!! liwalo na liwe bwana…!!, konda nishushe hapo magomeni hospitali..?” Nilijikuta naghairi kufika Mwananyamala ambapo ndio mwisho wa daladala hii na ndio malengo yangu kwa ujumla japo sikujua naenda kwa nani. Hivyo akili na mwawazo yangu ya ghafla yakabadilisha mwelekeo mzima wa safari yangu. Na kwa sasa nikashuka pale magomeni hospitali na mizigo yangu kisha nikaelekea upande wa pili nakupanda daladala ziendazo Posta kwa lengo la kushukia pale chuo cha biashara CBE ambapo ndipo nilipokuwa nasoma chuo na rafiki yangu kipenzi Aisha. Saa ya kwenye daladala ilikuwa jibu tosha kuwa inaelekea saa kumi na moja ya jioni. Haikunichukuwa muda sana kwani mwendo wa kutoka Magomeni hospitali mpaka chuo cha biashara CBE ni kama dakika saba hivyo nilishuka huku nambembeleza mwanangu Adrian mgongoni. “..twende mwanangu.., hapa ndipo nilipokuwa nasoma..??” Tayari akili yangu ilikuwa ni sawa na ya mwanangu Adrian kwani kuna kipindi nilikuwa nikiongea naye utadhani kuwa ananielewa nakunisikia kwa ninachokiongea. Mshipa wangu wa aibu niliuweka pembeni kwa muda nakuvaa sura ya mbuzi tena yule beberu kabisa. Nilijitwisha fuko langu la lambo kichwani huku kwenye kwapa nikiuweka mkoba wangu vilivyo na mgongoni nikimbeba mwanangu Adrian tena akiwa amepitiwa na usingizi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “..embuuu…!! embuu…!!, hivi tulikuwa tunakaa nae bweni lipi tena..?? ok..!! ok, nimeshakumbuka ghorofa G namba 13..” Chuo chote cha biashara CBE kilikuwa kimya sana na najua tu ikiwa hali kama hii ni dhahiri kuwa wanafunzi wote wanakuwa katika mitihani tena ile ya kumaliza chuo. Pale getini hakukuwa na mlinzi yeyote hivyo niliingia bila ya kuulizwa na mtu yeyote. Nilipishana na baadhi ya wanafunzi wachache sana tena wale masista duu na wengine mabrazameni bila ya kujali wala kujiogopa nilipishana nao huku akili yangu yote nikulifikia jengo G namba 13. “..samahani Anti.. eti namba 13 kuna watu…” Nilimuuliza mdada mmoja alioonesha sura yake ni ngeni kabisa machoni mwangu kwanza hata alikuwa hanifahamu kwani hakuonesha mshtuko wowote.. “..kwani wewe unamtaka nani..? Maana wanafunzi karibu wote wanafanya mitihani kasoro wale wa mwaka wa kwanza walioingia juzi juzi ndio wapo wapo humu mabwenini..” “..sawa..!!, unamfahamu Aisha.., anakaa chumba hicho hapo juu namba 13..?” “..Aisha..? Aisha..??, mhhh..!! Namfahamu wewe ni nani yake labda..?” “..rafiki yake wakaribu na nimesoma naye hapa hapa chuoni..” “””haloooo…!!! Eti rafiki yake wa karibu nimesoma naye..??, unahadhi wewe yakutembea na Aisha..? mwenye hipsi.., shepu shepu sio la mchina.. wakutembea na ‘Verosa’ sio daladala, bajaji wala teksi..? Alinitolea maneno ya umbea na yakuumiza sana roho tena kwa pozi huku mdomo akiyumbisha kana kwamba sina hadhi yakuongea naye yeye wala huyo Aisha. “..subiri hapo hapo nikakuangalizie maana nahisi utakuwa umekosea njia kwani Aisha nimjuaye mimi hawezi kuwa na mtu kama wewe ambaye hujui hata kujipodoa wala kuoga, mwenye kunuka makwapa na hilo toto sijui ndio kojo au lijimavi limeshajinyea..?” Aliondoka huku akiendelea kuongea maneno yake machafu na kwenda kumuita Aisha. Niliumia sana moyoni nakutamani hata kumrukia na kumpiga lakini niiliogopa kufanya vurugu yeyote katika maeneo ya hapa chuoni. Kwani niliamini nitakamatwa na tena ikijulikana nilikuwa nasoma hapa ndio nitaharibu kila kitu.hivyo nikawa mpole tena mjinga haswaa huku nimejibanza nakumsubiri huyo alieenda kumuita Aisha. Ilinichukuwa dakika kama nne nzima peke yangu. Harufu kali ya marashi ya ‘adorable’ ilioambatana na sauti ya viatu ndio ilinifanya nianze kutoa mchozi kwani ndio marashi niliokuwa nayapenda kutumia na rafiki yangu kipenzi Aisha tulipokuwa wote chuo kipindi kile. “..Aishaaaaa..?? Aisha rafiki yangu..?” Nilishusha fuko langu chini nakumkimbilia aisha huku nikitaka kumkumbatia lakini nilipofika karibu yake tu akanikwepa nakunifyonza huku macho akiyatoa vilivyo. “..wee chizi vipi..?” “..jamani Aisha embu niangalie vizuri..? umeshanikumbuka rafiki yangu kipenzi..?” “..sauti siyo ngeni.., embu nikumbushe unatokea wapi wewe..?” Maskini Aisha alikuwa ameshanisahau kabisa japo mimi nilishamtambua. Kuharibika kwangu sura na nyele zangu za kipindi kile vilitosha kunibadilisha nakuwa Tina feki. Hata nilipomwambia Aisha kuwa naitwa Christina ama Tina bado alikataa nakusema kuwa Tina yule wazamani alishakuwaga chizi wa mitaani na siwezi kuwa mimi. Nilitumia dakika kama kumi nzima za kumulelewesha hadi akanitambua. “..niwewe Tina..? hata bado siamini kipenzi changu kwanini umekuwa hivyo jamani..??, shetani gani aliokutembelea Tina ukabadilika kiasi kile..?? Ona sasa mwenzako nimetoka kumalizia mtihani wa mwisho.., si tungekuwa tumemaliza wote sasa hivi Tina..?” Aisha aliongea na mimi kwa uchungu wa hali ya juu huku akitaoa machozi kama vile mtoto mdogo. Alinitoa mule chuoni ndani nakunipeleka mpaka nje. Tukatafuta sehemu nzuri ya baa nakukaa kisha nikaanza kumsimulia yote yalionikuta kipindi sipo naye. Aliona na kufananisha maisha yangu kama vile sinema tena ile ya tamthiliya ambayo ya muda mrefu sana. Nilimuelezea kuanzia tulipoanza naye mpaka nilipomucha chuo nakuanza kufanya umalaya wangu tena kwa kumficha mambo mengi. Kuhusu kuathirika kwangu nilimficha lakini kuhusu huyu mtoto nilimdanganya kuwa ni mtoto wangu ambaye nilizaa na mchungaji yupo Mwanza kaniacha na kunitelekeza na mtoto. “..pole sana rafiki yangu Tina, ndio maisha jinsi yalivyo. Enhee kwa hiyo unaishi wapi kwa sasa..?” “Aisha..? hapa unaponiona sina mbele wala nyuma na naishi peke yangu na huyu mtoto wangu tena kwa kutangatanga..” Tukiwa bado tunaongea mara mwanangu Adrian akashtuka kutoka usingizini nakuanza kulia kwa sauti ya juu. Nilimfunua vizuri nakuanza kumbembeleza huku nikimtolea maziwa kwenye chupa.. “..mtoto wako mzuri sana Tina.., anaitwa nani..?” “..anaitwa Adrian. Kwa hiyo sasa hivi Aisha umeolewa au maana nakuona na pete ya uchumba shosti..?” Nilimbadilishia mada asiendelee kuniuliza juu ya huyu mtoto. Alikuwa amevalishwa pete lakini hakuniweka wazi kuhusu bwana anayeishi naye ila aliniambia tu ni mfanyabiashara tena wakimataifa hivyo si mtu wakukaa sana nayeye hivyo ni kama anaishi yeye na mfanyakazi tu. Alinichukuwa pale nakuelekea mpaka eneo aliokuwa amepaki gari lake na safari ya kuelekea kwake ikaanza kwani aliniahidi kuishi na mie mpaka mtoto atakapokuwa mkubwa ama mimi nitakapopata kazi yakueleweka nakujitegemea mwenyewe. “..Aisha..?, wewe ni rafiki wangu wa milele.., na sina rafiki kama wewe..?” Niliongea kwa kusisimka huku uso wangu ukitawaliwa kwa machozi ya furaha. Gari lake lilikuwa zuri sana na lenye vioo vyeusi vya kumfanya mtu wanje asiweze kuwaona. Mwanangu Adrian nilikuwa nimeshamshusha mgongoni nakumlaza siti ya pembeni yangu. Muda wote Aisha alikuwa akitabasamu nakucheka na mimi karibu njia nzima na hata tulipofika kwenye foleni alikuwa akinipigisha stori za chuo nilivyoacha gumzo kwa kila anayenijua na hata kitendo cha wazazi wangu kuja kunitafuta chuoni. Kifupi nilifarijika sana nakujiona mtu mwenye bahati ya mara nyingine tena bahati ya mtende. “..kumbe Aisha unaishi mbali hiivi…??, enhee..!! ni wapi hivi shosti maana hiyo safari hatufiki tu..” “..weee unafikiri mbali basi..?? ni hapo bunju tu.., tukivuka aka kapori tu tumeshafika..” Gari ilitembea kama alivyoniahidi kuwa tukivuka tu kapori tumeshafika. Giza nalo lilikuwa limeshatanda. Nilihakikisha mwanagu Adriani nimemfunika vizuri kwa ajili ya baridi ya mule ndani ya gari. Tukiwa bado tupo eneo la kale kapori mara Aisha akasimamisha gari kisha akaanza kufungua droo za mbele ya gari yake kana kwamba kuna kitu amekisahau au anakitafuta amekikumbuka. Ghafla akatoa bastola ndogo nakunielekezea kichwani mwangu.. “..hapo hapo ulipo Tina..??, usitingishike wala kuongea chochote na nitakufyatua usipotii amri hii..??” Mapigo yangu ya moyo yakabadilika nakuanza kutemeka huku kojo likichukuwa nafasi yake kunitiririka. Nikawa siamini kwa kilichonitokea. Nilibaki kimya kama alivyoniambia Aisha huku ile bastola iking’ang’ana katika paji langu la uso vilivyo tayari kwa kufyatuka. Sikuweza kujipindua zaidi ya kusikia tu Aisha akiongea na mtu kwenye simu. “..kazi yenu tayari haya sasa mko wapi mnipe changu..?” Aisha aliongea kwenye simu kwa sauti ya ukali na yakikatili kisha ndani ya dakika chache mlango wa gari kwa upande wangu ukafunguliwa. Tochi zilinimulika kisha nikashikwa na watu nisiowafahamu halafu kwenye gari nikamshuhudia Jerry kiingia kisha akambeba yule mtoto na kuondoka zao na Aisha huku wakiniacha nimekumbatiwa na watu nisiowafahamu. “..mnampeleka wapi mwanangu..??, mrudisheni..??” Nilitoa makelele ya nguvu lakini haikusaidia chochote zaidi ya ile gari kutokomea huku wale wavulana waliokuwa wamenishika kwa kunikumbatia wakianza kunivua nguo zangu na zao tayari kwa kunibaka kwa zamu… *********************** CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/  Walinigombania huku kila mmoja akinivuta huku na kule. Nilijitahidi japo kutoa sauti za makelele lakini haikusaidia kitu zaidi ya wale vijana kunipiga vibao na kisha kuniburuta mpaka eneo la kichakani kwenye giza totoro. Mwili wangu wote ukawa hauna thamani tena. Hawakuwa watu wazuri hata kidogo kwani walinifanya kwa nguvu na baada ya hapo wakachukuwa majiti nakunisokomeza ambapo walinisababishia maumivu makubwa na makali sana mwilini mwangu na haswa upande wa matiti yangu kwani walikuwa wakiyavuta na kuyafinya kwa kucha zao ndefu na hata wengine kuyauma kwa kutumia meno. Ndani ya kama nusu saa walikuwa wameshaniharibu sana na pia walikuwa wameshatawanyika kila mmoja. Uwezo wa kusimama sikuwa nao zaidi ya kujiburuta chini chini huku nikitafuta japo barabara kuu ya kuweza kutokea. Tumbo nalo lilianza kuniuma sana tena kule kuuma kwa kuvuta maeneo ya chini ya kitovu. “..nimekukosea nini eeh Mungu wangu..? Niangalie ninavyoteseka..? Weka japo mikono yako uniangaze na kunipa nguvu eeh Baba..?” Nilianza kumlaumu mwenyezi Mungu aliyeniumba nakujiona nimetengwa kabisa katika ulimwengu huu uliojaa mateso. Mikono yangu miwili ndio ilikuwa kama miguu kwa kujisukumia taratibu. Hatimaye baada ya mwendo kidogo nikaona gari kwa mbali linapita. Nilijaribu japo kutoa sauti ya ukali kwa makelele lakini ilishindikana kwani sikuwa na sauti kubwa tena na hata hivyo lile gari lilikuwa katika mwendo kasi hivyo halikuweza hata kuniona wala kusimama. Akili yangu sasa ikawa inamfikiria mwanangu Adrian niliyeporwa na rafiki yangu kipenzi Aisha akishirikiana na Jerry. “..na lazima niwatafute na kuwaua kabisa..?” Hasira yangu kwa sasa ikawa imefika kikomo kwani nilijihisi kutokwa na mishipa pembezoni mwa paji la uso wangu. Nilijikuta nimepata nguvu za ajabu tena zile za ghafla. Niliweza kuinuka na kwa sasa nikawa natembea haraka haraka mithili ya wanajeshi wakiwa katika mazoezi yao ya kwenda vitani. Haikunichukuwa mwendo sana mara kwa mbele yangu kidogo nikakutana na dalaldala pamoja na teksi teksi zikiwa zimepaki huku eneo lile kukiwa na watu wakifanya shughuli zao mbali mbali. Hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi haraka nakutambua kuwa pale patakuwa ni kituo cha daladala na pia ni maeneo ya makazi ya watu. Mwili wangu sasa ukaondoka na hofu ya kuwa bado porini. Furaha yote nikaihamishia ndani ya lile eneo huku nikilisogelea kwa tabasamu ya hapa na pale. Nilipofika tu pale kwenye mwanga kila mmoja akaanza kunishangaa. Nilijiangalia mwili wote kisha. “..Mamaaaaa..!!!!!, Mamaaaaaa…!!!” Maskini Tina mimi kumbe nilikuwa sijavaa hata nguo. Nilikuwa uchi wa mnyama na mwili wangu kwa sasa ulikuwa umegandia damu damu ambazo zilikuwepo maeneo yote ya kuzunguka mapajani, tumboni mpaka kwenye maziwa yangu. Aibu kubwa niliipata lakini sikuwa na jinsi zaidi ya akili yangu kunituma nirudi kule machakani nilipobakwa nikazichukuwe nguo zangu. Kwa mwendo wa haraka niligeuka nyuma nakuanza kuondoka zangu. Hatua mbili tatu mara uso kwa uso nikakutana na gari. “..Mamaa nakufaaa..!!” Mwili wangu wote ulikuwa uvunguni mwa gari lilikokuwa linapita njia na kwasasa lilikaribia kunigonga. Ni breki tu ndizo zilisaidia. Yule aliyekuwa akiendesha gari alishuka huku anaongea maneno kwa ukali. Kadri alivyonisogelea na ile sauti ilivyokuwa ikitikisa ngome ya masikio yangu ndivyo nilivyokuwa nikisisimka nakupata na wasiwasi kama namfahamu. Aliponifikia karibu tu. “..haa Aisha niwewe…? Kwanini unanifanyia hivi jamani..??, umenitumia vijana wanibake sawa…? Ukaona haitoshi ukanipora na mwanagu Adrian ukampa Jerry kisa pesa Aisha….??. Haya sasa si unataka unigonge..??, nigonge kabisa ili ndoto zako ziwe zimetimia si ndio..?” Niliongea kwa jazba sana baada yakugundua kuwa kumbe aliyetaka kunigonga alikuwa ni rafiki yangu kipenzi Aisha na kwa muda huu alishuka nakuniongelesha kwa hasira zake. Nikiwa bado nipo uvunguni mwa gari huku Aisha akiniongelesha mara nikasikia sauti ya mtoto wangu akilia ndani ya gari. “..Aisha mwanagu Adrian yuko wapi nasikia analia..??, nasikia analia.., yuko wapi..?” Hasira kali nilizoinuka nazo pale chini zilinifanya nimsukume Aisha nakuongoza moja kwa moja mpaka kwenye mlango wa gari lake bila kugeuka nyuma. Nilifungua mlango ule kwa hasira zote nakumshuhudia mwanangu Adrian akiwa anatapika ovyo huku kafungwa fungwa ovyo na makamba shingoni mwake. Nilianza kumfungua haraka haraka lakini kitendo cha kumalizia kumfungua tu zile kamba nikahisi kimya kwa mwanagu Adrian. Nikamtingisha bado kimya. Nikamgusa na kuegemeza kichwa changu kifuani mwake japo nisikie mapigo yake ya moyo napo kimya. Akili yangu moja kwa moja ikanituma kuwa mwanangu Adrian sinaye tena yaani ameshafariki.. “Adrriiiiiiiiiaaaaaaaaaaaaaaaaaaannnnnnn….???????, Adriiiiiiiiiiiiiiaaaaaaaaan…..??” Bado nilimuinua nakumtingisha tingisha lakini ndio kama nilikuwa najifurahisha na mdori kwani alishafariki muda mrefu. “..Aisha..?? Aisha…??, Aishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa..??” Nilishtuka kutoka usingizini huku jasho likinitiririka mithili ya maji ya chemu chemu yakifuata mkondo wake huku kwikwi kali sana ya hasira na maji kwa ujumla vikinishika vilivyo. Kizunguzungu cha ghafla kilichonishika nilijihisi naona kama ukungu mbeleni mwangu kwani macho yangu yalikuwa yameishiwa nguvu ya kuona vizuri. Nilishusha pumzi nakupikicha macho yangu huku nisiamini kama vile vyote vilivyonitokea kuwa ilikuwa ni ndoto. Eti mpaka rafiki yangu Aisha akanigeuka nakumchukua mwanangu Adrian. Haraka haraka nikageuka pembeni yangu nakumwangalia mwanagu Adrian ambaye alikuwa bado amelala. Nilimuinua nakumbusu kwenye paji lake la uso. “..inaonekana unampenda sana mwanao Adrian…?” Aliniongelesha rafiki yangu Aisha ambaye kwa muda huu tulikuwa bado tupo njiani kuelekea nyumbani kwake na alikuwa akiendesha gari. Nilijilaumu sana kuota ndoto ya ajabu kiasi kile lakini haina jinsi kwani ndoto haipangwi. Nilimgeukia rafiki yangu Aisha mara mbili mbili huku nikioneshwa kutetemeka kwa uwoga nakudhani huenda nilichokuwa nakiota kikanitokea muda wowote. “..ahh..!! itakuwa mandoto tu..!!, kwanza hawezi kunifanyia hivyo rafiki yangu kipenzi Aisha….” Nilijikuta najifariji kwa kuongea kimoyo moyo huku nikiachia tabasamu kwa kumwangalia Aisha. “..daah..!!, kumbe hujaacha kulala lala enhh..??” “..ennhh..!! shosti wangu kwa jinsi ninavyopenda kulala Tina mimi..? Yani ni kama ugonjwa kwangu toka kipindi kile tupo wote chuoni.., si unakumbuka hata darasani nilikuwa siingii ama nachelewa kisa usingizi..?” “.. ni kweli.., ila umelala sana, yani tokea tunatokea pale chuoni CBE umelala tu na mwanako wote. Tumepita kwenye mafoleni pale Morocco, Kijitonyama hadi Mwenge kote bado umelala tu Tina..?” “ndio hivyo..!!, wanasema usingizi mwanaharamu ukikushika. Lakini bado tu hatujafika aisha..?” “ujue ni vijifoleni tu vya hapa na pale ndivyo vinafanya hivi, lakini isingekuwa hivi..? tungekuwa nyumbani muda mrefu sana.. lakini hatuna muda mrefu tunafika..” Niliendelea kupiga stori mbili tatu na rafiki yangu kipenzi Aisha japo bado kale ka uwoga ka ndoto kalikuwa kakinitawala ndani ya halmashauri yangu ya ubongo. Ndani ya dakika kama kumi hivi tulikuwa tunatazamana na geti kubwa jekundu lililopambwa na nakshi nakshi za silva. Aisha alipiga honi kama mara mbili na punde akatoka kijana aliyekuwa amevaa kofia kuashiria kuwa huenda alikuwa ni mlinzi wa Aisha. Alitufungulia nakuingia mpaka ndani. “..Tina karibu na jisikie uko nyumbani. Hapa ndipo ninapoishi na mume wangu niliyekwambia kuwa kwa sasa ni mfanyabiashara na wala si mtu wa kukaaa sana hapa bongo kwani huwa anakuja na kuondoka siku hiyo hiyo au anakaa hata siku moja mbili anaondoka zake. Karibu ndani kipenzi changu..” Aisha alinikaribisha kwa ukarimu sana. Tuliingia mpaka ndani na akanikabidhi chumba kimoja. “..hiki kitakuwa chumba chako kuanzia sasa Tina. Jisikie uko nyumbani na jisikie upo kwako rafiki yangu kipenzi Tina..” “..haa..!!, sijui hata nikushukuru vipi mpenzi..!! Ahsante sana na ubarikiwe uendelee kuwa na moyo huo huo Aisha..”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Chumba kilikuwa nikikubwa sana ambapo ndani yake kulikuwa na kila kitu. Kuanzia choo na bafu. Kitanda kikubwa. Nilimvua mwanangu Adrian nguo zake nakumpeleka bafuni ambapo nilimuogesha nakisha nikambadilisha pampasi, baada ya hapo nikaoga na nilipotoka kuoga tu Aisha tayari alikuwa chumbani kwangu kitandani na Adrian ananisubiri nitoke kuoga. “..Tina nimekuletea nguo hizi hapa, mie huwa zinanibana sana si unajua kunenepa kwangu ovyo tena..!!” “..Ooh..!!, ahsante Aisha..” “..ila kuna kitu nahitaji ujue… Mwili wote ukanisisimka kwa haraka na ghafla kuanzia kichwani mpaka miguuni. Kutokana na kule kutetemeka nilijikuta kuishiwa nguvu mwilini nakuhisi kama kojo linaanza kunidondoka mtu mzima huku akilini nikiwa na shauku kubwa ya kujua ni kitu gani hicho anachotaka kuniambia Aisha. “…Eennhee shosti..!! kitu gani tena hicho mbona waniacha roho juu na njia panda mwenzako....??” “..njoo kwanza mpaka hapa kitandani.., halafu ukiwa katika kujifuta vizuri na kubadilisha nguo mimi nitakuwa nikikusimulia, sawa shosti wangu Tina..?” “..ni sawa tu hamna neno, au mtoko nini jamani..?” “..mbona una haraka kiasi hicho jamani hata sijakwambia ni kitu gani..?, siyo mtoko wala nini..??” “..Sasa ni kitu gani hicho cha kunitia roho juu mwenzangu, wangwi wangwi hadi umeninyima raha na kunipa karaha kwa muda..?” Muda wote Aisha ailionekana kama mtu wa masihara masihara kwani ni kweli alionesha kuna kitu anataka kuniambia, lakini hakuwa siriazi kwani alikuwa akicheka cheka huku akinipa mkono kwa kugonga. “..hivi yule mchumba wako wa zamani ‘Jerry’ ushawahi kumuona..?” Mapigo yangu ya moyo yalibadilisha uelekeo pale aliponitajia jina la ‘jerry’. Sikutaka kabisa kumsikikia Jerry masikioni mwangu Tina mimi na hata sura yake kwani yeye ndio chanzo cha mimi kuishi maisha haya ya shida nakutangatanga mpaka hivi sasa. “..kiukweli shosti wangu Aisha. Huyo ‘Jerry’ ndio kwanza nakusikia unamtaja wewe leo hii, kwani toka enzi hizo sikumtia machoni na si unakumbuka alichonifanyiaga kipindi cha nyuma mpaka tukamfanyizia nakumkata kata nanihii yake kwa kutumia viwembe si unakumbuka..?” “”..hehe heee..!!, halooo!!! Nakumbuka shosti..!!, lakini nadhani yale yalishapita siku nyingi sana, ila kuna jipya nataka nikujuze shosti wangu Tina ambalo hulijui..?” Sasa nikatuliza pumzi zangu huku nikimtolea macho Aisha aniambie ni kitu gani hicho.. “..haya niambie shosti kwani amekuwaje huyo Jerry..?” “ni stori ndefu sana Tina lakini maadam upo nitakusimulia kila kitu na utajua nakuelewa tu huyo Jerry. Kwanza kabisa unajua kipindi kile tumemfanyizia kwanza hakututambua kama ni sisi ndio tulimfanyia ule unyama wa kumkatakata nanii yake kwa viwembe hadi kumpelekea kuharibika njia ya kutolea mbegu za uzazi. Tina..?” “nakusikia endelea tu..?” “..najua hutaweza kuamini lakini inakubidi tu uanzae kuamini kwani Jerry kwa sasa amekuwa ni mtu wa karibu sana na mimi..?” “..bado sijakuelewa elewa Aisha , unamaanisha nini haswa..?” “..nimekuwa msaada mkubwa sana kwa Jerry katika maisha yake.. Kuna siku moja nilikuwa naelekea kufanya ‘shopping’ zangu pale Mlimani city na kwa bahati nikakutana nae uso kwa uso. Kwa kuwa nilikuwa katika kipindi kigumu sana cha chuo si unajua tena bumu likiisha tunavyotaabika sisi..?” “..ni kweli..?” “..basi nikajikomba Aisha mimi kwa Jerry nakujifanya namjua kuliko. Kwa kuwa siku hiyo alikuwa peke yake ikawa ni rahisi sana kumshawishi. Jerry alionesha yuko tofauti sana kwani alikuwa ni mtu mwenye msimamo haswaa. Lakini akaniambia yuko tayari kunigharamia kiasi chochote cha pesa endapo tu nitamtekelezea mambo mawili makubwa kwake..?” “..hee makubwa..!!, mambo gani tena..??” Akili yangu sasa ikawa kama imenivurugika huku nikibaki njia panda na nisielewe ni kitu gani hicho ambacho aisha ameambiwa na Jerry. Mawazo yangu yote yakanirudisha mpaka siku niliyoota kuwa nachukuliwa mwanangu na Aisha wakisaidiana na Jerry na kisha nikabakwa na vijana nisioweza kuwatambua.. “..inawezekana ile ndoto ikawa kweli na leo hii ikanitokea ‘live’..?” Nilijisemea kimoyo moyo huku sura ikinibadilika nakumuangalia mwanangu Adrian pembeni. Hasira kali iliyoamsha misuli pembezoni mwa uso wangu huku ikihamasisha dukuduku kali moyoni. Japo alikuwa hajamalizia kuongea lakini akili yangu ikawa imeshabadilika kwa kiasi kikubwa nakuona huenda nitatekwa tu. kuwa hapa hapanifai hata kidogo tena. “..ennhee Aisha ikawaje sasa ni mambo gani hayo mawili aliokuwa amekuomba huyo Jerry”.. “..aliniweka wazi kuwa yeye hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, amesumbuka sana kwa madaktari na mpaka kwa waganga wa kienyeji lakini imeshindikana. Hivyo akaamua aoe na kuishi na mwanamke ambaye yuko sawa nayeye ambaye hana uwezo wa kuzaa ‘mgumba’. Basi akaoa lakini mtafaruku umekuja kwa wazazi wa pande zote mbili wanataka wajukuu.. kilichofanyika Jerry akaniomba kwanza nimtunzie siri na aibu hii kubwa ambayo amehangaika nayo kwa muda mrefu sana bila ya kuwa na mtoto. Pili akaniomba apandikize mbegu zake kwangu kutokea hospitalini ili nishike mimba nakumzalia. “..hee.., halafu..?” “..kama nitashika mimba atakuwa bega kwa bega na mimi mpaka nitakapojifungua. Atahakikisha amenijengea jumba kubwa nakuniwekewa kila kitu ndani nitakachokihitaji. Pia mkewe atamsafirisha nje ya nchi kwa siri siri bila ya ndugu kujua chochote na atakaporudi atakuta nimeshajifungua hivyo atamchukuwa mtoto nakumlea. Tulijaribu mbegu zake karibu mara tano lakini ikashindikana mimi kushika mimba kwa kutumia mbegu za Jerry. Kwa kuwa tayari nilishaingia tamaa ya hela na makazi kama alivyoniahidi Jerry. Nikapanga dili na dokta kisha nikasafiri mpaka Morogoro kwa mpenzi wangu Almeida akanipa ujauzito hivyo nikamsakizia Jerry kuwa tumeshafanikiwa kushika mimba. Jerry alifurahi sana kwa kuwa nilikuwa katika kipindi kigumu. Ilinibidi nisimamishe kwanza mambo yangu ya chuo kwa muda wa miezi tisa huku na ujauzito. Nikatafutiwa mfanyakazi wa ndani ambapo hata hivyo haikuwa ikipita siku bila Jerry kunipigia simu au kuniletea vitu mbalimbali vya kuniliwaza..” “..kwa hiyo sasa huyo mtoto ukajifungua au ikawaje sasa..?” “tina..? yani mtoto nilijifungua salama bonge la toto mzuri kama huyo wa kwako. Hii nyumba na gari unavyoviona ameninunulia Jerry. Na mkewe ni rafiki yangu wa karibu sana na haipiti siku bila kunitembelea ama kunipigia simu na hivi nimeshamaliza chuo kabisa utamuona hapa kila siku..” Mapigo yangu ya moyo yakaishiwa nguvu na kwa sasa yakawa kama yamepigwa ganzi ama kumwagiwa maji tena yale ya barafu ambayo hutoa kama moshi. Kichwa kilianza kunigonga huku nisielewe nianzie wapi. Sikuwa na hamu tena ya kukaa hapa japo ndio kwanza ilikuwa siku ya kwanza. Tukiwa bado kwenye maongezi na Aisha mara tukasikia sauti ya gari ikipiga honi huko nje. Hatujakaa sawa mara tena Simu ya Aisha ikaita, akapokea.. “..yeahh honey mambooo..!!! Ni wewe karibu namimi ndio kwanza nimemaliza chuo leo vipi upo peke yako ama..?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “..sikuweza kutambua vizuri kuwa Aisha anaongea na nani zaidi yakuniaga kwa ishara huku akiniacha chumbani nakuelekea sebuleni..” Mawazo mengi bado yaliendelea kunitawala ndani ya halmashauri ya ubongo wangu. Sikuweza kujitambua Tina mimi. Nilihisi kama ndoto. Nilivaa nguo kwa kutetemeka mithili ya mtu mwenye ukoma au yule anayeumwa malaria kali sana. Midomo yangu ilikuwa ikitetemeka kwa haraka haraka mithili ya maji yanapochemka katika sufuria. Nilibaki nimeduwaa peke yangu huku nikiwa sipati jibu wala ufafanuzi wa hili jambo. Nilichokifanya niliiinuka taaratibu kisha nikamweka mwanangu Adriani vizuri kitandani nakuanza kunyatanyata kuelekea sebuleni huku mwanangu Adrian nikimuacha akiwa amelala fofofo. Niliendelea kunyata kimya kimya. Sauti za taratibu na za kimahaba kuashiria sebuleni kuna mtu na mume wake ndizo zilikuwa zikinivuta zaidi. Nilipokaribia nilifunua pazia la kuingilia sebuleni kwa utaratibu huku nikifumba jicho langu la upande wa kulia nakuliachia jicho la upande wa kushoto likifanya kazi yake ya kuangaza nakushuhudia tukio zima huku masikio yangu yakiwa sambamba na hilo tukio. “..Jerry..?? Jerry..? oohh…!! Nooo…!!! Aisha noo..??” Maskini Tina mie alikuwa ni Jerry katika himaya hii. Na kwasasa alionesha sura ya ukali huku akimuhadithia Aisha tukio zima nililomfanyia pale stendi miezi michache iliyopita. Alikuwa akimuomba sana Aisha msaada wa kunitafuta popote pale nilipo ili ampate mtoto wake. Jerry alikuwa akitoa machozi kama mtoto mdogo vile huku akimbembeleza Aisha wawe kitu kimoja kuhakikisha huyo mtoto anapatikana. Nikiwa bado nashuhudia Jerry akimbembeleza Aisha mara Aisha akainuka pale nakutoka huku akielekea sehemu ambapo nipo.. “..Jerry haiwezekani mwanangu wa damu yangu kabisa eti amchukue Tina anajua tulivyompata..?, embu subiri nakuja sasa hivi..?” Aisha alionekana kuwa na hasira zaidi kwani aliinuka kwa hasira na kwa shari. Nilichomoka kwa haraka huku nikielekea chumbani kwangu kumuwahi mwanangu Adrian lakini kabla sijafika chumbani Aisha akawa tayari ameshaniona kwa mbali kidogo akaniita kwa sauti ya kupaza na ya ukali.. “..Tinaaaaaaaaaaaaaaa….??????????????” *************************Nilionesha woga uliochanganyika na kusita sita huku nikibaki njia panda nisielewe nimsubiri Aisha afike karibu au niingie ndani kumchukuwa mwanangu Adrian. ”..aahh..?? liwalo na liwe bwana..?” Nilijikuta najijaza moyo wa kijasiri huku nikiingia mpaka chumbani kwa nguvu zote nikimchukuwa mwanangu Adrian ambaye bado alikuwa kapitiwa na usingizi mzito. Nilijitahidi kufanya haraka haraka nikakusanya vitu muhimu ikiwa ni pamoja na mkoba mkubwa uliokuwa na hela kidogo na nguo za mwanangu Adrian. Kadri nilivyokuwa naendelea kupaki kwa haraka haraka ndivyo na sauti ya viatu ilioashiria kuwa Aisha yupo njiani anakuja ilikuwa ikiendelea kunishtua ndani ya fikra zangu. Sasa nikawa Tina sugu haswaa tena yule ambaye hasikii la mkuu. Nilichukuwa khanga nakumfunga mwanangu Adrian mgongoni kisha ule mkoba nikauweka kwapani na baada ya hapo nikafanya ishara ya msalaba huku kichwa na mikono yangu nikikielekezea juu. “..eeh Mwenyezi Mungu nisaidie nakunilinda..” Nilijisalia kimoyo moyo nakuanza kutoka huku nikifuatisha mlango ule ule wakutokea. Ile nakata kona ya kutokea kwenye kikorido uso wangu moja kwa moja ukakutana na rafiki yangu Aisha. “..unakwenda wapi na mwanangu unampkeleka wapi..?” “..mwanako..? leo hii ndio amekuwa mwanako..? Aisha kipenzi nashukuru kwa wema wako ulionifanyia ila kumbuka huyo Jerry ni muongo kakudanganya kwanza sijawahi kuonana naye toka kipiindi kile tulivyomfanyia mchezo ule..??” Nilijitahidi kumdanganya Aisha lakini ndio kwanza kama nilikuwa naamsha mishipa yake ya hasira kwani alivimba nakutuna mara mbili ya Aisha yule nimjuaye mimi. Hakutaka kabisa kuniamini hata chembe na alichofanya nikukimbilia moja kwa moja kunivua khanga ile niliyokuwa nimembebea mwanangu Adrian. “..Aisha niache mbona huni..?” Kabla sijamalizia kuongea chochote nilishangaa Aisha kunitupia kibao katika shavu langu nakuanza kujihisi kizunguzungu. Sikutaka kabisa kumlegezea zaidi yakuendelea kuing’ang’ania ile khanga asiweze kuifungua kwani kama angeweza kuifungua ingekuwa rahisi kumchukuwa mwanangu Adrian. “..Jerryyyy???????? Jerryyy njoo nisaidie..?” Maskini Tina mimi nikawa katika vita kubwa yakuteteta mwanangu Adrian asiweze kuwa mikononi mwa Jerry na huyu Aisha kwani nilishajiwekea dhamira ya kutomwachia na kama nitafanya hivyo maisha yangu yatakuwa mabaya zaidi kwani sina tena kizazi wala uwezo wakuweza kuzaa Tina mimi. Makelele aliokuwa ameyatoa Aisha yakumuita Jerry tayari yalikuwa yameshapenyeza katika ngome ya masikio ya Jerry na kwa muda huu nilianza kuhisi sauti za viatu tena ikitembea kwa mwendo wa haraka haraka. Nilichokifanya niliinua mkono wangu nakuudumbukiza moja kwa moja mpaka kwenye mkoba nakuchomoa chupa ya maziwa ya mtoto ambayo ilikuwa bado na maziwa yamoto nakisha kumwagia Aisha usoni. Aisha aliinama chini nakuanza kutapatapa huku mikono yake yote miwili akijiziba usoni na kufikicha kwa yale maumivu niliyokuwa nimempatia. Aisha akiwa bado anagala gala pale chini, nikarudishia lile dumu la maziwa nakisha nikaongoza kuelekea sebuleni. Ilinichukuwa hatua tatu tu uso kwa uso na Jerry mwenyewe na tena safari hii aliweza kuchukuwa mikono yake nakuziba njia ili mnisieweze kutoka Tina mimi. “..kwanza nahakikisha nakuua..? na pili namchukuwa huyo mtoto wangu pumbavu mkubwa wewe..?” “..hapa tutauana na siyo kuniua na kuhusu mtoto sahau laba nife naye hapa sasa hivi..? baradhuri wewe usiye na hata huruma kwa binadamu. Umeniharibia shule sawa nimekubali ila kuhusu kumpata huyu mtoto ilo sahau Jerry..?” Hasira kali ziliendelea kunitawala ndani ya halmashauri ya ubongo wangu. Kwa safari hii mwanangu Adrian alikuwa ameshahamka na tayari alikuwa akilia kwa sauti ya juu. Nilitamani japo nimshike nakumbembeleza lakini sikuweza kwani tayari Jerry alikuwa karibu yangu na alikuwa kaniwekea mikono yake shingoni mwangu. Nilijihisi kutapika kwani Jerry alidhamiria kuninyonga kutokana na mikono yake kushikana vilivyo na shingo yangu. “..nakufa jamani nioookooeenn..?” Nilijitahidi labda kutoa sauti huenda majirani watanisikia lakini wapi ? haikusaidia chochote zaidi ya Jerry kukaza zaidi mikono yake huku nikihishiwa pumzi nakuanza kutapatapa mithili ya wacheza mieleka wakiangushana. Kitendo cha mimi kuishiwa nguvu kilimpa faraja na nguvu ya ajabu Jerry yakuweza kunifungua ile khanga yangu niliokuwa nimembebea mwanangu Adrian na kisha akamchukuwa mwanangu Adrian. “..twende mwanangu huyu shetani hafai angekuua..?” Jerry alimwambia mwanangu Adrian huku akimbusu japokuwa alikuwa mdogo sana kwani hakuweza kuelewa chochote zaidi ya kutoa macho. Jerry alifanikiwa kumchukuwa mawanangu mikononi mwangu na kwa safari hii hakutaka hata kumuaga Aisha kwani bado Aisha alikuwa anatapatapa huku akiendelea kufikicha macho yake yaliokuwa nimeyamwagia maziwa ya moto ya mtoto. Nilijiona sijielewi elewi kwani kila nikitaka kuinuka bado nguvu ziliniishia kabisa na pia shingoni kwangu kulikuwa kunauma sana. Taryari nilianza kuvuta taswira siku niliomchukuwa Adrian pale Ubungo nakutokomea zangu nakufananisha lile tukio kama tukio hili alilonifanyia Jerry leo hii. Mawazo mengi yalikuwa yanaendelea kutawala akili yangu huku nikiwa kama mtu aliyepigwa na bumbuwazi kwani nilijihisi mwanangu Adrian yupo tu kuwa hii ni ndoto lakini jibu lilibaki pale pale kila nilipomwangalia Aisha akiendelea kutapatapa. “..dada twende nimeshamaliza kazi..?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Nilikuwa kama sijiamini amini kwani ndani ya muda mfupi nilimshuhudia mfanyakazi wa ndani wa Aisha akiwa kambebelea mwanagu Adrian huku kamzungushia khanga zile zile alizonipora nazo Jerry pamoja na mtoto. “..unasemaje..? na Jerry yuko wapi..?” Bado nilikuwa sijiamini amini kama mwanangu Adrian amerudi mikononi mwangu tena. Nilitoka haraka mpaka eneo alipokuwa amesimama yule mfanyakazi. Nilipata furaha ya ajabu kwani kiukweli sikuweza kuamini kama kweli mwanangu Adrian amenusurika kuwa mikononi mwa Jerry. “..embu niambie umemfanyaje Jerry mpaka umempata huyu mtoto..?” “..wewe mwenyewe si unamuona huyo Jerry hapo chini alivyo..?” Niligeuka tena kwa mara ya pili nakumuangalia Jerry vizuri lakini bado alionekana akitapatapata huku pembeni kukiwa na sufuria kubwa. “yaan bado sijaelewa chochote..?” “..ujue nini dada..?” “eeh niambie..?” “..wakati mnagombana kuhusu mtoto hapo kwenye korido nilikuwa nikiwasikia tu kwa muda mrefu huku nikiendelea kumtayarishia dada Aisha maji ya kuoga. Kadri mlivyokuwa mnaendelea kugombana na maji ndivyo yalikuwa yanazidi kuchemka. Nilipomaliza ile natoka tu nije kumwambia kuwa maji tayari nashangaa nakuona wewe ukiwa chini unatapatapa vivyo hivyo na kwa dada Aisha. Kwa hiyo nilichoamua nikuchukuwa sufuria hivyo hivyo likiwa na maji ya moto nakumwagia jerry ambaye alikuwa kamchukuwa mtoto na kumwagia mgongoni mwake kisha nikamuhai kumchukuwa mtoto. Na nilipoimchukuwa mtoto nilimmalizia kumwagia Jerry yale maji ya moto sana mpaka eneo lote la usoni mwake kwani niliona yeye ndiye chanzo cha matatizo ya kumgombea huyu mtoto hapa..” “..ohh ahsante sana kwa kunisaidia nakumsaidia huyu mtoto..?” “..usijari Anti.. ila hapa mie kama nitakamatwa nitafungwa tu..?? hivyo nakuomba tutoroke wote samahani Anti twende kabla majirani wala mlinzi hajatokea hapa..??” Kwakuwa huyu Dada alikuwa ameshanisaidia kumpata mwanangu Adrian na pia alinisaidia kmteketeza Jerry hivyo haikuwa na budi kumchukuwa. Nilimpa mwanangu Adrian na kisha nikamfuata Jerry pale chini nakuanza kumsachi mifukoni mwake ili nitafute funguo za gari lake niweze kutoroka. Nillifanikiwa kuzipata ndani ya muda mfupi. “..chumbani kwa Aisha wapi..?” Nilimuuliza yule mfanyakazi akanionesha. “..nipe huyo mtoto na nakupa dakika mbili tu uingie usachi anapoweka hela zake kisha kwa haraka urudi tutoroke kabla mambo hayajawa makubwa hapa.” Yule mfanyakazi alifanya kama nilivyomuelekeza na ndani ya muda mchache tayari alikuwa amerudi kashikilia bahasha ndogo ilioonesha ndani yake patakuwa na kile nilichomuagiza. “..haya twende haraka haraka na tukifika hapo nje usioneshe kuwa na haraka haraka mlinzi atatugundua sawa..?” “..sawa nimekuelewa Anti..?” Nilimchukuwa mwanangu Adrian na kisha nikatoka na yule mfanyakazi huku nikimsihi mlinzi afungue geti nimuwaishe mwanangu hospitali anaumwa ghafla. Aliniuliza kuhusu Jerry na Aisha wako wapi hivyo nikamjibu kuwa wako chumbani kwao wametuachia ufunguo wa gari hivyo tunaenda hospitali hapo jirani nakurudi na huyu mfanyakazi wameniambia niende naye anisaidie. Ndani ya dakika chache tayari tulikuwa nje ya geti huku nikiendesha gari la Jerry. Pembeni yangu alikuwa yule mfanyakazi huku mwanangu Adrian akiwa anatoa tu macho pembeni yetu. Giza lilikuwa limeanza kuwa tororo kwani saa ya kwenye gari ilionesha tayari imeshatimu saa sita kasoro. Hata magari tuliopishana nayo hayakuwa mengi sana kwa usiku huu. Tulikuwa hatujielewi tunaelekea wapi lakini wazo likanijia la kuwa tuna pesa tulizozichukuwa chumbani kwa Aisha. “..ile bahasha uliochukuwa si unayo hapo..?” Nilimuuliza yule mfanyakazi niliokuwa nimetoroka naye. “..ninayo tena wala haiko mbali hapa..?” “..ni kiasi gani cha pesa ulichochukuwa..?” “..sijui ila ngoja niangalie vizuri..” Yule mfanyakazi aliichukuwa ile bahasha ambayo ilikuwa imetuna vilivyo kuashilia kuwa amechukuwa hela nyingi sana. Kadri alivyokuwa anaingiza mkono kwenye ile bahasha ndivyo nayeye alikuwa akibadilika sura nakutetemeka nakuwa kama mtu mwenye hasira sana. Ilinibidi kulipaki gari pembeni nakumuuliza. “..vipi embu toa ni shilingi ngapi zipo hapo..?” Maskini tina mimi nilikuwa nimeshaingia tena matatizoni kwani alivyochomoa ile bahasha haikuwa na pesa yeyote zaidi yakutoa bastola na kisha kunielekezea kwenye paji langu la uso. “..samahani najua huna hatia ila inanibidi kufanya hivi..?” “..jamani kwani imekuwaje..?? nimekufanyaje wee binti..?” “..Anti..? wala hujanifanya chiochote ila ninachotaka kusema namtaka mwanangu na wewe shuka chini sasa hivi kabla sijakufyatua..?” “mwanako..? yupi..? huyu hapa Adrian…?” “..ndio ni mwanangu kabisa wa damu na mimi ndio niliokuwa nimemzaa. Siri kubwa ilioko ni ya mimi na dada Aisha kuhusu huyu mtoto. Dada Aisha pale unapomuona hawezi kupata ujauzito kwani ameharibika kizazi kwa kutoa sana mimba ovyo kipindi cha nyuma. Na Jerry alikuwa akihitaji mtoto kwa udi na uvumba lakini kwa Aisha ikawa haiwezekani na ndipo wakaamua kunishirikisha mimi nilale na mlinzi wa pale ili nishike mimba niwazailie mtoto ambaye ndiye huyu uliokuwa umempora kutoka kwao. Inaniuma sana huyu mtoto kumuona akihangaika kwani nilijifungua kwa operesheni na hapa unaponiona bado nyuzi hazijakaza vizuri katika maumbile yangu ya sehemu za siri. Sasa sina jinsi zaidi ya kumrudisha mwanangu mikononi mwanangu na wewe sihitaji kukuua ila shuka mwenyewe niache na mwanangu nitajua nitakapoelekea..?” ****************** Bado niliendelea kuzubaa mwenyewe huku nikiishiwa pumzi taratibu nakuhisi kama mapigo ya moyo yanashindwa kufanya kazi yake. Nilijihisi mwili kunitetemeka huku miguu yangu ikikosa kabisa nguvu.“..lakini bint..?”“..lakini nini..? hivi unajua nimetumia ustaarabu wa hali ya juu kukuambia shuka uniache peke yangu. Sasa nitabadilika nikufyatue sasa hivi..?”Yule binti alionekana kuwa mkali kama mbogo.Nilibaki nimeduwaa huku nikimtolea macho. Nilichokifanya Tina mimi nilikubali kushuka ndani ya ile gari tena kwa shingo upande huku nikimtolea macho ya huzuni mwanangu Adrian.“kwaheri mwanangu.. kwaheri tutakuja kuonana hata siku nyingine..!!”Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kushuka ndani ya ile gari na machozi yakinilengalenga. Nilijipa moyo konde nakuamini hayo yote ni mapito tu na kama Jerry nimeweza kumuona tena hapa hapa kwenye Jiji kubwa basi ipo siku nitakutana tena na huyu mfanyakazi na ndipo atakaponitambua Tina mimi ni nani nimetokea wapi na purukushani zangu zikoje ndani ya hili Jiji..?. Kitendo cha kutembea kwa mguu hatua kama kumi mbele niligeuza tena jicho langu nakuangalia ile gari niliomuacha nayo yule binti. Ilikuwa bado iko pale pale huku taa zikindelea kuwaka kana kwamba gari mbovu au inamsubiri mtu aiendeshe. Sikuweza kuamini amini ninachokiona kwa macho yangu, niliyapikicha mamcho yangu vizuri nakuangaza tena. Kwa mbali niliweza kumshuhudia mtu kama Biggy yule kaka yake na Jeryy tena safari hii japo kwa mbaali kidogo nilimshuhudia akiongea na yule binti nje ya lile gari la Jerry.“.. hapa hapa ndio mwanya wangu, wamekwisha..??”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nilijijaza moyo wa kijasiri huku nikigeuza hatua kurudi katika lile eneo. Kwa mwendo wa taratibu mithili ya kumsindikiza bibi harusi aende akakate keki amlishe mumewe huku nikijificha ficha ili nisionekane mpaka karibu na lile eneo waliokuwepo, kisha nikatega ngome ya masikio yangu tayari kwa kusikia wanachokiongea Biggy na yule binti.“..nakuuliza tena wewe msichana..? mwenye hili gari yuko wapi na wewe unaelekea wapi usiku huu..?”“.kaka Jerry nimemuacha nyumbanni kwa dada Aisha wakiwa chumbani na hapa unaponiona naelekea hospitali kumpeleka huyu mtoto wake anaumwa..?”“mpumbavu na muongo tena mkubwa sana wewe. Wee unafikiri sijui chochote..? kwa taarifa ytako Jerry mwenyewe kanipigia simu kuwa umemuunguza na maji mwili wote na analia hajiwezi..? na huyo Tina yuko wapi Malaya mkubwa anayetaka kuendelea kuharibu tena maisha ya mdogo wangu Jerry..? hebu twende huko kwa Aisha alipokuwa.. twende..?”Bado nilikuwa nimejibanza huku nikiwasikiliza kwa umakini wa hali ya juu. Japo nilionesha kutetemeka lakini haikuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia. Biggy alimkaripia sana yule mfanyakazi na punde nikamshuhudia akimchukuwa nakumbeba mwanangu Adrian huku akiitumia ile ile bastola aliyechukuwa yule mfanyakazi na tena wakiondoka nakuelekea upande wa pili ambapo niliiona gari ya Biggy ikiwa amepaki.“..mmhh kweli nimeamini mwanaume, mwanaume tu,..? sasa Biggy ameichukuwaje chukuwaje ile bastola aliyokuwanayo yule binti..?”Ni kati ya maswali niliokuwa najiuliza bila ya kupata jibu huku nikiwasindikiza kwa macho mpaka walipovuka upande wa pili wa barabara ndipo na mimi nikalisogelea gari lile la Jerry waliloliacha nakuingia mpaka ndani. Haraka haraka niliwahi kufungua mlango kwa lengo la kuliwasha kisha niwafuatilie kwa nyuma lakini haikuwezekana kwani ufunguo wa gari tayari ulikuwa umetolewa ndani ya gari. Nilitoa toa zile nyaya za chini ya msteringi japo nifanye kama majambazi wanavoibaga magari bila kutumia ufunguo, napo halikuweza hata kuwaka. Hasira kali zikanijaa huku nikijihisi kama nimepatwa na kwikwi ya ajabu. Nilihisi mapigo ya moyo kwenda tena haraka haraka mithili ya mtu mwenye presha tena ile presha ya kushuka. Muda wote niliyatoa macho kwenye gari na upande wa pili wa barabara ambapo ndipo Biggy alikuwa akiielekea na yule mfanyakazi wa Aisha. Kwa upande wangu sikuwa na ujanja wa kuwasha gari lile niliokuwepo tena zaidi ya kusubiri miujiza itendeke lijiwashe lenyewe.“..ooh Mungu wangu sasa Biggy atakuwa wapi..? au..?”Kwa muda mfupi tu niliokuwa naendelea kukodoa macho kwenye gari la Biggy upande wa pili wa barabara. Mara kwa ghafla nikawa sipati majibu huku nikiona kama vile miujiza imetendeka ndani ya muda mfupi. Nilimuona yule mfanyakazi wa Aisha akitoka huku mikononi wake akiwa kamshikilia mtoto. Sikutaka kumlazia damu hata kidogo hapo hapo namimi nikaanzisha safari mpaka pale kwenye lile gari la Biggy na nilipofika nikamshuhudia Biggy akiwa mahututi huku damu nyingi ikimtawala maeneo ya tumboni mwake. Hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikanituma moja kwa moja huenda ile bastola ndio iliyosababisha yote hayo.“..pumzika kwa amani Biggy na namshukuru huyu binti kwa kuweza kunipunguzia mzigo kwani ni lazima ningekuua tu popote ulipo..?”Nilijisemea kimoyo moyo huku nikimshika Biggy kifua chake nakukisogeza kichwa changu mpaka kifuani mwake kuhakikisha kama kweli amekufa au la..!! Ni kweli kabisa Biggy alikuwa ameshakufa na mbaya zaidi pembeni yake niliishuhudia ile ile bastola alionitisha nayo yule Binti kipindi kile ikiwa imetapakaa damu chini.“..Pumzika kwa amani Biggy.., Ameni..!!”Nilimwambia Biggy japokuwa tayari alikuwa ameshapoteza uhai wa kuishi tena. Nilichokifanya niliichukuwa ile bastola nakuifuta futa kwenye kile kisketi alichokuwa amenipa Aisha pindi nilipotoka tu kuoga. Niliifuta vizuri nakutoka nje ya lile gari la Biggy haraka haraka huku nikiongoza njia ile niliyemuona yule mfanyakazi akielekea.Giza lilikuwa ni tororo sana na mbaya zaidi hakukuwa hata na mtu niliyeweza kupishana naye. Vichaka vidogo vidogo vilikuwepo japokuwa kwa mbali kidogo kulikuwa na taa nyingi zikimulika kuashiria kuwa kuna makazi ya watu maeneo yale. Ilinichukuwa kama dakika mbili mzima mpaka pale nilipomwona yule binti aliyemchukuwa mwanangu Adrian akiendelea kutembea peke yake. Nilianza kutembea hatua mbili tatu kwa haraka haraka huku nikijificha ficha pembezoni mwa barabara isiweze hata kuniona. Hatimaye mwendo wangu wa haraka haraka ulinisaidia kumfikia mpaka karibu ambapo kama machale yalimcheza akasimama kama sekunde kadhaa huku akiangalia mbele kisha akageuka nyuma kwa haraka huku akitingisha kichwa chake kwa dharau kana kwamba ameshaniona ama ameshajua mchezo mzima ninaotaka kumfanyia. Bado nilibaki namshangaa japokuwa hakuonesha hata wasiwasi. Nikiwa bado katika hali yakumshangaa huku nimejibanza pembezoni mwa barabara mara nikashuhudia mwanga mkali ukimulika eneo lile aliekuwepo yule binti halafu ule mwanga ukatoweka ghafla nakumshuhudia yule mwanangu Adrian akiwa peke yake pale chini huku kafunikwa na ile khanga niliyomfunika mara ya mwisho. Sikutaka kuonesha woga wowote zaidi ya kusogea mpaka karibu na eneo lile huku nikiendelea kujibanza na kujipa moyo uliochanganyikana na nguvu za kijasiri.“..Tina mwacheeee..?? mpumbavu weee..??”Kitendo cha mimi kumkaribia mwanangu Adrian papo hapo nilishtuka kusikia sauti mbili mbili za kike huku zikinisihi nimuache Adrian nisimshike. Sikutaka kuafikiana na zile sauti niliamini tu moja kwa moja atakuwa ni yule binti tu. Kutokana na ile bastola nilioichukuwa kwenye gari la Biggy ilinijaza nguvu za ajabu nakujikuta nikimchukuwa mwanangu Adrian nakumkumbatia kwa nguvu zote kisha nikaanza kutimua mbio huku nikiinyoosha ile barabara ya lami. Njia nzima sikutaka hata kugeuka nyuma japokuwa nilihisi kama nakimbizwa na umati wa watu kimya kimya. Jasho lilianza kunizunguka katika mwili wangu huku macho yangu yakianza kukosa uwezo wa kuona njia. Nilizidi kumkumbatia mwanangu Adrian kwa nguvu zote kifuani. Adrian alilia sana lakini sikuonesha kumbembeleza zaidi ya kuendelea kukimbia huku nikijiwekea imani kuwa nitasimama huko mbeleni endapo nitasikia zile kelele za watu wanaonikimbiza zikinyamzaza zenyewe.Hatimaye baada ya kukimbia kwa muda mrefu kidogo kukanipelekea kuishiwa kabisa pumzi nakujjikuta nikipunguza spidi ile niliokuwa nayo mwanzoni. Kwa muda huu nilisimama huku nikihema juu juu nakugeuka nyuma kwa ujasiri wa hali ya juu. “..Mungu wangu..!!! uhh uhh uhhh…!!!”Maskini Tina mimi niliweza kuona umati wa watu tena wengi wao wakiwa ni wazee, wakiwa uchi wa mnyama na kati ya hao wale waliokuwa mstari wa mbele niliweza kuwatambua kwani walikuwa ni wale wabibi wa kule Bagamoyo ambao walinisumbua sana kipindi kile nilivyopewa lifti mpaka nikatupwa kijijini maeneo ya karibia na Dodoma. Niligeuza macho yangu huku na kule huku mwili na hisia zangu zikiruhusu hali ya uwoga na kutetemeka kwa mstuko. Niligeuza tena macho yangu vizuri ninapoelekea napo sikuona tena njia zaidi yakuona kama mawingu huku wale wachawi wote waliowahi kunifanyia vibaya nikiwashuhudia na wamojawapo ni mke wa Steve yule ndugu yake na Jerry wa Bagamoyo, mwingine ni Shebby yule dereva boda boda wa Bagamoyo ambaye alinifanya vibaya mpaka nikajikuta nipo makaburini kule Bagamoyo. Kiujumla nilikuwa tayari katika himaya ya wachawi tena wale wachawi sugu waliokubuhu.“..haya mlete huyo mtoto mweyewe kabla hatujaamua kukuua kabisa..?”Aliropoka yule mfanyakazi wa Aisha tena kwa kujiamini huku akiniangalia kwa macho ya mg’aro wa ajabu. Nilijikuta nalegea mwenyewe nakumbusu mwanangu Adrian kisha nikamkabidhi yule binti ambaye alikuwa kitu kimoja na hawa wachawi. Kichwa kilinijaa maswali mengi yenye majibu ndani yake hata nikaamini kuwa Biggy atakuwa ameuliwa kwa nguvu za kishirikina na huyu binti. Walimchukuwa mwanangu Adrian kisha wakanicheka huku wakimkata kinanii chake mithili ya dokta anavyomtahiri mtoto mdogo wa kiume na kisha wakaanza kugombania damu damu zilizokuwa zinamwagika mwanangu Adrian..Nilijikuta uvumilivu ukinishinda Tina mimi nakuingilia kati ambapo kabla sijamfikia karibu mwanangu Adrian nilijikuta navutwa kwa kutumia kucha zenye ncha kali.“..we..!! we..!!! weee….?? Unataka kufanyaje..?”“nipeni mwanangu..??, nipeni mwangu nimesema..?”Sikuonesha kuwaogopa hata kidogo hawa wachawi kwani kwa sasa nilishawazoea na kama chanjo walishanichanja na kuniharibu karibu mwili wote. Niliamini liwalo na liwe na kama ni kufa Tina mimi basi wacha nife leo tena kwa kumgombea huyu mtoto mpaka nihakikishe nimempata.******Giza bado liliendelea kufunika karibu eneo lote. Niliweza kuyafumbua macho yangu japo kwa taabu sana mpaka nikajikuta naishiwa nguvu ya kuangaza. Kila mmoja alionesha kuwa bize na kile alichokuwa akikifanya. Sikuweza kuinuka chini nilipokuwa nimelala zaidi ya kugeuza macho tu na shingo huku nikiangaza huku na kule.”..hapa ni wapi..? nakuuuliza wewe hapa ni wapi..?”Nilishikwa na hasira kali huku niukimfokea dada mmoja aliokuwa amevalia kivazi kifupi kilichotengenezwa kwa kutumia magome ya miti. Muda wote alikuwa yupo pembeni yangu huku kashikilia burungutu la manywele ya binadamu akiyafumua kwa haraka haraka.“..unasemaje..??”“wewe ni nani na hapa ni wapi..? kwanza nani kanileta hapa..?”“…hee..!! hee…!!! heee!! Unachekesha kweli wewe..? yaani hizo chanjo zote unataka kusema hujitambui tu wewe ni mtu wa aina gani..? kwa taarifa yako hapa ni kwa mababu na mabibi zetu yaani hapa ni kuzimu..?”“sasa nimefikaje fikaje..? nani kanileta..?”“.. wewe si umeletwa na dad..”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Kabla hajamalizia kujibu nilishangaa yule mdada aliyekuwa akinijibu kushikwa kwa nguvu na mtu nisiyemfahamu nakuanza kuburutwa.“na wewe huna kazi hapa umelala lala tu..?”Mzee mwingine alinifuata nakunigombeza .Hata sikuwa namfahamu kwani uso wake ulionesha dhahiri umejereuliwa na vitu vyenye ncha kali. Na hakuwa na masikio wala pua na hata meno yake yalikuwa yamechomoza mithili ya picha zile za kutisha za mazombi. Yule mzee alininyanyua na kuniburuta kama alivyomfanya yule dada huku akinipeleka sehemu ambayo hata sikuwa naifahamu.“..huyu hapa mpeni kazi siyo analala lala tu hapa..?”Maskini Tina mimi tayari nilikuwa katika himaya ya wachawi na kwa sasa walinileta eneo ambalo walikuwa wakiwachinja watu nakuchuja damu zao na kisha wanazichemsha nakuwa supu ya kijani kijani. Nilikabidhiwa mwiko mkubwa kwa ajili ya kupindua pindua zile damu ili zisifuke katika sufuria. Katika maisha yangu huwa nayasikiaga tu mambo ya kichawi lakini leo hii nimeweza kujionea mwenyewe. Tayari nilikuwa kama mtumwa wao huku kina dada wengine wakija na mabakuli ya bati kuja kuchota ile wanayoiita supu ambayo ni damu damu za watu zilizochemka sana.Nikiwa bado kaika hali ya kuwatumikia tena kwa uoga wa hali ya juu mara.“hee..?? Unaitwa nani..? we mzuuriii..?”Alikuwa ni binti mdogo sana na aliponiona tu alinikimbilia nakunisogelea, kwa muda huu alionesha kunijia kwa ukaribu zaidi. Sikutaka kupoteza nafasi kwani watu waliokuwa wakizifuata zile damu walikiwa wamepungua. “..kwani hunijiui..? mimi mwenzako nimeletwa jana..”Nilimjibu yule binti mdogo dogo kwa kujiamini huku nikitaka kumdadisi kitu kutoka kwake.“..eti mwanangu umemuona wapi kwani wamemleta hapa na simuoni..? ni mchanga sana..?”“ahaa ndio wewe kumbee..? ujue hapa watoto wadogo wote tunawachanja chale mapajani mwao na kuwapeleka kuleee.. na mwanako yupo kule kule..!!”“wapi huko..?”“wanaishi kule kwani na wao huwa tunawatumia usiku kwenye malindo yetu..?”“..unasemaje..?”*************************.”Ndio hivyo kama nikuambiavyo kuwa hawa tunawatumia katika malindo yetu kwa muda wa usiku..?”“..sasa mnawatumiaje tumiaje..?”“..huwa hairuhusiwi kumwambia mtu yeyote lakini kwa sasbabu na wewe upo hapa kundini mwetu basi haina budi kukuambia kila kitu..”“..enhee niambie basii..?”“..yaan ni hivii, watoto wadogo tena wale wachanga kabisa huwa tunawachanja chanjo kwenye nanii zao vivyo hivyo mpaka kwenye vitovu vyao huwa tunawawekea alama ya herufi 666 na 999..”“…na baada ya hapo..??”“..baada ya hapo sasa wanakuwa wanatenda matendo kama watu wazima na wenye kujielewa kwa kusaidiwa na nguvu zetu za kishirikina na pia hata watu wa duniani inakuwa si rahisi kuwatambua kwani watoto hawa wana uwezo wakubadilika badilika kama wanyama..”“sasa ni wakina nani wanakuwa na mamlaka ya kukaa nao karibu au kwenda kuwatumia..?”“..Mtu yeyote ana mamlaka ya kuwatumia lakini endapo tu tamko litatoka kwa mkuu wetu kama unatakiwa kwenda sehemu fulani kufanya tukio..”Kila akiendelea kuniambia huyu binti na mwili wangu ulikuwa katika msisimko wa hali ya juu huku nikitamani sana hata iwe ndoto au kama inawezekana kwa muda huu huu niweze kwenda huko walipo hao watoto..”“naomba unipeleke basi mwenzangu..?”“..mhh..!! we nenda mwenyewe bwana kwani masaa machache yaliotoka nilikuwa na mtoto mmoja nikimchanja sasa endapo mkuu wetu akiniona tena maeneo yale ataweza kunifanyia vibaya..”Nilijipa moyo wa kijasiri nakuanza kuchomoka huku nikielekea sehemu husika walipo kundi la watoto ambao ndio wanatumika katika kuchezeshwa kama mizukule. Niliogopa sana lakini haikuwa na jinsi kwani lengo langu kubwanilitamani sana nimuone mwanangu Adrian japo nimtie mikononi mwangu nitaridhika. Kila nilivyokuwa nikipiga hatua ndivyo na halmashauri ya ubongo wangu nilihisi kama inamwagiwa barafu kali. Kitendo cha kufikisha mpaka hatua tano tu huku nikipishana na baadhi ya wazee wengine wakiwa hawajiwezi kabisa mithili ya wale omba omba wa mjini tena wale wenye ukoma. Wengi wao walikuwa wakinitolea macho tu nakupishana nao. Ardhi ilikuwa laini kama imewekewa manyoya huku ubaridi wake nikiufananisha na ule wa kwenye friza japokuwa haukuwa ukitetemesha miguu yangu kwa ubaridi wake. Sikutaka kukata tamaa zaidi ya kuendelea kusonga mbele huku mikono yangu nikiiweka kwa nyuma japo kiuoga uoga mpaka nilipokaribia eneo lile ambalo nilielekezwa na yule binti kuwa mwanangu Adrian na wenzake wapo maeneo haya. Hatimaye baada ya mwendo si mrefu sana na kwa mbali kidogo nikaanza kuhisi sauti za watoto wakilia kwa sauti kubwa. Na kwa muda huu sauti zile zilionesha kupaza sana japokuwa zote zilikuwa zikitokea eneo moja tu. Nikiwa katika hali ya kushangaa zile sauti bila ya kujua zinatokea upande gani mara kwa ghafla nikaanza kuhisi kama mtu ananishika kwa upande wa mgongoni. Taratibu niliinua mkono wangu wa kulia nakuanza kama kujipangusa kwa begani ambapo ndipo nilipokuwa nahisi kuna mtu ananishika. Ile hali ya ubaridi mkali tena ule niliokuwa nikiufananisha kama utakao kwenye friza kwa muda huu ukawa umetawala nakufika mpaka katika bega langu la upande wa kulia. Kila nikijitahidi kujipangusa tena bila kugeuka nakuangalia ndipo na ule ubaridi nikawa nauhisi kama unaniyeyukia katika bega langu taratibu ukivuja maji.“..Niache hukoo..??, niacheee…????”Nilitoa sauti kubwa na ya kupaza kabla sijageuka nakutambua ni mtu gani aliokuwa akinigusa ama kuniwekea kitu cha ubaridi katia bega langu la upande wa kulia. Maskini Tina mimi macho yangu na hisia vilikuwa tofauti kwani nilipogeuka tu nyuma ili kugundua ni nani, kumbe alikuwa ni kitoto kichanga kimenigandia kwenye bega langu la upande wa kulia. Nilijitahidi kuangaza kwa macho makali japo kumgundua vizuri yule mtoto lakini nilichoambulia kumgundua ni miguu tu kwani miguu ilionesha fika ni mtoto tena mchanga. Kila nikijitahidi kuichukuwa ile miguu yake nakuivuta kwa mbele kwa dhumuni la kumshusha begani kwangu lakini hali haikuwa hivyo kwani yule mtoto alianza kuyeyuka na kuwa barafu tena lile lichanganywalo na maji ya moto. Kuyeyuka kwa yule mtoto nakubakiwa miguu tu ndiko kulikuwa kukiendelea kunitisha huku nikiihisi kama vile nimeua kwani kiwili wili chote cha mtoto kilikuwa hakipo. Ndani ya muda mchache na ile miguu yote ikapotea kwa ghafla sasa nikabaki mimi kama mimi peke yangu. Sikuonesha kukata tama nikaendelea kupiga hatua nyingine mbele mpaka nikakutana na kundi kubwa la watoto wakiwa wamelala chini kabisa tena uchi wa mnyama.Zoezi la kumtambua mwanangu Adrian kati ya wale watoto waliokuwa chini likaanza. Baadhi yao walikuwa wakifanana mithili ya Wachina hivyo ikanipa wakati mgumu wa kumtafuta mwanangu Adrian.“… hapo hapo tulia na wala usiondoke…?? unafanyaje hapo muda huu na hao watoto..?”Haraka haraka nikageuza macho yangu kwa hofu ya hali ya juu huku nikiifuatilia sauti ilipotokea. Maskini nikamshuhudia mzee mmoja aliokuwa ana mvi nyeupe katibu eneo lote la usoni mwake. Nilishusha pumzi kwanza nakukata fundo la mate kisha nikamjibu.“..namhitaji mtoto mmoja simuoni Mzee..”“.. kwa ruhusa ya nani..? kwanza kwanini unanitiita Mzee hapa..? au hujafunzwa hapa wewe..? niite Mkuu..?”“..sawa mkuu nimekuelewa..”“haya unataka mtoto yupi na wanini sasa hivi..? kwani hapa kuna utaratibu wake kama mtu anataka mtoto..?”“..nakuomba sana muongozo Mzee..?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“..nimekwambia usiniite Mzee husikiii..?”Maskini Tina mimi nikawa kama vile nimefanya kosa kumuita Mzee badala ya Mkuu.. Alifanya ishara ambayo sikuitambua kisha nikashuhudia wametokea Mabinti kama watatu na mmoja wapo akiwa ni yule aliyekuwa mfanyakazi wa Aisha na kwa muda huu walikuwa uchi kabisa japo eneo la kwenye sehemu zao za siri ziliwekewa kitu kama mwanga mkali ambapo hata ufanyaje huwezi kugundua kama ni sehemu za siri. “..huyu mkamfunde kwanza halafu mumlete hapa amesema ana shida sana na mtoto na sijui ni mtoto gani..?”“..aliongea yule Mkuu ambaye nilimkera kwa kumuita Mzee badala ya Mkuu.Safari ya Tina mimi kutoka katika lile eneo niliokuwepo namfuatilia mwanangu Adrian kuelekea mpaka eneo nisilokuwa hata nikilifahamu ilianza huku nikiburutwa na wale Mabinti watatu. Yule mfanyakazi wa Aisha nadhani sijui alikuwa amenisahau ama ndio alikuwa kazini..? kwani hakuonesha hata kuwa na kumbukumbu vizuri juu yangu nilichokuwa nimekifanya wakati nipo nae sehemu huru ya duniani. Alisaidiana na wenzake kuniburuta. Japo kulikuwa kunatisha sana lakini kiukweli nilipapenda sana kwani hakukuwa na ardhi zaidi ya manyonya tena malaini sana kama yale ya sufi.“..Unatakiwa upige hatua kuanzia hapa mpaka unafika upande ule kulee halafu utaonana na Mama na Bibi zetu na kisha watakumbia nakukupa kitu hivyo utarudi tena hapa hapa ukipitia njia hii hii tunakusubiri kisha tutakurudisha kwa Mkuu wetu uliyemkuta kule kwa watoto..”Aliropoka kwa sauti ya ukali naya kukemea huku akisisitizia yule mfanyakazi wa Aisha huku akionesha macho ya ukali na meno yakimtoka mithili ya zile picha za kutisha.Nilifanikiwa kukanyaga zile nilizokuwa nimeambiwa. Miili mingi ya watu waliokufa ndio ilikuwa njia kuu. Na hata nilipofika katikati nilijikuta nikitema mate nakutapika nyongo hapo hapo chini nakuweza kuhamsha maiti moja.“..futa mate yako..?? nimesema futaaa….?”Ile maiti ilishtuka nakuamka kisha ikanikalipia kuwa niifute mate niliokuwa nimemtemea. Haraka haraka nilivuta nguo yangu nakuifuta eneo niliokuwa nimetema mate kisha ile maiti ikajirudisha pale pale ilipokuwa nakulala hivyo kuniacha nikiendelea na safari yangu ya kuendelea kuzivuka hizi maiti zingine. Hatimaye Tina mimi nikafanikiwa kuzivuka zile maiti zote mbele yangu na sasa nikawa upande wa pili huku nikigeuka nyuma nakuwatazama wale Mabinti niliowaacha kwa mbaali.“..sasa umeingia katika ulimwengu mwingine wa mafunzo..”Alikuwa ni Mbibi mweupe fupi sana akiongea na mimi huku akiniwahi kunishika mikono nakuniongoza katika eneo jingine nalo sikulijua hata ni eneo gani.. Nilipelekwa eneo ambalo sikuweza hata kuliamini kwani kulikuwa kama vile duniani. Mwanga mkubwa mithili ya jua, pipa kubwa lililokuwa limewekewa vitu vikiendelea kuchemka na huku wakina Mama wengine wakipakuwa. Hakukuwa na mwanaume hata mmoja. Na punde akanifuata mama mmoja alioonesha anachongo yaani haoni upande mmoja.“..karibu Binti..? unatakiwa unywe hii hapa halafu urudi ulipotokea..”“..hapana jamani siwezi kunywa..?”“..Binti..? yaani usije ukathubutu kusema hivyo tena kwani utafanywa kama wale uliopishana nao wamelala kwa hapo nje..!! Embu kunywa halafu ukamchukue huyo mtoto maana hiki ninachokupa kitakutia nguvu za kuweza kufanya jambo lolote huko ukiwa na mtoto bila ya kugunduliwa na mtu yeyote..”Nilijitahidi sana kugoma kata kata na hata kuwatishia naondoka zangu lakini haikuwezekana kwa Tina mimi kwani kilichofanyika nilishikwa kwa nguvu zote nakulishwa huku nikitishiwa kuwa endapo nitatapika nitaweza kuwafufua wale watu waliotandikwa chini hapo mlangoni hivyo mimi nitachukuwa nafasi yao kulala nakukanywaga kama mfu.. Maskini Tina mimi sikuwa na jinsi tena zaidi ya kukubaliana na ukweli japo nilikuwa siamini kwa asilimia zote lakini illinibidi kuamini hivyo nikaongezwa tena nakufakamia yale matapu tapu yao yaliochanganyika kama mauji uji hivyo hivyo nikijikaza nakutoka nje huku nikitoka nje nakuanza kuzikanyaga zile maiti kwa lengo la kuzivuka.Nilipofika katikati kabla sijamalizia kuzivuka zile maiti zote mara kwa ghafla nikajihisi kama kichefu chefu kikitawala katika kinywa changu huku kikiupa mdomo nafasi kuwa wazi nakuanza kutapika kile nilicholishwa na wale kinamama.. Nilitapika sana ukichanganyia na kukohoa hovyo. Maskini Tina mimi kitendo kile kikawa kama kimehamsha zile maiti nilizokuwa nimezikanyaga kama njia ya kuvukia upande wa pili. Walianza kuinuka mmoja baada ya mwingine huku wakinicheka kwa sauti za juu. Hapo hapo nikaaza kutambua baadhi ya maiti zilizoinuka. Niliweza kumshuhudia Mchungaji James akiwa kashikilia kitu kama ile Bibilia yake, Biggy akiwa na nguo zake zile zile nilizomwacha nazo mara ya mwisho, Baba Latifah naye alikuwa kamkumbatia mwanake Latifah na mwisho kabisa nikamshuhudia Aisha na Jerry wakishikana mikono huku wote kwa pamoja wakinifuata eneo nililiokuwa nimesimama. Na kwa upande wa Jerry alikuwa amebabuka maeneo ya usoni huku akimshikilia Aisha wake ambaye naye Aisha hakuwa anaona Vizuri zaidi ya kuonesha akifikicha macho kwa shida.“..Inaamaana Aisha na Jerry walikufa..?”Nilijikuta nimezubaa huku naongea mwenyewe na punde karibu wale wote waliokuwa wamefufuka wakawa wameshanikaribia kwa ukaribu huku baadhi yao wakinishikilia mabega kwa dhumuni la kuanza kunitafuna tafuna kisha wanilaze chini…Sasa nikavaa uhusika wangu wa Tina yule wazamani huku nikitimua mbio kuelekea sehemu ile niliowaacha wale mabinti. Kila nikijitahidi kupiga hatua kuwakimbia hawa watu waliofufuka nao walikuwa wanazidisha makelele ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanatibua ngome za masikio yangu sambamba na kuniletea msisimko wa ajabu ule uliochanganyikana na uwoga ndani yake. Baada ya muda mchache nilijikuta nimelowana karibia nguo zote si kwa jasho tu bali kwa yale matapishi niliokuwa nimeyatapika na kwa sasa yalikuwa yanasambaa katika mwili wangu wote huku yakileta harufu kali mithili ya gari la taka likikatiza katika umati wa watu wastaarabu.“..niokoeeni jamani..?? nyieee…?”Nilijitahidi kupiga makelele sana kwa upande wa mbele yangu kule nilipokuwa nimewaacha wale mabinti lakini haikuwa na msaada wowote zaidi ya kuwashuhudia wakinicheka huku wakipeana ishara ya mikono kana kwamba wananicheka kinafiki.“..Wee si Tina..? leo umejileta mwenyewe..? mwanangu yuko wapi..?”Alizungumza Jerry kwa sauti ya ukali. Maskini kwa upande wa uso wake eneo la mbele karibia lote lilikuwa limeharibika vibaya na hapo hapo halmashauri ya ubongo wangu ikafanya kazi haraka nakugundua kuwa huenda yale maji aliomwagiwa na yule mfanyakazi wa Aisha ndio yaliomsababishia ulemavu wake.“sasa inamaana hata huyo binti hamtambuai kama yupo humu humu ama..? na Aisha si huyu hapa anaonekana mzima tu..?”Ni kati ya maswali niliokuwa nikijiuliza mwenyewe bila ya kupata jibu huku nikiendelea kuwatolea macho mbele yangu ambapo tayari nilikuwa nikiwasubiri wanifikie karibu na kama kuna lolote wacha litokee tu kwani sikuwa tena na jinsi.Mapigo yangu ya moyo tayari yalikuwa yameshaushinikiza ubongo kukata tamaa kabisa kwa muda huu. Kiukweli walikuwa wanatisha kwani baadhi yao walikuwa hawana hata midomo sasa sijui ndio walikuwa wametoka kupata ajali ama la! Waliponifikia karibu kabisa walinizunguka huku Aisha akimshika Jerry wake mikono nakuanza kunikumbatia kwa kutumia nguvu zao zote. Walinikumbatia kwa nguvu zote mpaka nikahisi kuishiwa nguvu nakudondoka mpaka chini kabisa ambapo napo wote waliiinama mpaka chini nakuanza kunilamba lamba mithili ya zile koni za bakhresa.“..tumeghairii hatumtaki tena mwanetu..? tunakutaka wewe na piga ua hapa tunahakikisha tumekula nyama yako kisha tunakulaza pale tulipokuwa tuumelala!!”Waliongea wote kwa pamoja tena kwa sauti mbilimbili huku kila mmoja akigawana kiungo chake. Kuna waliokuwa wananishika matiti yangu nakuyavuta, wengine makalio yangu wanayafinya finya na hata baadhi yao walikuwa wakinichezea sehemu zangu za siri kwa kuzivuta vuta kwa nguvu kiasi cha kunisababishia maumivu makali sana mwilini mwangu. Maskini Tina mimi nikawa sina jinsi zaidi ya kuanza kuhisi kizungu zungu kilichochanganyikana na kukata tamaa ya kuishi nakujiona sasa huu ndio mwisho wangu wa kuishi.“..kwanini Tina mimi..?? kwanini jamani..??”NIliusemea moyo wangu pale chini huku ule umati wa watu wafu ukiendelea kunizingira nakunishika shika kila eneo la mwili wangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/********Saa saba za mchana jua lilikuwa kali sana. Kila mmoja alionekana akiwa na kitambaa cha kufutia majasho na hata wengi wao waliokuwa na hela waliweza kujipooza makoo yao kwa kukata kiu kwa kinywaji baridi chochote. Mwili wangu wote ulikuwa mweusi sana kutoka kwenye weupe ule niliokuwa nao kipindi cha nyuma. Nilijishika kichwani napo sikuwa hata na nywele zaidi ya ule ule upara wangu. Nikiwa bado katika hali ya kujishangaa mwenyewe mara akapita Dada mmoja mbele yangu nakumsimamisha.“..hapa ni wapi na nani kanileta hapa..?”“..hapa mbona ni Manzese Darajani kwani wewe hulijui hilo hapo Daraja..? au umetoka kijijini leo nini..?”Tina mimi sasa sikuwa hata nakumbukumbu kabisaa. Japo ni kweli macho yangu yalitazamana na Daraja kubwa lakini nafsi yangu ilikataa kabisa kuamini kuwa ni darajani Manzese kama alivyonimabia yule Dada kuwa hapa ni Manzsese darajani. Nilitoka katika lile eneo taratibu huku nikiongoza mpaka kituo cha dala dala ili kuhakikisha kama kweli hapa ni Manzese. Kitendo cha kufika tu maeneo ya kituo cha daladala nikamsikia kondakta wa daladala akimwambia mtu kuwa hapa ni Manzese.“..sasa nani kanileta hapa..? na ilikuwaje kuwaje mpaka nimefika hapa..?”Bado nilikuwa mtu wa kujiuliza mwenyewe bila ya kujipatia majibu akilini mwangu. Kila nikijitahidi kuvuta kumbu kumbu inanirudisha mpaka nyumbani Mwanza halafu basi sielewi ikawaje.“..embu ngoja.., Mwanza..?? Mwanza…??, Mchungani James halafu nikarudi Dar, Dar…? Dar…? Jerry..? aha haaa Aisha..? yap Aisha alinipeleka kwake halafu kama nilijifungua, Mwanangu yuko wapi..? Mwanangu yuko wapi..?”Maskini Tina mimi akili ikawa kama imeshaniruka kwa sauti ya ukali nikaanza kukimbia huku na kule nikipiga kelele kudai mwanangu. Baadhi ya watu walinishangaa na waliniona kama chizi lakini kiukweli ndio kumbukumbu zilizokuwa zimenirudia japo kidogo niliweza kutambua kuwa nilikuwa na mtoto. Nilikimbia huku na kule mpaka nikachoka mwenyewe kisha nikatafuta sehemu yenye kimvuli nakukaa chini huku nikichomoa matiti yangu nakuanza kuyakamua kwa nguvu.“..nyonya mwanangu nyonyaaaa.. nyonya enhhh..?”Bado nilikuwa katika hali ya kutojielewa elewa japo kidogo kidogo nilianza kupata ufahamu. Niliyarudishia maziwa yangu nakuanza kuongoza moja kwa moja kwenye kituo cha daladala kisha na mimi nikawa nasubilia kama abiria wengine.“..hatupakizi vichaa..? weee Dada unakwenda wapi embu shuka huko..?”Kwa hasira niligeuza jicho langu nakumtizama vizuri yule kondakta ambaye alikuwa hataki mimi nipande nakuniona kama chizi.“..mwacheni apande mimi nitamlipia, hivi nyie makondakta hamnaga hata utu..?”“wee mama vipi yaani ufanye utu kwa machizi ka hawa..?”Waliendelea kubishana huku Tina mie nikiingia ndani ya daladala wala hata sikujua inaelekea wapi zaidi ya kuingia na kukaa kwenye siti. Baadhi ya abiria waliokuwa pembeni yangu walikuwa wakiziba pua zao kana kwamba wamesikia harufu mbaya huku baadhi yao wakininyooshea vidole. Ilinibidi kuwa zaidi yam pole Tina mimi.Mwendo wa dakika kama ishirini ulitosha kabisa kufika mwisho wa kituo. Bado sikuwa na kumbukumbu ni sehemu gani zaidi ya kuendelea kiukodoa macho tu.“….Binti unaonekana unamatatizo sana ..?”“..wala mama sina hata tatizo..?”Hapana mwanangu sura yako inaonesha kabisa unamatatizo kwani nyumbani wapi..?”Aliendelea kunihoji yule Mama alienilipia nauli kwenye daladala na kwa kipindi hiki tulishuka naye pamoja ambapo alinisogelea nakuanza kuniuliza. Nilimjibu kwa shingo upande lakini hakuridhika zaidi ya kunishika mkono nakukubali kwenda naye huko kwake..***Unavyodhani huko anapopelekwa Tina kutakuwa salama kweli..? na huyo Mama ni mtu mwema kweli na nini hatma ya Tina katika story hii,..?***Biggy, Aisha, Baba Latifah na mchungaji James tayari wameshakufa hivi Tina kazi aliobakiza ni kwa Steve bagamoyo, Shebby huko huko Bagamoyo, Vonso, John mdogo wake Jerry ndio watakaofuata je unavyodhani itakuwaje kwa hao watu..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ MWISHO 

0 comments:

Post a Comment

Blog