Chombezo : Dokta Mimi Siumwi Huko
Sehemu Ya Tatu (3)
kwa vile mahali aliposimamisha gari hakukuwa na njia nyingine ya kutokea zaidi ya ile aliyoelekea yeye kwa miguu… “Mtasha mbona umekuwa mstari wa mbele sana kunizuia mimi nisifafanye uhalifu, inakuwaje wewe unashindwa kujizuia?” Mume wa Monica alisema akimwita mwenzake huyo kwa jina lake la utani.
Mara, mwenye gari alitokea
Alishtuka kuona gari lake limeharibika sehemu ya mlango huku timbwili likiendelea…
“Jamani vipi tena?” aliuliza kwa mshangao mkubwa.
Majibu aliyoyapata yalimfanya ajutie lakini akaahidiwa kulipwa fedha ili kwenda kutengeneza gari hilo japokuwa alikubali lakini kwa shingo upande.
Baada ya utulivu kurejea lakini huku wanaume wote wakiwa na hasira ya wivu, waliamua kwenda polisi ambapo Dokta Kisarawe aliwekwa ndani ili kupisha uchunguzi wa madai ya wanaume hao kwamba ametembea na wake zao na kuwapa ujauzito.
Baada ya kuandikisha maelezo, walirudi nyumbani. Wote walifikia nyumbani kwa Mtasha, mume wa Sulee ambapo kikao kilikaa na misimamo ilitolewa…
“Mimi bwana kwa upande wangu nasema wazi kwamba sina haja ya kuwa na mke kama huyu,” alisema mume wa Monica huku akimwangalia mkewe kwa macho yaliyojaa uchungu…
“Hata mimi, Sulee nakuandikia talaka zako tatu sasa hivi,” alikuja juu Mtasha na kutaka kumpiga tena mke wake kwa hasira…
“Sasa Mtasha si umeshasema unamwandikia talaka si ufanye hivyo, achana na kumpiga bwana,” alisema mume wa Monica.
Wanawake hao wawili waliangua kilio huku kila mmoja akimlaumu mwenzake kwamba alimsababishia lakini lawama za Monica kwa Sulee zilikuwa za kweli kwani yeye alipelekwa na shoga yake huyo ambaye alikuwa akiijua tabia chafu ya Dokta Kisarawe…
“Bila wewe Sulee mimi yasingenikuta haya. Ulijua Dokta Kisarawe ni mwingi wa habari ni kwa nini hukuniambia maana hata wewe ulishapitiwa…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Halafu nilimwambia dokta. Alikuwa akipenda kunishikashika sehemu zisizohusika na matatatizo yangu, nikamwambia dokta mimi siumwi huko yeye hakusikia,” alilalama sana Monica…
“Monica ni shetani, hata mimi nilimwambia dokta mimi siumwi huko wakati akipeleka mikono yake kwenye matiti yangu lakini hakutaka kunisikia. Tusameheni jamani.”
“Hakuna msamaha hapa… Ala!” wanaume wote walijikuta wakijibu kwa pamoja bila kutaarifiana…
“Kwanza ni muhimu kwenda kupima afya zetu maana kama mna mimba ina maana mlikuwa hamtumii kinga,” alisema mume wa Monica…
“Huko kuchepuka kwenu ndiyo faida yake mnaiona sasa,” alisema mume wa Sulee huku akikohoa. Hapo alikuwa akisaka karatasi ya kuandikia talaka mara moja.
***
Siku ya pili, Mtasha, yaani mume wa Sulee na mume wa Monica walikwenda kupima virusi vya Ukimwi. Walikutana na wake zao huko wakiwa na shangazi wa Sulee ambaye aliomba kuzungumza na Mtasha kabla ya kuingia kwa dokta. Kwa heshima Mtasha alikubali na akatoka pembeni…
“Baba najua unaniheshimu sana…”
“Kweli shangazi…”
“Mwenzio kanijia na talaka analia. Lakini aliponisimulia kisa hata mimi nilikuunga mkono mwanangu…”
“Nashukuru sana kusikia hivyo shangazi…”
“Enhee, lakini sasa nina ombi moja tu kwako…”
“Lipi hilo shangazi?”
“Msamehe Sulee.”
Mtasha palepale alijishika kichwa na kujikuna huku akitumbua macho, akakumbuka mema aliyowahi kuyafanya shangazi huyo kwake maana ana uwezo si wa kitoto.
Kuna mwaka Mtasha alipata kesi mbaya sana, uchumi wake ukayumba sana akajikuta hana hata pesa ya kula. Shangazi huyo wa mkewe akawa ndiye mfadhili wake kwani alikuwa akimpa pesa ya kula na pia alimsimamia kwenye kesi hiyo kwa kumuwekea wakili na akashinda.
Baada ya kushinda alimpatia mtaji akaendelea na miradi yake iliyosimama…
Wakati wa maongezi hayo, shangazi mtu hakumkumbusha kitu chochote Mtasha. Alimwacha ajipime mwenyewe tu…
“Da! Shangazi kusema ukweli umenipa wakati mgumu sana,” alisema mume wa Sulee…
“Kwa nini mwanangu? Kusameheana kumewekwa na Mungu na ukimsamehe mwenzako hata Mungu atapenda na kukubariki.”
“Ni kweli, lakini shangazi unalionaje hili la ujauzito?”
“Hilo unaweza kuliacha mikononi mwangu nikashughulika nalo.”
“Utafanyaje shangazi? Maana mimi kusema kweli siwezi kuishi na mke mwenye ujauzito wa mwanaume mwingine.”
“Ndiyo maana nimesema niachie mimi kuhusu hilo.”
“Shangazi maamuzi yako ni mema na nakuheshimu wewe sana, je vipi kuhusu kupima Virusi vya Ukimwi?”
Muda wote huo, mume wa Monica alipokuwa amekaa alikuwa akimtumbulia macho mume wa Sulee kama anayemwambia asithubutu kukubali hata siku moja maneno ya shangazi wa Sulee…
“Ndiyo maana tupo hapa! Wewe unadhani Sulee ana virusi?” alisema shangazi mtu huyo…
“Siwezi kusema anavyo au hana, ila kupima ni muhimu shangazi.”
“Kwa hiyo kama atakuwa salama utakuwa umepokea ombi langu siyo?
“Naamini hivyo.”
“Basi turejee kusubiri zoezi likamilike.”
Walirudi kwenye fomu. Mume wa Monica akamuuliza mume wa Sulee mazungumzo yao yalihusu nini…
“Shangazi anataka nimsamehe Sulee.”
“Uko tayari kwa hilo?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mh! Nimemwambia kama atakuwa hajaathirika naweza.”
“We unataka kumrudia Sulee?”
“Unajua nini mshkaji? Huyu shangazi amenisaidia sana katika maisha yangu kuliko mtu mwingine yeyote…”
“Kwa hiyo?”
“Kwa hiyo naweza kuangalia upya cha kufanya.”
“Mh! Nadhani sijakuelewa.”
“Kivipi?”
“Yaani pamoja na mambo yoote waliyotufanyia hawa Malaya wewe unakubali tuwasamehe, Mungu aniepushie hilo mawazoni mwangu,” alisema mume wa Monica na kumfanya mume wa Sulee kuwa na mawazo nusunusu tofauti na alivyoongea na shangazi mtu.
***
Majibu ya vipimo yalitoka, waliitwa mtu mmoja mmoja lakini huku wakiruhusiwa kwenda na watu wao kama wapo walioongozana nao.
Sulee alikwenda na shangazi yake huku akidondosha machozi kwa kuwa muda wa zamu yake ulifika. Alikuwa akitetemeka sana.
Monica, mumewe na mume wa Sulee walibaki nje lakini mume wa Sulee aliuliza kama itakuwa busara na yeye aende kwa vile yanaweza kutoka majibu ambayo yamechakachuliwa na shangazi huyo kwa vile alitaka ndoa ya Sulee iendelee kudumu.
“Noo, achana nao bwana. Wewe mbona hueleweki? Kwanza kama wao walitaka uwazi na ukweli kwa nini wasikwambie muingie wote?” alihoji mume wa Monica mpaka mwenyewe akaona ni kweli, akabaki kwenye fomu.
Baada ya dakika kama kumi, kilio kikubwa kikasikika kutokea chumba cha daktari…
“Uuuwi, Mungu wee nisaidie. Nitakwenda wapi mimi?” ilikuwa sauti ya Sulee…
“Ngoma tayari hiyo mwanangu, hakuna kurudiana wala kwenda mbele,” alisema mume wa Monica huku akichekelea. Alijua mpango wa shangazi mtu kuirejesha ndoa hiyo haupo tena.
Kwa upande wake, Monica alionekana kuwa mtu mwenye mchecheto zaidi kwani kila wakati alikuwa akisimama na kukaa. Aliamini kama Sulee ‘aliungua’ hata yeye yumo ndani ya ‘moto’ huo.
“Mmh! Sasa kama Sulee analia amegundulika kuwa na virusi je mimi? Maana mwanaume aliyemwambukiza yeye ndiyo huyohuyo ametembea na mimi,” alisema moyoni Monica huku akimtupia macho ya wizi mumewe.
“Monicaaa…” aliita jina muuguzi kabla hajamalizia, Monica mwenyewe alisimama haraka sana. Mara Sulee na shangazi yake wakatokea huku Sulee akichuruzika machozi.
“Pole Sulee,” alisema Monica lakini hakuitikiwa hata shangazi yake hakusema kitu.
“Baba tunaondoka, uamuzi wako ubaki kuwa palepale,” alisema shangazi mtu akimwambia mume wa Sulee. Alipita kwenye korido kwa aibu kubwa akiwa amejiinamia mpaka kwenye gari lake akifuatwa na Sulee kwa nyuma.
****
“Eee, thanks God. Asante Mungu, wewe ndiye muweza wa yote. Oooh! Si kwa nguvu zangu bwana bali kwa neema tu. Mimi Monica mimi kwamba sina virusi?” sauti ya Monica ilisikika kutokea kwenye chumba cha daktari.
Ilifika mahali akapiga na vigeregere kufurahia majibu ya vipimo vyake.
Mumewe alianza kuhisi ganzi akiwaza kwamba endapo mkewe yuko fiti halafu yeye akakutwa na ngoma itakuwaje?
“Itakuwa poa tu kwani maisha bado yataendelea,” alisema moyoni mume wa Monica huku akiangalia chini kwa mawazo.
“Mkubwa unasikia huko ndani? Shemeji yuko ngangari,” mume wa Sulee alisema.
“Eee, ndiyo sherehe inaendelea ndani.”
Mara Monica alitokea…
“My dear niko fiti, sina virusi wala vijidudu,” alisema Monica huku akirukaruka kwenye miguu ya mumewe…
“Kwa hiyo?” mumewe alimuuliza…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Heee! Hujapenda?”
“Hata nikipenda, kwani kuna nini? Si umekutwa upo fiti tu.”
“Hunisamehi?”
“Haitatokea Monica.”
Monica aliangua kilio mbele ya watu huku mumewe naye akiitwa kuchukua majibu yake. Kumbe Sulee na shangazi yake hawakwenda mbali, walikuwa kwenye gari wakisubiri matokeo ya mume wa Sulee, mume wa Monica na Monica mwenyewe.
“Mshkaji mimi nataka twende wote,” alisema mume wa Monica baada ya kuitwa jina lake na muuguzi mmoja.
Walizama wote mpaka kwa dokta na wakasema wote wamefika kwa kupima…
“Kwa hiyo majibu mnasikiliziana?” alihoji dokta.
“Ndiyo.”
Alianza kwa kuwashauri huku akiweka majibu ya wote sambamba, karatasi ya mume wa Monica ikianza juu.
“Sasa kwa kuwa mpo wote na wote mmepima na majibu yote yapo hapa baada ya ushauri niliowapa, wote mpo vizuri hakuna mwenye virusi vya Ukimwi,” alisema dokta. Walisimama, wakakumbatiana. Wakampa mkono dokta na kutoka nje huku wakicheka kwa furaha…
“Mungu anajua cha kufanya mshkaji, wale wanawake siyo kabisa,” alisema mume wa Monica…
“Lakini kama wewe huna na shemeji hana si mnaweza kurudiana?” alihoji mume wa Sulee.
“Na ile mimba?”
“Si utailea tu.”
“Mimi nilee mimba ya Dokta Kisarawe?”
“Kwani mshkaji kuna nini?”
“Haitatokea. Mara kumi angenibambika nisijue kuliko kujua.”
***
Sulee na Monica walikumbatiana kwenye gari huku wote wakilia. Kilio kikubwa kilikuwa kwa Sulee kwani alikutwa ameungua wakati mwenzake yupo fiti.
“Mwanangu nyie naona mambo mazuri maana naona vicheko,” shangazi wa Sulee alimuuliza mumewe…
“Mungu hamtupi mja wake shangazi. Mungu mkubwa bwana,” alisema mume wa Monica huku wakiondoka zao kwa mbwembwe wakicheka na kupigiana mikono na wakitembea kwa ujasiri wa hali ya juu.
Wake zao walikuwa wakiwatazama kwa macho yanayoendelea kujaa machozi wasijue la kufanya. Ghafla waliangua vilio mpaka watu wakajaa lakini hakukuwa na jinsi, waume zao walishaamua. Walijuta na kujuta kwa usaliti wakati waume zao walikuwa wakihangaika kusaka maisha
na siyo uhuni kama walio
kuwa wakifanya wakezao.
"shangazi mimi sijuwi kwa nini
jamani Yani nimetembea na Monica kwa mwanaume mmoja
lakini mwenza hana shangazi"
"pole Sulee Nimipango ya Mungu
wala usijari"
"Monica ladhima nijari
Moyo wangu una umia sana najuta na juta"
lakini shangazi yake sulee
hakuwa na wasiwasi kabisa
kuhusu suara hilo
"Sawa Sulee mimi narudi
kijijini nikaanze maisha mapya"
alisema Monica huku
akitokwa na Machozi sana"
"sikiliza Monica baki nasi hapa hapa mjini sawa utakaa na sisi"
"kweli shangazi oooh Asante Mungu wangu"
****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
baada ya miezi2:
Dokta kisarawe
alihama Dar na kuamia Morogoro
huko alikutana na kijana mmoja
aliye itwa Adams j maryo jr.
Aliye kuwa mfanya biashara
hapo Morogoro Dokta kisarawe
aliacha kazi ya udokta na kuanza kufanya biashara anazo fanya
Adams za Magari kutoka
japani Maisha yalisonga sana
kisarawe alikuwa mwembamba sana lakini alikuwa kaninepa vibaya ndani ya miezi mi3 tu
mambo yake yalikuwa safi
kutokana na Elimu yake kuwa kubwa sana alikuwa msaidizi
katika kampuni ya Adams Maryo.
Adams alikuwa akimtumia kisarawe katika mahesabu na hata akwenda nae japani
"Unajuwa safari moja tu nimeona
mabadiliko katika biashara yangu
kaka kisarawe"
"unajuwa kwa nini"
"hapana sijajuwa"
"tatizo lugha ulikuwa huiwezi
walikuwa wakikuibia sana bei ya gari moja walikuwa wakikuibia zaidi ya laki7 ya tz"
"sasa umenifungua akiri
kaka sasa kivipi"
"kulikuwa kuna pesa inayo tolewa
katika jumla ya manunuzi
wewe ulikuwa hujuwi"
"ok asante nakutegemea
kaka"
"tupo pamoja"
****
Sulee alikuwa mtu waku lia kila
Mara Monica alikuwa ndiye Mtu wa kumliwaza Muda wote
Mimba zao zote zilikuwa za miezi 7 kila Mtu Sulee alikonda sana
alishindwa kula Hakuwa na Furaha kabisa Moyoni mwake
alimchukia kabisa dk kisarawe
kwaku sababisha Ndoa yake
kuvunjika :
"Monica nina siri kubwa sana
kuhusu Sulee"
"siri gani hiyo Shangazi...
Ila wewe inaonekana haujatulia
kabisa unaweza ukamwambia"
"Shangazi wewe ndiyo nguzo
yangu katika maisha yangu yote kwa sasa siwezi kumwambia kabisa shangazi naumia
sana kumwona sulee akiwa katika
hari ile"
"Hata mimi najuwa
sana kutoa mimba nikosa sana
lakini je ukimsababishia
nidhambi pia?"
"shangazi mh hapo sijuwi
ila ni dhambi siyo kubwa"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"huna uwakika Monica"
"ndiyo"
"basi kuna jambo ambalo
nataka itoke ikitoka
Nahuakika sulee mwanangu atakuwa na Afya njema"
"sasa shangazi ni jambo gani hilo
nijuwe maana mimi na wewe ni walezi wake sasa kila siku
hari yake ina zidi kuyumba
ona anavyo pungua hata kama na H I V. Ni miezi michache sana
hawezi kuwa ana dhohofika
kiasi hiki huyu hata mawazo
yana changia"
"ngoja kesho takwambia"
"shangazi sawa"
"acha niende kazini
badae"
"kazi njema Mama"
"leo unaniita mama"
"yah kuanzia leo
takuita mama nasiyo shangazi
naomba ukubali"
"sawa maana wanangu wote
wapo makwao hapa sina
mtu wakunipa mahaba ya kuniita mama nita furahi sana"
****
Baada ya siku moja:
"Monica"
"Naam sulee"
"hivi imekuwaje wewe huna ukimwi na mimi ninao"
"kwa nini wauliza hivyo"
"nawaza sana sijuwi
kwa nini maana wote tumetembea na mtu mmoja
Dokta kisarawe mwenye
ukimwi"
"hata mimi sijuwi
ila punguza mawazo mpezi angu
una niliza sana napo kuona"
"hapana Monica najuta sana
Mume wangu tulikuwa tukipendana sana sana ujinga wangu umeniponza nilifanya vile
kuokoa ndoa yangu kumbe ndiyo
nilikuwa naipoteza jamani
hiii hiii mmh"
"nyamaza wangu
usilie Sulee"
"ina uma sana"
"jikaze sulee angalia upo katika
hari mbaya siyo vizuri kulia lia
kila mara"
Hari ya Sulee ilikuwa mbaya sana
Monica alitoka inje nakumwita dereva ili wampe msaada :
"dereva sulee kadondoka
hari yake mbaya sana twende tukampe msaada"
Monica dereva pamoja na mlinzi
waliingia ndani nakumkuta
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
sulee damu zikimtoka
kwa wingi ukeni"
"jamani jamani nisaidieni
kumchukua kumpakiza kwenye gari tumpeleke hospital"
walimchukuwa
nakumwingiza katika gari nakumpeleka hospital
kwa matibabu"
"shangazi sulee kazidiwa
sana na damu zinamtoka sana ukeni kapoteza fahamu"
"mko wapi sasa"
"tupo hospital kubwa hapa"
"ok nakuja"
Monica alishangaa sana
alipo kuwa akiongea na shangazi/Mama kwakuto jari sana
angekuwa mwingine ange piga kelele (uwii jamani mwanangu)
lakini ilikuwa tofauti kabisa"
"kutokana na kupanda kwa bp
kwa kiwango kikubwa sana
imesababisha mimba kutoka
sasa mlikuwa mkiishi vipi na
huyu hamkujuwa kama mama
mwenye mimba anatakiwa
usi muudhi wala kufanyishwa kazi ngumu"
"dokta hari ya mgonjwa
imebadilika ghafra sana"
"basi ni hivyo ila kuna vipimo
vingine bado havijaja subiri
sawa mgonjwa mleteeni ndizi laini na uji ok bado anawekewa damu"
"sawa daktar"
"Mama ila
hari yake inaendelea poa
ila mimba imetoka"
"yes"
"shangazi yes wakati kiumbe
kimetoka mbona sikuelewi"
"Monica ni story ndefu kidogo
Nihivi Mimi na doktar Tuli....
Tuli Ongea adanganye
kuwa sulee ana HIV ili
Mumewe amuache nilikuwa
sipendi Sulee akae na Mumewe
kwani alikuwa hana Hadhi ya kuwa na sulee kwakuwa
walipendana na kuwa na ndoa
sikuwa na jinsi ya kuwatenganisha kabisa niliamuwa iwe hivyo tulijuwa
sulee atakuwa katika
mawazo sana na kupandisha BP
itakayo sababisha kujifungua
kwa kupewa dawa ya kukisukuma kiumbe au kutoka mimba mpaka hapo safi atarudi katika hari yake ya kawaida"
"lakini shangazi ulivyo fanya siyo
vizuri kabisa unajuwa"
"nyie mmefanya vizuri au unaongea tu"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"hapana shangazi kuuwa na kumsariti mwenzako
dhambi hazi fanani shangazi"
"kwahiyo mimi ni muuwaji
eeh"
shangazi alifoka kwa hasira sana
mpaka Monica aka shtuka na kujiludi chini.
"sina mana hiyo shangazi
namaanisha kuwa"
"kuwa nini eeh"
"kuwa dhambi ni dhambi tu"
"umeona sasa mbona mimi namuokoa sulee awe na maisha safi wewe unataka kusema mimi
nina kosa wewe Moni nini"
"aah shangazi ila naona upo sahihi tu sijuwi na mimi nitoe hii mimba"
"hapana usitoe takusaidia kuilea sawa sulee nimehangaika nae
tangia mtoto wa miezi mi4 wazazi wake walikufa hivi unajuwa mimi siyo shangazi yake wa damu"
"sijuwi kabisa nilijuwa ni dada wa baba yake wewe"
"hapana baba yake alikuwa dereva tax alikuwa ana nibeba kutoka kazini mpaka nyumbani
tukawa kaka dada baba yake ni mtu wa kenya na mama yake ni mtu wa kenya nae walikutana hapa hapa dar wakawa wapenzi
mpaka waka owana na kumzaa
Sulee, walikufa kwa ajari ya gari
wakitokea Bagamoyo"
"ooh kumbe sasa sulee ana juwa kuhusu hilo"
"hapana kuhusu kufa ana juwa
kuhusu kama mimi siyo shangazi wa damu hajuwi naomba kuhusu suala hili usimwambie sawa"
"nimekuelewa"
baada ya miezi 3:
Sulee alikuwa fiti kama zamani
japo kuwa alikuwa hana furaha kabisa alijaribu kuwasiliana na Mumewe lakini haikuwa poa kwakuwa Sulee aliasirika
Mumewe na sulee mwenyewe walijuwa hivyo
isinge kuwa Rahisi kurudiana
kuwa wapenzi au wana ndoa.
Shangazi alikuwa akimletea
dawa ili ameze kama dozi
ya HIV kumbe zilikuwa za BP
kwakuwa alikuwa hazijuwi dawa
alikuwa akimeza tu Nae Monica
hari yake ilikuwa siyo zuri
kutokana na miezi9 kutimia
ghafra uchungu uka mshika
saa6 usiku ya juma tatu alikimbizwa hospital kufika tu nakulazwa kitandani alipiga kelele sana kuomba msaada kwakuwa uchungua aliusikia
manesi na madaktar walimchukuwa nakumpeleka
katika chumba cha kujifungulia
walimsaidia na kufanikiwa kuzaa
mtoto wa kike.
"hongera sana umejifungua
mtoto wa kike yupo salama"
"ooh asante Mungu"
"sasa wewe pumzika kwanza
sawa mama"
"sawa"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"jamani mzazi wenu
amejifunguwa salama mtoto wakike"
Sulee alifulahi sana kusikia hivyo
"Monica hongera sana mwenzangu fungu lako limekuja
kama wewe"
"sulee asante mwaya"
"sulee hongera sana"
"asante shangazi"
"mh hata mimi sijuwi
angekuwa wakike"
Swali hilo lilimfanya MONICA atoe
machozi
"Monica mbona una lia
acha uchuro badala ufurahi una lia"
"Monica nakumbuka mengi sana
siyo kwaajiri ya mtoto Mume wangu Sulee"
sule aliwaza sana nae alianza
kudondosha machozi kwa sababu
tatu moja ana, hiv mbili kaachika, tatu mimba imetoka:
"jamani mna lia na mimi nifanyeje eeh"
Aliuliza shangazi
bila kupewa jibu Monica na sulee walikumbatiana huku wakilia.
**
Maisha ya mume wa sule yalizidi kuwa magumu kifedha alitamani
kwenda kwa shangazi yake Sulee lakini aliona aibu kwenda kuomba
alivumilia lakini ilizidi sana
kuwa mbaya maana alizoeya
kupewa na shangazi
Nae mume wa monica
ali Rudi kijijini kutokana na maisha kuwa magumu aliingia katika madeni makubwa benk wakataifisha nyumba na gari
lake
**
Sulee kwa nini usiende kupima
tena ujuwe afya yako"
"mimi nasubiri kufa tu"
"hapana sulee nenda wewe
mimi hainiingii akirini eti mimi sina ukimwi na wewe unao
wakati mwanaume mmoja
tumetembea nae"
"inatokea hivyo monica"
"jaribu wewe nakushauri tu
uwenda Mumeo alifanya njama
tu kwa dokta ili akuambie una virusi ili akuache maana aibu tume wapa"
"mh ina wezekana eti lakini haku paswa kufanya hivyo.
"sulee haina haja ya
kufikiria kwa sasa maji yamesha
mwagika kuyazoa haiwezekani kabisa sawa"
"sawa ngoja kesho niende kupima tema hospital kama 4 kwauwakika zaidi uwongo Monica"
"fanya hivyo mpenzi wangu maana unaweza kuishi kwa mawazo wenda huna tatizo hilo
wangu"
"asante Monica"
"ila usimwambie shangazi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kama unaenda kupima sawa"
"kwa nini Monica"
"hupaswi kuuliza kwa nini
fanya hivyo"
_______________________________________
Dokta kisalawe alimsimulia Adams
Historia yake ya maisha aliyokuwa akiishi Dar najinsi alivyo kuwa akiwa fanyia wanawake za watu:
"Nihivyo Adams nilikuwa nikifanya dhambi kabisa
na sasa nimeamua kuokoka
sitaki dhambi tena"
"Uwamuzi wako mzuri sana
nakupa hongera sana mke wa mtu ni sumu kali sana usipende kupenda au kufanya mapenzi/sex nao utakufa mapema sana, ona mimi sina mke lakini sijihusishi na Mapenzi mpenzi wangu mimi ni kazi/pesa KISARAWE"
"Kweli nakuamini ndugu yangu"
"basi akiri yako wekeza kwenye
kazi jifunze nacho fanya sawa
usiwe na tamaa katika Mari yangu
ukiiba tu nikigundua nakupoteza asee sikutishi nakupa ukweli
angalia ulio wakuta wako vipi"
"sawa Adams nakuahidi sita fanya hivyo"
"asante kama itakuwa kweli"
_______________________________________
Kisarawe alizidi kuomba Mungu
na kutubu Dhambi zake zote yeye alikuwa mtu wakufunga na kusari
Mpaka Adams alishangaa sana
kubadilika sana alikuwa mkimya
sana hakupenda kabisa ku share na wanawake" Kisarawe vipi
mbona uko hivyo siku hizi"
"kivipi Boss"
"Hapana niite Adams inatosha
kaka"
"ok Adams"
"naona unabadirika sana
mkimya hupendi kukaa na akina dada"
"Adams nimeamua kubadilika
kidogo sipendi kukaa nao nataka
nisahau kabisa matukio yangu ya zamani nikikaa nao nitakumbuka
yaliyo pita na kuanza upya"
"Hivi ulishakuwa na mke"
"kwa nini una uliza hivyo"
"namaana yangu"
"Hapana sikuwa na mke"
"ndomaana ulikuwa ukitembea
na wake za watu"
"kwa nini"
"Ulikuwa huoni uchungu
wa mke ungekuwa na mke
usinge fanya hivyo, tuachane
na hayo kesho Naenda Dar
kuna kampuni moja nimeongea nao kuhusu gari wana hitaji"
"sawa Adams kwahiyo
kuhusu mpango wa sua kuhusu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
trekta zile kumi inakuwaje
wamefika milioni95 kila moja"
"ooh nilisaha wambie waongeze 20"
"sawa"
________________________________________
ADAMS akiwa maeneo ya mbezi
alihisi tumbo likimuuma
ndani ya gari yake alikuwa
na Dereva aliye mkodisha
kuendesha gari yake kutokana
na kuto zijua vizuri njia na msongamano wa magari
kama unavyo lijuwa jiji la dar
alikuwa akilala mika sana
dereva alishauri waende
hospital ya Amana
kupima/kupewa matibabu
dk10 walifika na kuchukuliwa
vipimo wakati wakiwa
katika chumba cha kupumzikia wagonjwa walikuwa wengi
wakisubiri majibu yao ya
vipimo walikuwa wakiangalia video iliyo kuwa ipo juu ya ukuta
wote wagonjwa walikuwa wakitazama juu katika video hiyo
lakini kwa Adams ilikuwa tofauti kidogo.
Macho yake yalikuwa kwa Binti
mrembo sana aliye kuwa kakaa upande wa kushoto kwake.
"kaka vipi mbona hivyo"
ilikuwa sauti ya dereva wake
iliyo muuliza:
"ona yule dada alivyo"
"aah kaka mbona kama hao wengi tu wapo hapa Dar tena wazuri kushinda huyo mgonjwa
pesa yako tu kama upo tayali niambie nikupeleke viwanja"
walikuwa wakinong'onezana
masikioni ili watu wengine wasisikie.
"hapana asee Roho yangu
imetua pale asee"
"sasa kaongee nae basi"
"poa subiri hapa hapa"
"Adams alivaa kiheshima sana
ilikuwa suti kwakuwa kulikuwa na joto sana alivua koti na kubakia na shati nyeupe na tai shingoni alipendeza sana.
"samahani kaka"
"bila samahani"
"Naomba nikae hapo ulipo
kaa nataka kuongea na huyu dada"
"ooh sawa kaa"
_______________________________________
Dada habari za kwako
nadhani una umwa maana naona
una mawazo sana muda wote naona umeinama chini"
"Matatizo kaka angu "
"pole sana, samahani kuna kitu nataka kuku uliza kidogo
naomba tukae pembeni kidogo"
"sawa labda wapi"
"kwenye kiti kile ile kama daktar ataita majina iwe lahisi kusikia"
"ok"
"Naitwa Adams j maryo jr.
Naishi Morogoro ni mfanya biashara"
"oh asante kuku fahamu"
"ok, nilikuona Muda wote upo
na hudhuni sana vp nini tatizo"
"Ni Afya yangu tu kaka:..
"Namba 11 ingia"
Ilikuwa sauti ya daktar
iliyo sikika hakuwa mwingine ni yule dada aliye kuwa akiongea na Adams aliinuka na kwenda.
"kaka ngoja niingie nisubiri"
"aliingia ndani kwa doktar..
Habari yako Dada"
"nzuri Doktar,Nipe majibu yangu
ilinijuwe kitakacho endelea katika Maisha yangu"
"Mbona una Haraka sana"
"Doktar ni umuhimu wangu
kujuwa"
"ok unaitwa Sulee siyo"
"ndiyo"
"ok Sasa mbona umekuja peke yako kupima"
"sina Mume wala mpenzi nipo mimi mwenyewe"
"Mh kwanini je mmeachana"
"ndiyo"
"kipindi gani tokea muachane"
"kama miezi 9 na siku kazaa"
"pole sana pole sana"
"doktar nina nini"
"hayo ni maisha yakawaida sana
leo wewe kesho mimi hupaswi kujutia Mungu ana kila sababu kwenye jambo lolote sawa sulee ona wewe ni mzuri sana lakini
leo hii una dosari katika maisha yako usikate tamaa kabisa Dada angu Mungu atakupa nguvu Na..
_______________________________________
Monica Alikuwa ana furaha
kubwa sana Moyoni kwakupata Mtoto japokuwa alikuwa akimkumbuka sana Mume wake
aliumia sana kwa kufikiria sana Jinsi Mumewe alivyo kuwa ana mjari na kumpenda
alijikuta akimuangalia Mtoto wake
huku machozi yakimtoka sana
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alianza kumchukia Mtoto wake aliye fanana sana na Kisarawe
alitamani kumtupa au amtelekeze
yule mtoto kwa shangazi
lakini aliona Mtoto hana Hatia
kabisa alizidi kumtunza na kujitahidi kumpenda sana.
___________________________________
Mume wa Monica Aliamuwa kuwa mkulima katika kijiji cha mlali kilichopo mkoa wa Morogoro
alilima mazao lakini yalimgomea
kabisa alikuwa akivuna kidogo sana"Hii itakuwa Radhi ya mke wangu tu kuachana tu maisha yamekuwa magumu sana kila ninacho kifanya kwangu siyo
imekuwaje sijuwi niende kwa Mganga, lakini hapana hapana
siwezi kufanya hivyo kwakuwa huku kijijini hawajuwi kama tumeachana na mke wangu ngoja ni rudi dar nika mtafute mke wangu tujetuishi wote lakini anaweza kukubali kuja kuishi huku sijuwi"
Hayo yalikuwa Mawazo ya
Mume wake na Monica
aliyo kuwa aki waza
___________________________________
Nakushauri Usichoke kutafuta
sawa sulee"
"Doktar doktar sikuelewi"
Sulee aliulza kwa ukali kidogo
huku machozi yakilenga lenga
huku akitetemeka kwa uwoga na presha kupanda"
"hapana sule kuachika siyo mwisho wa kuto pendwa au kupenda utapata Mume bora
na aliye sahihi kwaku kazana kuomba Mungu atakuonyesha"
"doktar nime asirika tawezaje kukaa na Mtu asiye na virusi"
"nani kakwambia kuwa ume Asirika eeh"
"soma hivi hapa vyeti"
"mh Hapana sule vipimo vyetu havisemi hivyo upo salama kabisa
sulee"
"hapana doktar hostpital iyo siunaijuwa nikubwa sana
itadanganyaje hivyo"
"huwezi kujuwa wenda kuna sababu kama ulivyo niambia kuwa umeachika miezi9 naa, wenda ninjama ya mumeo"
"sasa unanishauri vp doktar"
"kapime hospital mbili tena
utapataje majibu"
"asante doktar"
"haya karibu tena"
Sulee alitoka nje hakuwa na kumbukumbukama kuna kijana
nje aliye kuwa na maongezi naye
alitoka huku akielekea mlango wakutokea nje kabisa
"sulee mbona hivyo
jamani"
"nisamehe sana Adams"
"ehee ina kuwaje maongezi yetu"
"ooh tuakae pale"
Kabla ya kukaa
doktar akasikika akisema namba 25 ingia" ilikuwa ninamba ya Adams j maryo jr.
"sulee ni namba yangu hiyo
je uta nisubiri niingie"
"sawa usichelewe sana"
"sawa"
"Pita tu"
"Habari yako doktar"
"salama tu ,wewe ni Adams"
"ndiyo"
"tatizo lako ni mchafuko wa Tumbo tu utaenda Dukani
uta chukuwa dawa hizi nilizo andika sawa"
"sawa kwaheri"
"pita huku "
ADAMS ALIPITA NJIA NYINGINE
NASIYO ILE ALIPO TOKEA SULEE
ADAMS ALICHUKUWA DAWA DUKANI NAKURUDI PALE ALIPO MUACHA DEREVA NA SULEE.
"vipi dereva yuko wapi yule dada
yuko wapi"
"kaondoka mda kidogo kaka"
"khaa sasa sijuwi tampataje
asee"
"kaacha namba yake ya simu
hii hapa"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"afadhari sana ,bac twende zetu
asee"
________________________________________Sule hakutaka kurudi nyumbani
alienda hospital 3 tofauti kupima
tena mpaka saa3 usiku alikuwa akisubiria Majibu hospital zote3
Na majibu yote yalikuwa ni mamoja hana Virusi alikuwa na amani moyoni japokuwa aliambiwa arudi tena kupima baada ya miezi mi2/3
kiuwakika zaidi alirudi nyumbani
huku ana furaha sana.
"vp sulee mbona hivyo
una furaha"
"yani Mungu ashukuriwe
sina Virusi Monica"
"sasa iwe siri usimwambie shangazi sawa"
"mh kwa nini tena"
"utajuwa ukweli badae"
Monica alimwambia sulee vile
ili uadui usitokee kati yao na Shangazi yao
_______________________________________
miezi mi2 sulee alienda tena kupima alipata majibu tena kuwa hana virusi aliwaza sana ninani aliye fanya kitendo hicho cha kuambiwa ana h,i,v aliamuwa kwenda katika hospil ile aliyo ambiwa kuwa ana Virusi ilikumbana doktar yule
ajuwe ukweli.
Alipo fika alimkuta daktar wakike
"zakazi daktar"
"nzuri tu"
"nina shida"
"kiafya au kiofice
"kiofice"
"karibu"
"kuna siku nilikuja hapa kupima...
Kupima H.I.V. Na vyeti vya vipimo vyangu ni hivi hapa unaweza ukasoma.
"Yes inaonyesha umeasirika
Dada angu"
"ooh vizuri je nitarehe ngapi
hapo ina sema"
"eeeeeh eeeeeh ni 21/5/2014, mbona unaniuliza maswali sana"
"asante sana,uta juwa tyuu
usiwe na haraka, Je unaweza
kunisomea katika fairi la ofice hii alikuwepo nani tarehe iyo"
"aah kuna kazi nyingi zakufanya
sahizi niache nihudumie wagonjwa wengine"
Sulee aliingiza mkono
katika pochi yake nakutoka na
wekundu/pesa kazaa nakumpa yule dada/doktar akapokea
nakuweka katika Matiti yake.
"sasa naomba nisaidiye
kumjuwa ninani alikuwepo"
"ok subiri"
Baada ya dk5
Alisha pata jibu alikuwa ninani
"nimeona alikuwa ni
doktar john nimnene mweusi
ana nywele nyingi hivi"
"huyo huyo"
"sasa kafanyaje"
"habari ndefu sana wangu
angalia hivi vyeti nausome"
Doktar huyo alisoma
vyote vi nne alitoa pumzi
uphuuuu kisha akamtazama
kwa huzuni sana sulee kisha akainuka
nakumshika bega.
"sulee pole sana hiyo nikawaida yake huyo doktar hafai hata kwa dawa nakushauri fanya unavyo taka kufanya"
"ok nataka kujuwa ukweli tu
aliyemtuma afanye hivyo ninani"
"sawa"
Sulee alianza kufanya mipango:
alianzia Mahakamani
moja kwa moja kwakumshtaki
doktar john kwakumpa vipimo vyauwongo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kesi ilisumwa kort chemba
sulee hakutaka yawe makubwa
kwa doktar yeye alitaka ajuwe tu ninani alifanya vile tu.
Monica alikuwa akihisi kuwa ni Mume wangu ili tuachane, Lakini mbona alisema nisimwambie Shangazi kuhusu ilo suara.
Sulee alijiuliza moyoni
Doktar alibanwa sana mwisho akakubali kuwa alipewa pesa
na shangazi yake sulee adanganye majibu kuwa sulee ana ukimwi
ili aachane na Mumewe,(japo kuwa shangazi na sulee alikubaliana na Mume wa sule kuwa kama watakuwa wazima wote Mume wa sulee ange msamehe sulee)
"ok vizuri sana"
Kutokana na sifa za doktar huyo
kuwa mbaya anahusika na utoaji mimba NK. Mahakama iliamuwa kumfungia kazi kwa muda usiyo julikana.
Sulee ali Rudi nyumbani
huku akiwa na hasira sana
alikuwa ana hamu sana amkute shangazi yake
Lakini hakumkuta.
"kweli Monica doktar kakubali
kumbe shangazi ndiye kafanya tukio langu hilo eti kisa tuachane
na mume wangu, tulikubaliana
kama tutakuwa hatuna Virusi tungeendelea kukaa wote licha
yakuwa na mimba siyo yake"
"Sasa utafanyaje sulee"
"nataka kumchana live"
"Hapana Sulee kumbuka
hatuna pakwenda"
"potelea mbali liwalo na liwe
nimesha pagawa kasababisha kutoka kwa mimba yangu inauma sana nilikuwa nikikaa kwa Huzuni kama naumwa nilikonda kama
kweli na ngoma Monica siwezi kumsamehe Mimi"
"Sulee huoni kama ndiyo utakuwa
mwisho wetu wakukaa hapa"
"mmh popote mimi takwenda kukaa mimi"
"na mimi je"
"najuwa atanifukuza mimi
tu siyo wewe"
"hapana sulee atajuwa nime kwambia mimi hiyo siri"
"siri siri siri gani tena hiyo
Monica"
"kuwa wewe hauna ukimwi"
"mh mbona unanichanganya inamaana hata wewe ulikuwa ukijuwa kuwa mimi sina ukimwi
Monica mbona haukuniambia
mimi kwa nini kwa nini Monica
hukuniambia mapema
mpaka mimba yangu imetoka
Monicaaaaaa....
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment