Chombezo : Mrembo Mcharuko
Sehemu Ya Nne (4)
Alisema Harvey nikamsogelea, alikata keki nakunilisha baada ya akaniomba akanikiss shavuni nakufanya watu wapige makofi. Basi sherehe iliendelea adi usiku mkubwa watu walikula na kunywa uku mziki ukipogwa wapo waliocheza pia, Harvey aliniacha nakujumuika na marafiki zake.
niliisi kuchoka nikatamani kuondoka maana ilikuwa saa saba usiku, Mara nikamuona Harvey anakuja nilipo
"Twende tukalale naisi umechoka"
Alinambia akanishika mkono tukarudi chumbani, nilifikia kujitupa kitandani ata viatu sikuvua.
"Mmh jamani ndo umechoka ata kuoga utaki?"
Alisema Harvey
"Nitaoga kesho bwana"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimjibu akacheka, alinisogelea nilipo akanivua viatu nakuweka sehemu yake baada ya apo alipandisha miguu yangu nakunifunika shuka alafu akaingia bafuni kuoga sijui alimaliza muda gani akalala nilishtuka kumekucha nipo pekeyangu kitandani.
"Mh ameenda wapi uyu?"
Nilijiuliza nikainuka nakuingia maliwatoni kujisafisha nikaoga kabisa nakubadirisha nguo, baada ya nusu saa nikaona Harvey anakuja uku mwili wote umejaa jasho kumbe alikuwa anafanya mazoezi.
"Morning baby"
Alinisalimia nikamjibu akaingia bafuni kuoga kwanza, Mara nikasikia mlango unagongwa nilishtuka ni nani uyo nikaenda kufungua nakuona ni muhudumu ameleta breakfast nikamruhusu aingie nakuweka mezani alafu akaondoka.
Harvey alimaliza kuoga akatoka tukajumuika wote kunywa chai.
"Lisa leo nataka nikutembeze huone mazingira ya apa tulipo"
Alinambia nikamjibu sawa, basi siku iyo tukashinda ndani kulikuwa na tv humo nikawa naangalia movie uku Harvey yupo bize na laptop yake akisema kuna kazi za chuo anafanya japo kipindi iko alikuwa likizo akingojea kuingia muhula wa mwisho mwakani.
Hatimae jioni ikafika akaniomba tutoke sasa.
****
Matembezi yetu yalianzia kwenye Restaurant kubwa ambapo niliisi hii hotel ya kitalii sababu walijaa watu mataifa mbali mbali ambao walionekana pesa wanazo si chokambaya.
Vyakula mbali mbali vilikuwepo nilishangaa ata wahudumu wengine ni wachina, waphilipino sijui na watu gani, tulitoka apo nakuelekea sehemu ya kupumzika watu kulikuwa na swimming pool.
Madhari yake ilivutia sana uku watu wakiwa wamejiachia kama akuna kufa vile.
Basi tulitoka apo nakuelekea baharini kabisa sababu hotel imejengwa karibu na bahari.
"Harvey hii hotel ni yako?"
Nilimuuliza
"Akuu yangu niipate wapi mie kwetu maskini"
"Harvey kuwa serious bwana"
Alinigeukia nakukunja sura adi nikaogopa alafu akanishika mashavu kwa mikono yote miwili nakunivuta
"Babayangu kondakta na mama anauza mihogo mimi nasomeshwa na serikali sina uwezo wowote mwaah"
Alisema uku kashika mashavu yangu alafu akanibusu mdomoni nakuanza kukimbia uku akicheka, sikukubali namimi nikaanza kumkimbiza lakini sikumpata mwenzangu alikuwa mwepesi kwa sababu yakufanya mazoezi alikimbia mbali sana, nilichoka nikaamua nikae chini nusu saa ilipita bila Harvey kurudi bahati mbaya simu niliacha ndani nikainuka niifate japo nimpigie kuangalia mbele yangu namuona Harvey yupo na mwanamke wanakuja nilipo uku wameshikana mikono wanaongea nakucheka.
"Lisa wifi yako uyu anaitea Tecla"
Alipofika tu Harvey akanitambulisha.
"Tecla mamy wifi ako uyu anaitwa Lisa"
Alimwambia uyo msichana ambae alikuwa mwembamba mrefu alafu ni mweupe.
"Wow nimefurahi kukuona"
Alisema akinipa mkono nikaupokea baada ya apo Harvey akaondoka na uyo Tecla nakuniacha nikiwa mnyonge sana.
"Uyu ni mpenzi wake wa muda au mbona alinambia hana mpenzi inamaana kamtongoza sasa? Lakini wanaonyesha wanajuana kipindi kirefu"
Maswali mengi yalipita kwenye ubongo wangu nikakosa jibu nilishangaa moyo unaniuma sana adi nikajiona mjinga
"Sasa naumia nini wakati Harvey nilimkataa"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijisemea kwa unyonge nikainuka nakuelekea sehemu kilipo chumba chetu, basi nilifika lakin sikumkuta Harvey nikawasha television nakuangalia.
Baada ya nusu saa Harvey alikuja
"Kumbe usharudi nilikufata kule sijakuona"
Alinambia
"Niliamua nije uku"
"Pole mwaya nilikuacha pekeyako"
Alisema
"Apana usij...
Kabla sijaendelea macho yangu yakatua shavuni kwake nakuona lipstick kama yule mwanamke alimbusu apo moyo wangu uliniuma sikujua kwanini nikashindwa kuendelea kuongea nakubaki kimya Harvey wala akushtuka
"Vipi mbona ivyo?"
Aliniuliza sikumjibu akainuka nakuingia chooni ambapo alinawa nakutoka akanisogelea nilipo
"Lisa sorry sitaki nikuumize yule Tecla ni mfanyakazi wa apa jana akuwepo kazini leo nimekutana nae nikaamua nimtambulishe wewe ni wifi yake"
Alisema Harvey kwa upole sana.
"Sawa nimekuelewa"
Nilimjibu nakujiona mjinga naanzaje kuumia kwa mtu ambae ata uhusiano nae sina.
****
Tulimaliza wiki nzima apo hotel nikatamani kurudi nyumbani lakini nilikumbuka niliaga Christmas nitakuwa kwa bibi ikawa ngumu mimi kurudi ata nilipomwambia Harvey alinambia nisubiri bado anahamu yakukaa namimi.
Wiki nyingine ikaisha tukiwa wote hakuwahi kunambia neno lolote kuhusu mapenzi ila alinijali kwa kila kitu.
Siku moja akaniomba tutoke dinner tusile ndani na iyo siku kulikuwa na upepo uku kaubaridi kwa mbali pia.
Basi tukatoka nakutafuta sehemu yenye mwanga hafifu tukakaa apo chakula kililetwa tukala tulipomaliza tukawa tunapiga story.
"Ivi Lisa ukiiingia chuo utasomea masomo gani au nini mpango wako wa baadae ufanye kazi ipi?"
Aliniuliza
"Kiukweli bado sijajua"
"Mmmh mamy unaniangusha bhana unakosaje kujua sasa inabidi ujipange mapema"
"Aya nitafikilia ila nilitamani niisomee uchumi na biashara baadae nijiajiri mwenyewe"
"Ok ni wazo zuri pia ila usikurupuke fanya kile unaachokiweza"
Alinambia tukazidi kuongea mengi adi usiku saa tano ilipofika dalili zikaonyesha mvua inataka kunyesha ikabidi tumalize vinywaji vyetu nakuwahi chumbani ambapo baada ya muda mfupi mvua kubwa ilinyesha na baridi kali iliyofanya nitetemeke.
Bila kuchelewa niliwahi kitandani nakujifunika shuka ambalo alikusaidia kitu, Harvey akafungua kabati lilokuwepo humo ndani nakutoa blanket kubwa zito akapanda kitandani tukajifunika pamoja nakulala, mimi nilikuwa mwisho nikageuka ukutani nakumpa mgongo ambapo mara nikamsikia ananisemesha
"Lisa nikwambie kitu"
"Nambie"
Nilimjibu
"Geuka uku kwanza"
Alisema nikageuka, kutokana na giza lilokuwepo sikuweza kumuona nikajikuta nageuka nakufikia kifuani kwake ambapo bila kutegemea Harvey akanikumbatia niliogopa mapigo ya moyo yalienda mbio sana nilishusha pumzi ya hofu uku uoga ukinijaa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Subiri kwanza niwashe taa maana nakuona unaogopa"
Alisema Harvey akasogeza mkono wake karibu na meza kulikuwa na taa yenye mwangaza mdogo akaiwasha iyo nakufanya sasa tuonane.
"Lisa nikwambie"
Alisema
"Nambie"
"Naomba usiku wa leo nilale uku nimekukumbatia"
"Harvey jamani"
"Nakuomba sikufanyi kitu tofauti niamini"
Alisema nikiwa bado nipo kifuani kwake sikuwa na jinsi nilikubali alifurahi sana akanikiss kwenye paji la uso nakuzidi kunikumbatia adi tulipopitiwa na usingizi.
Asubuhi kulikucha bado hali ya hewa ilikuwa ya baridi na mvua kwa mbali Harvey akuweza kwenda mazoezini tulishinda pamoja ndani.
"Lisa nakupenda"
Alisema Harvey akinitazama.
"Harvey naogopa kuingia tena kwenye mapenzi"
"Lisa tambua binadamu hatufanani ata mimi pia yupo mwanamke alieniumiza lakini siwezi kuwachukia wanawake wote niamini nakupenda na sitokuumiza tena nipo tayari nisikutane nawe kimwili adi nitapokuoa nakuwa mke wangu"
Alisema kwa sauti yake ambayo haichoshi japo nilikuwa namkatalia ila hisia za mapenzi zilianza kuchipua juu yake nilisi kumpenda Harvey.
"Utaweza kweli tusikutane kimwili adi unioe?"
Nilimuuliza swali la kijinga wakati tunamiezi mitatu tunalala pamoja na ajawahi kuniingilia.
"Lisa ivi unajua tuna muda gani tupo wote na kulala pamoja ningekuwa nahitaji penzi lako unazani ningeshindwa kulipata? Amini wewe ni mke kwangu Lisa sitaki kukuchezea nahitaji uwe mama wa watoto wangu"
Aliongea kwa kumaanisha ni kipindi kirefu kimepita tukiwa pamoja akionyesha kunipenda sana nikakumbuka siku ile aliyonitambulisha kwa Tecla niliumia na sasa bado namkatalia anaweza kuwa na mwanamke mwengine itaniuma sikuwa na jinsi zaidi yakumkubali Harvey awe mpenzi wangu.
"Harvey nakupenda"
Nilimwambia uku najisikia aibu naangalia chini ilikuwa ni jioni tupo ndani uku amefungulia mziki mzuri wa Mapenzi ilitokea tu akaanzisha story tukiongea adi akafikia kunikumbusha bado ananiitaji sababu kilipita kipindi kirefu hakuwahi nitamkia.
"Wow unasema kweli?"
Aliniuliza akiwa aniamini nilichosema.
"Yes honey trust me i love you"
(Ndio mpenzi niamini nakupenda)
"I can't believe come on baby come to me please"
(Siwezi kuamini njo mpenzi njo kwangu tafadhari)
Alisema Harvey akisimama nikamsogelea tukakumbatiana kwa hisia.
"Nakupenda Lisa sitokuumiza"
Alisema baada ya apo akakaa kwenye kochi nakuniomba nimkalie mapajani kwake, alishika kiuno changu nakunivuta kwake zaidi midomo yetu ikagusana.
Harvey alianza kunyonya lips zangu taratibu uku akinipapasa kiuno changu akaendeleza utundu wake kwangu ambapo aliingiza ulimi wake mdomoni kwangu nikaupokea nakuanza kula romance, mwili wote ulinisisimka alijua kucheza na ulimi wake kinywani mwangu adi nikaisi kupagawa akuishia apo mikono yake ilizidi kuniminya kiuno changu, mapigo ya moyo wangu yaliongezeka kasi nikaanza kuhema sana uku pumzi zikitoka nakufanya hisia zangu zianze kupanda, Harvey alijua ilo akanikatisha nakutoa ulimi wake mdomoni mwangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Lisa sitaki kuvunja ahadi yangu kwako muda wakufanya mapenzi haujafika bado"
Alisema sikuamini ilo nilijua leo lazima angeniingilia.
Basi huo ukawa mwanzo wa mapenzi yetu kipindi chote tulikuwa pamoja tukicheza michezo mingi yakimahaba ila kamwe akuitaji penzi toka kwangu si kama alikuwa hana hisia namimi alikuwa nazo nilishuhudia ata sehemu zake zikiwa zimetuna kwenye suluali lakini akuwa tayari kuniingilia.
****
"Baby amka tukafanye mazoezi"
"Nimechoka bwana leo siendi"
Ni kawaida yetu ilikuwa kilasiku tunaenda pamoja baharini nakufanya mazoezi mwisho tunarudi kupumzika, mapenzi yetu yalishamiri mwezi mmoja ulitosha kuzoeana sana nakuwa kama wapenzi wa miaka mingi Harvey alinipenda sana nakunijali nikajikuta nampa upendo wangu wote nakusahau kama niliwahi kuumizwa kabla.
Mapenzi matamu sana umpate mwanaume anaekupenda kweli unajiisi kama malkia vile.
"Apana bwana twende inuka acha uvivu"
Alinambia lakini sikutaka kuinuka nilikuwa mvivu sana,
"Ooh utaki eeh subiri sasa nije kukumwagia maji"
Alisema akaenda kuchota maji nakuja nayo nilipomuona mwenyewe niliiunuka kitandani.
"Muone vile ningekumwagia kweli"
Alisema akicheka.
"Toka apa umenikatisha usingizi wangu"
"Usijal baby utakuja kulala tena"
Alinambia tukajiandaa nakutoka kwenda baharini.
Siku zilizidi kusonga adi ulipofika mwezi wa kumi na mbili ambapo sikukuu ya Christmas na mwaka mpya tulikuwa pamoja. baada ya apo tukafanya maandalizi ya safari kurudi nyumbani.
Niliwapigia simu wazazi wangu nakuwaeleza narudi walifurahi nakunitakia safari njema.
Siku ya kuagana ilikuwa majonzi sana kwetu tulishazoea kuwa pamoja kulala na kuamka tukiwa wote nasasa tunatengana iliniuma kuwa mbali na Harvey nilimzoea sana nakuisi kama tayari amenioa nakuwa mke wake.
"Lisa usilie mke wangu tambua nakupenda na sitokusaliti nitajizuia sitokuwa na mwanamke zaidi yako niamini"
Alinambia pale tulipokuwa tupo kwenye gari na kuanza safari.
"Usiniache mpenzi wangu"
"Siwezi mama niamini nakupenda"
Alisema akanikiss na safari ikaanza ilikuwa ni jioni saa kumi na moja ndio tulitoka.
Aliwasiliana na Gedion aje kunipokea alikubali adi usiku saa mbili tukafika ubungo sehemu ile aliyonichukua siku ninayoondoka ndio tulimkuta Gedion tukashuka nakumsalimia baada ya apo tuliagana na Harvey tukaondoka kurudi nyumbani.
Mama na Baba walifurahi kuniona nakuniuliza habari za bibi nikawajibu ajambo yupo salama.
Nilikuta chakula tayari tukajumuika pamoja kula baada ya apo kila mtu aliingia chumbani kulala.
***
Baba alianza kufatilia masomo yangu ambapo baada ya wiki moja nikaanza nikimalizia kidato cha sita.
Kilasiku tulikuwa tukiwasiliana na mpenzi wangu Harvey ambae alikuwa mwaka wa mwisho chuo.
Nilipopata nafasi nilitoka nakukutana nae uku akiniomba nijitunze nisiwe na mwanaume mwengine ata yeye pia alisema awezi kuwa na mwanamke mwengine.
Mapenzi yetu yaliendelea kushamiri kilasiku adi pale alipomaliza masomo yake ambapo ilikuwa na kaka Gedion alimaliza pia.
Baba aliandaa sherehe yakumpongeza iliyohudhuriwa na watu wengi nilisikitika Harvey hakuja kwani nayeye alifanyiwa sherehe na wazazi wake iliniuma sikuwepo.
Baada ya mwezi kupita namimi nikamaliza masomo yangu nakubaki nyumbani.
***
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku moja Harvey akanipigia simu anaitaji kuniona bahati nzuri ilikuwa wikiendi wazazi wote walikuwepo nikaaga naenda Mlimani city nilikubaliwa nikatoka adi maeneo ya Shekilango ndo alisema nitamkuta apo, basi nilifika nikamuona akiwa amesimama nje gari lake nikamsogelea tukakumbatiana kwa furaha baada ya apo akaniomba niingie kwenye gari.
"Tunaenda wapi kwani?"
"Naenda kukuuza"
Alisema akicheka namimi nikacheka pia.
"Kwaiyo umefurahia kuuzwa eeh?"
Aliniuliza
"Harvey acha utani bwana nambie wapi"
"Usijali mama utaona tu"
Alisema akawasha gari nakuingia barabara yakuelekea sinza.
Safari ikaanza apo adi adi aliposimamisha gari kwenye duka moja kubwa la nguo akaniomba nishuke nayeye pia akalocki gari tukaingia ndani ya ilo duka lakisasa kubwa lililojaa nguo za kike zakisasa nzuri sana.
"Chagua nguo unazopenda"
Alinambia Harvey nikaanza kuchagua nakumuonyesha uku nayeye akinisaidia kuchagua, nusu saa ilitosha nilichagua nguo mchanganyiko.
Mara nikamuona Harvey anakuja na gauni zuri rangi ya gold lilikuwa full viatu na mkoba wake. Harvey akaniomba nilijaribu kuvaa, akanionyesha chumba nikaingia humo nakuvaa liliinikaa vyema kama alinipima vile nikatoka anione.
"Wow malkia wangu umependeza sana naomba livae usilivue"
Alinambia tukatoka apo dukani nikashangaa ajalipa pesa nikamuuliza
"Inamaana izi nguo tumepewa bure au?
Alicheka kwanza
"Ivi kuna cha bure sikuizi jamani? Sorry sikukwambia ilo duka la sister"
Alisema nikastaajabu sababu duka kubwa nguo za bei nilivyoona akuna nguo ya elfu kumi pale labda hamsini kwenda juu.
Basi sikutaka kuuliza sana tukaaendelea na safari yetu adi tulipoingia msasani akasimamisha gari kwenye saluni kubwa ya kiume na kike akaniomba nishuke nakuingia ndani ambapo aliongea na msichana mmoja nakumwambia anitengeneze nywele zangu yeye alikaa nje kunisubiri.
Baada ya nusu saa nilikuwa mpya nilipambwa nakupendeza adi sikuamini kama ndio mimi Harvey akaja nakunichukua tukaingia kwenye gari tena.
"Mbona leo unafanya yote aya tunaenda wapi kwani?"
Nilimuuliza
"Usijali mama mbona unapresha sana?"
Alisema safari ikaanza tena tukielekea Ostabey adi sehemu moja kwenye geti kubwa alikuwa na remonti akabonyeza geti likafunguka nakuingiza gari ndani kwenye bonge la jumba lakifahari kubwa ambalo sikuwahi ata kuliona wala kufikiria kunasiku nitafika.
"Harvey apa ni wapi?"
"Ni kwetu nimekuleta nikutambulishe kwa wazazi wangu ondoa hofu naomba utelemke"
Mshtuko niliopata adi nikaisi mkojo umenibana sikuamini.
Basi ikanibidi nijikaze nakutelemka kwenye gari Harvey pia akatelemka nakuniongoza ndani uku moyo unanidunda sana.
Basi tuliingia nakutokea kwenye sebule kubwa nakuwakuta wazazi wake Harvey wakiwa wamekaa apo pamoja na dadayake walipotuona walifurahi nakuja kutulaki tukasalimiana kwa furaha nakukaribishwa.
"Baba na mama uyu ndo mkwe wenu ambae nataka kumuoa"
Alisema Harvey
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tumefurahi sana kumuona ni msichana mrembo mwanangu umejua kuchagua"
Alisema mama yake.
"Ni kweli kabisa mke wangu uyu binti anamfaa mwanetu mimi sina pingamizi nimefurahi kumuona"
Babayake pia akasema nakumfanya Harvey atabasamu, Mara dadayake pia akadakia
"Wifi mzuri nimempenda sana"
Alisema nakufanya nishukuru familia nzima imenikubali japo akuwepo mmoja ambae ni dadayake Harvey aishie marekani uyo ndo wa kwanza akafatia Harvey na wa mwisho ni uyu msichana niliemkuta anaitwa Dorcas.
Basi chakula kilitengwa mezani na msichana wa kazi wote pamoja tukainuka nakujumuika kula adi tulipomaliza maongezi yakaendelea.
"Mimi nashauri kesho ipelekwe posa nyumbani
kwao uyu binti"
Alisema babamkwe nikashtuka mbona mapema sana.
"Baba kesho apana ni mapema inabidi wazazi wake wapewe habari kwanza ili wajipange sio kukurupuka tu"
Harvey alikataa
"We chelewa wenzio wamuwahi uyu unaona alivyo mrembo unajua wangapi wanamtamani sasa ona kesho mbali wengine wapeleke wamchukue usije kulia apa"
Mama alisema nakufanya nicheke adi Dorcas pia alicheka
"Mama bwana usimtishe kaka Harvey"
Alisema uku akimuangalia kakayake.
"Labda tumuulize muhusika mwenyewe Lisa inawezekana kesho kuleta posa kwenu wazazi wako watakuwa tayari?"
Harvey aliniuliza nakunifanya nikae kimya kwanza nisikurupuke kutoa majibu ambayo sina uhakika nayo.
"Inawezekana japo imekuwa ghafla lakini nitaongea na wazazi wangu watanielewa"
Nilisema
"Basi ni vizuri sababu kesho kutwa naweza kusafiri kwaiyo nilitaka niondoke nikiacha uku posa imepelekwa adi nitaporudi baada ya wiki moja maandalizi ya harusi yafanyike"
Alisema uyo baba nakunifanya nisiamini kama kweli nimekubaliwa niolewe na Harvey tena haraka bila kungoja miaka wala nini nilifurahi sana.
Basi maongezi ya kawaida yakafanyika apo tukaongea adi jioni saa kumi na moja Harvey akasema anirudishe nyumbani.
Tuliagana vizuri familia yake walifurahi nakutamani kama ningekuwa tayari nimeolewa nisiondoke nibaki niishi apo.
Wakati tushaaga nakutaka kuondoka mamamkwe akavua mkufu wake mkubwa wa dhahabu ambao alikuwa ameuvaa nakuniomba anivalishe.
"Nimekupenda sana karibu kwenye familia yangu"
Alisema uyo mama nakunikumbatia.
"Haa sikubali wifi chukua izi bangiri namimi nakupa"
Dorcas alisema akivua bangiri zake za dhahabu nakunivisha, nilifarijika sana nikawashukuru nakuwagana mwisho mwisho tukaondoka.
" Harvey siamini kama familia yako imenikubali"
Nilimwambia tulipokuwa kwenye gari.
"Wazazi wangu awakuamini nilivyowaambia nimepata mchumba nataka kuoa baba akasema nikupeleke wakuone yani apo wamefurahi sana izo pongezi nitazopewa we acha usishangae kesho iletwe posa alafu kesho kutwa iwe ndoa"
Alisema tukajikuta tunacheka pamoja.
"Kweli nimeamini unanipenda"
"Nilikuahidi ilo Lisa lazima nikuoe"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alisema Harvey safari ikaendelea adi aliponifikisha karibu na nyumbani akanipatia nguo zangu ambazo alininunulia tukakumbatiana nakuagana nikaongoza nakuingia ndani ambapo nilikuta wazazi wangu wamekaa sebuleni wote waliponiona walishtuka.
"Hee wewe Lisa au nani?"
Aliuliza mama nikacheka
"Makubwa mama kumsahau mtoto wake"
"Sio ivyo naona umependeza sana tofauti na ulivyotoka"
Alisema mama.
"Subiri kwanza niweke vitu chumbani nakuja"
Basi niliingia ndani nikaweka nguo zangu alafu nikajifunga kanga nakutoka maana ile nguo nilovaa inanichora sana umbo langu.
"Baba na Mama nimepata mchumba na kesho wanaleta posa"
Niliwaambia
"Mbona imekuwa ghafla kwanza mchumba uyo umempata lini na unamjua tabia zake usije kuolewa na jambazi?"
Aliuliza Baba
"Baba ni rafiki yake kaka Gedion tulijuana mwaka jana kwenye happy birthday yule ambae alimuita mwisho nakumlisha keki"
Niliwaelekeza
"Yule kijana namkumbuka hee kumbe ndo mkwe alafu alikuwa anapenda kuja apa"
Alisema mama
"Ndio uyo anachotaka anioe niwe mkewe sio kunichezea"
"Ni sawa tumekuelewa asubuhi mamayako atafanya maandalizi yakuwapokea hao wageni tena majibu tunawapa kesho iyo iyo"
Alisema baba nilifurahi basi tukaongea mengi adi tulipokula na kuingia ndani kulala.
Simu niliacha chumbani nikakuta missed call kibao za Harvey na meseji akilalamika nimemchunia.
Nikaamua nimpigie
"Sorry mumewangu simu niliacha chumbani mimi nilikuwa sebuleni naongea na wazazi wamekubali kesho mlete iyo posa"
"Wow mkewangu kweli nimefurahi sana maana nilikuwa nawaza wakikataa itakuwaje?"
Basi tukaongea apo nakutakiana usiku mwema mwisho tukaagana nikakata simu nakulala.
****
Asubuhi kulikucha nikawahi kuamka nakufanya usafi kama kawaida japo siku ya leo nilifanya usafi kila sehemu wageni wakija waone kupo vizuri nilimaliza nakuandaa kifungua kinywa baada ya apo nikarudi ndani nakumpigia simu Harvey nimsalimie ambapi nikamuuliza muda ambao wageni watakuja akanambia ni jioni wawili babayake mdogo na mjomba ake.
wazazi wangu waliamka nao pia wakauliza kuhusu huo ugeni nikawaeleza wanakuja jioni ivyo tukaanza maandalizi.
Hatimae muda ulifika wanaume wawili wakapiga hodi nakukaribishwa na baba,mama mimi sikuruhusiwa kuonekana ivyo nilibaki chumbani kwangu nikatumia muda huo kuongea na mumewangu mtarajiwa.
"Vipi baby wameshafika uko?"
Aliniuliza
"Ndio wamefika sasa ivi yani honey ninafuraha ajabu"
Nilimwambia
"Usijali mkewangu ndoa yetu haitochelewa"
Alinambia nakuzidi kunifanya nifurahi basi tukaongea apo adi tulipotosheka alikata simu nikabaki natabasamu.
Baada ya nusu saa nikasikia mama ananiita nikatoka nakuona wale wageni wameshaondoka.
"Lisa posa ishaletwa na majibu tusharudisha"
Alisema baba moyo wangu ukaripuka kwa furaha.
"Kwaiyo mwanangu kusoma tena ndo basi?"
Aliuliza mama
"Asome nini muache aolewe uko"
Alisema baba nakunifanya nicheke basi kilichobaki ni kusubiria siku yakuletwa mahari.
*****
Wiki moja ikapita tukizidi kuwasiliana na Harvey uku akinambia mipango ya harusi kwao imeanza.
Akanijulisha pia jumapili wanaleta mahari niwaambie wazazi wajue.
Basi nikawaeleza ambapo maandalizi yakafanyika ndugu wote wakapewa habari baadhi walisema watahudhuria iyo siku.
Hatimae jumapili ikafika mahari ikatolewa kilipikwa chakula watu walikula nakunywa.
Baada ya siku chache nikafanyiwa kitchenpart ambapo walihudhuria wanawake watupu nilipata zawadi nyingi mamangu alikuwa mwenye furaha sana.
Ikabaki send off ambayo wanaalikwa upande wa kiume nayo maandalizi yakafanyila Land mark hotel ndio ilipofanyika nilipendeza sana nguo niliyovaa wifi yangu Dorcas ndie alinipatia uku wifi mwengine Joyce aliekuwa marekani yeye alijitolea shela nitalovaa siku ya ndoa yangu.
Send off iliisha salama na watu wengi wakamjua mumewangu mtarajiwa ambae alipendeza alivyovaa suti yake nzuri.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikuwa wa kwanza kuondoka na watu wengine walibaki wanaburudika na mziki adi usiku sana walipotawanyika.
Hatimae siku ya ndoa ikafika.
Maandalizi yakafanyika na ndoa ikafungwa kwenye kanisa la Mt Joseph posta baada ya apo sherehe ikapangwa iwe Dreams Hotel iliyokuwa posta mpya ni hotel ya nyota tano tulipotoka kanisani wote tukaelekea uko ambapo vyakula na vinywaji vya kutosha viliandaliwa.
Ni siku nzuri sana kwenye maisha yetu niliisi kama ndoto kumbe ni kweli nimeolewa na Harvey.
Ukumbi ulikuwa umepambwa vizuri nakupendeza watu wengi walijaa wazazi pande zote mbili walikuwa na furaha sana.
Tuliingia nakukaa mbele sehemu yetu ilipoweka na sherehe ikaanza apo.
Mumewangu alipendeza na suti yake rangi ya gold iliyoendana na shela langu jeupe zuri ambavyo vyote vilitoka marekani kwa wifi Joyce.
Sherehe ilianza watu walikunywa nakula tulipata wazadi nyingi sana ikiwepo nyumba ambayo wazazi wa Harvey ndio walituzawadia.
Hatimae usiku mkubwa ukaingia nakufanya tuwe wa kwanza kuondoka ukumbini uku wapambe wakitusindikiza adi kwenye hotel ambayo honeymoon yetu itafanyika apo.
Basi tulifika nakuingia chumbani hotel yenye hadhi yake wanaolala apo ni watu wenye pesa bila Harvey naisi ata mguu nisingewahi kukanyaga apo.
Nilikuwa nashangaa mandhari yake adi Harvey aliponishtua.
"Lisa mke wangu unashangaa nini?"
"Mmh amna"
Nilimwambia uku najisikia aibu nishaonekana mshamba.
Harvey akanisogelea nakunivuta kwake tukakumbatiana.
"Twende tukaoge mke wangu"
Alininon'goneza sikioni alafu akanibusu shavuni niliisisimka sana.
"Harvey jamani tangu lini tunaoga wote?"
Nikamuuliza
"Lisa mimi ni mumewako sio Harvey bwana alafu tangu leo tunaanza kuoga wote"
"Bwana mi naona aibu"
Nilimwambia nakumfanya acheke
"Maajabu ayo mke kumuonea aibu mumewake ila iyo aibu najua sababu sijawah kukunaniliu sasa leo nataka nikutoe aibu yote"
Alinambia akanifungua zipu ya shela langu nakunivua nikabaki na nguo ya ndani baada ya apo alinishika mkono tukaingia bafuni kuoga.
Tulimaliza nakurudi kitandani nikawahi mwisho nakujifunika shuka adi juu asinione.
Harvey alipanda kitandani nakunisogelea.
"Yani kujifunika ivyo ndo nisikuone au?"
Aliuliza uku anacheka nikajifanya nakoroma.
"Usanii unauweza mkewangu kumbe"
Alijibu kusema sikumjibu akanifunua shuka nakuliweka pembeni baada ya apo akanisogelea nakuja juu yangu
"Harvey bwana sitaki fujo"
Nilimwambia
"Ooh kumbe ujalala bado"
Alisema uku mikono ipo kiunoni mwangu alisogeza mdomo wake adi shingoni nakuanza kunilamba uku akinin'gata kimahaba.
Akuishia apo alipeleka ulimi masikioni mwangu akashuka mdomoni nakunyonya lips zangu alizidi kutelemka mwili wangu wote akinilamba nakuninyonya niliisi pumzi inakata, nilipagawa mwili ulinisisimka sana bila kutegemea nikaanza kutoa sauti ambazo zilizidi kumpa hamu Harvey yakuendelea kutalii mwili wangu, alikuwa mtundu sana alijua kucheza na maungo yangu nusu saa aliniandaa adi nikawa sijiwezi akaamua kuniingilia sasa ufanyaji wake ulikuwa tofauti James apo nikaamini kila mwanaume na utamu wake hawafanani.
Kilichosikika ni kilio kutoka kwangu ambacho kwa Harvey ulikuwa ni ushindi mkubwa kilio cha raha si maumivu kwake aliona kama kinanda kinambembeleza nakumpa stimu au mzuka wakuendeleza sebene lake.
Hatimae tulifika mwisho kwa pamoja adi nikakiri nimekutana na mwanaume wa nguvu sikuweza kuinuka kitandani mwili haukuwa na nguvu Harvey alinicheka.
"Pole mkewangu jamani"
"Sitaki umenifanya adi nguvu zimeisha"
Nilimwambia nakumfanya acheke nilijua apo kajiona mshindi sababu akuna kitu mwanaume anapenda kama kuona kamridhisha mwanamke.
"Basi sikufanyi tena nisamehe ila mkewangu we mtamu mmh adi natamani tena"
Alisema nikajikuta nacheka
"Si umesema utaki tena?"
"Naanzaje nisitake kwanza leo tutakesha akuna kulala"
Alisema kazi ikaanza upya nililalamika adi sauti ikanikauka Harvey alikuwa na hamu sana namimi akuweza kuniachia mapema adi lakini alijua kunifanya nifurahie mapenzi yake na sio kuwa kama ananibaka akuniingilia kwa nguvu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wote tulitosheka nakulala uku tumekumbatiana
****
Asubuhi kulikucha aliewahi kuamka ni Harvey akaniamsha namimi niliekuwa siwezi ata kusimama akanisaidia tukaingia bafuni nakuniogesha baada ya apo tukarudi chumbani, nikashangaa kuona breakfast mezani kumbe muhudumu alishaleta basi tukajumuika kunywa pamoja.
Wiki moja ilitosha kufurahia mapenzi yetu uku tukicheza michezo mingi yakimahaba na mumewangu baada ya apo tukaondoka nakuelekea ilipo nyumba yetu masaki tuliyopewa na wazazi wake Harvey.
Ilikuwa nyumba ya kawaida si kubwa sana lakini ni nzuri iliyopambwa kwa thamani nyingi zakuvutia.
Maisha yetu ya ndoa yakaanza apo, furaha amani upendo ulitawala juu yetu wakwe zangu walinipenda sana nakunithamini mumewangu pia alizidisha mapenzi kwangu kilasiku adi nikajiisi malkia nakusahau matatizo yote
Kil nilichotaka nilipewa Harvey akutaka nifanye kazi nilikuwa nashinda nyumban kila wikiendi tulikuwa tunatoka nakwenda sehemu nyingi kutembea.
Hatimae mwaka mmoja ukaisha.
"Lisa mkewangu ninafuraha sana leo tunatimiza mwaka mmoja wa ndoa yetu"
Alinambia mumewangu tulipokuwa kwenye fukwe za bahari tukipunga upepo.
"Ata mimi mumewangu ninafuraha ni jambo lakumshukuru mungu sana"
"Natamani leo hii tungekuwa tunafurahia tukiwa na mtoto wetu"
Alinambia Harvey
"Usijali mumewangu mungu atatupatia watoto"
Nilimwambia bila kujua nini kinaendelea kwenye familia yao adi siku moja nikapata ugeni nyumbani kwangu ni mama mkwe, wifi yangu Dorcas na mama mdogo wa Harvey.
Niliwakaribisha vizuri lakini maneno waliyoniambia nilijikuta machozi yananitoka bila kutegemea ambapo ilionyesha jinsi gani wamenichoka
Ni asubuhi na mapema niliamka pamoja na mumewangu nakumchagulia nguo atakayovaa kazini pamoja nakumuandalia kifungua kinywa baada ya apo niikamsindikiza adi nje alipopanda gari.
"Kazi njema mumewangu"
"Asante mkewangu ubaki salama"
Tuliagana kwa furaha akawasha gari nakuondoka.
Nilirudi ndani nakufanya usafi nyumba nzima nilipomaliza nilitenga chai nakuanza kunywa sababu asubuhi tunaoga pamoja na mumewangu iyo ndo desturi tuliyojiwekea tangu siku ya kwanza tulipofunga ndoa adi sasa mwaka mmoja atujabadirisha.
Nikiwa nakunywa chai Mara nikasikia honi inapigwa nje na mlinzi akafungua geti baada ya apo nikasikia gari linaingia ndani nilishangaa ni nani uyo au mumewangu karudi ikanibidi nitoke kuangalia ambapo nikakutana na mamamkwe, mkwe mdogo yani mamayake mdogo Harvey na wifi yangu Dorcas, nilifurahi kuwaona nikawakaribisha ndani kwa furaha.
"Waoo jamani karibuni sana naona leo sapraizi asubuhi tu nimepata baraka"
Niliwaambia uku nikitabasamu.
"Mfyuuuuuuuuuuu eti baraka na kweli hii ni sapraizi tumeamua kukufata sababu tunaona umejisahau apa unaona kama unaishi na babayako sijui kuzaa huzai kazi kuvimbiana tu kama gunia la mahindi"
Maneno yalimtoka uyo mama mdogo aitwae Neema mchina sababu amejichubua sana adi amekuwa na ukijani weupe umepitiliza alafu ni shangingi sana nguo zake za bei uku akivaa madhahabu mengi mwilini cheni mahereni makubwa, pete vidole vya miguuni vyote adi mikononi katapakaa dhahabu kazi yake kutembea na wanaume wenye pesa tu ajawahi kuolewa wala kuzaa.
Nilistaajabu maneno aliyonambia nikamgeukia mamayake mzazi Harvey
"Mama mbona sielewi jamani?"
Nilimuuliza kwa upole jibu alilonipa machozi yalinitoka bila kupenda
"Usichokielewa kipi apo? Au ulitaka kuolewa na mwanangu mwisho umuue urithi mali mwaka mzima uzai unachotegemea nini nyumba itakushinda hii nataka wajukuu mimi"
Sikuamini maneno ya uyu mama ambae alikuwa akionyesha kunipenda nikifurahi nakufarijika nimepata mkwe mzuri kumbe ni tofauti mara wifi nae akaingilia
"Machozi yako kayatoe Leba wakati unazaa sio apa unasikia? Unajitawala unaona umefika eeh kakayangu utaki kumzalia kazi kujinenepea unamkosesha ata raha ya ndoa"
Walinichangia kwa maneno wote ata sikupata wakunisaidia nilibaki nalia machozi yauchungu yakinitoka nakufanya ile furaha yangu itoweke moyo wangu uliuma sana.
"Jamani ata mimi natamani mtoto ila mungu ajanijaalia bado"
Nilijaribu kujitetea
"Ivi ujawahi kutoa mimba wewe sema kweli?"
Neema mchina akaniuliza
"Apana mama sijawahi"
Nilimjibu
"Aah koma wee usiniite mama sijazaa mie tusizeeshane"
Alisema nakunifanya nitamani ata kucheka kwa maneno yake.
"Ila kama kweli unataka mtoto twende kwa mganga upate dawa sio kusema mungu ajakujaalia utakufa bila kuzaa"
Alisema nikaogopa maneno yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wewe Lisa unataka mtoto au utaki na kama utaki kwenda kwa mganga hii nyumba utaondoka tulete mwanamke anaezaa"
Alisema mamamkwe nikaona nikubali tu kwenda kwa mganga.
Basi apo wakafurahi tena wakaondoka uku wakicheka nakuniacha mnyonge ata hamu yakula sina.
***
Usiku alirudi mumewangu nikamuelezea yote alisikitika sana lakini akaniomba nikubali kwenda sababu anatamani sana mtoto.
"Mkewangu nakuomba kubali kwenda natamani sana kuitwa baba najua sisi ni wasomi hatupaswi kuamini waganga ila tambua tunashida inabidi tuwaamini labda tutafanikiwa"
Alisema Harvey sikuwa na jinsi nikamuelewa japo moyowangu uliniuma sana nilijua atakataa lakini amweungana na ndugu zake sikuweza kujizuia kilio cha kwikwi kikanishika nakumfanya aanze kunibembeleza.
"Nyamaza mamangu usilie nakuomba"
Alinisii akiwa kanikumbatia mwisho nikapitiwa na usingizi adi kulipokucha ilikuwa ni wikiendi asubuhi tu alikuja Mamamkwe na Neema mchina ambapo hawakuwa na maongezi mengi sana
"Tumekuja kumfata uyu bibie twende uko kwa mtaalamu"
Alisema Neema
"Aah mamdogo ebu tumia ustaarabu basi apa ni kwangu na uyu ni mkewangu pia naweza kukubali au kukataa asiende ustaarabu muhimu"
Harvey alichukia sababu kufika tu bila salamu Neema akaanza kuropoka.
"Ooh umekuwa siku izi sasa unaweza kunijibu ivyo mimi mamayako? Au kisa uyu kinyago ndo anakupa jeuri ushalishwa limbwata eeh?"
Alizidi kusema na kwa mara ya kwanza nikamshuhudia Harvey amechukia niliogopa sana.
"Mama nakuomba umwambie ndugu yako naweza kumpiga ata risasi za miguu na asinipeleke kokote ujinga nyumbani kwangu sitaki uyu mke nimemuoa mimi hamjaoa nyie mnajuaje kama mimi labda nina matatizo kwanini mumlaumu yeye eti azai kwani alipenda kuwa ivi au hamjui kama ata sisi tunaumia kukosa mtoto pia jana tulikubaliana aende uko kwa mganga atibiwe lakini wewe Neema uliekosa adabu ambae ata ndoa ujui ni nini kizazi huna unakuja kumwambiaje mkewangu we umezaa au?"
Alifoka Harvey nakunifanya nitetemeke adi nikaamini msemo unaosema muogope mtu mpole akichukia anakuwa mkorofi sana leo nilijionea kwa Harvey yule ambae muda mwingi alikuwa anacheka tabasamu alitoki usoni mwake leo amekuwa mkali adi nitamani kukimbilia chumbani.
Maneno yake yalimgusa sana Neema nakumfanya awe mpole mamamkwe nae akaingilia nakumuomba mwanae apunguze hasira.
haikuwa kazi rahisi ilichukuwa muda sana mwisho wakaelewana mie nilikuwa kimya nasikiliza tu baada ya maelewano wakapanga iwe lini siku yakwenda kwa mtaalamu au waniletee dawa nitumie bila kwenda.
"Apana uyu inabidi aende kwanza"
Alishauri Neema
"Sawa ila sitaki alale uko mnaenda nae na mumrudishe mkewangu"
Alisema Harvey wakamkubalia baada ya apo nikaingia chumbani kujiandaa na mumewangu akaja pia
Nilikuwa namuogopa alijua ilo akanisogelea nakunikumbatia kisha akanikiss mdomoni.
"Nakupenda mkewangu"
Alisema akiniangalia usoni uku anatabasamu.
"Nakupenda pia mumewangu"
"Naomba usiniogope sawa alafu akikusema lolote uyu Neema niambie"
Alisema ila nikamuitikia tu lakini sikuwa tayari kusema kitu nisije kuvunja undugu wao.
Basi nilijiandaa nilipomaliza nikatoka nakuungana na hao wamama tukatoka nje nakupanda gari walilokuja nalo safari ikaanza.
Ilituchukua masaa matatu tufakifa ni bagamoyo kunaitwa Mlingotini.
Tulifika tukashuka kwenye gari nakuanza kutembea Neema ndie alikuwa mwenyeji wetu akituonyesha njia kwenye mapori ndani ndani adi tulipofika sehemu moja tukaona kijumba kidogo cha nyasi mbele kuna pembe kubwa limefungwa vitambaa vyekundu na vyeusi.
Mara tukasikia sauti kutoka ndani ikisema
"Karibuni karibuni sana ingieni kinyumenyume"
Sauti ilitokea ndani ikasema ivyo niiliogopa nakuanza kutetemeka uku nikijiuliza
"mtu yupo ndani amejuaje nje kuna watu?"
Sikupata jibu, basi akaanza Neema kuingia kinyume akafatia mama mkwe wa mwisho nilikuwa mimi.
Humo ndani kulijaaa tunguri nyingi zilizozungushiwa mahirizi makubwa uku ngozi za wanyama zimetandikwa chini nakuwa kama zuria uyo mganga alijifunga kaniki nyeusi chini juu kifua wazi anamahirizi shingoni yananin'ginia kama cheni, jicho moja kajichora na unga mweupe alikuwa anatisha kama mchawi.
Akaanza kupiga manyanga uku anaimba nyimbo zisizoeleweka
"Najua shida yenu ni mtoto hesabuni mshafanikiwa mimi mchepe wa mchepule ndio kiboko ya matatizo"
Alisema
"Tawile mganga"
Neema akaitia kidogo nikapata faraja nitafanikiwa kupata mtoto nakuona uyu mganga ni mkweli.
"Sogea apa mbele we binti"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliniita nikakaa kwenye ngozi iliyokuwa mbele yake akachukua tunguri moja nakuniweka kichwani akaanza kuimba uku anafanya kama anatwanga na kifimbo kidogo baada ya apo akatoa ile fimbo iliyokuwa na rangi nyeusi akanipa mdomoni nilambe ilikuwa kama mkaa vile, baada ya apo akafungua kibuyu nakutoa unga mweupe akamimina kwenye karatasi nakunipa
"Hii dawa utaoga siku saba"
Akatoa mzizi mmoja nakunipa nichemshe nakunywa siku saba pia alafu akanipa na mafuta akinambia nijipake sehemu za siri kabla yakukutana na mumewangu.
"Baada ya mwezi majibu mtayaona"
Alisema mganga kwa kujiamini sana.
Basi Neema alitoa pesa akaweka tukaanza safari yakurudi nyumbani uku akimsifia yule mganga.
"Namuamini sana yule babu noma Lisa we jiandae kupata mtoto"
Alisema akiwa anafurahi sana, japo sikupenda kwenda kwa mganga lakini nilitamani nipate tu uyo mtoto.
Basi tulifika nyumbani usiku wakaniacha nakuondoka zao.
"Pole mke wangu"
Alinambia mumewangu nikamshukuru nilikuta ameandaa chakula tukajumuika pamoja kula baada ya apo tukaingia kulala.
Asubuhi ilifika nikaanza kutumia dawa adi zilipotimia siku saba nikamaliza dawa zote.
Hatimae mwezi mmoja ukafika sina dalili yoyote ya kuwa na ujauzito.
Mamamkwe alipopata habari akamwambia na Neema ambae alienda kwa waganga zaidi ya watano akaja na furushi la dawa nikaanza kutumia miezi sita ikapita akuna mimba wala ujauzito.
Nilikonda raha ya ndoa sikuipata kilasiku nikawa mtumwa wa madawa na mimba sipati ndugu wa mumewangu walinichoka nakuniita mgumba sizai mara tasa amani ya moyo wangu ilitoweka nikawa mtu wakulia kilasiku mumewangu akawa mfariji wangu ila mwisho nayeye alichoka nakuwa mlevi kilasiku anarudi amelewa nikaamua kuwashirikisha wazazi wangu juu ya ndoa yangu.
"Mwanangu ndoa zina mitihani mingi inahitaji uvumilivu mkabidhi mungu ndoa yako atakusimamia kwa kilakitu"
Mamayangu alinambia tangu apo nikaanza kwenda kanisani nikuhudhuria ibada zote nikisikia sehemu kuna mkutano wa injili naenda naomba sana nafunga lakini akuna matokeo yoyote
"Eeh mungu si unipe uyo mtoto jamani kwanini ulinipa mume nakunifanya nisizae naitwa mgumba naitwa tasa mie mungu wangu nihurumie"
Moyowangu unauma unachoma sana naumia wakunifariji sina, wazazi na ndugu wa mumewangu walinichoka nakuniona kama kinyago thamani yangu ilitoweka sikuwa yule Lisa nilesifika kwa urembo na umbo lakuwapagawisha wanaume nilifujika nilikonda macho yote yalipoteza nuru nakuwa mekundu adi natisha.
Mwaka mwengine ukafika bila mtoto shetani alitawala ndoa yangu Harvey akaanza kulala nje, nilipokuwa nikimuuliza kwanini arudi nyumbani anasingizia kazi nyingi ofisini.
Ikanibidi nimshatie mamayake ambae alinijibu
"Mwache alale nje ata mwezi kuliko kulala ndani na mwanamke mgumba usiezaa tena kuanzia leo ukome kuniambia upuuzi mfyuu"
Alisema uyo mama nilijuta kuingia kwenye familia hii kukosa mtoto kulininyima raha ya dunia kuna muda nilitamani nijiue kabisa.
Mumewangu akuonyesha kunijali kwa lolote ata ikitokea siku analala nyumbani anakuja amelewa nakuingia chumba cha wageni kulala.
****
Dunia yote niliona imenielemea ndoa ilikuwa chungu Harvey alibadirika mapenzi juu yetu hayakuwepo tena alinionyesha wazi amenichoka akunipenda tena.
Niliamua kurudi nyumbani kwetu ambapo baba alinikatalia kubaki nirudi kwa mumewangu
"Wewe ni mke wa mtu unaanzaje kurudi nyumbani bila mumeo au talaka? aya rudi ukamalizane na mumewako sitaki kukuona"
"Baba mumewangu amebadirika analewa alali nyumbani ata siku mbili arudi"
Nilisema uku nikilia
"Ayo ni kawaida kwenye ndoa muhimu uvumilivu tu rudi kwa mumeo"
Sikuwa na jinsi niliondoka uku nalia nilipofika nje mama akaja
"Lisa mwanangu kavumilie yakikuzidia rudi nyumbani mamayako sijafa ni mzima achana na uyu babayako mimi nipo"
Alisema mama nikamshukuru nakuondoka kurudi nyumbani kwangu nilishangaa kukuta mlango umefunguliwa nilipoingia ndani nikamkuta Harvey amekaa sebuleni uku glass ya wine ipo mkononi.
Aliponiona naingia akuuliza akanirushia ile glass usoni nakunipasua
"Unatoka wapi malaya wewe yani kuzaa huzai unaona bora kufanya umalaya eeh?"
Aliongea uku akivua mkanda wake nakuanza kunitandika nao mwilini nilijaribu kujitetea nikimwambia
"Nisamehe mumewangu nimetoka kuwasalimia wazazi wangu"
"Iko ndo umeona kisingizio uwasalimie unafaida gani wewe bora ungewapelekea mjukuu unaenda mwenyewe ili iweje tena unatoka bila kuaga shenzi kabisa"
Alisema akizidi kunipiga sikuweza kujitetea tena alinipiga adi alipotosheka akaniacha
"Subiri si unajiona umefika nyumba utaiona chungu hii utatoka bila kufukuzwa"
Alisema ivyo nakutoka nje nikasikia mlio wa gari nakujua ameondoka kabisa, maumivu niliyokuwa nayasikia ayana mfano sikulia kwa ajiri ya kipigo bali kwa jinsi Harvey alivyobadirika nilijikuta namlaumu mungu kwanini ameamua kuchukua furaha yangu yule mwanaume mpole mwenye kunipenda nakunithamini leo amekuwa kama shetani iliniuma maumivu yalinijaa nililia bila kupata wakunibembeleza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikainuka nakuingia bafuni kuona usoni nilipasuka kwenye paji nilioga nilipomaliza nikaingia chumbani nakumpigia simu mama kumueleza sababu kwenda hospital niliogopa.
Usiku huo huo mama alikuja na dawa akanipaka nakunipa zakumeza kupunguza maumivu.
"Pole mwanangu"
Alisema uku akionyesha hudhuni
"Mama nampenda sana mumewangu naamini mungu atambadirisha"
Nilisema kama kujifariji
"Najua maumivu unayopata nakuomba yakikuzidia rudi nyumbani"
Alisema mama hakukaa sana aliondoka zake.
Nilibaki mnyonge siku mbili Harvey akurudi nyumbani adi siku ya tatu akaja usiku na mwanamke akiwa amelewa sana akanifukuza chumbani nakuingia yeye na mwanamke wake maumivu niliyoyasikia hayaelezeki
Sikutegemea kama mumewangu angefikia hatua yakuleta mwanamke ndani ya nyumba namimi nikiwepo iliniuma sana.
"Harvey mumewangu nimekukosea nini mimi?"
"Koma mimi sio mumeo wewe ni housegirl humu ndani beba takataka zako zote humu utoke iki chumba hakikuhusu ni changu kuanzia leol utalala chumba cha wageni"
Alisema nakunifukuza ndani nguo zangu zote akatoa kabatin nakunirushia nje ya mlango baada ya apo akaingia chumbani na uyo mwanamke wake nakujifungia.
Nililia sana nakumlaumu mungu kwanini ameruhusu aya yote yatokee sikuweza kulala nilikesha nalia adi asubuhi sikuweza kutoka nje nilisikia mlio wa gari nakujua Harvey ameondoka.
Huo ukawa mwanzo kilasiku alikuja na wanawake wapya nililia mwisho nilizoea nakukaa kimya nikiangalia nini mwisho wake.
Aliona sifa leo kaleta mwanamke mnene kesho mwembamba, Mara mweusi Mara mweupe warefu kwa wafupi wakawa wanapishana ndani wenye maumbo na wasiokuwa na maumbo kila aina nyumba iligeuka gesti sasa adi nilimpuuza nakumuona ni mjinga baada ya mtoto atapata magonjwa sikutaka kumsemesha lolote asije akajirudi akutane namimi aniambukize magonjwa yake bora afe mwenyewe.
Siku moja nilikaa nakuwaza naishi kwenye hii nyumba ili iweje ikiwa mwanaume mwenyewe ndo uyo cha wote nikaamua kumshirikisha mamayangu anipe ushauri nifanyaje
"Sasa kama mwanaume kafikia hatua yakuleta wanawake ndani unachosubiri apo nini?"
"Sasa mama nifanyeje maana sielewi"
"Akuna chakufanya zaidi ludi nyumbani muache na uhuni wake"
Alisema nikamuelewa
Baada ya apo nikamsubiri Harvey arudi usiku ambapo sikujali amelewa wala mzima siku iyo nilijiandaa sababu nilishamchoka tabia zake nilikuwa mpole lakini kwa dharura nikaamua niwe mrembo mcharuko yule Lisa alievurugwa alirudi sasa.
****
Ilikuwa usiku saa tano nimekaa sebuleni nacheki tv na si kawaida yangu muda huo nakuwa chumbani nimejifungia Harvey alikuja akashangaa kunikuta nipo sebuleni,
"Wewe malaya unafanya nini apo yani unajiachia kuangalia Television unajua nilinunua bei gani?"
Alianza kufoka uku akiwa na mwanamke pembeni.
Siku iyo nilijiandaa kabisa nilivaa kipensi kufupi kama naenda club juu nina t-shirt ambayo haiwezi kuchanika haraka, sikumjibu ila nilisimama nakumgeukia yule mwanamke kwanza
"Umewezaje kuingia kwenye nyumba yangu ukiwa na mumewangu unajiamini kitu gani haswa?"
Nilimuuliza
"Mimi amenambia hana mke anaishi pekeyake"
Alisema uyo msichana ambae alikuwa mnene kiasi amejazia.
"Sasa sikiliza kama yeye ajasema mie ndo nakwambia uyu ni mumewangu wa ndoa kwa usalama wako ondoka kabla sijakuvuruga"
Nilisema uku nimekaza sura nikionyesha sina masihara
"Lisa Lisa nitakupasua naomba ukome kuniingilia mambo yangu mwanamke tasa wewe uzai nani akutake?"
Harvey aliingilia kusema
"Sawa mimi tasa sizai tangu uanze umalaya wako ushatia mimba wanawake wangapi zaidi naisi wamekupa maradhi tu mwanaume malaya wewe kilasiku kuleta wanawake wapya humu ndani alafu we binti utakuwa wa mia mbili umalaya wako kuokota wanaume ovyo utakufa na ukimwi"
Niliongea kwa hasira maneno yalimchoma Harvey akanivamia anipige sikukubali nilikumbuka enzi nipo shuleni nilikuwa napigana adi na wanaume nikaona nipambane nae na vile amelewa ndo kabisa.
Tulivaana ngumi zikaanza apo yule mwanamke alipoona ivyo alitoka mbio nakutuacha.
"Lisa nakuua leo"
"Sema tutauana uwezi kuniua mimi pekeyangu"
Nilikuwa chini yeye juu akinipiga japo nilijaribu kujitetea alipoona haitoshi akasimama akiyumba nakuvua mkanda anipige nao sikukubali nilikuwa na glass mezani nikachukua nakumpiga nayo ya usoni ikampasua.
"Aaah Lisa umeniumiza"
"Kufa kabisa shetani we"
Nilimjibu nikamuacha anatokwa na damu nikaingia ndani nilishafungasha mizigo yangu nikabeba nakutoka nje nilipoenda adi barabarani nikapata bajaji iliyonipeleka adi nyumbani.
Saa sita usiku walishangaa wazazi wangu imekuwaje uku nina damu jicho moja limevimba na kipensi nilichovaa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Aya imekuwaje tena?"
Baba akauliza
"Nimemchoka yule mwanaume malaya kilasiku kuleta wanawake ndani leo nimepigana nae video hii apa"
Muda ambao Harvey aliingia niliweka simu yangu sehemu ya rekodi sababu nilijiandaa kwailo nilijua ugomvi lazima utokee na ushahidi niwe nao nilitaka niende mahakamani kudai talaka, basi nikawaonyesha video baba alicheka sana
"Kumbe ujaacha ucharuko wako ila umekusaidia bila ivyo uyu mwanaume angekuumiza"
Alisema baba
"Wewe baba Lisa nawe sasa unacheka nini ebu tulaleni jamani kesho tuongee iweje"
Mama alisema
"Sio kuongea nataka kwenda mahakamani nikadai talaka yangu"
Niliwaambia
"Sawa kesho tutapanga iweje kapumzike mwanangu"
Alisema baba nikaingiza ndani mabegi yangu nakuoga nikalala kwa amani bila kumuwaza Harvey.
Asubuhi kulikucha tukaweka kikao baada ya apo nikaongozana na wazazi wangu adi mahakamani nakufungua kesi yakupigwa na Harvey pia nikitaka anipe talaka yangu basi tuachane barua ya wito ikaandikwa nakupelekwa kwa Harvey ambae alishtuka sana alipoipata akawaambia ndugu zake tarehe 20/4/2015 akaja mahakamani kesi ikasikilizwa apo hakukuwa na mjadala akaandika talaka nakunipatia sikutaka chochote kutoka kwake wasijekusema sijazaa sijui mali sijachuma nae nilichoshukuru roho yangu ipo salama.
Basi kesi ikaisha nakurudi nyumbani japokuwa niliachana na Harvey bado moyowangu haukutaka kumsahau nilimkumbuka kilasiku nikikesha nalia nakutamani siku zirudi nyuma niwe nae moyo wangu ulikuwa na kidonda kikubwa sikujua lini kitaisha, furaha ilitoweka nakuwa mnyonge muda wote mfariji pekee alikuwa ni mamayangu adi siku moja akaja chumbani nakusema anamazungumzo namimi
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment