Chombezo : Mrembo Mcharuko
Sehemu Ya Tatu (3)
Basi niligandisha macho yangu mwilini mwake namtazama, Dominic alikuwa na six pack yaukweli uku anagarden tumboni adi niliisi mwili kunisisimka japo sikuwahi kushiriki mapenzi ila alionyesha alikuwa anafanya mazoezi sana nakuuweka mwili wake vizuri yani kwa msichana mpenda mwanaume handsome ambae hana kitambi kwa uyu babamdogo alimpata basi nikazidi kumtizama uku nikikumbuka siku tuliyoenda kumpokea airport pia hakuwa mtu wakushinda nyumbani mara nyingi alikuwa anatoka kufatilia kazi zake, nakumbuka ata sikukuu ilipofika alinipatia elfu arobaini ninunue nguo na bibi nae akanipa elfu ishirini.
Izo nguo nilizonunua sasa majanga! Kitop kilichonibana maziwa tu na chini kipensi kifupi kama dance wa Koffi Olomide vile, basi nikazidi kukumbuka nilipokutana na marafiki zangu wakanishawishi twende club tulipofika wakaagiza pombe mmoja Tusker mwengine Castle namimi nikaletewa Castle lite niligoma lakini wakaniomba nakunishawishi adi nikanywa, wenzangu wakapata mabwana humo humo club mie waliponitafutia mwanaume nilikataa basi walipotosheka kunywa wakaondoka nakuniacha nimelewa sana nakumbuka alikuja mwanaume mmoja akanishika mkono basi sikujua ilikuwaje adi sasa niliposhtuka nipo Lodge na babangu mdogo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wewe Lisa ivi nani kakufundisha kunywa pombe?
Aliniuliza Dominic, nikashindwa ata lakumjibu
"Yani jana kama kabati nikaingia pale club nashangaa nikakuona wewe ndo umelewa hujielewi tena wanaume walikuwa wanakumendea nikaamua nikuchukue nakukuleta apa ulivyokuwa tungi vile isingekuwa poa nikupeleke nyumbani"
Aliongea akinieleza nilibaki kimya najilaumu tu.
"Ba mdogo nisamehe marafiki zangu ndio wamenishawishi"
"Unajua Lisa wewe si mtoto ni mtu mzima inabidi uwe na maamuzi yako sio unafata tu mkumbo"
"Sawa nimekuelewa lakini nitarudije kwa bibi nitasemaje?"
Sikuwahi ata siku moja kulala nje niliogopa sana.
"Usijal tutaenda wote ebu kaoge kwanza mie tayari"
Alinambia tatizo likaja nitainukaje na izo nguo nilizovaa, Mara nikamuona anacheka
"Mbona huendi sasa unaogopa nini wakati mimi ndio nimekuleta adi apa ndani?"
Baba mwenyewe kijana nikaona sio kesi nikainuka nakwenda chooni nikabadirisha nguo nakuvaa gauni
Lefu nililotoka nalo nyumbani niliweka kwenye handbag langu.
Basi nilipotoka nikamkuta Dominic nae ameshavaa tukaondoka nakuelekea kwenye mgahawa kwanza tukanywa chai baada ya apo tukarudi nyumbani.
****
"Aya mtu na mwanae mnatoka wapi maana jana wote hamjalala ndani sikukuu iliwanogea eeh?
Kufika tu bibi akaanza maneno.
"Mama jamani ata salamu akuna?"
Dominic nae akasema
"Aya hamjambo?"
Basi tukamsalimia wote.
"Uyu mjukuu wako amelala kwa rafiki zake jana alienda mziki wakatoka muda mbaya kwaiyo akaamua alale uko alafu mimi mmmh naniliu mama ivi utaki mkwe kwani?"
Alisema nakumfanya bibi acheke
"Nataka umlete nimuone sio unaishia nae vichochoroni"
"Basi usijali nitamleta tu"
Apo tena kesi iliishi kila mtu akaingia chumbani kwake.
"Baba mdogo we noma duh siamini sijagombezwa"
Nilimwambia nikicheka tulipokuwa mezani tumekaa
"Mambo madogo sana ayo usijali"
Basi tulikula pamoja na Suzy nae alikuwepo.
Siku zikazidi kusonga uku nikiwa na marafiki wengi basi siku moja kuna rafik yangu mmoja akanambia nimsindikize kwenye harusi ya dadake anaolewa, nikamkubalia siku ikafika tukajiandaa nilimuaga bibi tukaenda adi uko ni mbali tena kijijini si uku nilipo mjini.
Uko ndo kwa babayake Mage uyo rafiki yangu.
Basi kulifungwa rusha roho ya nguvu apo mziki unarindima ile mbaya namimi ndo ugonjwa wangu huo, walipika chakula apo watu wakala muda wa kumchukua bibi harusi ukafika akaja mumewake na wapambe akachukuliwa baada ya apo watu wakaingia uwanjani nakucheza.
Mara akawekwa msaga sumu alipandisha mashetani yangu nikaingia kati sasa kama nilivyo kichaa sikubakisha kitu nilikata mauno balaa watu wote walinipisha nakuniangalia mie utasema anaeolewa ndugu yangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mage nae akawa anajishaua aoekane mie kanileta yeye basi wanaume si wakajua ilo nakuanza kumfata awaunganishe kwangu kuna ambao walimpa pesa akapokea bila kuniambia, Basi nilicheza apo adi hamu ikaisha nakutoka kupumzika ilikuwa jioni.
"Shosti unajua kucheza adi raha twende nikakununulie soda"
Alisema Mage nikakubali apo usiku ulikuwa umeingia saa moja.
Basi uko mapori mengi hakupo wazi sana.
Tukatembea adi dukani tukanunua tunarudi uku tunakunywa, tukafika sehemu moja kuna pori kubwa alafu akuna nyumba karibu apo,Mara kwa mbele tukaona wanaume watatu wamesimama barabarani.
"Mh Mage wakina nani wale wasijekutudhuru bure?"
Nilimuuliza
"Usijal bwana wapo na mambo yao twende usiogope"
Alinambia tukazidi kwenda tulupokaribia tu nikashangaa wote wamenishika nakunivutia pembeni kwenye kichaka
"Nyie wakina nani? Mnataka kunifanya nini Mageeee nisaidieee"
Nilipiga kelele lakini ni bure Mage alikimbia nakuniacha mikononi mwa hao wanaume
"Oya tulia uyo Mage amekula pesa zetu amekuleta uku kwaajiri yetu kwaiyo toa mzigo huo"
Alisema mmoja
"Dah alafu anamiuno balaa na ilo zigo sasa adi nilidindisha mchana nilipomuona asituzigue apa atulie kama ananyolewa"
Maneno waliyosema yalinifanya nguvu ziniishe kabisa bila kutegemea machozi yalinitoka nakujuta kuwa na marafiki wanafki alienisabababishia leo nataka kubakwa.
Mara nikashtuka kanga nilovaa imevutwa uko
Basi nilizidi kupiga kelele bila mafanikio yeyote wale vijana walidhamiria kunibaka ambapo kanga ilitupwa nikabaki na gauni fupi nililovaa ndani wakanilaza chali apo chini kwenye majani bila kujali naumia au vipi, mmoja akaja kunishika mikono na mwengine miguu akaitanua alafu mmoja nikamuona anavua suluali aningilie
"Mungu wangu nakufa mimi leo nimekoma kuamini marafiki najuta mimi"
Nilisema kimoyomoyo uku machozi ya uchungu yananitoka sikuweza kujitetea,
"Oyaa fasta basi piga mzigo nasisi tuufaidi"
Alisema yu alienishika mikono.
Nikamuona uyu kashavua nguo yake ananiinamia sasa nilisi nguvu zinaniisha pamoja na umapepe wangu lakin sikuwahi kushiriki mapenzi nilifikiria ayo maumivu nitakayoyapata apo tena si mwanaume mmoja ni watatu niliisi kufa kabisa mwili uliisha nguvu nikajikatia tamaa yakuishi.
"Lazima nijiue sitoweza kuishi tena kwa unyama ninaotendewa"
Nilisema nikizidi kulia.
Ghafla nikashangaa yule mwanaume aliekuwa juu yangu alipigwa na gongo zito akadondoka pembeni, mara sijakaa vizuri na hao wengine wawili nao wakapigwa wote wakapoteza fahamu apo apo.
"Uko salama dada hawajakuumiza?"
Alisema uyo mwanaume ambae alinisaidia sikuweza kujibu nilibaki nalia tu akanisogelea nakunisaidia kuinuka nikachukua nguo zangu nakuvaa baada ya apo akanishika mkono yule mwanaume nakuniambia niende kwao.
Tulifika ni nyumba ya udongo, akaingia ndani nakumuita mamayake ambae alitoka akamueleza amenisaidia nilikuwa nataka kubakwa uyo mama alihudhunika nakunipa pole baada ya apo nikaandaliwa maji yakuoga nilipomaliza nikaletewa chakula mwisho nikaonyeshwa chumba nilale, ni kitanda cha kamba niliogopa nikaweka mkeke chini nakulala apo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****
Maisha yangu mapya yakaanza apo kijijini ambapo sababu sikujua kule kwa bibi kunaitwaje kibaya zaidi simu sina niliiacha nyumbani sikuja nayo uku.
"Kwaiyo uku umeletwa na nani?"
Aliniuliza James ambae ni uyo mkaka alienisaidia
"Rafiki yangu anaitwa Mage ndie niliekuja nae pia ndo aliepokea pesa ya wale wanaume"
Nikisema neno rafiki moyo wangu unauma sana nilikoma kuamini kila msichana nakujenga mazoea nao.
"Pole sana kwaiyo bibi yako anaishi wapi?"
Aliniuliza
"Mjini kule bomba mbili sijui mi ata sikumbuki ndo mara ya kwanza kuja"
Niliongea uku matumaini yakurudi kwetu yakiwa hayapo.
"Sawa usijali ngoja nitafute nauli nitakupeleka kwenu"
Alisema James nikamuelewa.
Maisha ya apo nyumbani kwao yalikuwa ni yakawaida sana, hawakuwa na uwezo yani ni maskini.
Siku zilizidi kusonga pesa ilikuwa ngumu kupatikana, Asubuh na mapema baridi kali tunaamka mimi na Mama James tunaenda kisimani kuchota maji ni mbali nusu saa tunatembea, ni maisha magumu ambayo sikuwahi kuwaza kama kuna siku nitakuja kuishi niliamini ule usemi asiefunzwa na mamaye ufunzwa na ulimwengu kweli ulimwengu ulinifunza.
Siku moja nilipewa jiko nipike nikashindwa ilikuwa aibu kwangu msichana mkubwa sijui kupika! Basi yule mama akunisema wala kunitenga alianza kunifundisha kazi zote mwezi mmoja ulitosha mie kujua kilakitu nilimshukuru sana.
Bado pesa haikupatikana James alikuwa hana kazi maalumu yakumpatia kipato anaangaika tu siku anapata na siku anakosa.
Kuna siku tunalala na njaa nilishazoea maisha ayo nakuona kawaida tu.
Mama James alikuwa na mashamba yake akaondoka kwenda kulinda ngedere wasiaribu nakutuacha wawili nyumbani.
James alikuwa kijana aliejazia mwili yote kutokana na kazi ngumu anazofanya alikuwa mpole mcheshi sana tukiwa wote tunapiga story sana, wiki ikapita tukiwa wenyewe ukaribu juu yetu ukaongezeka adi tukajikuta hisia za mapenzi zinashamiri kwenye mioyo yetu.
Bila kutarajia tukawa wapenzi tuliopendana sana, usiku mmoja tukiwa tumekaa kwenye mkeka nje tukiongea nakucheka alinisogelea karibu nakunikiss
"James naitaji nikupe zawadi"
Nilimwambia akatabasamu
"Zawadi gani mkewangu?"
"Usichana wangu naomba uutoe"
"Unasemaje Lisa acha uongo we bado msichana?"
Aliuliza kwa mshangao asiamini
"Sijawahi kama siku ile ningebakwa ingekuwa ndo mara ya kwanza"
James alinikumbatia kwa nguvu asiamini nilichomwambia, akanibeba nakunipeleka chumbani kwake akanilaza kitandani.
Kilichosikika ni sauti yangu ya kilio alifanikiwa kunitoa nililia sana.
"Pole mkewangu nashukuru kwa zawadi hii nakupenda sana Lisa"
Alisema nakunibusu akatoka nakuniandalia maji moto kisha akanipeleka bafuni nakunisafisha.
Upendo ulishamiri juu yetu akuna alietaka kumuacha mwenzake tulipendana sana.
Siku zikazidi kusonga adi nikafikisha miezi mitatu nipo kwao bado adi siku moja tukasikia taharifa ya habari kuwa ninatafutwa bahati nzuri alipata pesa ya nauli kikwazo kikabaki kuondoka nakumuacha mwanaume alieniingiza kwenye mapenzi.
"James nakupenda mimi sitaki kuondoka"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliongea uku nalia
"Najua mamangu unanipenda lakini wazazi wako wamekukumbuka nenda wakakuone uwaondoe hofu mimi nipo utanikuta"
Alijitahidi kunibembeleza
"Niahidi hautonisaliti"
"Siwezi mkewangu nakupenda sana niamini"
Alisema akanikumbatia basi tukajikuta tunashiriki mapenzi nakuagana akanisindikiza adi stand nikapanda gari nakurudi nyumbani sababu kwenye radio walitangaza jina lake iyo sehemu niliulizia adi nikafika nyumbani.
"Waoo mjukuu wangu ulikuwa wapi jamani"
Bibi aliponiona alifurahi nakuja kunikumbatia.
Nilikaa wiki moja nikatakiwa nirudi Dar es salaam sababu matokeo ya kidato cha tano yalitoka nilipata alama nzuri nakutakiwa kuendelea.
Basi nikajiandaa na sana ikaanza kurudi nyumbani kwa wazazi wangu nikiwa Lisa mpya kabisa.
Nilifika nikapokelewa na wazazi wangu kwa furaha sana tukaongea mengi sikutaka kusema kuhusu kubakwa wala kuwa na james ilikuwa siri yangu.
Basi siku iyo nikapumzika asubuhi na mapema niliamka nikafanya usafi nyumba nzima nikajaza maji kwenye matenki yote ndani nikapika chai na chapati za maji nikaweka mezani.
Watu walipoamka wakashangaa nani amefanya ivyo sababu yule msichana wa kazi aliondoka kwao.i
"Hee leo tumeingiliwa na jini humu ndani au?"
Aliuliza baba
"Ata mie nashangaa imekuwaje au Lisa?"
Mama akauliza
"Lisa ajui kuosha ata kijiko ataweza kufanya kazi zote izi?"
Baba nae akasema ilikuwa ni wikiendi hawakwenda kazini wote
Mara nikatoka chumbani nakuwasalimia kwa heshima na adabu wote wakapigwa na butwaa
Nilikuwa nikifika nawasalimia wote kwa pamoja
"Shikamooni"
Alafu nakaa nakunywa chai, lakini leo tofauti kwa heshima zote nikamsogelea mama
"Shikamoo mamangu"
"Shikamoo babangu"
"Kaka shikamoo"
Mshangao walioupata sijui kama kuna alieitikia iyo salamu! Walibaki wamezubaa
"Jamani karibuni chai"
Nikachukua jagi la maji na bakuli chini nikaanza kuwanawisha wote adi nilipomaliza nakuombea chai kabla atujala.
"Fumbeni macho tuombe
Utubariki mungu wetu sisi na chakula chetu tupate nguvu zakukutumikia vyema amina karibuni"
Yote yaliyotokea ni kama naigiza vile baba akavunja ukimya nakuongea.
"Kwani Lisa umekuwaje sijaelewa bado?"
"Baba nimebadirika nimekuwa Lisa mpya mimi sio yule wa mwanzo, chai inapoa jamani tunyweni"
Akuna alieongea tena tukanywa adi tulipomaliza nikatoa vyombo nakupeleka jikoni kuosha.
"Mama leo tunakula nini nipike?"
"Nilipanga iwe pilau au wewe unaonaje?"
"Oh sawa nenda kapumzike mimi nitapika"
"We Lisa unajua kupika au unataka babayako akupige?"
"Mama izo ni zilipendwa haitokei ata siku moja nikapigwa ila naisi baba atanipenda sana"
"Mmmh aya"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alisema mama akaondoka, nikaosha nyama nakuiweka jikoni uku nikikata viungo vingine nakuanza mapishi yangu.
Pilau lilinukia nyumba nzima nikiwa napika mara kaka Gedion akaja jikoni
"Waoo pilau linanukiaje dah kumbe mrembo wangu unajua kupika ivi"
Mwenyewe alikuwa sharobaro uyo balaa kavaa modo imembana juu anazo headphone kaweka kama rubani vile yani anaishi kiswaga swaga tu sio akae kishamba alafu ongea yake sasa kwa mapozi sijui kama hao mademu zake hawamuongi pesa
Basi akaanza kunichokoza makusudi ata sikumjibu.
Mwisho akatoka zake namimi nilishaivisha nikaweka kwa hotpot nakupeleka sehemu yakulia chakula nikatenga apo.
Nilipomaliza nikaingia chumbani kwanza nioge nakubadirisha nguo.
Mara nikakumbuka kitu nilichukua simu yangu nakufuta namba za mashoga zangu wote sikutaka kabisa kuwa na rafiki wala nani zote nilifuta nikabaki na namba za ndugu zangu basi.
Nilimaliza kuoga nikatoka nakuwaita wazazi waje kula.
"Mmmh chakula kitamu"
Kila mtu alikisifia.
****
Siku zikazidi kusonga uku nikiwa nimebadirika kabisa ata ngoma ipige nje kwetu sitoki ndo kwanza najifungia chumbani, niliacha kuzura ovyo muda mwingi nashinda tu nyumbani, lugha za ajabu matusi, kuwachamba watu, heshima mbaya vyote niliacha nakuwa msichana mwenye adabu zangu ninaejielewa si yule mvaa kanga moja nakutembea kanga niliivalia suluali ndani nakutoka.
Baba alinipenda nakuwa rafiki yake sasa uku mara kwa mara akija ananiletea zawadi adi Gedion akawa anaona wivu, kipindi iko walikuwa wanafatilia kuhusu masomo yangu ambapo ilipokamilika nikaanza kidato cha tano kwenye shule ya kulipia iliyokuwa mbezi beach inayoitwa Kentoni.
Masomo yalikuwa magumu ila nilijitahidi nakuweka akili zangu apo sikutaka kuwa na marafiki nilikuwa pekeyangu zaidi nilikuwa mpole sana uwezi kuamini kama ndio mie Lisa mcharuko ambae adi nilikuwa napigana.
Wanaume hawakuacha usumbufu juu yangu lakini sikutaka kukubali nakumsaliti James mwanaume wa maisha yangu nilimpenda sana.
Siku zikazidi kusonga adi nilipomaliza ayo masomo nakusubiri niingie kidato cha sita.
Mwezi wa tisa ilikuwa birthday ya Gedion basi akafanyiwa sherehe kipindi iko yupo chuo mwaka wa pili.
Wanachuo wenzake walijaa apo nao mahandsome balaa yani masharobaro hao na wasichana pia hawakukosa nikaisi ata wifi yangu atakuwepo apo japo sikujuakama anae msichana mmoja wakudumu.
Basi muda wakulishana keki ulifika akawaita wazazi bila kunisahau namimi pia, nilivaa kiheshima gauni lefu lililonikaa vyema mwilini japo umbo langu halikujificha.
"Napenda kumuita rafiki yangu kipenzi Harvey aje mbele"
Alisema Gedion nikamuona mkaka mmoja amesogea mbele nakulishwa keki na Gedion wakakumbatiana apo, yule kaka jamani alipendeza mavazi yake na muonekano wake kwa ujumla alikuwa mrefu walilingana na kaka Gedion ata maumbo yao wote modo walijua kuchaguana marafiki.
Basi sherehe iliendelea apo watu wakinywa na kula, Mara ghafla namuona Gedion na mwenzake wanakuja nilipokaa nilijitenga sikuwa na mtu.
"Hi mamy mambo"
Alisema uyo mkaka akaniomba anikumbatie sikuwa na jinsi nilikubali maana alikuwa na swaga zakizingu inaonyesha kwao mambo safi.
"Lisa uyu rafiki yangu anaitwa Harvey and Harvey uyu mdogo wangu kipendi anaitwa Lisa tumezaliwa wawili tu sisi"
Alitoa utamburisho Gedion
"Oh poa nafurahi kufahamiana na mtoto mzuri ila ndugu yangu unadada mrembo ivi huniambii jamani au utaki shemeji?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alisema uyo Harvey nakumfanya Gedion acheke.
"Time is over mamy sorry can you give me your nomber please?"
(Muda umeisha mamy unaweza kunipa namba yako"
Alisema Harvey
"Mmmh apana siwezi alafu Gedion sipendi kuniunganisha kwa wanaume nitamwambia baba"
Nilisema nikainuka nakuondoka niliwaacha wananiangalia sijui waliongea nini nikaingia zangu chumbani nakulala.
"Nakupenda sana james sitokusaliti kamwe"
Nilisema nikikumbatia mto nakulala.
Ghafla nasikia simu yangu inaita kuangalia namba ngeni sikujua nani nikaona nipokee tu
"Halo"
"Hallow mom umelala?"
Sauti nzuri ya kiume ambayo muongeaji alijua kuitumia niliisi mapigo ya moyo yalisimama kwa muda
"Wee...wewee..na...a..niii?
Nikauliza uku nikitetemeka.
"Is me Harvey"
(Ni mimi Harley)
Nilishtuka sana
Nilishtuka kusikia ni Harvey aliepiga simu.
"Wewe unataka nini?"
Nikamuuliza kwa ukali sikutaka mazoea nae.
"Mmm jaman mtoto mzuri ivyo kuwa mkali ata haipendezi but sina mengi mamangu nikutakie usiku mwema bye"
Aliongea nakukata simu nikabaki nimeganda na simu sikioni uyu kaka alijaaliwa sauti ya mahaba adi mwili ulinisisimka.
"Siwezi kukusaliti James wangu mungu nisaidie mimi"
Nilisema nikazima simu nakulala.
Asubuh kulipokucha niliwahi kuamka kama kawaida nakufanya usafi nikapika chai nakuwatengea wazazi wangu ambao walikunywa nakwenda kazini, kaka Gedion yeye alikuwepo nyumbani hakwenda chuo.
Basi nikarudi ndani kuoga nilipokuwa navaa simu yangu ikaita namba sikuijua nikapokea
"Mambo mamy uko poa?"
Niliposikia sauti tu nikamjua ni Harvey
"Niko poa sijui we"
"Mimi mzima, nimekumisi nakuja home Kwenu walau nikuone tu moyo wangu uridhike nambie nikuletee zawadi gani?
Aliniuliza
"Mh pole nipo shule sipo nyumbani"
Nikamjibu
"Lisa ufai kuwa muongo jamani"
Akasema
"Bwana sipo nyumbani nikudanganye kwanini sasa"
Nilimjibu kwa ukali kidogo
"Aya mama sorry kwa usumbufu bye"
Alinambia nakukata simu.
"Uyu mkaka ananitakia nini mimi jamani aaah"
Niliongea nikiwa nimechukia sikupenda kusumbuliwa tena nikatoka nakumfata Gedion chumbani kwake nikaingia bila hodi nakumkuta amekaa kavaa boksa tu anachezea laptop yake! Nilitoka mbio nakurudi chumbani kwangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tabia yakumpa rafiki yako namba anisumbue sipendi tena mwambie anikome"
Nikamtumia meseji kwenye simu.
"Njo chumbani"
Akanijibu
"Vaa nguo kwanza"
"Kwani nipo uchi njoo"
"Sitaki adi uvae"
Basi tukajibishana apo mwisho akanambia anavaa suluali niende nikakaa dakika kidogo nikaenda nakumkuta amevaa tayari.
"Aya nambie mrembo"
Alisema nakukaa kunisikiliza
"Gedion mimi nina mpenzi wangu yupo kule kwa bibi nampenda sana sitaki kumsaliti nakuomba usiniunganishe kwa wanaume wengine sitaki"
Nilimwambia
"Mm we Lisa uyo mpenzi umempata lini? Acha izo bwana mkubali Harvey anakupenda sana atakuoa kabisa awezi kukuchezea namjua yule"
Akaongea akiniangalia
"Sitaki sitaki nimesema nina mpenzi wangu uyo Harvey simtaki"
Niliongea kwa hasira nakuanza kutoka
"Kwanza unakula nini nataka nikapike?
Nilimuuliza kabla sijafungua mlango
"Ugali na kuku rosti"
"Muone unapenda kula vizuri"
"Alafu kuna mgeni so pika ugali mkubwa"
Alisema sikumjibu nikatoka zangu nakuingia jikoni kupika.
Nilimaliza nikawa natenga mezani, Ghafla nikasikia gari linapiga honi nje mara Gedion akatoka ndani nakufungua mlango wa nje nakutoka nikashangaa ni nani uyo aliekuja maana baba au mama kurudi ni usiku sio mchana ilikuwa saa saba
Sikutaka kufatilia sana nikaachana nae, basi nikiwa natenga chakula nikamuona Gedion kaingia ameongozana na mwanaume mwengine nilipomtizama ni Harvey!
Moyo ulishtuka adi sahani niliyoshika ikadondoka chini nakupasuka.
****
"We nae vipi unavunja vyombo?"
Aliuliza Gedion akicheka sikumjibu nikainama kuokota nakuingia jikoni niliweka kwenye sehemu yakutupa taka, nilipotoka nikaongoza adi chumbani kwangu
"Lisa njo tule unaenda wapi?"
Gedion akaniita sikumsikiliza nikaingia chumbani, mara mlango ukafunguliwa akaingia Harvey
"Wewe nani kakutuma uingie chumbani kwangu?"
Nilitahamaki nikamuuliza.
"Sorry mamy naomba twende tukale pamoja pia nimekuletea zawadi hii"
Alitoa mfuko nakunikabidhi
"Harvey..
Niliita kabla sijaendelea kuongea alinikatisha maneno yangu
"Shiii nakuomba pokea alafu inuka chakula kinapoa"
Alisema akanishika mkono nakuniinua tukatoka nakungana na Gedion mezani tulipoanza kula pamoja.
Japokuwa niliongea kwa ukali Harvey hakujali ilo aliniongelesha kwa upole na sauti yake iliyokuwa nzuri, basi tulikula tulipomaliza nikaingia jikoni kuosha vyombo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Harvey na Gedion waliingia chumbani kwao namimi nilipomaliza nikaenda ndani kwangu.
Cha kwanza ilikuwa kuangalia zawadi gani aliyoniletea nikafungua mfuko nakukuta pafyumu nzuri ambayo napenda kuitumia nilitabasamu nakujua ni Gedion ndio atakuwa amemwambia sababu yeye hawezi kujua, pia nikaona chocolate nikajikuta nacheka nakuanza kuila, sababu napenda sana chocolate.
Basi nilijilaza kitandani nakupitiwa usingizi nilikuja kushtuka nilipoisi mtu ananigusa mwili wangu nilipofumbua macho nikamuona Harvey
"Wee..umefata nini?"
Nilikurupuka nakumuuliza
"Nimekuja kukuaga naondoka"
"Mmmh aya safari njema"
"Nashukuru mtoto mzuri"
Alitabasamu nakufanya dimpoz zake zionekane basi alitoka Gedion akamsindikiza adi nje alipoondoka zake.
***
Siku zikazidi kusonga uku Harvey akizidi kujenga ukaribu namimi kipindi chote iko hakuwahi kunitamkia ananipenda zaidi ya urafiki wa kawaida japo dalili zote zilionyesha ananitaka kimapenzi ila hakuwahi kunambia nikajua Gedion amemueleza nina mpenzi tayari.
Ilikuwa kawaida yake usiku kabla yakulala lazima aniage nakunitakia njozi njema pia Asubuhi akiamka tu lazima anisalimie nakunitakia siku njema.
Sikuweza kumkwepa Harvey tukazidi kuwasiliana adi siku moja akaniomba nitoke kuna sehemu anaitaji kwenda namimi.
"Naanzaje kutoka baba nitamwambiaje?"
"Lisa nimeongea na Gedion utatoka nae yeye ndie atakae muaga baba usijali"
"Mh sawa"
Nilibaki kuguna tu.
Hatimae wikiendi ikafika ni jumamosi kaka Gedion akamuomba ruhusa baba anataka kutoka namimi tukatembee beach
"Ni vizuri umtoe dadayako siku izi amekuwa mtu wakushinda ndani tu"
Baba akamwambia
"Ndio nataka kumchangamsha"
Alijibu Gedion basi akaenda kujiandaa namimi pia nikawa chumbani kwangu najiandaa japo sikuipenda ile safari.
"Lisa naomba uvae nguo nzuri itayokubana umbo lako sawa eeh"
Gedion akatuma iyo meseji kwa simu nikabaki nacheka tu.
Basi nikatafuta gauni langu fupi kiasi linaishia juu ya magoti nikavaa linabana ni la mpira lilinichora umbo adi nikajikuta najitamani.
Basi nikajipulizia marashi mazuri yale aliyoniletea Harvey baada yakuwa tayari tukatoka Gedion alichukua gari ya baba tukapanda humo.
Safari yetu ilienda adi masaki sijui sehemu gani pale kuna hotel kubwa yakifahari akaweka gari packing nakushuka akaongoza njia yani humo ni wazungu tupu na watu wachache walioonekna wanapesa zao hotel nzuri upepo tu unavuma uku watu wachache wapo kwenye swimming pool wanaogelea na vichupi vyao basi tukaongoza adi sehemu kwenye viti tukamkuta Harvey amekaa apo aliponiona alitabasamu akainuka nakunikumbatia
"Wow you are beautiful and unanukia vizuri"
Alipenda kila neno lake kuchanganya kizungu pia basi akaniachia nakunikaribisha nikae ambapo nilipigwa butwaa Gedion simuoni ikabidi nimuulize yupo wapi
"Kwani ajakwambia amekuleta apa kwaajiri yangu?"
Nilishtuka aliposema ivyo sababu nilijua tutakuwa pamoja.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Apana hakunambia"
"Ok usijali lakini maybe yupo na girl wake but ukitaka kuondoka atakuja kukuchukua so ondoa hofu"
Alinambia
"Mh sawa"
Nilimkubalia, mara akaja muhudumu nikaagiza kinywaji sababu Harvey nilimkuta anakunywa wine sijui whisky ile tena inaonyesha ya bei sana.
Nilipoletewa kinywaji Harvey akaagiza na chakula.
Basi tukapiga story kidogo chakula kikaja tulikula pamoja baada ya apo akaanzisha maongezi.
"Lisa nikwambie kitu?"
Aliniuliza
"Nambie Harvey"
"Ivi unajijua kama wewe ni Mrembo sana?"
"Jamani sasa unanambia au unaniuliza?"
"Yote ni sawa tu ila sikufichi Lisa wewe ni mzuri sana unaweza kumvutia mwanaume yoyote lijari"
Alisema kwa sauti ya utulivu ambayo haichoshi nilichokuja kugundua kwake alikuwa anajua kucheza na ulimi wake nakutoa maneno matamu hakuwa kama wanaume wengine
wanaobwatuka, Harvey alijua kutumia sauti yake kumfanya mwanamke asichoke kuisikia.
"Stop joking Harvey"
(Acha utani Harvey)
"Lisa serious not joking"
(Lisa nipo makini sio utani)
Alisema akiniangalia tulipokutanisha macho yetu akanikonyeza nakunifanya nijisikie aibu nikatizama pembeni.
Harvey alisogeza kiti karibu yangu akanishika mikono yangu nakuniangalia
"Lisa naomba tizama macho yangu kuna kipi unakiona"
Alisema nikamuangalia nakugundua yupo kwenye mapenzi mazito juu yangu, niliogopa sana nikamkumbuka james.
"Lisa nakupenda sana natamani siku moja uwe mkewangu"
"Apana Harvey haiwezekani nina mpenzi tayari"
Nilijaribu kuitoa mikono yangu lakini nilishindwa alinishika kwa nguvu.
"Najua msichana mrembo uwezi kukosa mwanaume ila naomba nifikilie ombi langu nakuhitaji sana"
"Lakini Harvey wewe si unae mpenzi?"
Nikamuuliza nakumfanya haiachie mikono yangu nakukaa vizuri kwenye kiti chake.
"Nilikuwa nae ila kwasasa sina, sitaki nikufiche Lisa nakueleza ukweli, nilimpenda sana Clara nikampa kila alichohijati zaidi adi familia yake niliihudumia nilipanga aje kuwa mke wangu,mama wa watoto wangu lakini ikawa tofauti Clara hakuwa anaridhika alinichanganya na wanaume wengine, mara kwa mara nilimfumania iliniuma sana akihitaji kiasi chochote cha pesa nilimpa adi gari nilimnunulia sikutaka asumbuke kupanda daladala, hali ya kwao ni ngumu waliishi nyumba ya kupanga na mamayake nikawaonea huruma nilimwibia pesa baba nakuwajengea nyumba, baba alichukia sana nilipochukua pesa zake lakini sikujali, nilichotaka ni kumpa furaha msichana wangu na familia yake, Lisa maumivu kilasiku yalinijaa Clara sijui alitaka roho yangu nimpe mimi nife au nini sababu kilakitu nilimpatia lakini bado akutosheka sitosahau siku moja nilimfumania na mwanaume aliniponza nikapigwa na yule mwanaume akisema namchukulia mwanamke wake, amna siku nilikuwa na hasira kama iyo najuana na polisi wengi tu nilichokifanya ni kupiga simu nakuwaambia Clara na mwanaume wake wamenifanyia fujo kwaiyo wakawekwe ndani adi nitapoamua mwenyewe kwenda kuwatoa adi sasa miezi miwili imepita bado wapo ndani yani nina hasira na Clara lakini kamwe siwezi kuchukia wanawake wote sababu najua hamfanani kila mwanamke na akili zake na sijaogopa kuanzisha uhusiano mwengine kisa kuna mmoja alinitenda vibaya najua mungu hakupanga awe mke wangu"
Alimaliza kusema Harvey uku macho yamekuwa mekundu kuonyesha jinsi gani alikuwa na hasira.
"Naenda toilet nakuja mamy"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alinambia nakuinuka nikabaki namtizama Harvey alikuwa msafi mwenye kujipenda kimavazi alivutia kumuangalia.
Baada ya muda kidogo alirudi nakukaa
"Pole nimekuacha pekeyako"
Alisema akitabasamu
"Amna bwana usijali"
Mara muhudumu akaja na vinywaji nakuweka akaondoka.
"Harvey tumbo litapasuka jamani mimi nimetosheka"
"Mmmh Lisa jamani yani iyo red bull moja tu ikupasue tumbo ebu kunywa uko"
Alisema sikuwa na jinsi nikaendelea kunywa na giza lilishaanza kuingia
"Usiku umeingia mwambie Gedion aje tuondoke"
Nilimwambia
"Kwani umeshachoka kukaa namimi?"
"Apana sio ivyo"
"Mbona unataka kuondoka nyumbani unawahi nini?"
Aliniuliza nikakosa lakumjibu Harvey akasogea karibu yangu zaidi nakuniambia nisimame
"Kunanini tena?"
Nilimuuliza
"Simama mara moja nikwambie"
Basi nikasimama nayeye pia akasimama nilikuwa mfupi kwake kichwa changu kilishia maeneo ya kifuani kwake.
"Mmmh Harvey we mrefu"
Nilimwambia nakumfanya acheke alafu akanikumbatia
"Nakupenda Lisa"
Aliongea kwa sauti ndogo sikioni kwangu adi mwili ukanisisimka zaidi harufu ya marashi aliyopuliza yalikuwa yananukia vizuri sana bila kutarajia namimi nikamkumbatia.
Harvey alifarijika sana akuniachia haraka alizidi kunikumbatia sana mwisho akanikisi kwenye paji la uso.
"Nakuhitaji Lisa plz nikubali niwe mwanaume wa maisha yako"
Alisema nikamkumbuka James
"Apana Harvey haiwezekani siwezi kuwa nawe"
Nilimwambia nikajitoa mwilini mwake, maneno yangu yalimuumiza sana moyo wake alijisikia vibaya lakini sikuweza kubadirisha msimamo wangu nilimpenda sana james.
"Ok mama siwezi kulazimisha sababu mapenzi ni maridhiano ila muda wowote ukitaka kuwa namimi nakukaribisha milango ipo wazi"
Alisema nakutoa simu yake kumpigia Gedion aje kunichukua.
Basi nilikaa kimya nikimsubiri baada ya nusu saa alikuja wakaongea kidogo mwisho wakaagana.
"Lisa jaman naomba nikuage"
Alinambia Gedion akatangulia mbele kidogo nakumpa nafasi Harvey alienisogelea kanikumbatia na kunibusu shingoni.
"Ufike salama mrembo wangu"
Alisema akaniachia nikaondoka.
Tulifika nyumbani saa mbili usiku sikutaka kukaa sebuleni nilikuwa nimechoka nikaingia chumbani kulala.
Mara simu yangu ikaitwa jina ni Harvey nikapokea
"Lala salama malkia wangu but ilove you mwaah"
Alisema nakukata simu.
Nilijikuta natabasamu tu nakujilaza kitandani adi usingizi uliponipitia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****
Siku zilizidi kusonga adi ilipofika mwezi wa kumi na moja nikaomba wazazi niende kijijini kwa bibi ata Christmas nikale uko nia yangu muda huo nikautumie kuwa na mpenzi wangu James nilimkumbuka sana.
Basi hawakuwa na tatizo nikakusanyiwa zawadi zakumpeleka bibi lakini mimi pia nikanunua zawadi ya James na mamayake nikawape.
Ila nilitaka kupanda gari la abiria sikutaka kupelekwa na baba au mama, wakanielewa siku ikafika nikajiandaa nakuvaa suluali yangu nzuri ya bluu iliyoikaa vyema juu nikapiga top nyeupe.
Gedion alitoka nakunisindikiza stand ya mkoa ubungo japo si mbali lakini tulitoka na gari, tulipofika ubungo mataa akasimamisha gari pembeni nakuongea na simu kama anamuelekeza mtu aje.
Basi baada ya nusu saa nikaona gari limekuja nakupaki pembeni yetu akashuka Harvey mara Gedion nae akatelemka nakuniomba namimi nishuke.
"Kuanini kwani unajua nachelewa na tiketi sijakata bado?"
"Usijali bwana Harvey anakupeleka adi kwa bibi teremka upande humo kwenye gari"
Alinambia nakunifanya nishangae sana, mara Harvey nae akasogea kwenye gari letu
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment