Search This Blog

Monday, October 24, 2022

NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI - 3

 







    Chombezo : Nyumba Iliyojaa Dhambi

    Sehemu Ya Tatu (3)



     Nilikuwa bilionea, tena mkubwa, ilikuwa ni vigumu kuamini kama nilikuwa na kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni mia mbili kwenye akaunti yangu. Sikuamini kama ni mimi kweli ndiye nilikuwa na kiasi hicho cha pesa.

    Niliondoka Posta huku nikiwa makini kuliko siku zote katika maisha yangu. Nilihisi kama ningegongwa na gari na hivyo kupoteza kiasi changu chote hicho kilichokuwa benki.

    Nilitembea kwa tahadhari sana na si hivyo tu, yaani siku hiyo hata daladala sikupanda kwa kuhisi kwamba ingeweza kupata ajali, abiria wote wakafa nikiwemo mimi.

    Yaani niliogopa kufanya mambo mengi, nilikuwa natembea tu kurudi mtaani lakini sikutaka kupita barabarani kwani bado mawazo ya ajaliajali yalikuwa yakinijia kichwani mwangu.

    Nilikuwa bilionea lakini nilivyokuwa nikitembea nilionekana kama sina pesa. Kichwani mwangu kulikuwa na picha za wanawake wengi wazuri, niliwakumbuka marafiki zangu walipokuwa wakiniambia kuhusu mademu wakali waliokuwa wakipatikana katika klabu za usiku, achana na hao, niliwakumbuka wale mademu wakali waliokuwa wakionekana kwenye video nyingi za hapa Bongo, yaani kwa akili yangu, nilitaka nilale na wote hao.

    Niliondoka mpaka mtaani, nikatulia kwanza na kuanza kuyafikiria maisha yangu, sikuamini kama kweli nilifanikiwa kuwa na kiasi hicho cha pesa. Nilitaka nikachukue kidogo kwa ajili ya kwenda kutumia.

    Nilikuwa na kadi yangu ya ATM, kutokana na ushindani mkubwa wa kibenki, kipindi hicho ulipokuwa unajisajili tu na kupata akaunti yako ulikuwa ukipewa kadi yako hapohapo na si kama zamani ambapo ulitakiwa kusubiri kwa wiki nzima.

    Nilikwenda mpaka kwenye mashine ya ATM iliyokuwa Sinza. Niliwaona watu wakiwa wamepanga mstari wakiingia kwa zamu kuchukua pesa. Nilitamani nisimame na kuniambia wanipishe kwani mimi nilikuwa na pesa zaidi yao wote, hata ukizichanganya wasingeweza kunifikia.

    “Jamani! Mpaka pesa ziishe humo!” nilisema kwa hasira mpaka jamaa aliyekuwa mbele yangu kuanza kucheka.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zamu yangu ilipofika, nikaingia kwenye kibanda kile. Tangu nizaliwe sikuwahi kuingia sehemu kama hiyo lakini sikutaka kupata maelekezo kwa mtu yeyote yule kwa kuwa sikutaka watu wajue kama nilikuwa na kiasi hicho cha pesa.

    Nilifuata maelekezo na hatimaye kuchagua lugha ya Kiswahili na kutoa kiasi cha shilingi milioni mbili na kuondoka zangu. Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kununua simu ya kupangusa kisha kuanza kuulizia kuhusu nyumba.

    Kwanza sikutaka kufikiria kuhusu biashara, makazi yalikuwa bora kabisa. Niliulizia madalali, hatimaye nikakutana na mmoja na kumwambia hitaji langu la nyumba.

    “Unataka nyumba ya kiasi gani?” aliniuliza.

    “Yoyote nzuri! Kwanza zinapatikana?” nilimuuliza.

    Dalali yule hakuniamini, kwa jinsi nilivyoonekana na kumwambia kwamba nilitaka kununua nyumba vilikuwa vitu viwili tofauti. Nilichoka, sikuwa na nguo mpya, yaani kwa akili yangu ilivyokuwa, nilianza kununua simu kabla ya nguo.

    “Twende huku tajiri,” aliniambia japokuwa bado hakuonekana kuniamini.

    Tulikwenda mpaka kwenye nyumba moja kubwa. Ilikuwa Kijitonyama, haikuwa nzuri sana lakini kwa kuwa nilikuwa na pesa, nilijua ningeirekebisha na kuifanya nitakavyo.

    Nikapelekwa mpaka ndani na kuonana na mwenye nyumba, dalali akaanza kuongea naye na kumwambia kwamba mimi ndiye nilikuwa mteja pekee niliyepatikana.

    Mwenye nyumba akaniangalia, alionekana kunishangaa, ilikuwaje niwe na pesa za kununua nyumba na wakati muonekano wangu tu nilikuwa kama fukara fulani hivi.

    “Huyu ndiye anataka kununua nyumba?” alimuuliza dalali huku akionyesha mshangao.

    “Ndiyo!”

    “Acha masihara!”

    “Huyu ndiye bosi. Niambie, kiasi gani?” alisema dalali.

    Mzee yule hakutaka kujibu kitu, bado alikuwa akinishangaa, kwake nilionekana kuwa kama kituko fulani hivi. Akatuambia kwamba alikuwa akiiuza kwa shilingi milioni themanini kwa kuwa alitaka kuondoka hapo na kwenda kuishi Mbagala, maisha ya mjini eti yalimchosha.

    “Mbona nyingi sana?” nilimuuliza mzee huyo.

    “Si unaona Juma! Nilikwambia umeniletea mhuni unabisha! Sasa milioni themanini ina wingi gani?” aliuliza baba mwenye nyumba.

    Maneno yake yalinikera sana, nilitamani ninunue nyumba yake na nimnunue mpaka yeye mwenyewe. Ila pamoja na kuumia hivyo, sikutaka kuonyesha hasira zozote zile zaidi ya tabasamu pana.

    “Basi sawa! Nitakulipa hizo milioni themanini,” nilimwambia ili kuepusha maneno.

    Nilichomwambia ni kutaka kuona hati ya nyumba hiyo. Hilo halikuwa tatizo, akamuita mtoto wake wa kike aliyeitwa Zamaradi ili alete hati ya nyumba.

    Kwanza hiyo sauti ya huyo Zamaradi ilivyoitikia, jinsi ilivyosikika masikioni mwangu, nikajua tu kwamba huyo angekuwa bonge moja la demu.

    Baada ya sekunde kadhaa, kweli hati ikaletwa, huyo Zamaradi nilipomuona, alikuwa bonge la demu. Mtu mzima udenda ukanitoka, shetani aliyekuwa ameniacha, akanirudia na kunipa mtego mkubwa.

    “Hapa hatoki mtu,” nilijisemea.

    Nikabaki namwangalia tu Zamaradi mpaka akashtuka kwamba nilikuwa namkodolea macho. Akayageuza macho na kuniangalia, mtoto jicho kama kala kungu, macho yalirembulika mpaka nikachanganyikiwa.

    “Mzee mimi ndiye nataka ninunue hiyo nyumba,” nilimwambia mzee huyo pasipo kutarajia.

    “Haina shida. Usiwe na hofu kijana. Ni milioni themanini tu,” aliniambia.

    “Hakuna shida nitalipia,” nilisema na Zamaradi kuondoka hapo.

    Unajua kwa nini nilisema hivyo? Ni kwa sababu Zamaradi alikuwepo hapo. Yaani kwa jinsi tulivyoonekana, dalali alionekana kama mnunuaji na mimi nilionekana kama dalali.

    Nikaichukua ile hati na kuiangalia, kulikuwa na jina la huyo mzee. Niliporidhika nikampa. Kichwa changu kilikuwa kikifikiria kuhusu Zamaradi tu, alikuwa demu bomba ile kinoma, akili yangu iliniambia kwamba piga ua lazima nikaongee naye lakini si kuvumilia kubaki sebuleni hapo.

    Kwa kuwa huyo mzee hakuwa na nguvu sana, nikamwambia ninahitaji kwenda chooni kujisaidia, niliamini kwamba angemuita Zamaradi kumpeleka mgeni kwenda huko, na mimi ningefanya yangu.

    Kweli bwana! Akamuita msichana huyo na kumwambia anipeleke chooni. Mungu anipe nini tena? Nikasimama na kuanza kwenda huko huku tukiwaacha wao sebuleni pale.

    Nilibaki nyuma ya Zamaradi huku nikimwangalia alivyoumbika. Jamani Mungu fundi, acheni masihara. Mpaka leo ninaamini kuna watu aliwaumba akiwa kwenye mood nzuri sana, na wengine aliwaumba kwa kuwaambia “Na nyie kaijazeni dunia tu manake hakuna namna.”

    Ila kwa mtoto kama Zamaradi, nikahisi kwamba Mungu alisubiri siku ya wikiendi, ambayo hana kazi nyingi, siku aliyokuwa na furaha na kuanza kumtengeneza huyu mtoto. Yaani alikamilika kila idara kiasi cha kuedelea kunitoa udenda.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Zamaradi!” nilimuita, nilishindwa kuvumilia, akageuka na kuniangalia.

    “Abee bosi!” aliitikia, nikaachia tabasamu.

    “Mungu fundi sana, anajua kuumba si mchezo!” nilimwambia.

    “Kwa nini?”

    “Umeumbika mno, u mzuri mpaka unaboa. Hebu naomba namba yako ya simu kwanza,” nilimwambia.

    Mtoto alishasikia mimi ndiye niliiyetaka kununua nyumba yao, nilishatamba pale sebuleni, ataachaje kunimba namba, akanipa na kuniambia nimbipu manake alihisi asije akawa amekosea, nilivyofanya hivyo ikaita.

    “Nakupenda sana,” nilimwambia, sikutaka hata kujivunga.

    “Mh! Jomoniiii! Hebu nenda chooni kwanza.”

    “Sijabanwa na haja nilitaka tu kuongea na wewe,” nilimwambia.

    Mwenyewe akafurahi. Hapo ndipo nilipoamini kwamba mimi ni rijali, yaani sijui ilikuwaje ila nikajikuta nipo karibu naye na kuanza kubadilishana mate.

    Pesa! Pesa! Pesa! Aliyezianzia Mungu anamuona, sijajua alikuwa na lengo gani kwenye dunia hii. Yaani ndiyo kwanza Zamaradi aliniona kwa mara ya kwanza, hakunijua nilikuwa nani lakini alivyonipokea mikononi mwake, kama mpenzi wake ambaye aliishi naye kwa miaka kumi.

    “Nakupenda sana,” nilimwambia kwa sauti ndogo ambayo niliamini kuwa itampagawisha.

    “Nakupenda pia!”

    Baada ya hapo nikajiweka sawa na kurudi sebuleni na kuanza kuendelea kuongea nao. Tulikubaliana malipo kufanyika kesho, tena cash, hivyo tukaondoka.

    Nilienda kuchukua chumba hotelini, nilipoingia tu, kitu cha kwanza kilikuwa ni kumpigia simu Zamaradi, alinipagawisha mno na kuanza kuonja utamu wa pesa.

    “Bebi! Nimekumiss sana,” nilimwambia.

    “Kweli jamaniiii!”

    “Ndiyo! Mwili wako una joto tamu sana, yaani nilivyokukumbatia , nilihisi raha kama nimeona mlango wa pepo. Zamaradi, unaufanya moyo wangu udunde, ndum ndum ndum....” nilimwambia.

    “Jamaniiiiii”

    “Wewe u mzuri mno, una tabasamu zuri, una meno mazuri, macho ya goroli, Zamaradi, umeumbika, unajua kucheka, una sura ya kitoto, umejazia, Zamaradi, hakika hakuna mwanaume anayeweza kukuacha akikupata,’ nilimwambia kwa kumchombeza.

    “Jamaniiiii! Nasikia aibu huko!” aliniambia kwa kasauti kake ka kubembeleza.

    “Zamaradiiiiiiii....nipo radhi nikose kila kitu, yaani pesa, kuingia peponi, nikose furaha lakini nisikukose wewe, ni mwanamke wa kipekee sana, ni mwanamke unayehitaji kuwa na furaha muda wote, unahitaji kutabasamu, kujaliwa, kusikilizwa, ni mwanamke unayetakiwa kuwa kwenye ulimwengu wako wa kipekee, Zamaradi, katika dunia hii hakuna mwanamke mzuri kama wewe,” nilimwambia, nilimsifia sana.

    “Jamaniiiiiiiiiii” aliniambia, nahisi muda huo alikuwa aking’ata kidole chake.

    “Zamaradi mpenzi, naomba ufungua mikono yako, unikumbatie, nikubusu, nikuonyeshee jinsi ulimwengu wa mapenzi ulivyo, nikaribishe mpenzi, nionje radha ya mate yako kwa mara nyingine, Zamaradi, kuwa mama wa watoto wangu,” nilimwambia kwa sauti ile tamu kabisa.

    “Kwani hujaoa bebi?”

    “Ningeoaje na wakati sikuwa nimeonana nawe? Zamaradi! Be mine mamiiiiii, unautetemesha moyo wangu....let me love you senyorita,” niliendelea kumchombeza.

    Siku hiyo ndiyo nikaamini kwamba na mimi mkali kwenye maneno matamu, nilimfanya Zamaradi ajisikie kuwa mwanamke mzuri kuliko Mila Kunis, nilimwaminisha kwamba moyoni mwangu hakukuwa na yeyote yule.

    Siku hiyo nilikesha nikiongea naye tu. Sijui alikuwa na bwana au peke yake, kitu nilichokuwa nikikiangalia ni mimi kuwa naye tu. Nakumbuka siku hiyo nililala majira ya saa saba na asubuhi nikapanga kwenda benki.

    Ilipofika, nikachukua begi langu na kwenda benki kwa lengo la kuchukua pesa hizo. Nilihitaji kuchukua milioni tisini kwani nilijua kungekuwa na dharura.

    Sikutaka kwenda na dalali, nilikwenda peke yangu. Niliingia benki nikiwa na begi langu lililokuwa na nguo ndani, unajua kwa nini? Kwa sababu ya kubadilisha.

    Nilijua kwamba unapotoka kuchukua pesa nyingi benki na unapotoka, huwa kuna watu wanakufuata kwa ajili ya kukuua na kukuibia pesa, sasa kwa sababu nilikuwa mjanja, nilitaka niwachezee mchezo mpaka washangae.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilihitaji kiasi hicho cha pesa, niliambiwa nisubiri wakati wakiendelea kufanya process za mimi kupata kiasi hicho cha pesa. Baada ya saa moja, nikapewa na kuanza kuondoka.

    Hapo benki, unapotoka, kwa kuwa ipo kwenye ghorofa refu, kabla ya kwenda nje kuna lifti, hivyo nilichokifanya ni kwenda kwenye lifti kama ninataka kwenda juu, humo ndani, nikabadilisha nguo zangu na kuchukua zilizokuwa kwenye begi, nikavaa na kofia kabisa kisha kuteremka kutoka kwenye lifti na kuchukua nyingine, nikaanza kushuka.

    Nilitoka huku nikiwa na muonekano mwingine kabisa. Kwa kawaida sehemu hiyo si ya kupaki bodaboda, ila kwa mbali niliwaona vijana wawili, walikuwa na elementi, walisimama pembeni ya bodaboda yao huku wakiangalia kule kwenye jengo lile la benki, nikajua tu kwamba walitonywa kuna mtu ametoa milioni tisini hivyo walitakiwa kunifanyia uninja, kumbe hawakujua kama mimi mwenyewe nilikuwa ninja.

    Nikawaacha wakiendelea kumsubiri mtu aliyevalia suruali ya kitambaa na fulana nyekundu, kumbe huyu aliyetoka ambaye alivalia pensi ya jinsi, fulana ya bluu na kofia nyeusi na kubeba begi ndiye mtu ambaye walitakiwa kumfuata, ila kwa kuwa hawakugundua kutokana na maelekezo waliyopewa kuwa tofauti na jinsi nilivyokuwa, nikawa huru kuondoka bila kufuatwa na yeyote yule.





    Siku hiyohiyo nikamtafuta dalali na kumwambia kuhusu mzigo niliokuwa nimechukua, hakukuwa na kitu cha kupoteza kwani siku zote pesa ni mwanaharamu kwa sababu unaweza kujiona tajiri asubuhi lakini wakati wa adhana ya Magharibi ukawa masikini wa kutupwa.

    Tulipofika nyumbani kwa akina Zamaradi, baba yake akaitwa na kumlipa pesa zake na hatimaye kuinunua nyumba hiyo. Kiukweli haikuwa nzuri sana kama nilivyowaeleza lakini niliamini kwamba baada ya kuwa nayo basi ningeweza kuirekebisha na kuwa moja ya nyumba nzuri sana hapa Dar es Salaam.

    Wakati hayo yote yakiendelea sikuwa nimemuona Zamaradi, wakati mwingine nilijiongelesha kwa sauti kubwa ilimradi tu anisikie na kama alikuwa chumbani aje sebuleni lakini wapi.

    Tulifanya biashara kwa amani kabisa na hivyo kuhitaji mwezi mmoja kwa ajili ya kujiandaa kuondoka mahali hapo. Hilo halikuwa tatizo lakini pia nikamwambia dalali kwamba nilihitaji kununua kiwanja maeneo ya Goba kwani pia nilitaka nishushe mjengo mkubwa wa kuanza maisha yangu.

    Ngoja nikwambie kitu. Nilikuwa na pesa, tena nyingi mpaka wakati mwingine nilitamani sana kuombwa na mademu hivyo hii nyumba ya Sinza nilitaka niirekebishe ili iwe inatumika kwa ajili ya kulala na warembo tu, halafu ile ya Goba ambayo ningeijenga iwe ya mwanamke mmoja tu ambaye angekuja na kuwa mke wangu.

    Tulipoondoka tu, nikampigia simu Zamaradi na kuongea naye, nilimwambia kwamba nilitoka kwao, aliniambia kuwa alikwenda kwa mama yake mdogo aliyekuwa akiishi Temeke ila angerudi muda si mrefu.

    “Nije nikufuate?” nilimuuliza.

    “Wapi? Huku Temeke?”

    “Yaap!”

    “Nimetoka! Sasa hivi nipo hapa Veta!” alinijibu.

    “Hebu naomba uteremke hapo Ilala Boma mamii!”

    “Wewe upo hapo?”

    “Hapana ila nitafika kabla yako!” nilimwambia harakaharaka.

    “Halafu!”

    “Nataka tukae hapo Lamada tuongee kidogo,” nilimwambia.

    “Sawa love.”

    Akakata simu, nilihisi mwili wangu kama ukimwagiwa maji ya baridi, sikuamini mtoto angenikubalia kirahisi namna ile, nguvu ya pesa ilikuwa kubwa kupita kawaida.

    Haraka sana nikaelekea kwenye kijiwe cha bodaboda na kutaka kuchukua moja ya kuniwahisha haraka sana kwani kutoka hapo Veta mpaka Ilala hakukuwa mbali, kazi kwangu kutoka huku Sinza mpaka hapo Ilala.

    “Oya! Nataka unipeleke Ilala Boma,” nilimwambia dereva mmoja.

    “Haina noma! Pakia!”

    “Unajua kuendesha kwa kasi? Nataka niwahi!”

    “Wewe tu braza!”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Basi kama vipi, hakikisha hii pikipiki inapaa,” nilimwambia sentensi ambayo ilimaanisha nilikuwa na haraka kupita kawaida.

    Nilichomwambia ndicho alichokifanya, alikuwa na haraka kupita kawaida. Aliendesha pikipiki mpaka huku nyuma nikahisi kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wangu, na pesa zangu ningeziacha benki.

    Baada ya dakika tano hivi tukafika Ilala Boma, nikateremka, nikamlipa elfu kumi na kumwambia abaki na chenji wakati mimi nikiingia ndani ya Hoteli ya Lamada ambapo nikaelekea mapokezi na kuchukua chumba.

    “Nataka kile cha bei ya juu kabisa. Si mna VIP hapa?” niliuliza.

    “Ndiyo!”

    “Naomba,” nilimwambia.

    Haraka sana nikapewa, wakati nikielekea juu, Zamaradi akanipigia simu na kuniambia kwamba tayari alifika hapo Ilala Boma, nikamwambia aje hapo hotelini wakati nikiandaa mazingira.

    Nikaingia ndani ya chumba hicho, nilipokiangalia kitanda tu, nikasisimka ile kishenzi, sikuamini kama siku hiyo nilikuwa nammaliza huyu Zamaradi kiwepesi namna ile.

    Nikakilalia kwanza ili nijue kina uwezo gani, nikakukuruka hapo kitandani nikaona uwezo wake mzuri hivyo nikamsubiri. Baada ya dakika kadhaa simu ikapigwa kwa kuwa niliacha maelekezo kuhusu yeye pale mapokezi, nikaipokea na kuhitaji niletewe mpaka chumbani, nikaletewa.

    Nilipomuona Zamaradi akiingia, mapigo yangu ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu, nilipagawa, niliweweseka kupita kawaida. Kwa jinsi alivyokuwa amefungasha nikaona leo ilikuwa ni shida mahali hapo.

    Kwanza kwa mbwembwe nikamfuata na kumshika kiuno, nikamvutia kwangu na kuupeleka mdomo wangu sikioni kwake na kumnong’oneza.

    “Leo ndiyo leo! Yaani itakuwa kama nilifungwa jela miaka kumi,” nilimwambia kwa sauti ndogo na ya kunong’oneza sikioni kwake.

    “Una uhakika?”

    “Una pumzi za mbio ndefu?” na mimi niliuliza.

    “Zinatosha za kukimbia kutoka hapa mpaka Mlandizi!” alinijibu kwa sauti ndogo pia sikioni mwangu.

    “Tuongeze mpaka Chalinze! Yaani leo mpaka zile chipsi uziite chishiiiii....na pepsi uiite peshiiiii...” nilimwambia na wote kuanza kucheka.

    Kabla ya kitu chochote kile ilikuwa ni lazima umfanye msichana kuwa rafiki yako, ni kweli tulikuwa tumechati, tena sana tu lakini kulikuwa na uhitaji wa kumfanya kuwa rafiki zaidi.

    Sikutaka kukurupuka, nilikuwa bingwa wa kufanya makosa sehemu zote lakini chumbani halikuwa mojawapo. Nilijua jinsi ya kutafuta urafiki kwanza, kuzungumza kana kwamba sikuwa nikihitaji kitu chochote kutoka kwake.

    Tulikuwa kama marafiki wa muda mrefu, nilijitahidi alijue tabasamu langu, ajue jinsi lipsi zangu zilivyokuwa zikicheza, yaani kwa kifupi nilitaka ajue kila kitu kutoka kwangu, na auzoee mwili wangu pia.

    Pale kitandani, huku tukiwa tunapiga stori, nikasimama na kuvua fulana yangu na suruali yangu kisha kuelekea bafuni kuona.

    Mapenzi yalikuwa ni usafi wa hali ya juu, wakati mwingine watu waliyachukia kwa sababu wengine walitaka kuyafanya kuwa uchafu.

    Nilijua kabisa kwamba mapenzi ni uchafu lakini si wa kunuka jasho wala mdomo, ilikuwa ni lazima ujiandae, ujisafishe kote halafu ndiyo uje ule uchafu wa kwenye sita kwa sita.

    Hakuna siku ambayo nilioga kwa umakini kama siku hiyo, nilitoka nikiwa msafi mno na nilihisi kwamba kama ningekuwa naoga hivyo kila siku basi hata taulo lisingekuwa linachafuka.

    “Vipi? Maji yapo tayari!” nilimwambia.

    Akasimama na kuvua nguo zake, akabaki na ile ya ndani tu. Nilishtuka sana, nilimwangalia huku nikiwa namtamani kupita kawaida. Wakati mwingine nilitamani hata kumrukia kwani nilichanganyikiwa kupita kawaida.

    Akafungua mkoba wake na kuchukua khanga na kujifunga kisha kunigeukia na kuanza kutoa tabasamu pana.

    “Kwa hiyo hapo umevaa khanga moko?” nilimuuliza huku nikitabasamu.

    “Hahah! Fala sana wewe...” aliniambia huku akitoa tabasamu la mbali.

    Akaondoka na kuelekea bafuni. Kitu cha kwanza nikazima simu yangu, sikutaka nisumbuliwe, katika tukio kama hilo ulitakiwa utulie kama unanyolewa, halikutakiwa kuingiliwa na kitu chochote kile.

    Alipomaliza kuoga, akatoka, akakaa kitandani na kilichotokea hapo, hakifai kuandikika mahali hapa.

    Tulichukua masaa mawili, tukamaliza na kuelekea bafuni. Kila mmoja wetu alikuwa na furaha tele, sikuamini kama ningempata Zamaradi kirahisi namna hiyo, yaani kuniona jana tu, kupata sifa kwamba nilikuwa na pesa basi leo alijirahisisha na kulala naye.

    Tulipomaliza kuoga tukaondoka zetu huku mtu mzima nikijisikia mwepesiiiii kiasi kwamba niliona wepesi wangu ungenifanya hata kupaa angani kama ndege.

    ***

    Nisikilize! Mimi na Zamaradi tukawa wapenzi, alinipenda sana lakini wakati huo nilikuwa nikifikiria mambo mengine kabisa. Alikuwa akinipigia sana simu na kuzungumza naye, alihitaji niwe na mapenzi fulani hivi ambayo sikuwa nayo kwa sababu nilijua kwamba alipenda pesa zangu na si jinsi nilivyo.

    Hivyo naye nikapelekana naye kipesapesa kama alivyotaka. Wakati huo nilikuwa nikifanya mambo yangu na nyumba ile kuanza kubadilishwa taratibu.

    Mpaka wakati huo siku nimemwambia Nurat ukweli, tulikuwa tukionana na kuzungumza mambo mengine lakini mambo ya kumwambia kuhusu pesa, hayakuzungumziwa kabisa.

    Nilichokuwa nikimpendea Nurat ni kwamba alinithamini sana. Nilipokuwa sina pesa, alikuwa akinisaidia sana na hata siku hiyo ambayo tulionana, alijua kwamba sina pesa hivyo alinipa shilingi elfu hamsini.

    Moyo wangu ukahisi kabisa kwamba huyu ndiye alikuwa msichana pekee ambaye nilitakiwa kuishi naye. Unapompata msichana ambaye anakujua ulivyo, huna kitu, anakusaidia, huyo ni mtu muhimu sana ambaye unatakiwa kuishi naye, haijalishi wangapi watakuja mbele yako, mtu wa kwanza kabisa awe huyo anayekusaidia unapokuwa na shida.

    “Edward! Hivi kwa nini tusifanye Friends With Benefits?” aliniuliza huku akiniangalia machoni kwa macho ambayo yalionyesha kabisa kunipenda na kunihitaji.

    “Ndiyo nini hiyo?”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yaani tunakuwa marafiki, siku nikiwa na hamu ya kufanya mapenzi, nakupigia simu, tunaonana na kufanya, hata wewe ukiwa na hamu, unanipigia nakuja na kufanya. Tukiwa na shida tunasaidiana, tusiwe wapenzi, ukipata mpenzi, nitambulishe, sitojisikia wivu, hiyo ndiyo maana yake,” aliniambia.

    Unajua nilishtuka sana! Sikuamini kama duniani kulikuwa na kitu kama hicho. Yaani uwe na msichana, awe rafiki yako halafu ukitaka kuduu naye, unampigia simu, anakuja na kumalizana halafu hamjuani mpaka siku ambayo mwingine angekuwa na hamu.

    Nilimwangalia Nurat, sikummaliza hata kidogo, maneno yale hakutakiwa kuniambia mrembo kama yeye, kwa nini tufanye hivyo na wakati nilikuwa nampenda?

    “Mbona umekaa kimya?” aliniuliza.

    “Unajua nakupenda sana, sasa unaposema tuwe hivyo, kwa nini usinipe nafasi tu ya kuwa nawe?” nilimuuliza.

    “Edward! Mimi ni Mwarabu, najua unajua matatizo yetu! Kuwaambia kwamba nimepata mpenzi, mweusi, halafu hauna pesa, hawawezi kunielewa. Tuwe kama nilivyokwambia,” aliniambia.

    Nilijifikiria sana kwa sekunde kadhaa, nikajiona ni mjinga sana kama nisingekubaliana kuwa kama alivyoniambia. Basi nikatingisha kichwa changu na kumwambia nilikuwa radhi kuwa kama alivyosema, akaniambia twende sehemu kutembea.

    “Wapi?”

    “Wewe twende tu.”

    Kuanzia hapo nilimuona Nurat akiwa kwenye hali ya kawaida, alikuwa na mhemko kupita kiasi. Niliogopa, mimi na Mwarabu wapi na wapi, halafu nilishasikia kwamba watu wahivyo walikuwa wabaridi, hawakuwa kama ngozi nyeusi, hivyo niliamini hata siku ambayo tungekuwa faragha nisingeweza kufurahia kabisa.

    Wakati tukitembea, alikuwa akinishika mkono, nilijitahidi kuukwepesha lakini wapi. Akakodi Bajaj, tukapanda na kuondoka mahali hapo.

    Humo ndani ilikuwa balaa, yaani ndiyo niliamini kwamba siku hiyo ingekuwa ni ya kwanza kulala na msichana wa Kiarabu. Mara aniegemee, mara anishike huku na kule, yaani akaanza kuuchaji mwili wangu hata kabla hatujafika huko.

    Wakati mwingine nilitamani tu ghafla bin vuu tuwe chumbani kwani nilizidiwa nguvu na kuona muda wowote ule ningemwambia dereva Bajaj atupishe na mimi ningemlipa kiasi chochote alichotaka.

    Tuliondoka mpaka tulipofika chaka fulani hivi lililokuwa Sinza Kwa Remmy, tunateremka na kuelekea kwenye hiyo loji. Sikuwa nikiamini kilichokuwa kikienda kutokea, nikaanza kumkumbuka mshikaji wangu fulani ambaye kila siku alikuwa akiniuliza hivi:

    “Edward! Hivi ni bora ulale na mwanamke mwenye shepu nzuri ila sura mbovu au ulale na mwanamke mwenye sura nzuri ila mbaumbau?”

    Jibu langu nililokuwa nikimpa ndiyo siku hiyo nilikutana nalo kwa Nurat. Alikuwa mzuri mno lakini dada wa watu alikuwa kama kapigwa pasi nyuma. Hii ingenisaidia mno kwa sababu wakati mwingine baada ya kuchafua sana shuka unaonekana kuchoka, sasa kama mtu sura mbaya utainjoi vipi kurudi tena, hivyo niliamini kwamba msichana akiwa na sura nzuri anakuhamasisha kukurudisha mchezoni.

    Basi tukaingia, akachukua chumba na kwenda huko. Tulipofika, akakaa kitandani na kuniangalia. Nilikuwa najua sana kuigiza hasa eneo kama hilo, nilijifanya mshambuliaji nisiyelijua goli kumbe upande wa pili nilikuwa mfungaji mzuri kama Messi.

    “Mbona umesimama huko. Njoo huku basi,” aliniambia, nikajifanya nyoka wa maonyesho kumbe hakujua kama nilikuwa kobra mwenye sumu kali.

    “Naogopaaaa...” nilimwambia huku nikitabasamu.

    “Sasa unaogopa nini? Hebu njoo,” aliniambia na kunivuta mpaka kitandani.

    Kwenye mapenzi nilijifunza hivi: Hata kama ulikuwa konkodi, uwezo wa kumiliki hata wanawake watatu au wanaume watatu faragha lakini ukitaka kumdatisha mwenzio ni lazima ujifanye muoga flani, ukiguswa huku unashtuka, mara hutakitaki, mara hivi na vile.

    Hiyo itamfanya hata mwenzako kuwa na hamu ya kutaka kufanikisha lengo lake, ndivyo nilivyomfanyia Nurat kiasi kwamba akahisi kama vile sikuwahi kuwa na msichana faragha.

    “Baby! I just need you right now!” aliniambia kwa Kizungu, bado nikajifanya kama boya fulani hivi.

    “Lakini.......”

    “Shiiiiiiii...I just need you right now. I’ve been waiting for this moment, please, just give me what you’ve got,” aliniambia huku akianza kunipapasa.

    “Nurat...lakiniiiiiiiii....” nilijifanya kama kujitetea.

    Mtoto wa Kiarabu hakutaka kunisikiliza, yaani alichanganyikiwa kabisa. Akaniona kuwa mgeni, akahitaji kunifundisha hesabu za 3+6 lakini cha ajabu nikamuonyesha ni jinsi gani naweza kuifanya 5y+8x na kumtafutia thamani ya x na y.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “What do you know about? Doggie?” aliniuliza huku akiniangalia.

    “No! I know many of them. The 69, The Ship, variation, the pillow lift, the bum lift, over the edge, The jumping frog, legging....na nyingine nyingi,” nilimwambia huku nikimwangalia usoni.

    “How do you know all of this?” aliniuliza kwa mshangao.

    “I am a big fan of Kamasutra,” nilimjibu huku nikimwangalia usoni kwa macho yauliziayo ‘Nianze mimi ama wewe?’



    Siku hiyo ilikuwa ni ya kipekee sana kati yangu na Nurat. Tulitulia ndani kwa zaidi ya saa moja na baada ya kumaliza, akaondoka kuelekea kwao huku akionekana kuwa na furaha mno.

    Aliniambia ukweli kwamba tangu azaliwe hakuwahi kukutana na mwanaume aliyekuwa na nguvu kama mimi. Nilishangaa sana, nikajiuliza maswali mengi mno kuhusu vijana wa Dar, sikujua tatizo lilikuwa nini ndiyo maana biashara ya mchuzi wa pweza ilikuwa kubwa sana Dar es Salaam kwa kuwa hawakuwa siriazi faragha.

    Nurat hakuniacha mikono mitupu, akanipa na pesa za matumizi, nakumbuka ilikuwa ni zaidi ya shilingi laki moja ambayo yote nilimtumia Zamaradi kwa kuwa niliona kwangu si kitu kwa kuwa nilikuwa na zaidi ya bilioni.

    Maisha yangu yaliendelea, baada ya kuinunua nyumba ya akina Zamaradi nikafanya mpango wa kununua kiwanja tegeta ambapo huko nikaanza kujenga. Nilitaka kuwa na nyumba kubwa, yenye kila kitu ndani kwa mtu yeyote ambaye angefanikiwa kuingia basi ajue kweli aliingia kwenye moja ya nyumba kali sana hapa Afrika.

    Baada ya kukamilisha kununua kiwanja, nikapanga mipango yangu ya kujenga jumba hilo la kifahari, nikanunua ramani ya nyumba yenyewe lakini tatizo moja ni kwamba kiwanja kilikuwa kidogo na nyumba niliyoitaka ni kubwa mno.

    “Hiki kiwanja cha nani?” nilimuuliza mwenyekiti wa mtaa ambaye naye alifanya kazi ya udalali wa viwanja huko tegeta. Nilimuulizia kiwanja kilichopakana na changu.

    “Kuna mwanamke mmoja hivi anafanyaga biashara za kwenda Dubai, ndiye mwenye kiwanja hiki,” alinijibu.

    “Mi nataka nikinunue, anauza kiasi gani?” nilimuuliza.

    “Mmh! Sidhani kama atauza, aliniambia kwamba anataka kuja kujenga hapa mwaka huu na mafundi kashatafuta,” alinijibu.

    Nilijua tu kwamba ningefanikiwa kununua kiwanja chake kama tu ningeonana naye. Nilimwambia mzee huyo aliyeitwa kwa jina la Hamadi kwamba aniunganishe naye ili nizungumze kwani nilihitaji mno kuwa na kiwanja chake.

    Hilo halikuwa tatizo, akakubali na hivyo kunipa namba yake ya simu. Nilimpigia siku hiyohiyo na kujitambulisha, nilimwambia kwamba nilikuwa na shida ya kuzungumza naye hivyo kama lingekuwa jambo jema basi tukutane sehemu na kuonana.

    Hakukuwa na tatizo, baada ya saa moja tukaonana katika Mgahawa wa KFC uliokuwa Mikocheni na kuanza kuzungumza.

    Alikuwa mwanamke mtu mzima kidogo lakini kwa jinsi alivyoonekana, alipenda mno mambo ya ujana. Kichwani alikuwa na wigi la Peruvian, vidoleni aliweka kucha za bandia, alivaa viatu virefu huku akiwa na sketi fupi ambayo ilipanda mpaka juu ya mapaja.

    Pamoja na ugwadu wangu kwa watoto wa kike lakini huyu mwanamke hakunivutia hata kidogo. Alijitahidi hata kukibusti kifua chake lakini yote hayo yaligonga mwamba mbele yangu.

    “Naitwa Edward,” nilimwambia huku nikitoa tabasamu, tena kwa kumuonyeshea heshima, kwa kuwa alinikuta hapo, nikasimama na kumpa mkono.

    “Naitwa Miss Maria,” aliniambia.

    Sikutaka nimwambie moja kwa moja kuhusu mpango wangu, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuzoeana kwanza ili hata nitakapomgusia suala langu kusiwe na tatizo lolote lile.

    “Ila umependeza sana! Unaonekana kama binti wa miaka kumi na nane,” nilimwambia, kwa kifupi nilikuwa nikimpaka mafuta kwa kutumia mgongo wa chupa.

    “Ahsante sana! Yaani nimetoka Dubai, nimechoka, nilipanga leo niende kulala pale Serena Hotel lakini daah! Simu yako ikanifanya nije kwanza kuzungumza na wewe,” aliniambia, hapo tu nikapata picha kwamba alikuwa mwanamke wa kupenda sifa, na mimi kumjaza mtu ndiyo zangu, nikaanza kumpampu ili aendelee kujisifia.

    “Nilisikia kwamba unafanya biashara!” nilimwambia.

    “Yeah! Ofcourse nafanya. Unajua maisha haya ya ajabu sana. First day kwenda Dubai, nilishangaa sana, unajua it was like surprise kwangu, yaani majengo ya kule ni balaa. It came a time mpaka nikawa najiuliza hivi nilifika peponi ama bado nipo hapa duniani?” alijigamba.

    “Duuh! Kwa hiyo hata China ushafika kwenda kuchukua bidhaa?”

    “Yaani huko ndiyo nakwenda kama kariakoo vile, I’m just flying anytime ninayotaka,” aliniambia.

    “Hebu niambie kwanza China kupo vipi, yaani nataka nijue bhana,” nilimwambia kwa lengo la kumfanya aendelee kujisifia kama alivyofanya.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyie hapa duniani kuna watu wanajua kujisifia, aliniambia mambo mengi, sijui alikwenda China, alifanya biashara nyingi mpaka akakutana na Jack Ma, yule bilionea wa China.

    Nilibaki nikizisikiliza tu pingu alizokuwa akinifunga, hakujua kama mimi ni mjanja basi akajiona anajua sana kumbe na mimi nilikuwa na tageti zangu.

    “Daah! Kati ya watu waliofanikiwa, wewe ni mwanamke wa chuma,” nilimwambia.

    “Yaani usione hivi. Maisha haya nisingepambana hata gari nisingenunua.”

    “Naona jitihada zako, umekuja na Verrosa new model.”

    “Kuna nyingine nimeiacha nyumbani, ni Range SUV. Niliinunua kwa kuiagiza kutoka Japan, ila siipendi kwa kuwa ipo juu juu sana. Mimi napenda kama Verrosa. Kuna Hammer moja niliagiza, nikaona kama it is not my type, nikampa my young sister, naye ikamshinda manake inakula sana mafuta, she sold it,” aliniambia.

    Kwanza nikashusha pumzi ndefu, nilitamani kucheka lakini nikapiga moyo konde niendelee kumsikiliza. Alinipiga sana fiksi na mwisho wa siku nikaanza kumwambia kuhusu mpango wangu.

    Alinisikiliza, kwa jinsi nilivyoonekana tu alinichukulia kawaida sana kwa kuwa nilivalia kikawaida mno.

    “Unataka kununua kiwanja changu?” aliniuliza.

    “Ndiyo! Natamani niwe nacho, kimekaa sehemu nzuri kidogo,” nilimwambia.

    “Una hela? Mimi mwenzio Mchaga, pesa mbele kama tai,” aliniambia.

    “Sina hela ya kutosha, kwani unakiuza kiasi gani?”

    “Milioni kumi!”

    “Milioni kumi?” niliuliza kwa mshtuko.

    “Ndiyo!”

    Kwanza nikabaki kimya, nilikuwa na pesa lakini haikuwa ya kutumia hovyo kiasi hicho, kama kweli alikuwa akikiuza kwa bei hiyo inamaana kwamba nisingeweza kununua kwa sababu tu nilijiandaa kukinunua kwa shilingi milioni tano tu.

    Huyu mwanamke aliyeitwa Maria japokuwa alikuwa mtu wa sifa lakini namsifu sana kwa kuwa alikuwa na akili mno. Unajua kwa nini? Ngoja nikwambie kilichotokea hapo baada ya kuona nasitasita kutoa milioni kumi.

    Akapiga simu sehemu na kuanza kuongea na mtu mmoja na kumwambia kwamba alitaka kuonana naye na ingekuwa vizuri kama wangekuja wote wawili, sikujua hao walikuwa akina nani lakini kwa jinsi alivyokuwa akiongea, alionekana kuwa mtu fulani ambaye alizoeana naye sana.

    Akanihamisha kabisa kutoka kwenye suala la kiwanja na kuzungumza mambo mengine ya kujifagilia kama kawaida yake. Tuliendelea na mazungumzo kama nusu saa hivi ndipo nikaona gari fulani aina ya IST ikipaki na milango ilipofunguliwa, aisee waliteremka wasichana warembo ile balaa.

    Naweza kusema kwamba hao ndiyo walikuwa mademu wa viwanja, waliofaa kuishi jijini Dar es Salaam na kwenda kwenye Ukumbi wa Element kama ilivyokuwa kwa wengine warembo.

    Walitembea kwa mwendo wa maringo mno kana kwamba hii ardhi waliyokuwa wakiikanyaga haijawahi kuchimbiwa choo. Walinata na walikuwa wakali ile kinoma, Maria akasimama na kuwafuata, akawapokea na kuwaleta palepale.

    Nilishindwa kubaki kimya, mimi mwenyewe mdhaifu kwa watoto wa kike hivyo kila nilipokuwa nikiwaangalia, moyo wangu uliniambia ‘Hawa unapiga, ukishindwa utakuwa mzembe sana’.

    Akanitambulisha. Mmoja aliitwa Doreen. Huyu alikuwa mwembamba kama Miss Tanzania, mweupe, alipokuwa akitabasamu vishimo viwili vilikuwa vikionekana mashavuni mwake, sura nyembamba na kitovuni alitoboa kipini kitu kilichonichanganya sana.

    “Hi Doreen,” nilimsalimia huku nikimshika mkono, ulikuwa lainiiiiiiiiii.

    “Hi!”

    “Naitwa Edward!” nilijitambulisha.

    “Ahsante kwa kukufahamu love,” aliniambia, akanishtua kishenzi, yaani kidogo tu nishaanza kuitwa love.

    “Na huyu anaitwa Amanda,” aliniambia.

    Huyo Amanda naye alikuwa mkali ile balaa, sura yake ilikuwa pana kidogo lakini alikuwa na sura ya kitoto mno, alijaajaa na huku nyuma ilikuwa si mchezo, yaani yangekuwa yale mambo yetu angewekwa kwenye kipengele cha ‘Big Booty’.

    “Hi Amanda!”

    “Hi Baby love,” naye akanirudishia.

    Mpaka hapo nilishapagawa kinoma. Muda wote huyo Maria alikuwa akiniangalia tu, alikwishajua kwamba nilipagawa hivyo akaanza kuniambia kuhusu ishu ya kiwanja.

    “Kwa hiyo bwana mimi kiwanja nauza milioni kumi, upo tayari?” aliniuliza.

    Yaani hili swali nililiona la kitoto sana, mbele ya mademu wakali kama wale, niseme milioni kumi sina si ungekuwa ujinga huo? Huo ndiyo ujanja alioutumia, aliamini kwamba kama angewaita wanawake hao wauri, kidume mimi ningekubaliana na bei yake kwa sababu nisingetaka kujishusha, na kweli nikakubaliana naye.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yaani milioni kumi ikanitoka na kukubali kulipana siku hiyohiyo, yaani kila kitu ningemalizana naye siku hiyo. Baada ya kukubaliana, tukaenda benki huku nikiongozana na wote watatu na tulipomaliza tukaenda kwenye kiwanja na kukinunua.

    “Aya sasa! Kazi kwako,” aliniambia Maria.

    “Kivipi sasa mbona sijakuelewa!”

    “Au hutaki niwaambie warudi?” aliniuliza.

    Hapo nikapata jibu alimaanisha nini. Nisingekuwa mjinga kumwambia sikutaka na hivyo warudi. Mshikaji wangu ninapokwambia kwamba nilikuwa na mambo ya kishetani sana niamini tu, kwa sasa nimebadilika kwa sababu tu nimeoa na nina familia yangu nyumbani.

    “Kwa hiyo wote wawili?”

    “Yeah! Threesome! Au hutaki?” aliniuliza.

    “Mbona umeng’ang’ania sitaki tu!”

    “Hahaha! Kazi kwako! Ila wanaendaga hotelini tu hao,” aliniambia.

    “Hilo pia si tatizo.”



    ITAENDELEA





0 comments:

Post a Comment

Blog