Search This Blog

Monday, October 24, 2022

MWAJUMA UTAMU - 4

 







    Chombezo : Mwajuma Utamu

    Sehemu Ya Nne (4)



    Usiku wa siku hiyo nilihakikisha nimempagawisha Samir vya kutosha, ingawa kuna imani ipo kuwa wanaume ndiyo waliyozoeleka kuwa hatari zaidi wakati wa kufanya mapenzi na kuwaridhisha wanawake lakini kwangu ilikuwa ni kinyume chake, nilijua kufanya mapenzi na kumtoa jasho mwanaume, kukurukakara na purukushani zote za kitandani nilizijua.

    Siku iliyofuata Samir alinilipa pesa kama tulivyokuwa tumekubaliana na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa biashara yetu.

    Japokuwa niliendelea kupata pesa lakini akili yangu ilikuwa ikifikiria kununua kiwanja kisha kuanza ujenzi wa nyumba yangu, nilikuwa nikifikiria pia kufungua biashara zangu mwenyewe.

    "Fungua akaunti Facebook kisha Create page uanze kujitangaza, utapiga hela ndefu," alinishauri Savela nilipomuelezea mipango yangu.

    "Hiyo imekaa vipi?" nilimuuliza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ukifungua utakuwa ukipost picha na video za ngono halafu utakuwa ukitangaza biashara, lazima utapata wateja ila katika hizo picha utakazokuwa ukipost jaribu kuzikata kichwa usionekane," alinijibu kwa ufafanuzi kisha akaendelea kuzungumza.

    "Biashara sasa hivi imebadilika, kuna wateja wengi sana mitandaoni, wapo baadhi ya wanaume wanaogopa kwenda Sinza kutafuta Malaya, wengine wanaogopa kuonekana, kwa kutumia njia hii ya mtandao ni lazima utawapata wateja wote hao tena wengine wapo nje ya nchi kama vile Kenya, Uganda na nchi nyingine," aliniambia.

    "Na hao wateja wa nje ya nchi nitawafikiaje?"

    "Wengine pesa ipo, wanakufuata au wanakutumia kila kitu, kazi yako ni kwenda kuwapa mapenzi tu."

    Nilipoambiwa hayo nilishangaa, sikutaka kuamini kama mtandao wa Facebook ungeweza kunitengenezea kiasi kikubwa cha pesa kiasi hicho. Savela hakuishia hapo tu, aliendelea kuniambia jinsi biashara ya uchangudoa ilivyokuwa ikifanyika katika mitandao ya kijamii.

    "Mmh ya kweli hayo?"

    "Wewe endelea kuzubaa, wenzako tunazidi kupiga pesa hapa mjini, hatutumii nguvu nyingi halafu leo jioni kuna buzi mmoja naenda kukutana naye."

    "Yupi huyo?"

    "Ni wa Facebook, anaonekana ni mtu mwenye hela zake, leo lazima nikatanue nae," alinijibu Savela.

    Nilihisi kuchanganyikiwa mno, nilipoambiwa biashara hiyo ilivyokuwa ikifanyika mitandaoni, nilitamani kuifanya.

    Kwa kuwa nilimiliki simu ya kupangusa wala haikuwa kazi sana, nilichokifanya niliingia katika mtandao huo, nikajisajili, nikawa nina akaunti yangu, moyoni nilikuwa nina hamu kubwa sana ya kupata pesa na njia hiyo ndiyo niliiona kuwa rahisi ukitofautisha na ile ya kwenda kujiuza Sinza kwani kuna kipindi biashara ilikuwa ngumu kufanyika, muda mwingine wateja hawakupatikana kwa wakati.

    Hakuna binadamu asiyeipenda pesa katika duniani hii, pesa ndiyo kila kitu, japo kuna baadhi ya watu hawaamini hilo, lakini huo ndiyo ukweli.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikia, mtu ukitaka kuvaa upendeze ni lazima pesa itatumika kununua nguo, ukitaka kula, kuishi maisha mazuri, pesa bado itahitajika na hii ndiyo sababu tunasema pesa ndiyo kila kitu.

    Niliipenda pesa kuliko kitu chochote kile katika hii dunia, nilizaliwa katika familia yenye dhiki kubwa, wazazi wangu hawakuwa na pesa, niliishi maisha magumu mno nilipokuwa Mtwara, mpaka kufikia kipindi ambacho Bi Magreth mke wa Mzee Gidion anakuja kunichukua na kinileta mjini kwa lengo la kufanya kazi za ndani kiukweli sikutaka kuamini.

    Kwa kuwa nilizaliwa katika familia iliyojaa dhiki hivyo nilitamani kuishi maisha mazuri. Kipindi ambacho Mzee Gidion alianza kunitongoza ilikuwa ni rahisi mimi kumkubalia kwasababu alitanguliza pesa, aliniahidi mambo mengi mazuri ambayo angeweza kunifanyia.

    Naweza kusema tamaa ya pesa ndiyo iliyonifanya nikajikuta nikitembea na Daniel pamoja na Oscar.

    Nilikuwa tayari nimeshafungua akaunti Facebook, nilikumbuka kufungua na ukurasa ambao niliutumia kupost picha zangu za utupu. Jina ambalo nilikuwa nikilitumia lilikuwa ni hili la Mwajuma Utamu.

    Kazi niliyokuwa nimeibakiza mbele yangu ilikuwa ni mimi kujipiga picha za utupu kisha nikawa nazipost katika mtandao huo.

    Mwanzoni wakati naanza kupost hakukuwa kuna like nyingi nilizozipata wala comment lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga ongezeko la watu waliyokuwa wafuatilaji wa ukurasa wangu huo waliongezekana tena kwa kiasi kikubwa sana.

    Safari hii kila picha niliyokuwa nikiipost ilipata like nyingi na comment za kumwaga na hivyo wateja kuanza kujitokeza kwa wingi. Kwa kuwa niliweka namba yangu ya simu katika kila post, wateja hawakupata shida ya kunitafuta, walinipigia simu, tukaongea biashara na baada ya makubaliano biashara ya mapenzi ikafanyika.

    Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu, nililala na wanaume wengi sana, ndani ya mwaka mzima nilikuwa nikiifanya biashara hiyo mpaka kufika mwaka 2013 nilikuwa tayari nimetengeneza kiasi kikubwa sana cha pesa.

    Huwa sipendi kusimulia kila kitu nilichokuwa nikifanya wakati wa kufanya mapenzi kwasababu naamini maandishi haya yanasomwa na watu wa rika zote, ninachotaka kuwaandikia hapa ni mafunzo kwani biashara hii sio nzuri na sikushauri uifanye, nataka niwe mfano bora wa kukupa funzo fulani utakalojifunza baada ya kuisoma simulizi hii ya maisha yangu.

    Kuna wasichana wengi sana hapa mjini ni matajiri, ni maarufu, wanapohojiwa na waandishi wa habari kusema siri ya mafanikio yao huwa wanadanganya, wanaficha kwa kusema kuwa wanafanya biashara inayowaingizia kiasi kikubwa cha pesa.

    Sisemi haya kwa kuwakosoa wale wasichana wachapa kazi, wapo baadhi yao kweli wanafanya biashara, wameajiriwa katika makampuni makubwa na wanalipwa pesa ndefu tu.

    Nilisafari mikoa mbalimbali ya nchi hii kama vile Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya, Iringa na maeneo mbalimbali ya jiji la Daresalaam, nilikuwa nikiwafuata wanaume ambao nilienda kufanya nao mapenzi na ni kwasababu walikuwa na dau kubwa la pesa.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ziliendelea kukatika, siku moja nilikutana na mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Martin Sepeku, huyu alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa sana hapa mjini.

    Nilifanikiwa kulala naye, kwa kuwa nilifahamu alikuwa na pesa hivyo nilipanga kumpa mapenzi ambayo asingeweza kunisahau katika maisha yake, hilo nilifanikiwa tena kwa asilimia zote mia moja.

    Taratibu akaanza kukolea, penzi langu likamlemvya. Katika kipindi hicho alikuwa bado hajaoa, alipofanikiwa kuuonja utamu wangu hakutaka kuukatisha, akaniambia kuwa alinipenda hivyo tukaingia katika mahusiano kwa miadi ya kunioa hapo baadae. Hilo halikuwa tatizo, nilimkubalia lakini moyoni mwangu sikumpenda isipokuwa nilizipenda pesa zake na huo ndiyo ulikuwa ukweli.

    Sepeku akaanza kunionyesha mapenzi ya dhati, nilikuwa nina ndoto ya kumiliki nyumba, gari na vitu vingine vya thamani, vyote hivyo Sepeku aliahidi kunitimizia.

    Baada ya kupita mwezi mmoja Sepeku alininunulia nyumba maeneo ya Msasani, ilikuwa ni nyumba ya kifahari na kama haitoshi pia akaninunulia gari pamoja na kunifungulia biashara mbalimbali.

    Nilifurahi sana, ndoto yangu ilikuwa tayari imetimia lakini kama wasemavyo wahenga kuwa tabia siku zote hujenga mazoea, ndivyo ilivyokuwa kwangu, sikuacha biashara ya uchangudoa, niliendelea kuifanya lakini niliifanya kwa siri, Sepeku hakujua kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu.

    Siku ziliendelea kukatika, baada ya miezi miwili kupita palianza kuzuka tetesi za jini mweusi ambaye alikuwa akiwachukua machangudoa na kwenda kuwaua.

    Mauaji yalitokea na waliyokuwa wakiuwawa kikatili walikuwa ni machangudoa tu. Ni katika mauaji hayo Savela na yeye aliweza kuuliwa kikatili kisha mwili wake kutupwa katika ufukwe wa coco.

    Kifo chake kiliniumiza mno, sio mimi tu niliyeumia zaidi bali hata machangudoa wengine waliumia pia.

    Hali hiyo ilituogopesha sana, hatukujua muuaji huyo alikuwa ni nani na kwanini aliamua kufanya mauaji hayo. Kila changudoa alisema lake, tetesi ilizozagaa ni kuhusu Jini mweusi, yaani muuaji huyo aliitwa jini mweusi kwasababu waliyomuona walisema alikuwa akitembelea gari lenye rangi nyeusi.

    Tetesi za jini mweusi zilitufanya tukaanza kuishi maisha ya hofu, kila changudoa akaanza kuwa makini na usalama wa maisha yake, gari lolote lenye rangi nyeusi lililoonekana likiingia na kupaki eneo hilo la Afrika sana tulipoliona tulikimbia, tuliamini ndiyo jini huyo mweusi aliyekuwa akiwaua machangudoa.

    Hali ya sintofahamu ilitukumba, jeshi la polisi liliingilia kati, msako dhidi ya muuaji huyo ukaanza kufanyika lakini haikuishia hapo tu, pia walianza kuwakamata machangudoa na kuwafikisha mbele ya sheria.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vyombo vya habari navyo havikuwa mbali, viliendelea kuripoti taarifa za muuaji huyo ambaye alisumbua sana na mpaka kufikia wakati huo hakukuwa na dalili zozote za kupatikana kwake.

    Kipindi hicho ukurasa wangu ya Mwajuma Utamu ulikuwa umefikisha wafuatiliaji 500,000. Ulikuwa ni ukurasa ambao baadae niliutumia kwa kuwauza machangudoa wengine.

    Suzie huyu alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu lakini pia alikuwa ni changudoa, alikuwa akiishi hostel. Nilifahamiana naye kipindi ambapo tetesi za jini mweusi zilivuma.

    Suzie alipofahamu nimepata mwanaume tajiri ambaye alininunulia gari pamoja na nyumba ya kifahari maeneo ya Msasani, hakutaka kuamini, alionekana kunishangaa kupita kawaida.

    Kwa jinsi alivyokuwa akiniangalia usoni, macho yake yalionyesha kuniuliza kwanini niliendelea kufanya biashara ya uchangudoa wakati nilipata mwanaume ambaye alikuwa na pesa na tayari alinifanyia mambo makubwa katika maisha yangu. Kama tatizo ni biashara alinifungulia tena zaidi ya moja.

    “Kwanini usitulie tu na Martin, anaonekana kweli nakupenda?” aliniuliza Suzie.

    “Hapana siwezi,” nilimjibu

    “Kwanini au hujampenda?”

    “Sijazoea kuwa na mwanaume mmoja katika maisha yangu, nisipofanya mapenzi na wanaume zaidi ya wawili najiona kama sijakamilika.”

    “Jitahidi kwa Martin, anaonekana kuwa mtu mwema kwako.”

    “Nitatulia lakini sio sasa, acha niendelee na uchangudoa wangu mpaka pale nitakaposema basi.”

    “Sawa ila kuwa makini maana siku akigundua kuwa wewe ni changudoa nadhani huo ndiyo unaweza kuwa mwisho wa mahusiano yenu.”

    “Hilo haliwezi kutokea na hata kama likitokea siogopi kitu kwanza nishamchuna sana,” nilimwambia.

    Urafiki wangu na Suzie uliendelea kila siku, nilimshauri ajipige picha za utupu kisha nikamuweka katika ukurasa wangu, huko nilimtafutia wateja, nikamuunganisha nao, safari ya kupiga pesa mitandaoni ikaendelea.

    Nilifanya mambo yote hayo lakini Martin Sepeku hakufahamu kilichokuwa kikiendelea, alikuwa ni mtu wa kusafiri mara kwa mara. Safari zake nyingi zilikuwa ni za nje ya nchi hivyo ilikuwa ni vigumu kugundua lolote.

    “Nataka kukuoa Mwajuma uwe mke wangu kabisa,” aliniambia Martin siku moja kabla ya safari yake ya kwenda Dubai.

    “Unafikiri itawezekana?” nilimuuliza.

    “Kwanini isiwezekane kwani ugumu uko wapi?”

    “Dini.”

    “Dini sio tatizo mpenzi wangu ninachokitaka ni kufunga ndoa na wewe, nakupenda sana Mwajuma.”

    “Nakupenda pia Martin lakini….”

    “Nipo tayari kubadilisha dini kwasababu yako, nikirudi kutoka Dubai nataka nihalalishe mahusiano yetu au hupendi kuona siku nakuwa baba wa watoto wako na wewe unakuwa mama wa wanangu?”

    “Napenda.”

    “Basi nikubalie hili litimie kwanza.”

    “Sawa litatimia,” nilimjibu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kichwa kilianza kuniuma baada ya kumsikia Martin alihitaji kufunga ndoa na mimi kipindi atakaporudi kutoka safari yake ya Dubai. Kiukweli sikuwa nimejipanga katika hilo wala moyoni mwangu sikuwa nina mapenzi ya dhati na Martin.

    Nilichokuwa nimekifuata kwake ni pesa pamoja na mali alizonimilikisha. Suala la kufunga ndoa nililiona kuwa gumu hasa kwa mtu kama Martin ambaye sikumpenda kutoka moyoni mwangu.

    Nilipomueleza Suzie habari hizo alionekana kufurahi, aliniambia nisikubali nafasi hiyo ipotee, alienda mbali zaidi na kuniambia kama angekuwa ni yeye angekubali tena bila kipingamizi chochote.

    “Ungekubali?” nilimuuliza.

    “Ndiyo mimi ningekubali shoga yangu, embu angalia jinsi maisha yalivyokuwa magumu, angalia tunavyoteseka katika biashara hii, wakati mwingine tunakutana na wanaume wenye maumbile makubwa, kwasababu tunahitaji pesa tunakubali kufanya nao mapenzi, tunapata maumivu makali sana, hivi hii biashara tutaifanya mpaka lini?” aliniuliza Suzie kwa uchungu kisha akaendelea.

    “Kama huyo mwanaume anakupenda na ana malengo na wewe naomba utulie naye, hii biashara ni bora ukaachana nayo tu,”aliniambia.

    Maneno ya Suzie yalianza kuniingia, niliyatafakari na kuona kuwa yalikuwa na ukweli mtupu lakini tatizo lilikuja sehemu moja, sikumpenda Martin kutoka moyoni mwangu, kwake nilifuata pesa na maslahi mengine ambayo nilikuwa tayari nimeshayapata.

    Nilipoona Suzie ananig’ang’aniza nikubali kuolewa na Martin ilibidi nilimueleze ukweli kuwa sikumpenda kama alivyokuwa akiamini, nilimpendea pesa zake na hiyo ndiyo ilikuwa tamaa yangu.





    Suzie aliendelea kunishauri nikubali kuolewa na Martin kwasababu alikuwa na pesa na pia alionekana kuwa na malengo na mimi, hakutaka kuona nikiipoteza bahati hiyo. Kwake ulionekana kuwa kama wimbo wa taifa.

    “Hata kama humpendi lakini angalia jinsi alivyojitoa kwako hivi ni mwanaume gani ambaye anaweza akakubali kufanya mambo yote hayo hata kama anakupenda?”

    “Usiuzungumzie moyo wangu Suzie, nimeshakwambia kuwa simpendi Martin mbona hunielewi na sioni sababu ya kuolewa naye.”

    “Mwajuma unajua unaichezea bahati, wasichana wengi wanaitafuta bahati hiyo wanaikosa halafu wewe unaipata lakini unaichezea.”

    “Suzie hivi hakuna stori zingine za kuzungumza?”

    “Utakuja kuijutia bahati hii unayoichezea.”

    “Sidhani kama kuna siku nitakuja kuijutia, kwanza hilo haliwezi kutokea halafu nimekumbuka baadae ninatakiwa nikameet na Damian.”

    “Who is Damian?” (Damian ndiyo nani?)

    “Mpenzi wangu, mume wangu mtarajiwa,” nilimjibu.

    Suzie alibaki akinishangaa baada ya kumwambia nilikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine aliyejulikana kwa jina la Damian.

    Hii ilionyesha picha ya umalaya, yaani sikutulia na mwanaume mmoja, maisha yangu yalikuwa ni ya kudangadanga leo nilikuwa kwa mwanaume huyu kesho nilikuwa kwa mwanaume mwingine.

    Huyu Damian nilikutana naye kwenye klabu moja iliyojulikana kwa jina la La Charz ambayo ipo Sinza Mori.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mahusiano yetu yalianza mara baada ya kunichukua usiku mmoja na kwenda kufanya naye mapenzi nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach.

    Alikuwa ni mwanaume mwenye uwezo mkubwa wakati wa kufanya mapenzi, ingawa nilishawahi kujiapiza kuwa sintokuja kujihusisha na mahusiano na mwanaume aliyenichukua kwa lengo la kwenda kufanya mapenzi lakini kwa Damian ilikuwa tofauti na kiapo hicho, nilijikuta nikianzisha mahusiano naye ya kimapenzi bila kutarajia.

    Baada ya kupita kipindi fulani penzi likawa tayari limeota mizizi, nilikuwa sisikii wala sioni kwa Damian, wakati huo nilikuwa tayari nipo katika mahusiano na Martin.

    Hata hivyo sikuacha biashara ya uchangudoa mitandaoni, niliendelea nayo kama kawaida.

    Nilipomwambia Suzie kuwa nilikuwa katika mahusiano na Damian alionekana kunishangaa sana, alihitaji kumfahamu mwanaume huyo zaidi na hata nilipomwambia maisha yake alimuona kuwa wa kawaida sana.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog